JK: Siku za madiwani wanaouza maeneo ya wazi Dar zinahesabika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK: Siku za madiwani wanaouza maeneo ya wazi Dar zinahesabika

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, May 26, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 26, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Rais Jakaya Kikwete, akiwasili katika eneo la mradi wa Mpango wa Huduma ya Maji na usafi wa Mazingira kwa Jamii Mrosso Mburahati katika ziara yake jijini Dar es Salaam kuangalia hali ya upatikanaji wa maji. Kulia kwake ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Mark Mwandosya.  Rais Jakaya Kikwete amesema siku za madiwani wanaouza viwanja vya wazi jijini Dar es Salaam zinahesabika.
  Hivyo amewaonya wajiepushe na vitendo hivyo, vinginevyo atawataja kwa majina kabla ya hatua nyingine kuchukuliwa dhidi yao.
  Rais Kikwete alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam, alipofanya ziara ya siku moja kuangalia matatizo ya maji yanayowakabili wakazi wa jiji hilo.
  Alisema anawajua kwa majina madiwani wanaouza maeneo ya wazi na kuwataka waache mara moja kwa kuwa wanawanyima haki watoto wanaotumia sehemu hizo kwa ajili ya michezo.
  "Mimi nawajua madiwani wenye tabia hii, lakini sitaki tufike mbali, nataka waache mchezo huo," alisema.
  Pia, Rais Kikwete alisema serikali kuu haitatoa fedha kwa ajili ya kugharamia uzoaji taka jijini hapa, badala yake aliziagiza Manispaa za Temeke, Kinondoni na Ilala kuweka mipango itakayowezesha kutumia mapato yao kufanikisha kazi hiyo.
  Alitoa kauli hiyo kufuatia ombi la Diwani wa kata ya Kijitonyama, Omari Kimbau, aliyeomba serikali kuu kuzisaidia manispaa kutimiza mpango wa uzoaji taka.
  Rais Kikwete alisema uchafu katika jiji hilo umekithiri, kiasi cha kutia aibu wakati watendaji wapo lakini wanashindwa kuchukua hatua stahiki.
  Rais Kikwete alikiri kuwepo tatizo la upatikanaji wa maji, hivyo kuwaagiza watendaji wa Kampuni ya Maji Safi na Maji Taka (Dawasco) na wale wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (Dawasa) kuweka mikakati ya kulimaliza.
  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco, Alex Kaaya, alisema tatizo la maji katika jiji la Dar es Salaam litaweza kupunguzwa kwa kiasi kikubwa ifikapo mwaka 2013.
  Alisema Dawasco inatarajia kuongeza uzalishaji katika mitambo ya Ruvu Chini na Ruvu Juu ifikapo Julai mwaka huu.
  Kaaya alisema mahitaji ya maji kwa jiji la Dar es Salaam lenye wakazi zaidi ya milioni nne ni lita za ujazo milioni 450 kwa siku wakati upatikanaji wa sasa ni lita milioni 272 kwa siku.
  Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa, Richard Mutalemwa, alsiema ili kupata maji ya uhakika inahitajika mitambo mipya ya kusukuma maji, kwa kuwa iliyopo ni mwaka 1976 na kwamba imechoka.
  Rais Kikwete aliigiza Dawasco kuacha tabia ya kuwapelekea wateja wao ankra wakati maji hayatoki katika maeneo yao.
  Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Mark Mwandosya, alisema serikali ina mpango wa kuchimba maji katika eneo la Kimbiji na Mpera ili kumaliza tatizo la maji.
  Rais alitembelea maeneo ya Mburahati, Kimara Mavurunza na Keko Tololi na kisha alikutana na watendaji wa mkoa wa Dar es Salaam katika ukumbi wa Karimjee.  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #2
  May 26, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,944
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Hivi diwani si anachaguliwa na wananchi! Yeye akiwataja majina inawasaidia vipi wananchi? Hizo hatua zitakazofuata ni za kichama au kiserikali? Kama kiserikali yeye nafikiri hana uwezo; kama kichama atakuwa na uwezo kwa wale wa CCM tu. Kama mahakamani basi atajikuta hata yeye mwenyewe anashitakiwa kwa kununua eneo la wazi. Diwani ni kama mbunge, maamuzi si ya diwani mmoja mmoja, ni ya kikao cha madiwani kama bunge. Sasa je ni kweli diwani mmoja anaweza kuuza kiwanja peke yake? Je, inawezekana kumshughulikia diwani mmoja peke yake bila mwenyekiti wa halmashauri au meya? Je, anauwezo wa kulishughulikia baraza zima la madiwani? Je, huu sio usanii!!??
   
 3. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #3
  May 26, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Wala rushwa anawajua kwa majina - aliwataja au kuwachukulia hatua?

  Wauza unga anawajua kwa majina - aliwataja au kuwachukulia hatua?

  JK you make me hate you more when you keep on making such false promises!
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  May 26, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  grrrrrrrrr.. c'mmon man!
   
 5. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #5
  May 26, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,469
  Likes Received: 5,847
  Trophy Points: 280
  Anawajua na watapita kura za maoni kugombea halafu watagawa tena hayo maeneo......CCM weneyewe ndio mabingwa wa kutwaa maeneo ya wazi kama BIAFRA,pale Mwinjuma opposite Meridian.....hata pale Mango/Vijana palikuwa open space kabla ya Tanu Youth League(TYL) kupachukua...Kirumba.....the list goes on....so these diwani are just scapegoats
   
 6. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #6
  May 26, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Awataje na maMeya pia sio madiwani tu. Akishawataja hao, awataje na wale vigogo waliotaka kugawana eneo la wazi lililo kule Msasani!
   
Loading...