JK: Sijawahi kusema serikali yangu itajenga Barabara kupitia Mbuga ya Serengeti

Ikwanja

JF-Expert Member
Jul 12, 2011
2,082
581
Wana JF, nimesikia sasa hivi kutoka TBC taifa kuwa Kikwete aka Vasco Dagama kuwa hajawahi kusema popote kuwa serikali yake itajenga barabara ya rami kuunganisha Arusha na Mara kupitia mbuga ya Serengeti. Amesema hayo akimwambia Zuma kuwa yeye ni mtu wa mazingara.

Mimi ninvyokumbuka ni kuwa alisema tajenga na alisema hata watu wasemaje yeye anawajali wananchi wake. wenye video ya hayo mambo tujuzeni tafadhali. nimesikitika sana kwa rais wetu kuwa mwongo. hii ni janja ya kuomba misaada.

naomba mwogozo wenu.
 
Huyu jamaa ni mwepesi wa kusahau maana atasema hata zile hotels alizo jenga kule mbugani hakuwahi kumpeleka Lowasa Bungeni kutetea ujinga ule au leo kasahau .
 
hiyo karibuni ni lini katika kipindi gani?????????? Isije ikawa majungu
 
ukiwa na mtu kama huyu usifanye mambo aliokuagiza maana utaumbuka..

Mungu Ibariki Tanzani
Mungu mnusuru Rais..
 
Mbona mtu wenye ni Bogus, hajui chochote hata Matatizo ya nchi hajui, hajui kama Nchi ipo gizani anasikia, hajui kuwa kuna mgao anaambiwa, hajui kama nchi imemshinda, bali anasikia. Hajui kwanini Tanzania ni maskini, anasikia watu wakisema, Hajui kama nchi imeja rushwa, anasikia tu. Kila Kitu hajui na hajui chochote zaidi ya kusikia kwa watu.

Hata Watanzania hawajui kwanini Dowans imelipwa, Watanzania hawajui kwanini walimchagua Kikwete 2005.
 
another kikwete record duh, hii mimi nilimsikia kwa masikio yangu wala sikuambiwa na mtu.

nadhani kunatatizo kubwa up stair
huyu jamaa aka check up stair kabla ajauza nchi bila kujua
 
''Lairs should have good memories'' otherwise lazima wakubambe sasa huyo tunamuona coz ndio tabia yake, kwani aliwahaidi watanzania watakua na maisha bora lakini sasa hivi ni kila mtanzania na jiza.
 
Wana JF, nimesikia sasa hivi kutoka TBC taifa kuwa Kikwete aka Vasco Dagama kuwa hajawahi kusema popote kuwa serikali yake itajenga barabara ya rami kuunganisha Arusha na Mara kupitia mbuga ya Serengeti. Amesema hayo akimwambia Zuma kuwa yeye ni mtu wa mazingara.

Mimi ninvyokumbuka ni kuwa alisema tajenga na alisema hata watu wasemaje yeye anawajali wananchi wake. wenye video ya hayo mambo tujuzeni tafadhali. nimesikitika sana kwa rais wetu kuwa mwongo. hii ni janja ya kuomba misaada.

naomba mwogozo wenu.

Kiswahili basi ndugu yangu; hebu angalia maneno hayo yenye rangi nyekundu!
 
Hata kule Kigoma alishawaahidi kua mkoa wao ataugeuza na kua kama Dubai! Lakini alishakana na kusema hakusema bali ulimi hauna mfupa!
 
kwa taarifa zaidi hii ilikuwa katika taarifa ya habari ya saa saba leo mchana. na hiyo ni taarifa iliyotolewa na Salva aki quote mazungumzo ya kikwete na zuma
 
Bado kidogo tu atasema hakuwahi kuahidi ''maisha bora kwa kila Mtanzania'' atasema watu tulimuelewa vibaya. Huyo ndio Vasco !
 
Back
Top Bottom