JK si mwanasiasa makini

Mkerio

Member
Mar 12, 2006
35
0
JK wakati analihutubia bunge alisema kulikuwa na udini kwenye uchaguzi na atajitahidi kutibu makovu. Waelewa tulijua kuwa CCM ilitumia udini na sasa wanataka kuacha udini baada ya uchaguzi. Cha kushangaza gazeti la Habari Leo linaendeleza udini wa hatari. Leo waneandika Zitto anachukiwa Chadema kwa vile yeye ni Mwislamu. Pamoja na kwamba wana nia ya kuigawa chadema kwa misingi ya dini, wajue chadema ina wafuasi wa dini mbalimbalimbali wanaweza kufikia milioni 5 na zaidi. Kuwagawa watu milioni 5 kwa udini ni kuligawa taifa na haitaishia chadema itawatafuna CUF na CCM pia. JK ana uhusiano na Habari Leo. Kukaa kwake kimpya kunadhihirisha bado unaamini kwenye mbinu hii dhaifu na ya hatari ya udini kuigawa nchi vipande vipande. Hapa ndio tofauti kubwa inajionyesha kati ya JK Nyerere na JK huyu. Nyerere alikuwa thinker na aliyekuwa na uwezo ukubwa wa kutumia hoja za kisiasa kutafuta kuungwa mkono. Hawa wanatafuta kuungwa mkono au kupambana na wapinzani wao kwa kutumia dini. Mungu ibariki TZ!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom