Jk si mtu wa watu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jk si mtu wa watu

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Bobby, Oct 28, 2010.

 1. B

  Bobby JF-Expert Member

  #1
  Oct 28, 2010
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,683
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Nimekuwa nikikerwa sana sana na mabango ya kijani yaliyoonea nchi nzima yanayotaka kutuaminisha kwamba mgombea urais wa thithiem ni mtu wa watu hivyo tumpe nafasi nyingine. Alipewa nafasi ya miaka mitano kuonyesha kwamba yeye ni mtu wa watu hakufanya hivyo lakini kupitia mabango yaliyokosa ujumbe anataka kutumainisha kwamba yeye ni mtu wa watu. Kukerwa kwangu na mabango haya kumeongezeka zaidi baada ya kuvuja kwa habari kwamba kumbe mabango haya yasiyo na idadi nchi nzima japokuwa hayana ujumbe wa maana zaidi ya picha zilizochakachukiriwa eti kodi yangu imetumika kuyaprint huko Canada. Mpaka sasa hakuna aliyekanusha so huenda hizo habari zikawa ni habari za kweli kwani yule mzee wa kisomari mtaalumu wa kukanusha asingeweza kuvumilia kiasi hiki. Naomba kwa ufupi nitumie mabango hayo machache kati ya mengi kueleza kwanini JK si mtu wa watu.

  (1) Kuna moja liko pale karibu na fire ambapo jk kama vile mfalme taratibu anafungua kioo cha cruiser yake V8 iliyojaa kiyoyozi na kumpa mkono bibi aliyechoka mbaya. Ujumbe unasema tunawajali wazee. Haya kama si matusi ni nini jamani? Eti kuwajali wazee ni kumpa mkono mzee ilihali serikali yako hakuna chochote ilichowafanyia hao wazee? Hivi wale wazee wa EAC wamelipwa haki zao? Na wale wazee wa kambi ya wazee morogoro wanaoishi gizani kwa kushindwa kulipa bill ya Tanesco ya milioni moja? JK wewe si mtu wa watu wala huwajali wazee.

  (2) Kuna jingine jk anaonekana kambeba mtoto mdogo, ujumbe wa bango unasema watoto wote ni wa kwetu. Huu ni upuuzi mwingine baba. Hivi watoto wote wa watanzania wangekuwa wako kama akina hassan na wengine ungethubutu kuruhusu huduma mbovu kiasi kile katika mahospitali ilihali waziri wako mmoja anatumia gari ya million 400? Wale akina mama zaidi ya 500 kwa kila 100000 wanaokufa kila mwaka wakati wa kujifungua kwa kukosa huduma za afya angeacha waendelee kupotea ilihali mafisadi wanaendelea kufisadisha koda zetu?

  (3) Bango jingine linamwonesha akimsikiliza mzee mmoja na ujumbe unasema eti jk ni msikivu. This is very cheap jamani acheni hizo. Hivi JK angekuwa msikivu kwa kwa watanzania angethubutu kukarabati ikulu kwa billion 29 wakati kiliomita moja kutoka hapo ikulu kuna watoto hawana madawati ya kusomea na akina mama Amana na temeke hospital wamelala sakafuni baada ya kujifungua?

  (4) Jingine liko machinga complex pale, jk anaoneka ameshika bilauli ya nyanya ya majasiriamali. Jamani hivi wale wakulima kule Nkasi na kwingineko ambako mazao yao yamekosa soko kwa ukosefu wa miundo mbinu na serikali imekaa kimya? Na je zile vouchers za ruzuku za mbolea za mabilioni zilizoliwa na mafisadi na hakuna lolote lililofanyika bado mnatuambia serikali inajali wajasiriamali? Huwezi kuwa mtu watu wakati hakuna chochote unachofanya kuonyesha kwamba unawajali hao watu. Watu pekee jk ameonekana anawajali ni marafiki zake, lowasa, chenge, mramba na wengineo ndio maana yuko tayari kuwashtaki leo kwa kuliibia taifa na kesho akasimama jukwaani kuwapigia debe wachaguliwe kuwaongoza wananchi. This is really shame na huenda hakuna kwingine duniani yanawezekana haya zaidi ya Tanzani.

  Nimalizie kwa kusema jk si mtu wa watu kama mabango yanavyosema unless tuambiwe kwamba kwa definition ya ccm kuwa mtu wa watu ni kuwapa mkono vikongwe, watoto na wengineo ilihali matendo ya serikali yako ni kinyume na infact wapo wengi ambao wanapoteza maisha kwa uzembe wa serikali yako.
   
 2. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #2
  Oct 28, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 721
  Trophy Points: 280
  yale mabango yasikupe shida

  bado 2 days!
   
 3. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #3
  Oct 28, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  5) Kuna linalonikera zaidi lipo njia Panda ya kigogo linaonyesha Jk yupo maabara na wanafunzi limeandikwa Elimu bora najiuliza elimu ipi kama shule za kata hazina waalimu,maabara na maktaba
  6) Lingine lipo kinondoni mama anamtoto wake naye yupo pembeni limeandikwa TUNAJALI, unajali nini wakati vifo vya wakinamama wajawazito vinaongezeka kila mwaka.
  7) Lingine lipo Ocean road yupo na mama limeandikwa UPENDO WA MAMA kuna mantiki gani yakuweka mama yake au ndo inaonyesha kifamilia zaidi
   
 4. Emma Lukosi

  Emma Lukosi Verified User

  #4
  Oct 28, 2010
  Joined: Jul 22, 2009
  Messages: 932
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  CHADEMA ikishinda atatueleza alikotoa ela za mabango. Sh@##nzi kabisa.
   
Loading...