JK sasa avalia njuga mimba mashuleni!!!!

The Khoisan

JF-Expert Member
Jun 5, 2007
15,360
12,947
JK avalia njuga mimba mashuleni

2008-07-21 08:39:53
Na Lulu George,PST, Muheza

Rais Jakaya Kikwete, amelitaka Jeshi la Polisi, kutumia vipimo vya kutambua vinasaba (DNA) ili kuwabana wanaowapa mimba wanafunzi.

Alisema matumizi ya DNA yataharakisha taratibu za kiupelelezi na kupata ushahidi ili kuwanasa wale wanaowapa mimba wanafunzi na baadaye kuwakana.

Aliitoa agizo hilo mwishoni mwa wiki wilayani Muheza wakati alipokuwa akipokea taarifa ya maendeleo ya wilaya hiyo kufuatia siku tisa ya kukagua shughuli za maendeleo mkoani Tanga.

Rais Kikwete alisema tatizo la mimba kwa wanafunzi linakuwa kubwa kwenye maeneo mengi hapa nchini ambapo wahusika hushindwa kuchukuliwa hatua za kisheria kwa kutokukutwa na hatia.

Alisema hatua hiyo inatokana na mfumo hafifu unaochukua muda mrefu katika ukusanyaji wa vilelezo vya ushahidi.

Kufuatia hali hiyo Rais amezitaka mahakama kutoa ushirikiano kwa serikali katika kukabiliana na tatizo hilo kwa kuharakisha usikilizaji wa kesi pamoja na utoaji hukumu kwa watakaobainika kuhusika na vitendo hivyo.

``Ndugu zangu tatizo hili ni kubwa lakini hii inatokana na watuhumiwa kutochukuliwa hatua za kisheria, kumbe maabara za DNA tunazo kwa nini hatuzitumii wahusika wanaachiwa kwa sababu tu ya kukosekana kwa ushahidi..naomba sasa kila mtumishi wa serikali kwa wakati wake awajibike ipasavyo,``alisisitiza Rais Kikwete.

Awali akiwasilisha taarifa yake kwa Rais, Mkuu wa Wilaya ya Muheza Bi. Zainab Kondo, alisema kuanzia Januari hadi sasa watoto 49 wamepata ujauzito na hivyo kukatishwa masomo.

Bi.Zainab alifafanua kwamba 36 kati yao ni wa shule za msingi ambapo 13 ni wa sekondari zilizopo wilayani humo.

Alisema kufuatia hali hiyo kesi 26 kwa kipindi cha mwaka 2007 hadi 2008 zimefikishwa mahakamani na moja tu kati ya hizo ndiyo iliyotolewa hukumu.

Wakati huo huo Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete, amewataka wanawake kuwatunza watoto wa kike wasipate mimba kwani wanaweza kuambukizwa Ukimwi.

Mama Kikwete alisema wanawake wana wajibu mkubwa wa kuwalinda watoto wao ili waweze kuepukana na vishawishi ambavyo vimechangia kwa kiasi kikubwa watoto wa kike nchini kurudi nyuma kimaendeleo kwa kutotimiza malengo yao.

``Wakina mama wenzangu tunawajibika kuwalinda watoto wetu na kuhakikisha wanatimiza malengo iwapo hawatapata elimu ya kutosha ni dhahiri kuwa wataendelea kubaki nyuma katika suala zima la kuharakisha maendeleo na dhana ya kuondokana na mfumo dume itaendelea kuwa ndoto kwa wanawake wengi hapa nchini``,alisisitiza Mama Kikwete.

Tangu Rais Kikwete aanze ziara yake mkoani hapo Julai 14 mwaka huu,Wilaya ya Muheza imetajwa kuongoza katika tatizo la mimba kwa wanafunzi kwa mujibu wa taarifa zinazoendeleo kutolewa kwenye wilaya mbalimbali mkoani hapa.

SOURCE: Nipashe
 
Atavalia njuga mangapi?ana kilele nyingi lakini hatuoni vitendo.Amejaa pororjo tuu.
Mr President incase you didnt know,tumekuchoka and incase you have forgotten am herer to remind you that actions speak louder than words.
 
Raisi badala ya kudeal na macro affairs za nchi anaanza kukomaa na micro affairs.
Kama ni kweli he has lost his direction
 
Tatizo linalosababisha Mimba Mashuleni ni lipi?

Je Umasikini uliopita kiasi katika jamii zetu pamoja na sheria zilizopitwa na wakati?.

Je yote yako kwenye uwezo wa watendaji wetu?

Je RAIS amevalia njuga tatizo ambalo hajui chanzo chake?

Je hawa watoto wanajua kwanini wanasoma?

Je nani anatakiwa kuwaelimisha watoto maana ya kupata elimu?
 
Raisi badala ya kudeal na macro affairs za nchi anaanza kukomaa na micro affairs.
Kama ni kweli he has lost his direction

Hapo na anapo onyesha usanii wake, yaani hiyo kazi nayo ni ya kufaywa na Raisi? hapo kazi ya waziri wa Jinsia na watoto itakuwa ipi?

Ama kweli.. labda anatafuta pa kutokea baada ya hotuba za kila mwisho wa mwezi kugeuka shubili!
 
Raisi badala ya kudeal na macro affairs za nchi anaanza kukomaa na micro affairs.
Kama ni kweli he has lost his direction

Wewe, mimba kwa wanafunzi ni topical national issue kwa kiongozi anayeangalia mbali. Rais yupo sawa kuvalia njuga lakini sina uhakika kama njia anayojaribu kutumia kama ni sawa.
 
"[...Awali akiwasilisha taarifa yake kwa Rais, Mkuu wa Wilaya ya Muheza Bi. Zainab Kondo, alisema kuanzia Januari hadi sasa watoto 49 wamepata ujauzito na hivyo kukatishwa masomo....]"

Hivi ni kwa nini bado mpaka sasa wasichana wakipata mimba wanakatishwa masomo ? Sioni sababu yoyote ya kumfanya msichana huyo asiendelee na masomo, kisa kazaa. Inakuwa kama adhabu mara mbili, wakati bwana mhusika kama mwanafunzi, basi anaendelea na masomo yake bila taabu na kufanikisha maisha yake mbele ya safari. Tuamke Tanzania na kwenda na wakati.
 
Wewe, mimba kwa wanafunzi ni topical national issue kwa kiongozi anayeangalia mbali. Rais yupo sawa kuvalia njuga lakini sina uhakika kama njia anayojaribu kutumia kama ni sawa.

Tatizo la mimba ni national issue, lakini uzito wake kamwe hauwezi kulinganishwa na ufisadi unaofanywa ndani ya nchi yetu. Huku ni kubaraguza tu, kutaka kuzungumzia issue nyingine nyingine lakini ile ambayo Watanzania wengi tunataka kumsikia akitoa kauli yake anaendelea kuwa bubu!!
 
Poor Kikwete
Fanya kazi yako kama Rais acha kufanya vitu ambavyo sio kazi yako
Unaacha kufalia njuga Mafisadi unaenda kwenye Mimba??

kweli umekosa muelekeo wewe

Kaona kazi zake haziwazi sasa anacheza mipira ya watu.
 
Wa Mwanzo amtafute Mahita na kumfanyia hayo madudu ,lakini kukimbilia mashule ni kutafuta kupota wazimu maana kondomu zinagaiwa bure na elimu ya ngono nayo inafundishwa na kufundisha namna ya kudunga mimba sasa Mh.anaamrisha mambo mepya kwamba fanyeni mfanyavyo lakini hakuna kuzalishana.Tunaweza kusema sasa nanihii ni free ila kosa ni kudungishana mimba.Huyu Muungwana hajui hata anazungumza kitu gani ,si angelitamka tu kama kweli anataka kuwalinda watoto washule kuwa mapenzi na mtoto wa shule ni kosa la jinai.
 
Wewe, mimba kwa wanafunzi ni topical national issue kwa kiongozi anayeangalia mbali. Rais yupo sawa kuvalia njuga lakini sina uhakika kama njia anayojaribu kutumia kama ni sawa.

Jamani kila siku amelivalia njuga, amelivalia njuga. Sasa hizo njuga si zitakuwa zimejaa mpaka zinamfanya ashindwe kutembea. Mara ya kwanza kumsikia akilivalia njuga suala hili ni mwaka 2006 huko huko Tanga, alafu akaenda Lowassa tena tanga naye akalivalia njuga. Halafu Kikwete na Lowassa wote wakaenda kusini tena kulivalia njuga. Tena wakati mwingine wakasema wamelivalia njuga na kutaka wahusika wakamatwe. Kila siku wanasema wanalivalia njuga, maneno matupu kuliko vitendo

Basi Kikwete sasa ni "Mzee wa Kulivalia Njuga", maana amevalia njuga kila kitu, madawa ya kulevya, ufisadi nk

Asha
 
Wa Mwanzo amtafute Mahita na kumfanyia hayo madudu ,lakini kukimbilia mashule ni kutafuta kupota wazimu maana kondomu zinagaiwa bure na elimu ya ngono nayo inafundishwa na kufundisha namna ya kudunga mimba sasa Mh.anaamrisha mambo mepya kwamba fanyeni mfanyavyo lakini hakuna kuzalishana.Tunaweza kusema sasa nanihii ni free ila kosa ni kudungishana mimba.Huyu Muungwana hajui hata anazungumza kitu gani ,si angelitamka tu kama kweli anataka kuwalinda watoto washule kuwa mapenzi na mtoto wa shule ni kosa la jinai.

Halafu yule mkuu wa wilaya aliyetajwa kumpa mtoto wa shule mimba naye ameshavaliwa njuga tayari? sasa imefika wakati wa kuwataja wote ili wavaliwe njuga.

Sasa tutoe orodha wa kuvaliwa njuga! I am for DNA Test now...

Asha
 
JK avalia njuga mimba mashuleni

2008-07-21 08:39:53
Na Lulu George,PST, Muheza

Rais Jakaya Kikwete, amelitaka Jeshi la Polisi, kutumia vipimo vya kutambua vinasaba (DNA) ili kuwabana wanaowapa mimba wanafunzi.

Alisema matumizi ya DNA yataharakisha taratibu za kiupelelezi na kupata ushahidi ili kuwanasa wale wanaowapa mimba wanafunzi na baadaye kuwakana.

Aliitoa agizo hilo mwishoni mwa wiki wilayani Muheza wakati alipokuwa akipokea taarifa ya maendeleo ya wilaya hiyo kufuatia siku tisa ya kukagua shughuli za maendeleo mkoani Tanga.

Rais Kikwete alisema tatizo la mimba kwa wanafunzi linakuwa kubwa kwenye maeneo mengi hapa nchini ambapo wahusika hushindwa kuchukuliwa hatua za kisheria kwa kutokukutwa na hatia.

Alisema hatua hiyo inatokana na mfumo hafifu unaochukua muda mrefu katika ukusanyaji wa vilelezo vya ushahidi.

Kufuatia hali hiyo Rais amezitaka mahakama kutoa ushirikiano kwa serikali katika kukabiliana na tatizo hilo kwa kuharakisha usikilizaji wa kesi pamoja na utoaji hukumu kwa watakaobainika kuhusika na vitendo hivyo.

``Ndugu zangu tatizo hili ni kubwa lakini hii inatokana na watuhumiwa kutochukuliwa hatua za kisheria, kumbe maabara za DNA tunazo kwa nini hatuzitumii wahusika wanaachiwa kwa sababu tu ya kukosekana kwa ushahidi..naomba sasa kila mtumishi wa serikali kwa wakati wake awajibike ipasavyo,``alisisitiza Rais Kikwete.

Awali akiwasilisha taarifa yake kwa Rais, Mkuu wa Wilaya ya Muheza Bi. Zainab Kondo, alisema kuanzia Januari hadi sasa watoto 49 wamepata ujauzito na hivyo kukatishwa masomo.

Bi.Zainab alifafanua kwamba 36 kati yao ni wa shule za msingi ambapo 13 ni wa sekondari zilizopo wilayani humo.

Alisema kufuatia hali hiyo kesi 26 kwa kipindi cha mwaka 2007 hadi 2008 zimefikishwa mahakamani na moja tu kati ya hizo ndiyo iliyotolewa hukumu.

Wakati huo huo Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete, amewataka wanawake kuwatunza watoto wa kike wasipate mimba kwani wanaweza kuambukizwa Ukimwi.

Mama Kikwete alisema wanawake wana wajibu mkubwa wa kuwalinda watoto wao ili waweze kuepukana na vishawishi ambavyo vimechangia kwa kiasi kikubwa watoto wa kike nchini kurudi nyuma kimaendeleo kwa kutotimiza malengo yao.

``Wakina mama wenzangu tunawajibika kuwalinda watoto wetu na kuhakikisha wanatimiza malengo iwapo hawatapata elimu ya kutosha ni dhahiri kuwa wataendelea kubaki nyuma katika suala zima la kuharakisha maendeleo na dhana ya kuondokana na mfumo dume itaendelea kuwa ndoto kwa wanawake wengi hapa nchini``,alisisitiza Mama Kikwete.

Tangu Rais Kikwete aanze ziara yake mkoani hapo Julai 14 mwaka huu,Wilaya ya Muheza imetajwa kuongoza katika tatizo la mimba kwa wanafunzi kwa mujibu wa taarifa zinazoendeleo kutolewa kwenye wilaya mbalimbali mkoani hapa.

SOURCE: Nipashe

Hapa Rais wetu alikuwa anahutubia taifa kuhusu mimba hizo hizo, hii ilikuwa mwaka 2007 http://www.freemedia.co.tz/daima/2007/6/7/habari21.php

Asha
 
Waziri Mkuu naye alishustushwa sana na mimba hizo, toka mwaka 2006 alishasema wakamatwe. Sasa kama ingetekelezwa wangekuwa jela wanasubiriwa kupimwa DNA lakini ahaaaa wapi

http://www.habaritanzania.com/articles/1693/1/Mimba,-ndoa-za-wanafunzi-zamtisha-waziri-mkuu

Kwa hiyo ni vyema hao jamaa zetu wakafunga midomo yao kama hawawezi kuchukua hatua.

Utafikiri wanaguswa vile kumbe wanasema sema wapate kura za wanawake na vijana wa kike. Waonekane wanajali, kumbe nyuma ya mlango nao wanabeba vitoto vya shule

Kwani unafikiri serikeli ya JK wana jipya. Hawajui wanachokifanya ndiyo sababu wanang'ang'ania mambo kama hayo. Tatizo la JK alikuwa Katibu wa wilaya kwa muda mrefu sana. Hivyo such politics ndiyo anaziwezea, hili la urais tumechichomekea wenyewe. Pamoja na Mkapa kumweka wizara ya Nje kwa miaka kumi ili improve naona jamaa bado yuko palepale hajabadilika.
 
mazingaombwe... tatizo la mimba kwa wanafunzi halianzi kutatuliwa na Polisi! Linaanzia kwenye familia na kuta za nyumba zetu. Unless tuanzishe Polisi wa Maadili ambao watawafuata watoto wetu kila wanapokwenda na kuona wanazungumza na nani? Vinginevyo, tatizo hili ni la familia kwanza kabisa na ni kuanzia kwenye familia ndiko tutaweza kulikabili.

Halafu kwanini anasema "Kumbe maabara za DNA tunazo"..

a. Alifahamishwa lini kuwa tuna maabara za DNA kwa sababu neno "Kumbe" linaashiria ndio amegundua tu kuwa tunazo.

b. Kwanini anasema "tunazo" kana kwamba tunazo nyingi? Kwa ufahamu wangu chombo hicho ni kimoja tu tena kwa mkemia mkuu. Ama tunazo maabara nyingine zinazofanya DNA testing?
 
Tatizo analotakiwa kuli valia njugu ni sababu zinazoletaeleza wanafunzi kujiingiza katika suala hilo, na ukikuta kama huko kwetu Lindi, Singida, Tabora na kwa ujumla vijijimni , ni sababu za kiuchumi na kutokuwa na Shughuli mbadala abazo zitawaepesha au kupunguza muda wa kudungana mimba.
Nitatoa kisa Kimoja
Kuna siku nilikutana na kijana moja anapelekwa polisi kisa kapiga kuku wa jirani ambaye aliingia kwao kula Mboga mboga, hivyo akawa anaomba pesa za kulipa fidia na kuwapa Polisi, Mimi nikamwambia Badala ya kutumia nguvu zake kupiga kuku wa jirani na kupelekwa polisi ambako nako wanamtoa hela ni vizuri akatumia nguvu hizo kuweka senyenge ambayo itazui kuku wa jirani kuingia kwao kwani itakuwa na two positive effects, ya maendeleo hapo kwao na kuzui huo uharibifu wa kuku.
Vivyo hivyo JK akijikita na Maendeleo huko Vijijini kutakuwa na Multiple effects ya kukuza uchumi, kulenda maendeleo na elimu pia.
 
Aisee...kweli raisi tunaye..ni nafuu ningempigia Prof Shayo tu nijue kura yangu imepotea kuliko huyu bwana...sasa watu wanahangaika na maisha..kila kitu ni juu..mambo yanakua magumu kila jua likichomoza..matumaini ya mtanzania wakawaida kabisa yanazidi kudidimia kadri anapofumbua jicho asubuhi...wakati wengine wanakula kodi ya mwananchi huyu kilainii na wanaishi kama wako visiwa vya Hawaii..anaacha kuguswa na mambo nyeti na mazito kama hayo..anavalia njuga mimba za wanafunzi sasa...inamaana hajui maana ya ku deligate au ni vipi...waziri wa elimu yuko wapi..mkuu wa mkoa..na wa wilaya je????? sheria zikowapi zinazowapa nguvu hao nilio wataja hapo juu kuhusu izo mimba kwa wanafunzi mpaka aonekane analivalia njuga hilo swala..na sio ufisadi unaotutafuna nchi ambao unahitaji nguvu nyingi na uwepo wake wa karibu na hata sauti yake tu kwa kuukalipia...lakini hafanyi ivyo..ana kalipia mimba..!!!! jamani Raisi wetu vipi?????? Ningemuona anabusara hata kabla ya Kuropoka mbele ya kadamnasi...angejiuliza kwanza izo mimba nyingi zinatokana na nini...?? tafuta chanzo...nafikiri angekijua..angejilaumu sana kwa mtu kama yeye kusimama mbele za watu na kuwaambia anavalia njuga ilo swala...........

Yaani kwa kifupi anavalia njuga Symptoms. Hopeless
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom