The Khoisan
JF-Expert Member
- Jun 5, 2007
- 14,931
- 12,229
JK avalia njuga mimba mashuleni
2008-07-21 08:39:53
Na Lulu George,PST, Muheza
Rais Jakaya Kikwete, amelitaka Jeshi la Polisi, kutumia vipimo vya kutambua vinasaba (DNA) ili kuwabana wanaowapa mimba wanafunzi.
Alisema matumizi ya DNA yataharakisha taratibu za kiupelelezi na kupata ushahidi ili kuwanasa wale wanaowapa mimba wanafunzi na baadaye kuwakana.
Aliitoa agizo hilo mwishoni mwa wiki wilayani Muheza wakati alipokuwa akipokea taarifa ya maendeleo ya wilaya hiyo kufuatia siku tisa ya kukagua shughuli za maendeleo mkoani Tanga.
Rais Kikwete alisema tatizo la mimba kwa wanafunzi linakuwa kubwa kwenye maeneo mengi hapa nchini ambapo wahusika hushindwa kuchukuliwa hatua za kisheria kwa kutokukutwa na hatia.
Alisema hatua hiyo inatokana na mfumo hafifu unaochukua muda mrefu katika ukusanyaji wa vilelezo vya ushahidi.
Kufuatia hali hiyo Rais amezitaka mahakama kutoa ushirikiano kwa serikali katika kukabiliana na tatizo hilo kwa kuharakisha usikilizaji wa kesi pamoja na utoaji hukumu kwa watakaobainika kuhusika na vitendo hivyo.
``Ndugu zangu tatizo hili ni kubwa lakini hii inatokana na watuhumiwa kutochukuliwa hatua za kisheria, kumbe maabara za DNA tunazo kwa nini hatuzitumii wahusika wanaachiwa kwa sababu tu ya kukosekana kwa ushahidi..naomba sasa kila mtumishi wa serikali kwa wakati wake awajibike ipasavyo,``alisisitiza Rais Kikwete.
Awali akiwasilisha taarifa yake kwa Rais, Mkuu wa Wilaya ya Muheza Bi. Zainab Kondo, alisema kuanzia Januari hadi sasa watoto 49 wamepata ujauzito na hivyo kukatishwa masomo.
Bi.Zainab alifafanua kwamba 36 kati yao ni wa shule za msingi ambapo 13 ni wa sekondari zilizopo wilayani humo.
Alisema kufuatia hali hiyo kesi 26 kwa kipindi cha mwaka 2007 hadi 2008 zimefikishwa mahakamani na moja tu kati ya hizo ndiyo iliyotolewa hukumu.
Wakati huo huo Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete, amewataka wanawake kuwatunza watoto wa kike wasipate mimba kwani wanaweza kuambukizwa Ukimwi.
Mama Kikwete alisema wanawake wana wajibu mkubwa wa kuwalinda watoto wao ili waweze kuepukana na vishawishi ambavyo vimechangia kwa kiasi kikubwa watoto wa kike nchini kurudi nyuma kimaendeleo kwa kutotimiza malengo yao.
``Wakina mama wenzangu tunawajibika kuwalinda watoto wetu na kuhakikisha wanatimiza malengo iwapo hawatapata elimu ya kutosha ni dhahiri kuwa wataendelea kubaki nyuma katika suala zima la kuharakisha maendeleo na dhana ya kuondokana na mfumo dume itaendelea kuwa ndoto kwa wanawake wengi hapa nchini``,alisisitiza Mama Kikwete.
Tangu Rais Kikwete aanze ziara yake mkoani hapo Julai 14 mwaka huu,Wilaya ya Muheza imetajwa kuongoza katika tatizo la mimba kwa wanafunzi kwa mujibu wa taarifa zinazoendeleo kutolewa kwenye wilaya mbalimbali mkoani hapa.
SOURCE: Nipashe