Jk sasa ashahibiana na mikhail gorbachev wa urusi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jk sasa ashahibiana na mikhail gorbachev wa urusi

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Rutashubanyuma, Oct 15, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Oct 15, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,552
  Trophy Points: 280
  JK SASA ASHAHIBIANA NA MIKHAIL GORBACHEV WA URUSI


  1. Wote wawili waliingia madarakani kwa mbwembwe za mageuzi kwa JK ilikuwa ni “Ari Mpya, Nguvu mpya na Kasi mpya” na kwa Gorbachev ilikuwa “Glasnot na Perestroika”. Wote walipwaya katika kufanikisha ahadi zao za kitapeli na wananchi waliwachukia na kupoteza imani nao.  1. Wote waligeuza taratibu za kuwapata viongozi waliochini yao lakini walighaili kuyafikisha mageuzi hayo kwenye nyadhifa zao. Huu ni ubinafsi wa kimasomaso kabisa. Yaani inakuwaje wale wa chini ndiyo uone nafasi zao zipitie kwenye tanuru la kidemokrasia lakini nafasi unayoishikilia kibosile useme la hashaaaaaaaaaa…………….Huu ni ubaguzi wa kimafia kabisa ambao kwenye kitabu cha “Animal Farm” kiliuumbua na kuuita “All animals are equal but some animals are more equal than others.  [FONT=&quot] i.[FONT=&quot] [/FONT][/FONT]JK aliruhusu kura ya maoni kuamua wabunge ndani ya Chama chake (CCM) lakini aligoma wanachama hao hao kupiga kura ya maoni katika wagombea uraisi cheo chake alichokuwa nacho!!!!!!!!!


  [FONT=&quot] ii.[FONT=&quot] [/FONT][/FONT]Gorbachev naye aliruhusu Mameya na Magavana wa majimbo ya USSR kuchaguliwa moja kwa moja na wananchi lakini alichelea kuruhusu nafasi yake kufuata nyayo hizo kwenye nafasi yake na kuiachia Politburo au kamati kuu kwa maana ya CCM kuendelea kuamua nani awe Raisi. Magavana kama Yeltsin walipata nguvu ya wananchi ambayo yeye Gorbachev hakuwa nayo na washindani wake kisiasa waliitumia katika kumwondoa madarakani.  1. Wote JK na Gorbachev walikabiliwa na upinzani mkali katika siku za mwisho za tawala zao za kiimla kutokana na matatizo ya kiuchumi ambayo yalikuwa hayavumiliki pamoja na mageuzi ya kidemokrasia ya shingo upande kutoiridhisha jamii. Viongozi wote hawa walishindwa kuzisoma alama za wakati na matokeo yake walijikuta wakifungashiwa virago vyao na wapigakura.
  MWISHO.

  Gorbachev alifutwa kazi na mabadiliko yake mwenyewe aliyoyaanzisha na JK yupo hatihati kumkabidhi Dr. Slaa katika mazingira hayohayo: Yaani uchumi umedorora, ufinyu wa demokrasia na kukosekana kwa utawala bora ni baadhi ya mambo yatakayomfuta kazi JK tarehe 31-Oktoba- 2010.

  Hali hii JK hakuitarajia na sasa ameghafilika kiakili na kupigwa tafurani la nguvu hata hawezi tena kuyazungumzia matatizo na changamoto zinazoikabili nchi hii changa duniani badala yake amejikita kwenye hoja za kufikirika za “umwagaji wa damu”

  KARIBU SANA DR. SLAA NA CHADEMA NA ALAMSIKI JK NA CCM
   
Loading...