JK: Rushwa ilikithiri sekta ya misitu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK: Rushwa ilikithiri sekta ya misitu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by SMU, Nov 28, 2008.

 1. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #1
  Nov 28, 2008
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,923
  Likes Received: 2,071
  Trophy Points: 280
  Source: Majira, Ijumaa 28 Nov 2008

  Na Mwandishi Maalumu, Mahenge

  RAIS Jakaya Kikwete amesema kiwango cha rushwa katika sekta ya misitu na maliasili kilikuwa kimevuka mipaka na amewataka viongozi nchini kuongeza juhudi za kupambana na hali hiyo kwa vile hiyo ni sekta yenye uwezo wa kuiingizia Serikali mapato makubwa.  Alisema mazao ya misitu na maliasili yana uwezekano mkubwa zaidi wa kuiingizia mapato Serikali kuliko sekta ya wanyamapori.

  “Tatizo ni kwamba kiwango cha rushwa katika sekta hii kilikuwa kikubwa mno.

  "Tatizo kubwa ni kwamba watu katika sekta hii walikuwa wamekaa miaka mingi katika vituo vile vile vya kazi kwa miaka mingi, wakaota mizizi, na wakaweka mitandao ya rushwa na kuiibia Serikali,” alisema.

  Rais Kikwete alisema hayo juzi alipokuwa akipokea taarifa ya utendaji wa Serikali katika Wilaya ya Ulanga katika siku ya tatu ya ziara yake mkoani hapa.

  Baada ya kuwa ameulizia na kupewa majibu kuhusu hali ilivyo katika Idara ya Maliasili wilayani humo, Rais alielezea jinsi alivyolazimika kuchukua hatua za kusafisha sekta hiyo baada ya kuingia madarakani.


  “Tatizo kubwa katika sekta hii ilikuwa ni uvunjaji wa sheria na ukosefu mkubwa wa maadili ... ni hali hii iliyonilazimisha kutoa agizo la Rais kuamuru kuwa wote waliokuwa wamekaa katika kituo kimoja cha kazi kwa miaka mitano au zaidi wahamishwe mara moja,” alisema Rais na kuongeza:  “Najua zoezi hili lilikuwa la gharama kiasi, lakini ilikuwa lazima kulifanya. Maofisa wengi walikuwa wanavuna misitu wanavyotaka; kama mali yao. Walikuwa wanatoa vibali vya uvunaji wa mkaa. Watu walijisahau kabisa. Tulikuwa tumefikia hatua isiyokuwa na heshima kabisa.”  Alisema tatizo ilikuwa ni rushwa kukua mno na kwa viwango cha juu na kwamba maofisa walijenga mitandao ya rushwa na kuinyima Serikali mapato.  “Kwangu ulikuwa uamuzi mgumu na wenye gharama. Lakini ilibidi tuanzie mahali pa kurekebisha hali hiyo. Angalau tuwasambaze ili waanze upya, ili angalau 'laini' zao za 'michuzi' zivurugike,” alisema.  Wakati huo huo, Rais Kikwete alisema Rais hawezi kuwa mahakama ya kutatua migogoro ya miliki za vitalu vya madini na wala suala hilo haliwezi kutatuliwa kwa walalamikaji kuzungukia maofisa wa Serikali.

  Alisema njia bora zaidi ni watu kutafuta jawabu mahakamani, badala ya kushinda wanazunguka katika ofisi za Serikali au kumwendea Rais.


  My take;

  Hivi dawa ya rushwa ni kuwahamisha watu vituo vya kazi au wizara. It never works, never worked for Mramba et al. Mheshimiwa Rais, rushwa (ufisadi) ni kosa la jinai na mahakama ndio sehemu mahsusi kwa kadhia kama hizi.
   
 2. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #2
  Nov 28, 2008
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  PCCB ujumbe umefika ..get busy!
   
 3. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #3
  Nov 28, 2008
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,923
  Likes Received: 2,071
  Trophy Points: 280
  Naanza pia kujiuliza ilikuwaje akamchagua Zakia Meghji kuwa waziri wake wa fedha (tena kulikuwa na tetesi kuwa alitaka awe mgombea mwenza badala ya Shein) iwapo sehemeu aliotoka ilikuwa inanuka rushwa kiasi hiki?
   
 4. m

  mnyama Member

  #4
  Nov 28, 2008
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hizo ni siasa tu, hakuna rushwa ya kutisha kwa maafisa misitu. Hawa ni moja ya watu ambao wanafanya kazi ngumu sana na kwa kiasi kikubwa kwa kujitolea. Na wala hakuna lolote lililofanyika zaidi ya kubadilisha viongozi wa ngazi za juu tu waziri, na katibu mkuu. Rushwa ilikuwa inatoka juu. Mtu anatoka Dar na makaratasi yote ya kuvuna misitu, wewe unategemea afisa misitu wa wilaya atafanya nini. Rushwa imekithiri kwa maafisa misitu walioko wizarani palae Dar. Na wengi wao hawajaguswa.
   
 5. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #5
  Nov 28, 2008
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Samaki huanza kuoza kuanzia kichwani....rushwa kubwa ni kwa viongozi na ndio hao wanapaswa kuanza kushughulikiwa.Maafisa misitu nao kwa viwango vyao wanahusika maana kwenye rushwa kuna kale kamsemo kuwa kila mtu anakula mezani kwake.Hawako wasafi kiihivyo.
   
Loading...