JK Rais wa kwanza mchumi aliyeboronga uchumi wetu...

fuatilia global economy ww acha chuki.uchumi wa dunia umedorora na umeyumba,we upo dunia gani?tanzania isnt isolated frm the world

Kudorora kwa uchumi wa Magharibi hakujaadhiri uchumi wa sub-Sahara countries so far. Hata RSA ambao trading partiners wao wakubwa ni EU hawajaadhirika kaasi hicho. Sasa wewe unayesema haya sijui kuadhirika kwetu kunatokana na ukosefu wa misaada tuliyozoea kupata ambayo sasa imekuwa migumu ama??

By the way, hivi ile stimulus package ya JK iliishiwa wapi vile???
 
we umeifanyia nn nchi au una lalamika km mude.

kutoam Maoni pia ni kuifanyia jambo kubwa katka nch yako....sio kla cku 2naambia na kuulizana we umeifanyia nin nch yako mpaka kuingia humu na kutoa Maon ye2 nalo ni jambo kubwa toa upuuz wako we kwan umeifanyia nin?
 
Acha urongo na vijisababu vya wakereketwa wa CCM.
JK amechaguliwa lini kuwa Rais? Hiyo global economic crisis imeanza 2005?
JK alikuta hazina ya kiasi gani kuweza kulipia huduma kwa muda gani, leo iko vipi? Deni la taifa likiwa dola ngapi na sasa limefika kiasi gani?
Nadhani JK anashikilia rekodi ya kusafiri nje kuliko walomtangulia na bado hajafika 10 yrs!

2mefatilia na 2meona kwel hata nch za wenze2 wanaporomoka kiuchumi ila wanawajbka na sabab zlizowapelekea kuwa hvyo ila je Tanzania 2mefanya nin kupambana na hal ye2 usiangalie msiba wa wenzako wanalia vp wakat wako unao
 
fuatilia global economy ww acha chuki.uchumi wa dunia umedorora na umeyumba,we upo dunia gani?tanzania isnt isolated frm the world

Kwa nini umewahi kukimbilia kwenye chuki na sio uelewa mdogo? Reading between the lines, wewe una upenzi. Mimi nilifikiri ungemwambia HAELEWI lkn badala yake uamwambia ana CHUKI. Kuna jambo lolote hapo linaashiria chuki? Am sorry to tell you this, you are PATHETIC.

Tukirudi kwenye mada: Kuporomoka kwa uchumi wa dunia si kigezo cha jumla cha kuporomoka uchumi wa Tanzania. Nikukumbushe kuwa, wakati mmoja anaporoomoka lzm huwa yupo anayepanda, na ndio maana haya tunayojijumuisha nayo na kujifanya ni common issue CHINA wao hawajaathirika nayo sanasana wametake advantage kuwa main suppliers wa kila kitu.

Tukirudi hapa kwetu, uchumi wa Dunia umetuathiri sio kwa sababu tumekosa masoko ya bidhaa zetu, bali ni kwa sababu waliokuwa wanatuwekea chochote kwenye bakuli hawafanyi hivyo. Je ndugu yangu usiye na chuki, hilo ni jambo la kujivunia?

Wakati Wachina wanainua wa kwao kwa mgongo wa kuporomoka kwa wa ulaya, Tanzania imeshindwa (kwa miaka 8) ku-take advantage ya UKAME WA KENYA (tukiitwa wajinga tunakuwa wakali). Miaka 8 ya Ukame Kenya imewafanya wawe importers wa chakula kutoka South Africa huku sisi tulio aribu tumeshindwa kupandisha pato letu la fedha za kigeni kwa kuwauzia mahindi na mchele.

Serikali hii iliyokosa wabunifu, badala ya kuzalisha chakula cha kulisha nchi, imeishia kunyang'anyana mazao na wakulima ambao kama wangeruhusiwa kuuza mazao yao Kenya wangeneemeka zaidi na kilimo kingechukua sura mpya katika Tanzania. Ukienda Kibaigwa katika soko la mahindi utaona jinsi wakulima wanavyofanywa watumwa na serikali kwa kupewa jukumu lisilo lao la kulisha nchi huku serikali yenyewe ikijikita kwenye kuuza madini na kuiba kinachopatikana.

Sasa ndugu yangu usiye na chuki hebu fikiria: kama serikali ingetumia nguvu kazi ya MAGEREZA na kutumia haya mashamba ya Serikali (ambayo wameona namna pekee ya kuyatumia ni kuwapa wageni walimie mazao ya biashara kwa jina la ubinafsishaji) kuzalisha akiba ya chakula na wakulima wakawa huru kuuza mazao yao huko Kenya ambako kwa sasa ni smuggling tu ndio means of supply, kungekuwa na mkulima maskini? Kama Serikali inannunua mahindi yangu kwa Tshs 320/kg na Mkenya anakuja kununua kwa Tshs 450 kwa kilo, nimekosa nini mimi mkulima mpk nilazimishwe kuiuzia serikali ambayo inao uwezo kulima mazao yake ila tu kwa kukosa ubunifu na mbinu za uzalishaji, inakalia nguvu kazi na mtaji na kuishia kukimbizana na wakulima wanaojitahidi kuboresha maisha yao.

Ni akili za kijibwa koko *x'yz'x*,~/* kujilinganisha na wazungu uchumi wao ukishuka na kusema tuna tatizo la pamoja, lkn unapopanda na wa kwetu ukadorora hatujilinganishi na kusema tuna sababu za pamoja ila sisi tumekosa akili. Mimi sio mchumi, lkn hilo halinizuii kuona kama tunayo nafasi ya kuinuka kupitia migongo ya jirani zetu ambao wao Bleu Band, Omo, Colgate, Panadol na bidhaa nyingine nyingi tunaziona masokoni mwetu.

Tuache ujinga wa kujifariji eti tu kwa kuwa hata fulani naye kafeli, mbona akifaulu hatufaulu naye?


Wewe ulieanzisha mada nakuunga mkono, na huyu anayekukosoa ni akili ya hawa hawa viongozi wetu wasiojua kuwa kinachoangaliwa ni kiasi gani cha rasilimali kimekuwa exploited na sio jirani anaumwa kiasi gani na kujifariji wakati hatulingani kwenye input.
 
Wakuu nadhani kwa sasa wote tumeshaona na kujua kuwa Mzee wa Kaya ni bomu kuliko tulivyofikiria. Cha muhimu sio kuendelea kulaumu tu maana hata tukilalama kila dakika, hamna kitakachobadilika. cha msingi ni kuanza kufikiria jinsi ya kujinasua na hili janga tulilo nalo. Mkuu wa kaya hamsikilizi mtu kwa sasa maana anafikiria jinsi ya kumaliza mbio hizi wakati kila mtu aliyemzunguka anataka akabidhiwe hicho kijiti cha kukaa magogoni hapo 2015 (kama atafika akiwa bado ikulu). Its better tuanze kutafuta njia mbadala za kujiletea maendeleo kuliko kuwalalamikia magamba wakati wao wanaendelea kuiba tu. Kama vipi tuanzishe TAHRIR SQUARE YETU pale soko la ferry
 
1.JK mchemfu. Zaidi ya kutafuta ukubwa sijui alitaka nini kwa kuwa rais.

2. Kusoma shuleni uchumi hakukufanyi uwe mchumi kama vile kusoma shuleni muziki kusivyokufanya kuwa mwanamuziki au kusoma shuleni ukristo kusivyokufanya kuwa mkristo. Ili kuwa mchumi inabidi ufanye mambo ya kichumi. JK hafanyi mambo ya kichumi na kwa hiyo si mchumi.

3. Vivyo hivyo unaweza kuwa mchumi bila kusoma shuleni uchumi kama unavyoweza kuwa mwanamuziki bila kusoma muziki au unavyoweza kuwa mkristo bila kusoma shuleni ukristo. Kwa kigezo hiki Mkapa ni mchumi zaidi ya Kikwete katika mambo kama kudhibiti mfumuko wa bei, ingawa hakusomea uchumi.

4.Kusema "JK rais wa kwanza mchumi aliyeboronga uchumi wetu" kunaweza kutafsirika kama kulikuwa na marais wengine wachumi waliofanya vizuri kabla, na sasa JK kafanya vibaya.Hatujawahi kuwa na, na hatuna, rais mchumi.

5.Hatujawahi kuwa na rais aliyefanya vizuri kiuchumi, period.
 
Mkuu wapo wananchi wanaelewa matatizo yalio ndani ya serikali ya Mkuu wa kaya na baadhi yao ambao wako naye serikalini,lakini unafiki ndio unatusumbua wapo tiyari kuita spade is big spoon.Na upande mwingine wako wananchi wezetu wenye akili timamu hawako tiyari kukosoa maovu ingawa wanayaona lakini hutumia kisingizio cha ni mwenzao kwa hivyo hakuna haja ya kuhoji.Na kuna wengine kutoka makundi hayo mawili wananeemeka na uwalakini wa seikali na wananguvu ya fedha hupandikiza fitina na kupotosha ukweli kwa wananchi walio wengi ambao hata hawaelewi chanzo ni nini.Hivyo tuko nchi mmoja lakini tunalichukulia tatizo hilo tofauti Tanzania imegeuka HAMAS na FATAR za PLO hatuko tiyari kukubali kwa kukubali yanayokubalika.
 
Mkuu wapo wananchi wanaelewa matatizo yalio ndani ya serikali ya Mkuu wa kaya na baadhi yao ambao wako naye serikalini,lakini unafiki ndio unatusumbua wapo tiyari kuita spade is big spoon.Na upande mwingine wako wananchi wezetu wenye akili timamu hawako tiyari kukosoa maovu ingawa wanayaona lakini hutumia kisingizio cha ni mwenzao kwa hivyo hakuna haja ya kuhoji.Na kuna wengine kutoka makundi hayo mawili wananeemeka na uwalakini wa seikali na wananguvu ya fedha hupandikiza fitina na kupotosha ukweli kwa wananchi walio wengi ambao hata hawaelewi chanzo ni nini.Hivyo tuko nchi mmoja lakini tunalichukulia tatizo hilo tofauti Tanzania imegeuka HAMAS na FATAR za PLO hatuko tiyari kukubali kwa kukubali yanayokubalika.

Kati ya hao wanaoita "spade is big spoon" basi utawasikia wengine wakisema "rais ana nia njema lakini anaangushwa na washauri wake" "rais ni mchapakazi ila washauri tu ndio wazembe" na upuuzi mwingine kama huu.

Rais makini hawezi kuwa na washauri kama hao in the first place!
 
fuatilia global economy ww acha chuki.uchumi wa dunia umedorora na umeyumba,we upo dunia gani?tanzania isnt isolated frm the world
Kwahiyo Rwanda, Mauritius, Cape verde na China hazipo duniani? Acha propaganda bwana! kwani kudorora kwa uchumi duniani kuna uhusiano gani na ccm kutumia mabilioni ya Tanesco kununua wapiga kura na kuwalipa wachakachuaji? mdororo wa uchumi ndo unaowasukuma nyie kulipana posho masaa 24 mpaka watu wamehamishia kazi hotelini ili walipwe posho? Mgao wa umeme unahusiana nini na mdororo wa uchumi duniani? Mafuta kuwa bei rahisi Zambia lakini ghali Tz inahusiana na mdororo wa uchumi?
 
Kama mtu wa digrii moja anastahili kuitwa mtaalam wa uchumi basi nchi hii imejaa wataalam.
 
Back
Top Bottom