JK, Rais aliyewekea Doa Kubwa Tanzania. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK, Rais aliyewekea Doa Kubwa Tanzania.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by STEIN, Nov 19, 2010.

 1. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #1
  Nov 19, 2010
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Wakati viongozi wengi wamekuwa wakikumbukwa na watanzania hata baada ya kumaliza muda wao watu hutamani sana waongezewe muda wa uongozi mfano baba wa Taifa mwl.Juliua Nyerere.

  Lakini kwa huyu mambo yamekuwa tofauti kama ifuatavyo:

  1. Ni rais ambaye wananchi wamekuwa wakimzomea hadharani kutokana na utendaji wake wa chini mno. mfano ni katika issue nyingi ambazo mafisadi wamekwapua kodi za wananchi amekuwa akiwatetea siku zote na kuwaita wachapakazi sasa sijui kigezo cha kuwa mchapakazi ni kuwa mwizi au.

  2. Ni rais ambaye ametea mawaziri waliokuwa wakizomewa na wananchi live hata kwenye shughuli zao za kiutendaji za kila siku maana hawana jipya.

  3.Ni rais ambaye Wabunge waliamua kumtoa waziri mkuu na swahiba wake ambaye hadi leo haamini kama watu hawamtaki na bila aibu JK anang'ang'ani eti Lowasa kastaafu, wakati alituhumiwa kwa wizi wa kodi za wananchi.

  4. Ni rais ambaye amekuwa akizomewa na wananchi hadi wananchi wanafikia hatua ya kutupia msafara wake mawe hii inaonyesha watu wamechoka na maneno na matendo yake.

  5. Ni rais ambaye kutokana na unyanyasaji anaoufanya, watu wamekuwa wanavunja majukwaa yake wakati wa kampeni zake, mfano kule kwa wamasai waliochomewa nyumba zao kis kupisha mwekezaji mwaarabu awinde vizuri wanyama hii ni aibu.

  6. Ni rais ambaye ametumia sana nguvu za dola, magazeti, redio kujiweka madarakani kama tulivyoona mwaka huu.

  7. Ni rais anayetetea wageni huku akidai waTZ ni wadokozi mfano kweye uzinduzi wa hoteli za arusha.

  8. Rais ambaye haelewani na wafanyazi mfano bif na Tukta, wazee wa EAC etc.


  Kwa hayo yote inaonyesha kwamba wananchi wamechoka na wako tayari kwa mabadiliko kwa gharama zozote zile.


  Peoples Power mapambano hadi 2015 bila kuchoka.
   
 2. Mabel

  Mabel JF-Expert Member

  #2
  Nov 19, 2010
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,018
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Nimekupata mkuu STEIN, pia ni RAHISI ambaye hajui kwa nini wananchi anaowatawala (maana hawaongozi huyu si kiongozi) ni masikini wa kutupwa.
   
 3. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #3
  Nov 19, 2010
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kumbe wanamabadiliko tupo wengi na kazi yetu ni moja tu kuhakikisha tunasambaratisha hili genge la mafisadi hadi wanaisha serekalini.

  Maana wamekuwa wengi hadi wanakera.
   
 4. A

  Aikaotana Senior Member

  #4
  Nov 19, 2010
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 199
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huwa nashangaa ukasuku wa wakereketwa kama wewe, na ninafikiri ni mtoto wa Siasa za Tanzania Kama ambavyo Nyerere alikuwa na mabaya yake na Mazuri yake,pia Mwinyi alikuwa hivyo lakini najua kwa watoto kama wewe ambao wanaangalia matokeo na sio chanzo sishangai! kwanza kabisa mimi sikubaliani na ukiritimba wa ccm ambao unahitaji mabadiliko na fikra mpya , Lakini hapa sio mahali pake , Napenda kukufahamisha kuwa raisi Kikwete atakumbukwa sana kwa kubadili Siasa hata leo na wewe ukajua siasa. Ameleta uhuru wa vyombo vya habari kwa kiasi kikubwa na ni Rais ambaye ametukanwa na wajinga kama wewe na akatupilia mbali, Hakuna asiyefahamu kuwa ingekua enzi za Mkapa Mtikila angekua ndani, Kashfa zote za ufisadi zimeanzia awamu ya tatu, Madini,Buzwagi,Rada , Ndege ya RAis, EPA na mengine mengi ni wakati huo ambapo mlikua mnaambiwa ni wavivu wa kufikiri ndio mana mnahoji vitu hivyo. Ni wakati huo ujambazi ulikuwa juu kuliko kipindi chote cha hoistoria ya nchi hii.KIKWETE AMEIBUA , ANAYAFANYIA KAZI AMEANZA KUCHUKUA HATUA NA MATOKEO YANAONEKANA.
   
 5. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #5
  Nov 19, 2010
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Aikaotana, marais wote ni binadamu na hivyo kila mmoja ana mapunguvu yake. Kitu kinachosemwa hapa ni je kuna jambo lolote ambalo JK ametenda katika kipindi chake cha uongozi linalompambanuo na rais waliomtangulia? Katika upande wa maovu ni mengi. Kwa mfano ametumia ofisi yake katika kudhoofisha vita dhidi ya ufisadi; amekuwa rais ambaye hatulii ofisini kwake; amekuwa rais ambaye amegeuza taasisi ya urais kuwa ya wanafamilia na pengine kubwa kuliko yote, katika chaguzi zote mbili ametumia rasilimali nyingi ya umma visivyo halali ili kujihakikishia ushindi. kwa upande wa mema sioni kama kuna jambo lolote aliloanzisha yeye; hili la uhuru wa vyombo vya habari, ni rais Mwinyi ndiye aliyeweka msingi imara wa jambo hilo. Hata hivyo leo hii ni vigumu kusema kama tunavyo vyombo vya habari vilivyo huru; kwani inavyoelekea kwa kutumia ushawishi na nguvu za dola vyombo vingi vya habari vimewekwa mfukoni.
   
 6. w

  werema01 Member

  #6
  Nov 19, 2010
  Joined: Feb 10, 2010
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu kumbuka hayo ni matokeo ya wakati. Wakati ni kama umri, ukifika huwezi zuia. Mfano, ukifikia uzee mvi utaota tu... Kuficha atanyoa upara, au apake dawa ila ukweli ni kwamba amezeeka na ndo maana ana mvi. Ndo kilichomtokea si kwamba anapenda, uzuri yeye kaacha mvi uonekane sababu anaelewa ndo wakati.
  Pili hayo mabaya si vyombo vilivyo chni yake vyenye majukumu hayo vilivyoibua... Ni inteligensia ya vyama vya upinzani kama Chadema na vyombo vya habari kama Mwanahalisi, Tanzania Daima vimeibua kwa faida ya Taifa na si ubinafsi kama wako wa kutetea upupu. LEGACY, ndo kitu bora duniani as long as man DIES
   
 7. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #7
  Nov 22, 2010
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Nitajie Kitu ambacho JK kama Rais atasimamia kama si kuishia kulipiza kisasi, na kufanya starehe ikulu, kubeba wageni kutoka nje kubariki wachukue rasilimali zetu bure na akiulizwa chanzo cha umasiki wa tanzania ni nini anabaki kudanganya hajui wakati jibu liko wazi.

  Peoples power
   
 8. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #8
  Nov 22, 2010
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Nimekupata mkuu maana tukisema tujipongeze kwa aliyoyafanya hata nchi jirani kama kenya, Rwanda, Burundi watatushangaa tunapongezana kwa Dhahabu, Tanzanite, Wanyama wetu na Magogo kuchukuliwa bura maana watu wengine wanataka tusiyaseme haya tubaki tuna pongezana kwa JK kufanya uzembe kama rais.

  Dawa ni kutomtambua maana hata wenzetu duniani watajua anajilazimisha ila waTZ hawamtaki huyu jamaa kwa sera zake mbovu.
   
Loading...