JK: Pesa zetu za kodi kulipia ununuzi wa shule za umoja wa wazazi-CCM? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK: Pesa zetu za kodi kulipia ununuzi wa shule za umoja wa wazazi-CCM?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Phillemon Mikael, Jun 7, 2009.

 1. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #1
  Jun 7, 2009
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,847
  Likes Received: 2,420
  Trophy Points: 280
  KODI ZETU KUTUMIKA KUILIPA CCM KWA AJILI YA SHULE ZA WAZAZI[TULIZOZICHANGIA UJENZI] ZINAZORUDISHWA SERIKALINI BAADA YA JUMUIA KUZISHINDWA!!!

  Katika inayoonekana kama mbinu ya kupata pesa za kampeni mwaka 2010 ..rais ametoa tamko kuwa serikali itawalipa umoja wa wazazi fidia za kutaifisha mashule yao yaliyotapakaa nchi nzima ,watalipwa kwa bei ya soko....hizo ni zile shule ambazo mimi na wewe tulichangia kujenga kwa nguvu zetu au michango enzi zile za ujamaa,na ccm hawakutoa hata senti kuzijenga kama ilivyo kwa mali zake zote...sasa kodi yetu in billions itazinunua hizi shule toka CCM......huu ni wizi wa mchana ..tuunganeni kuupinga...

  angalia sehemu ya hotuba ya rais.....!

  “Ndugu wajumbe;
  Imezungumzwa hapa kwamba tusifanye makosa kama ya siku za nyuma ya kukabidhi mali za Chama Serikalini. Ndugu zangu hakuna aliyetoa uamuzi wa kukabidhi bure mali za Chama na Jumuiya kwa Serikali. Mali hizo zitakabidhiwa kwa kulipiwa thamani halisi ya majengo na vifaa. Hivyo Jumuiya haitakula hasara. Italipwa malipo stahiki na itazitumia fedha hizo kwa kufanyia shughuli nyingine ikiwa ni pamoja na kuwa na miradi ya kiuchumi.”


  Jakaya kikwete  HII si halali hata kidogo ..kwani miradi mingi ya chama tumeijengwa kwa kukwatwa mishahara,nahisi huu ni mpango wa jk kusaka pesa za kampeni!!

  Vijana wengi wa leo hawajuwi kuwa majengo yote ya ccm nchini tumeyajenga kwa kukwatwa mishahara ,viwanja vyote vya michezo kama ccm kirumba ,sheikh amri abeid,majimaji etc…ukumbi wa chimwaga……etc

  Ni muhimu mali zote za chama zirudishwe kwenye halmashauri!!

  Na kikwete asitumie kodi yetu kulipia shule za wazazi..zilizojengwa kwa nguvu za wananchi!!!
   
 2. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #2
  Jun 7, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,542
  Likes Received: 18,172
  Trophy Points: 280
  Moja ya matatizo makubwa sana katika uendeshaji wa siasa za vyama vingi nchini, ni kuwepo kwa uwanja wa mapambano ambao sio tambarare, 'level playing field'. CCM inaingia uwanja wa mapambano ya kunyang'anyana kisu huku kimeshika mpini wengine washike kwenye makali.

  Hii ni kwasababu, mali zote za CCM, ni kodi za wananchi, hivyo mfumo ulipoanza, ilitakiwa CCM irudisha mali zote na kuanza moja ndipo tungepata ushindani ulio sawa.

  cCM ambayo ina nguvu kubwa ya kiuchumi kutokana na kodi zetu, inatumia na itaendelea kutumia nguvu hizo kushikilia mpini wa siasa za Tanzania kwa miongo kadhaa ijayo hali itakayopelekea lazima ishinde maeneo yote yenye umasikini na njaa kali.

  Huo mkakati wa kuzinunua shule za wazazi ni mpanga mmoja kati ya mingi kutunisha mfuko wa hazina kuu ya CCM kuelekea 2010 kwa ushindi wa kishindo
   
 3. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #3
  Jun 7, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,689
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  PM,

  Mjadala wa namna hii nadhani ulifanyika mwaka 92, mali zote zilifanyiwa evaluation, CCM ikanyang'anywa zingine na zingine zikabaki chini ya Serikali.

  Nakumbuka kama sikosei CCM ilinyangawa ukumbi wa Chimwaga nk.

  Hiyo statement yako ki-siasa iko sahihi lakini kisheria sidhani kama iko sahihi.

  Mungu Ibariki Tanzania
   
 4. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #4
  Jun 8, 2009
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,847
  Likes Received: 2,420
  Trophy Points: 280
  nakubaliana na wewe kasheshe....lakini sijui kama tume ya nyalali ilituuliza juu ya mgawanyo wa mali tulizoichumia ccm...simply hatukushirikishwa pale ccm walipoamulia kujitwalia mali tulipoingia chaama kimoja...

  sasa jk anabariki jumuia wazazi wafidiwe kwa investment gani waliofanya..kwanza tumejenga shule tukawapa waendeshe ...wamekuwa wakikusanya ada wanakula ..yet tuzinunue tena shule kwa bei ya soko??..kama sio sanya sanya ya wazi ya mwaka 2010 ni nini???

  ccm inahodhi sana mali zetu..angalieni mitaani viwanja vyote vya wazi wamejimilikisha ....wanajenga maduka...ipo siku wananchi watavamia kwa nguvu mali za ccm..wachukue jasho lao.....

  ccm waanaishi kwa utaratibu wa mbuzi...viongozi wa mashina wanakula kwenye viwanja vya wazi...wa mikoa kwenye majengo na viwanja vya michezo[kama kile cha iringa au mbeya ..wanakula wasipopanda vimejaa mbigiri,ukarabati hakuna]...wa taifa wanakula kwenye ufisadi.....

  hizi mali zote zikabidhiwe kwenye halmashauri zetu waziendeshe...tutakuwa na sauti..
   
 5. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #5
  Jun 8, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Hizi shule nyingi ziko hoi; nilifikiri serikali ingezichukua bila gharama yoyote na kuondoa mzigo wa uendeshaji toka jumuia ya Wazazi. Sasa hii ya kulipa gaharama ya majengo na mambo mengine naona kama ni aina fulani ya wizi unaandaliwa.

  Mali ni ya CCM, wao wenyewe watatoa thamani ya mali zao, wao wenyewe watanunua kwa niaba ya serikali na sisi wananchi, kweli hapo kuna usalama?

  Jumuia imeshindwa kuziendesha shule, ingefaa serikali itaifishe bila kulipa gharama zozote.
   
 6. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #6
  Jun 8, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135

  Mkuu wizi mtupu! yaani hii ni ''super EPA''
   
 7. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #7
  Jun 8, 2009
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Mimi kwa kweli mnanishanganza
  Mali za CHADEMA ,CUF n.k sio kodi za wananchi? Naomba kuelimishwa.
   
 8. N

  Nsesi JF-Expert Member

  #8
  Jun 8, 2009
  Joined: Nov 20, 2008
  Messages: 374
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni wazi kuwa huo ni mkakati wa kuchota fedha za kampeni zao kwa ajili ya uchaguzi wa 2010 baada ya ile mianya ya kule BOT, tanesco kupitia mikataba ya wizi kama richmonduli, iptl etc kubainika.

  Inakuwaje leo hao wazazi wa ccm waridhie kuchukuliwa kwa shule zao wakati huko nyuma walipinga hatua hiyo ya shule zao kuchukuliwa na serikali, tena kwa maneno makali yaliyomtisha Mramba akiwa RC wa Mbeya.

  Mramba aliwahi kupendekeza baada ya kubaini ubababishaji mkubwa kwenye shule hizo ambazo mkoani humo ndizo zilikuwa zikiongoza kwa kusajiri watoto wengi, lakini walimjia juu na kumtisha. Sidhani kama leo hii viongozi wa serikali wa wakati huo waliothubutu kupendekeza zikabidhiwe serikalini wanaweza kufunua vinywa vyao leo hii kwani bado wanayakumbuka maneno makali ya viongozi wa jumuiya hiyo.

  Sasa leo iweje hao hao wanaridhia shule zao kuchukuliwa na serikali, hapana , huu ni mkakati ulioandaliwa na CCM kuchota fedha zetu za kodi.

  Hii ni nchi ya ajabu sana, badala ya kuwekeza kwenye kilimo ili tuzalishe chakula cha kutosha na kuondokana na aibu ya njaa tunawaza fedha za kutumbua kwenye kampeni, badala ya kuboresha shule za sekondari za kata ambazo ziko hoi zikiwa hazina maabara, nyumba za walimu na vyumba bora vya madarasa, Bwana Mkubwa awaza jinsi ya kuchota kodi zetu kwa ajili ya watu wake kutumbua wakati wa kampeni zao mwakani, vipaumbele vya bwana mkubwa ni matanuzi na si uzalishaji, wizi mtupu.
   
 9. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #9
  Jun 8, 2009
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,847
  Likes Received: 2,420
  Trophy Points: 280
  hivi are you serious mzee?????

  ni lini CUF ,chadema AU tlp....waliwachangisha wananchi vijijini tena kwa kuwakata mazao au mishahara ili wajenge majengo yaoo.....

  ni chama gani zaidi ya ccm kinamiliki viwanja vya michezo au vya maeneo ya wazi mijini....

  yaani kweli ina maana wewe huoni kuwa huu ni wizi...au unautetea ....[tuseme ,....miafrika ndio tulivyo auuu??]...sikuelewi kabisa...eti unatetea ccm walipwe pesa za kutuuzia shule ambazo ..zilijengwa kwa nguuvu za wananchi ,,,,na miaka yote wamekuwa wakikusanya ada!! du ...
   
 10. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #10
  Jun 8, 2009
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Rudi nyuma wakati wa uanzilishi wa vyama vingi vilifanyiwa nini na serikali?
  Tena kama sikosei hata fedha ya kapeni walikuwa wanapewa.na hizo posho wanazopata sio jasho la wananchi?

  Ama wananchi wananyonywa tu pale wanapochangia directly?? kwa mfano kujenga shule kwa nguvu, lakini wakinipiga kondi la nguvu na baadhi lake wakapewa CHADEMA kama posho na wakajenga pale makao mkuu yao na kule kwingine hilo si jasho la mwananchi.

  Sielewi labda unieleweshe zaidi.
   
 11. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #11
  Jun 8, 2009
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,847
  Likes Received: 2,420
  Trophy Points: 280

  bado sikuelewi ...kwa hiyo unaongelea ruzuku.....kwa akili yako unafikiri ruzuku ipo kumnufaisha nani ....?????..... hiyo inahalalisha nini kununua shule za jumuia kwa bei ya soko .... shule zilizojengwa kwa nguvu zetu mimi na wewe....shule za wananchi ....yaani tunazinunua mara ya pili......!!.....

  jamani simuelewi mkamap....anamaanisha nini....nipo gizani...unasema baada ya kuingia vyama vingi vyama vilipewa pesa au una maana ..mwaka 1995 ambapo wagombea ubunge ndio walipewa rusuku ya milioni 1 kila mgombea na milioni 5 kila mgombea rais....??

  hapa hujaelewa naongelea mali za chama zilizochumwa kabla ya mwaka 1992..wakati tukiwa chama kimoja ??
   
 12. F

  Froida JF-Expert Member

  #12
  Jun 8, 2009
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Hivi naomba munikumbushe walipotaifisha shule za wakatoliki, na madhehebu mengine ya kikristo walilipa fidia au ndio serikali itaanza sasa
   
 13. H

  Heri JF-Expert Member

  #13
  Jun 8, 2009
  Joined: Aug 28, 2007
  Messages: 242
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Serikali kuchukua shule za wazazi ni kosa.
  Kwanza kabisa , shule nyingi ambazo zianitwa za wazazi hazikuaanzaishwa na jumuiya ya Wazazi. Wakati wa Nyerere shule binafsi hazikuruhusiwa kuaanzishwa (pamoja na hospitali). Shule ambazo ziliruhusiwa zilikuwa za jumuiya. Shule nyingi zika anzishwa kupitia mgongo huu. Hizi shule zilikuwa zikilipa royalties kwa Jumuiya za wazazi. Shule ambazo ziliaanzishwa na jumuiya nyingi zilikufa na kuacha madeni makubwa.
  Kimsingi hizi shule zinajitegemea kwa kila kitu. Wengi wao wameweza ku form partnership na na shule nje ya nchi. Waalimu wao wanawalipa vizuri kutegemeana na uwezo wao.
  Kwa habari nilizonazo , waalimu kwenye hizi shule , wameanza kutafuta ajira kwenye private schools.
  shule za serkali zinadaiwa either mishahara , chakula na general provisions. Kuchukua hizi shule za wazazi ni kujiongezea mzigo.
   
 14. n

  nmiku Member

  #14
  Jun 8, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kwa uelewa wangu hizo shule zimejengwa kwa pesa kutoka kwa wananchi irrespective of party affiliation. That being the case, it is daylight robbery on the part off CCM and as you guys have already pointed out, it is totally unacceptable in strongest terms. If the so called jumuia ya wazazi has failed to operate them, the government is supposed to take over the schools without paying anybody a single sent and operate them for the betterment of the lower bracket majority. Vinginevyo kama serikali (CCM) inaona vipi, iuze hizo shule to the highest bidder na pesa zipelekwe hazina kwa ajili ya maendeleo ya wananchi. Kwa upande mwingine serikali (CCM) iweke wazi kwa wananchi uchunguzi kamilifu uonyeshao hizo shule zimeshindikana kuendeshwa na tume huru ihusishwe kuamua kifanyike nini.
   
 15. S

  Shingo Senior Member

  #15
  Jun 8, 2009
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 127
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Hizi shule zilijengwa kwa kujitolea na michango ya wananchi wakati mwingine bila kupenda. Watu walikuwa wakikatwa pesa kwenye kila kilo ya mazao wanayouza wengine wakikatwa kwenye mishahara.

  Uamzi wa kuchangia ilikuwa si hiari ya mchangaji kwani automatically watu wote walichukuliwa kuwa members wa jumuiya ya wazazi, kama vijana wote walivyochukuliwa members wa jumuiya ya vijana na wanawake wote members wa wa jumuiya ya wanawake.

  Baada ya kuingia vyama vingi vya siasa CCM ikafanya hila na kuzihamishia shule hizi kwenye jumuiya yao ya wazazi kinyemela. Hii jumuiya imekuwa ni mzigo mkubwa kwa shule hizi kwani muda mrefu jumuiya imezigeuza shule mradi wake ikizila bila kufuta mdomo. Kuonyesha jinsi ambavyo jumuiya hiyo ilivyofirisika kioganaizesheni, shule hizi imeshindwa kuziendesha. Nyingi ziko kwenye hali mbaya ya kunuka na inatakiwa zirudishwe kwa wananchi (kama shule zao za kata).

  Mpango wowote wa CCM kuziuza serikalini utakuwa ni wizi wa mchana kweupe. CCM wajichotee tu hizo hela hazina, lakini huu usanii wa kuiuzia shule serikali, ni usanii wa kijinga mno. Kuna shule nyingine mpaka sasa zilisharudishwa serikalini kama shule za kata kutokana na hiki kinachoitwa jumuiya ya wazazi kushindwa kuziendesha kabisa.

  Sasa wanataka wachote fedha kwa kisingizio cha kuuza shule? hii ni laana...
   
 16. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #16
  Jun 8, 2009
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,847
  Likes Received: 2,420
  Trophy Points: 280

  la kusitisha ni kuwa kauli ya kuwa ccm wazazi wasijali watalipwa kwa bei ya soko ...inatolewa na kiongozi mkuu kuliko wote yaani rais...kwa hiyo kwa kifupi tayari ni agizo linalosubiri utekelezaji na kuingizwa kwenye bajeti ya mwaka huu ili ccm- wazazi wapewe hayo mabilioni yenye jasho na damu zetu!!

  ni aibu kwa rais kutoa kauli ya kifisadi kama ile.........ahhkht!!!
   
 17. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #17
  Jun 8, 2009
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Tatizo ni tatizo la kifilosofia hapa na miono tunatofautiana kuona.
  Mimi kwa miono yangu ni kwamba wakati tunajenga hizo shule,viwanja vya kilumba nk wote tulikuwa wanachama wa CCM.

  Kujitoa kwetu CCM sio na mali za wakati huo tulizozitengeneza tukiwa huko eiza kwa kupenda ama kwa utashi tuziwanyang'anye waliondelea na u CCM.
  Mimi nafikiri mambo yanafuata protocols na si nadhalia za mtaani,Mfano ukiwa na mke na ukampa mimba mkeo na tukaenda na kukubaliana kuandikisha mahakamani mtoto atayezaliwa atakuwa wa mkamap kutokana na sababu hiz na zile na mtoto kweli akazaliwa wewe utakosa haki kutokana na makubaliano yetu japo kihalisia ni mwanao.Hizo ndizo kanuni.

  Swali kwako. Naomba unieleze mradi walio nao vyama vya siasa vya upinzani uliowapatia kujiendesha na kujenga majengo yao.?

  Na kama hawana je unakubali ni fedha inayotoka serikalini yani kwa kodi yetu ndio inawaendeleza? na kama ndiyo je siku wakiamuwa kuza majengo yao tufanye je?
   
 18. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #18
  Jun 8, 2009
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,847
  Likes Received: 2,420
  Trophy Points: 280


  kweli tunatofautiana kimtazamo..nadhani hapo tatizo ni tutoke vipi..mwaka 2010...!! fundings za uchaguzi ..anayeshabikia uamuzi wa jk..labda na yeye ataambulia chochote ccm wakilipwa mabilioni ya kuuza shule zake...

  ndio tunatofautiana sana....nakua mfano wa chama kingine cha ukombozi KANU ...walikuwa wakimiliki miradi mingi ikiwemo ukumbi wa mikutano wa kimataifa KICC ....wao wamerudisha ....wamebakiwa na ofisi zao mikoani ..wilayani etc...

  matunda ya kuwa chama cha ukombozi ni pamoja na kuwaachia ccm wabaki na maofisi yao yote...lakini tunaomba PUBLIC utilities warudishe kwenye halmashauri husika....nadhani mnakumbuka wakazi wa IRINGA hadi leo wananyimwa haki ya kuona mechi kubwa baada ya CCM mkoa Kugomea halmashauri ya manispaa kuutwaa uwanja wa soka wa samora kwa ajili ya ukarabati mkubwa..sio haki...!!...isingekuwa tatizo kama ccm wangekuwa watunzaji.....lakini viwanja vinakufa,mashule yanakufa,maeneo ya kuegesha magari yanahitajika kwa ajili ya watoto wetu ...yalikuwa maeneo ya wazi....IPO SIKU!!!...VITARUDI TU!!...hata ndani ya ccm kuna viongozi ambao wakitwaa dola wapo tayari kurudisha public utilities na ndio tutawaunga mkono!!
   
 19. S

  Shingo Senior Member

  #19
  Jun 8, 2009
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 127
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  MkamaP,

  Unafanya kosa la kuamini kuwa wote tuliokuwa tunaitwa wana CCM enzi hizo tumehamia vyama vya upinzani. Nadhani the great majority we are not part of any political movement kwa maana ya vyama vya siasa. This means wote tunapoteza haki ya ownership ya mali hizo tu kwa kuwa kuna vyama vipya vimeanzishwa na wengine tumeshindwa kuji-identify kama CCM?

  Msema kweli ni mpenzi wa mungu. Hizo mali za wananchi ambazo CCM ilijibinafsishia zitakuja wageuka siku moja. Jambo moja limeshaonekana wazi. CCM kufirisika kioganaizesheni maana yake ni kuwa mali hizo nyingi zimebaki kama magofu na suluhu ya CCM ni kuzigeuza pesa kwa kuziuza.

  Shule zinauzwa serikalini, kama si matakwa ya CCM kuchota hela kuna logic yoyote ya CCM kuziuza? Kwa nini zisirudishwe kwa halmashauri za wilaya husika? Hivi viwanja vya michezo na mali zingine nazo hatimaye watauza tuu. Sasa CCM watuambie hizo hela wanazochota ndo zitawasaidia? Ukifirisika umefirisika tuu. Baada ya kuuza na kutapanya hizo hela kwenye uchaguzi CCM watafanya nini?

  Hizi mali zingine wanazouza zitawalaani....... Afadhali muuze vingine hizo shule za wananchi muwarudishieni shule zao. Msizitumie kama kisingizio cha kuchota fedha. Kuna siku zitawageuka hizo.
   
 20. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #20
  Jun 9, 2009
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Mkuu
  Tatizo la umasikini na kushindwa kufuata sheria na kanuni ndilo tatizo kubwa la ss wtz.
  Kwa mlengo wangu .Ni kosa kubwa tunalofanya kila kufeli kwetu lazima sababu yake iwe imesababishwa na jirani .Hili ni kosa kubwa na ndilo linatutafuna sie watanzania ni kosa la kimilongo hadi karne na karne.

  Tunashindwa kuona kabisa tatizo la Tanzania linasababishwa na sisi watanzania wala halina uhusiano wowote na CHAMA wala itikadi.Kama ni magofu kwanini uone tu magofu ya ccm ambayo angalau bado bado yapo na ushindwe kuona magofu ya vyama vya ushirika na viwanda vilivyooza na vingine kupotea kabisa.?

  Mie nafikiri tunajaribu sana kutafuta njia za mikato kwa kujaribu kujidaganya.Tatizo la TZ ni tatizo la kitanzania zaidi ya kichama
   
Loading...