JK peleka wabunge course ya English wajue kusalimia!!!!

First Born

JF-Expert Member
Jul 11, 2011
5,310
1,473
Ni baadhi ya matatizo ya aibu kabisa wabunge tumezoea kuwaona nayo!

Mbunge mzima, mwakilishi wa wananchi, ulienda kutoa na kutetea hoja mjengoni unalala waziwazi!! Hapa wahusika mnawajua,

lingine la lugha, kama hujui English ya nini unajifanya unaitumia? Nakupa mifano miwili ya wabunge, mmoja wa jimbo langu kabisa...

Mh Jitu V Soni (CCM), yeye anaropoka na kujidai kuwa mbunge mwenye cheo cha kuwawakilisha wabunge kule SuA, Lakini anadai wanafunzi wa pale hawana tofauti na wa sekondari za kawaida ambazo hazina maabara. Eti wao wanajifunza kwa vitendo zaidi badala ya practicle!!! Mhh


Mbunge wa Serengeti, Mh Kebwe, (CCM) anadai Tanzania kuna maeneo makubwa ya vijana kujiajiri, hivyo ni aibu kulalamika kwamba hakuna Unemployment(akiongelea kwa jinsi ya positive) mhh!! Braaaaa!

swali.
Wanalazimishwa kutia vionjo vya Kiingereza?
 
Bunge kwa Kiingereza ? Hata hao wanaoitwa ma Dr ni watupu hakika ukiwasikiliza wanaongea kiingereza dakika tano utasikia you know you know kibao .Then eti ndiyo wana tunga sheria kwa kiingereza mh
 
Wanasema iliugombee ubunge matakwa ni kujuwa kusoma na kuongea kiswahili sijui haya matakwa yapo wapi ila imewai kusikia Mgombea Ubunge kwa ticket ya CCM anajitetea hivyo.
 
Jamani ukikaa muda mrefu bila kutema ''yai'' siku ukitaka kutema ni ''vapour'' tu.Mazingira ya kazi pia yanaweza kufanya yai kugeuka Viza.Nilikaa kwa muda mrefu kama miaka sita kwenye halmashauri maake kiswahili ndio ''oral'' ndio ''written'' baadae nikapata kazi UN mzee vocabular nyingi zilipotea ikabakia zeee.....zeee lakini siku hizi naona kama idadi ya zee na you know zimepungua.

Huko Manispaa na Halmashauri kuna kibarua kwani neither practise nor perfect.
 
Hii ndo nchi yetu yenye maajabu,tunaandika mikataba na mijadala kwa kiingereza then ikifika bungeni inajadiliwa kiswahili huku wabunge wengi hawajui kiingereza.je wanachojadili wanakielewa kweli?
 
Lugha rasmi za Bunge ni Kiingereza na Kiswahili. Sasa kwa nini mbunge ajilazimishe kuongea Kiingereza kama hawezi??? Wao wenyewe ndiyo wana jiaibisha. Ila hii pia inaonyesha kiwango chetu cha elimu nchini maana baadhi ya hao wabunge wanao ua lugha ya malkia ni "university graduates".
 
hahahahahaha!! Hapo patakuwa patamu, sipati picha Sugu atakavyochana kihiphop

Sugu atapiga kiingereza cha Amerika si ameishi kule' hakuna atakayemwelewa! HATA HVYO MBONA KUNA KANUNI INAYOKATAZA KUCHANGANYA LUGHA? Kama ni kiingereza ni kiingereza tu! Na kama ni kiswahili ni kiswahili tu! Spika alaumiwe kwa kutokusimamia kanuni'
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom