JK NYERERE: Ukishakula nyama ya mtu hutaacha bali utaendelea kuila tu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK NYERERE: Ukishakula nyama ya mtu hutaacha bali utaendelea kuila tu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by TEMILUGODA, Sep 3, 2012.

 1. T

  TEMILUGODA JF-Expert Member

  #1
  Sep 3, 2012
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 1,367
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Leo nimekumbuka maneno yaliyosemwa na mwanafalsafa gwiji wa Tanzania,hayati mwalimu JK NYERERE miaka kumi na sita iliyopita pale kwenye ukumbi wa simba grill,alisema'dhambi ya ubaguzi ukisha itenda hutaacha bali utaendelea kuitenda,ni sawa na kosa la kula nyama ya mtu,ukishakula nyama ya mtu mara moja,hutaacha bali utaendelea kuila tu'.

  Ndugu zangu nimeandika maneno haya baada ya kugundua dhambi ya police ya kubagua raia[hawa ni CHADEMA,hawa ni ccm na mwisho hawa ni cuf na wale ni adc nk]Kwa mipango niite ya kijinga inayoratibiwa na watu wasiomjua Mungu,eti CDM mwaka huu hautakwisha itakuwa imesambaratika,tunashuhudia kasi ya ajabu ya polisi wa nchi ya roho ya mauaji wakidhani ni [mechanism]ya kutisha watu[threatenin]kama walivyofanya watawala wa kikoloni kwa wapigania ukombozi wa nchi yetu.Kwa kuwa hadi sasa polisi wameshaua maelfu ya raia wetu, ninashauri wanasheria wote wanaopenda roho[uhai wa watanzania kwa mapenzi ya mola],waende kwa kasi ya ajabu kwenye mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai (The Hague) na kulishtaki jeshi uchwara la Tanzania kwa kasi hii ya mauaji.

  Chadema kikiendelea kupambana tu na dola ambayo imeshakula nyama za watu[mchawi]wengi, hakitakuwa na kasi ya kuiangusha bali upole kwa makosa ya gvt organs yanayoashiria chadema wanauwa nyani[CCM]kwa kuangalia usoni.Mimi binafsi imeniuma sana kwa mauaji ambayo yanaendea hapa TANZANIA kwa kupitia polisi,mathalani polisi waliua mahali fulani wakajitetea eti aliyeuawa alipigwa na kitu kizito,aaaah siku chache baadae wakaua tarime,siku chache tena wameua IRINGA KWETU.

  NAWASHAURI VIONGOZI WA DINI WAACHE KUZUIA RAIA WASISHIRIKI SENSA,BALI WAZUI MAUAJI YANAYOFANYWA NA DOLA.NAWASHAURI WASANII WAACHE KUTUNGA NYIMBO NA MAIGIZO YA KUSIFIA DOLA HII kwa kuwa watashiriki kula nyama za watu.MWISHO MAWAZIRI WASIRA NA NCHIMBI NAWASHAURI ONDOENI MPANGO HUU WA VITISHO KWA RAIA KWANI THE HAGUE ITAKUFA NA NINYI KABLA 2013 HAUJAISHA.MUNGU NINAKUOMBA UZUIE ROHO ZA UKATILI NA MAWAZO MABAYA KWA KILA MWENYE KUSHIKA MADARAKA KM.POLISI,MAWAZIRI,TISS NK.SISI SOTE NI NDUGU.
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Sep 3, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,416
  Trophy Points: 280
  Yeye Nyerere alijuaje yote hayo?

  Alishawahi kuila?
   
 3. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #3
  Sep 3, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Baada ya kustaafu Mwalimu Nyerere CCM walianza kula nyama ya binadamu naona bado hawaachi
   
 4. T

  TEMILUGODA JF-Expert Member

  #4
  Sep 3, 2012
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 1,367
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Remember philosophers are great thinkers,wewe hujasoma thread hii bali umesoma tittle tu,kama watanzania tutakuwa na mzaha kwenye mauaji haya,walahi radhimu tutahukumiwa na Mola na itafika kuonyeshana vidole hata kwenye nyumba za ibada.ROHO MBAYA YA KUFIKIRI UJUMBE WA MWL.kana kwamba eti aliwahi kuila nyama ya mtu ikushukie wewe mwanaharamu.
   
 5. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #5
  Sep 3, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,416
  Trophy Points: 280
  Alisema hivyo au hakusema?
   
 6. RGforever

  RGforever JF-Expert Member

  #6
  Sep 3, 2012
  Joined: Apr 3, 2011
  Messages: 6,187
  Likes Received: 1,908
  Trophy Points: 280
  Ni Philosopher hata Mumchukie kivipi kwenye VITABU vya Ulimwengu Yupo na anasomwa Dunia nzima........ Tatizo lenu ndo hilo tu hamtaki kuelewa maana mmeshawekewa chuki na Nyama mmeshaila tayari
   
 7. T

  TEMILUGODA JF-Expert Member

  #7
  Sep 3, 2012
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 1,367
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Asante kwa darasa hili maana kuna wajinga wengi.
   
 8. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #8
  Sep 3, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  Ni greater think ni sawasawa na einsten alivyosema ngamia anaweza penya kwenye tundu la sindano akikimbia na speed ya light,mwalimu alitumia falsafa hyo kutokana na simba kwa sisi tuliokulia porini simba akila nyama ya mtu basi ni lazima huyo simba auawe maana akiachwa ataendeleea kula mpaka basi.
   
 9. U

  Ubungo JF-Expert Member

  #9
  Sep 3, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mwalimu Nyerere was a great thinker.
   
 10. mangusha kitoi

  mangusha kitoi Member

  #10
  Sep 3, 2012
  Joined: Aug 25, 2012
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watanzania wenzangu, tukio la Mafinga huko Iringa halijatokea kwa bahati mbaya, kama kuna mtu amefanikiwa kuona picha za polisi wakitoa kipigo kwa Mwangosi utagundua lile kundi la polisi lenye silaha za kivita, mafimbo makubwa na mabuti yao walikuwa ba jitihada za ziada katika kuhakikisha ndg yetu Mwangosi anatoweka duniani mapema iwezekanavyo. Jamani mtakuwa mashahidi muda si mrefu mkuu wa kile kikosi atapandishwa NGAZI na kuwa boss fulani hivi. Atapongezwa kwa kufikia malengo, Time will tell!
   
 11. t

  thatha JF-Expert Member

  #11
  Sep 3, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Dhambi hiyo itawatafuna wote POLISI na CHADEMA, hakuna wa kujitetea hapo. Kuna haja ya Polisi kuwaacha CDM wakafanya mikutano yao pamoja na kwamba wanaifanya kwa vurugu kubwa sana tofauti na vyama vingine. Vivyo hivyo kwa kuwa CHADEMA sasa mikutano yao inaonekana kuendelea kuua, iko haja ya wao kutafuta njia mbadala ya kujionesha kwa wananchi badala ya kuendelea kutoa kauli ambazo zinaendelea kuwachochea wananchi. SLAA amesikika akisema kuwa "Hata wakiua Viongozi wote, madailiko hayazuiliki" Mbona mpaka sasa hakuna kiongozi wa CDM aliyeuawawa na badala yake wanateketea watu wasiokuwa na hatia.
   
 12. t

  thatha JF-Expert Member

  #12
  Sep 3, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Nakumbuka sana kuna siku MNYIKA alihojiwa kwa nni bendera yao ina rangi nyekundu, na jibu lake lilikuwa: "WATANZANIA MSIDANGANYWE KUWA HATUKUMWAGA DAMU WAKATI WA KUDAI UHURU" Sasa ndiyo haya tunayoyaona.
   
 13. t

  thatha JF-Expert Member

  #13
  Sep 3, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Tushike lipi, POLISI waliokusanyika pale ndiyo waliomuua Mwandishi au bomu lililorushwa ndilo lilimuua?
   
 14. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #14
  Sep 3, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,780
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  jitahidi unapotoa maoni yako kupunguza chuki na hasira yako kwa CDM.
   
 15. mzamifu

  mzamifu JF-Expert Member

  #15
  Sep 3, 2012
  Joined: Mar 10, 2010
  Messages: 3,497
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  polisi ni sehemu ndogo na muhimu ya dola. inafanya kazi moja kati ya nyingi za dola nayo hasa ni kulinda usalama wa raia na mali zao. Kuna kosa la kiufundi ambalo mara nyingi laweza kufanywa na polisi nalo ni lile la kujilinda na kulinda dola na kusahau wajibu wa msingi. ni lazima basi polisi ijitahidi kuepuka kuumiza raia, ni lazima raia waone waziwazi kuwa wako salama chini ya polisi pasipo shaka yoyote. pia polisi ijue kuwa sasa ni CCM na kesho inaweza kuwa chadema lakini wajibu wao utabaki uleule. KULIKO KUZUIA MIKUTANO KWA MABOMU NA SILAHA KWA SABABU WATU WAMESHINDWA KUTII AMRI NI BORA KUICHA MIKUTANO IENDELEE KISHA BAADA YA MIKUTANO HIYO VIONGOZI WAHUSIKA WAISHTAKIWE KWA KUKIUKA AMRI HALALI HAPO KUNA UWEZEKANO WA KUEPUKA GHASIA. polisi fanyeni kazi na mahakama
   
 16. M

  Mtz.mzalendo JF-Expert Member

  #16
  Sep 3, 2012
  Joined: Jul 22, 2012
  Messages: 357
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nyerere mwenyewe alikula nyama za watu ndio alizungumza haya
   
Loading...