JK Nyerere Resignation letter from St. Francis College Pugu in 22 March 1955

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,485
b2ff76b6-2d01-43a4-940f-425d5f17616d.jpg

We have to learn this Philosopher who make critical thinking to make choice between White colour job at St. Francis and Politics.

After he made a critical thinking he come up with a conclusion that, he has to resign his colour job in order to have time to work for TANU. As you can I agree with me that his decision helped to make Tanganyika /Tanzania and Africa in General free from colonial rule.

You and I we have to learn from this, because Late Mwl. JK Nyerere thought that at that time Native employees were not free, so to choose to continue to be employee in white color job would never help to solve the problem of lack of freedom and the better things was about the future, his choice become more important for the present and future generations in Tanzania and Africa in General.

This letter will remind you and I and our leaders to make decisions / choice on things which will bring present and future benefits for all.

====

ILIKUWA mwaka 1955 mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliamua kufanya maamuzi magumu ya kuamua kuachana na kazi yake ya ualimu kwenye Shule ya Sekondari Pugu iliyokuwa ikimpa kipato cha kujikimu na kuendesha maisha yake.

Alifanya maamuzi hayo ya kuachana na kazi yake hiyo na kuingia rasmi kwenye shughuli za kisiasa kupitia chama cha Tanganyika African National Union, ambazo kwa wakati huo hazikuwa na malipo zaidi ya kujitolea na wakati mwingine zilipelekea mtu kutiwa hatiani na kubambikiwa kesi.

Barua iliyoandikwa na Mwalimu Nyerere baada ya kutafsiriwa kutoka lugha ya Kiingereza kwenda lugha ya Kiswahili.

S. Francis College,

Pugu,

22 Machi, 1955.

Mwalimu Mkuu,

St. Francis College

Pugu.

Mpendwa Padri,

Nimelifikiria chaguo ulilonipa, kati ya kazi yangu shuleni na uanachama wangu katika T.A.N.U na nimefikia uamuzi kwamba lazima nijiuzulu katika nafasi yangu shuleni.

Lakini sasa najikuta nimekabiliwa na chaguo kama hilo. Kwa vile TANU inaingiliana na kazi yangu shuleni, suala hilo ni la kibinafsi na hivi karibuni au baadaye nitalazimika kupunguza shughuli zangu katika TANU au kuchagua kati ya TANU na shule. Katika hali hiyo chaguo lingekuwa la kweli; na kama ningegundua kwamba nisingeweza kuyafanya mambo yote hayo mawili kikamilifu ni dhahiri kwamba ningeiacha shule na kwenda kushughulika na TANU. Lakini iwapo kujiuzulu kutoka TANU kutanifanya niendelee na kazi yangu, suala hilo linakuwa ni la uamuzi wa kikanuni. Ni nani nchini Tanganyika yuko huru kujiunga na kuiongoza TANU? Kinadharia ni watu wote wasiokuwa waajiriwa wa serikali. Katika hali halisi nafahamu kwamba waajiriwa wa serikali za mitaa hawako huru, au ni kwamba hawana uhuru kuliko walimu wa mamlaka za kidini. Na kama uhuru wa walimu hao wa kidini utatiliwa mashaka, hali ingekuwa ya mashaka kwani sioni sababu yoyote kwa nini kila mwajiri asitoe masharti kama hayo kwa waajiriwa wake; na uwezekano huo ungekuwa wa kusikitisha. Kwa hiyo, ni lazima nijiuzulu kama njia ya kupinga hali hiyo.

Ninasikitika kwamba shughuli zangu katika TANU ni dhahiri zimeathiri utendaji wangu wa kufundisha; ninasikitika kuhusu matatizo ambayo yatajitokeza kwako na kwa wenzangu kwa muda kutokana na kujiuzulu kwangu; ninasikitika pia kwa matokeo ya kiuchumi ambayo yataikumba familia yangu.

Ningekuwa katika nafasi yako, Padri, ningefanya kama ulivyofanya wewe; tumaini langu pekee ni kwamba utaona inawezekana kwamba ungekuwa katika nafasi niliyo nayo mimi ungechukua hatua kama ambayo nimeichukua.

Nakushukuru wewe na Mapadri wengine kutokana na kushirikiana nami siku zote. Nitazihitaji sala zenu zaidi kuliko ilivyokuwa hapo nyuma. Endelea, Padri, kuniombea.

Mwanao mpendwa katika Kristo,

Julius Nyerere.

Baada ya kuandika barua hiyo rasmi Mwalimu Nyerere alijiunga na chama cha TANU.

Mwalimu Nyerere kutokana na uzalendo wake mkubwa kwa taifa hili aliamua kujitoa mhanga na kupoteza malipo yake ya ualimu na kuingia katika mapambano ya kudai uhuru ambako hatma yake Desemba 9, 1961 alifanikisha nchi yetu kuwa huru na tangu wakati huo tupo huru mpaka leo.

72392455.jpg
Mwalimu Nyerere (watatu kutoka kulia) akiwa na viongozi wengine enzi za uhai wake.

e500d40f-f6b0-4b06-ad3f-b90f2e0010ad.jpg

Uzalendo huu wa Nyerere ni wa kuigwa na mfano kwa viongozi wengine ambao siku zote wanapaswa kuweka kwanza maslahi ya taifa mbele, haijalishi wataumia kiasi gani. Ametufundisha jambo kubwa na muhimu rejea kwenye barua yake aliyoiandika nanukuu “ninasikitika pia kwa matokeo ya kiuchumi ambayo yataikumba familia yangu.” Katufundisha kwamba ukidhamiria kuitumikia nchi yako kwa uadilifu hutaogopa wewe au familia yako kuteseka na njaa, lazima ujitoe bila kujali ni kiasi gani utaumizwa na maamuzi yako, Taifa kwanza.

(picha zote za Mwalimu Nyerere ni zile zilizopigwa enzi za uhai wake wakati akiitumikia nchi yake kwa uadilifu mkubwa)

Imeandaliwa na;

Leonard Msigwa/GPL/MTANDAO.
 
Barua ya kujiuzulu ualimu ya Julius Kambarage Nyerere ilikuwa barua ya kuacha kazi ya ualimu katika shule ya Mtakatifu Francis, Pugu, Dar es Salaam.

Barua ya Nyerere kujiuzuru ualimu.
Mchakato wake na sababu zilizopelekea kujiuzulu
Hotuba aliyotoa Nyerere pale Mnazi Mmoja ambapo aliwaeleza watu kuhusu safari yake kwenda Umoja wa Mataifa ilikuwa ndiyo mwanzo hasa wa historia mpya ya Tanganyika. Kabla ya hapo Waafrika wa Tanganyika hawakupata kuonyesha shauku na matumaini katika mustakabali wao. Katika viwanja vya Mnazi Mmoja Nyerere aliwaeleza halaiki ya watu wenye furaha na waliokuwa wakimsikiliza kwa makini kuwa miongoni mwa mataifa kumi na mbili yanayounda Baraza la Udhamini saba kati yao yalitoa idhini kuwa muda wa utawala wa ndani wa Tanganyika utakapowadia, Waafrika lazima wapewe nchi yao.

Katika hotuba yake Nyerere alitilia mkazo sera ya TANU kuhusu mahusiano mema baina ya Waafrika na watu wa mataifa mengine na aliwaonya wanachama wa TANU ambao walikuwa wameanza kuwabagua watu wa rangi tofauti kuwaambia kuwa hivyo haikuwa sawa. Alisisitiza juu ya umoja miongoni mwa wananachi na hatimaye aliwadhihaki wasikilizaji kwa kuwauliza ikiwa wangesubiri kwa miaka ishirini na tano kuwa huru. Halaiki hiyo ya watu kwa pamoja ilipiga kelele, "hapana". Wananachi kwa pamoja walijibu kwa sauti kubwa wakisema walitaka uhuru kesho au kesho kutwa.

Cheche za TANU na mshtuko kwa Padri Walsh

Julius Nyerere akiwa UNO mwaka 1955.
Nyerere ambaye alikuwa akiogopa kuchukua uongozi wa TANU tangu 1953 alikuwa amefarajika sana na mshikamano huu ulioonyeshwa na wananchi. Sasa ilikuwa dhahiri kwake kwamba rafiki yake Abdulwahid, Ally, Dossa Aziz, John Rupia na uongozi mzima wa TANU pamoja na lile Baraza la Wazee lilikuwa limemsafishia njia kuongoza harakati kwa niaba yao. Lakini Padri Walsh na Wamisionari katika shule ya Mtakatifu Francis, Pugu, walitazama harakati hizi kwa mtazamo mwingine kabisa. Wamishionari hawakuweza tena kumvumilia Nyerere kuwa mmoja wa walimu katika shule yao. Hatima ile ile iliyowasibu wazalendo wengine kabla yake sasa ilimkabili Nyerere. Aliambiwa ama abakie mtumishi mtiifu wa kanisa au ajiuzulu; Kanisa halikuweza kukaa kimya na kumuangalia Nyerere akiwatumikia mabwana wawili.

Nyerere alilipeleka tatizo hili kwa Clement Mtamila, Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya TANU. Mtamila aliitisha mkutano wa kamati kuu nyumbani kwake mtaa wa Kipata na TANU ilijadili tatizo hilo. Miongoni mwa wajumbe wa kamati ile mbali na Rupia na Kambona walikuwa Bibi Titi Mohamed na Bibi Tatu bint Mzee. Kamati Kuu ya TANU ilimshauri Nyerere ajiuzulu. Tafarani hii ilitokea wiki chache tu baada ya kurudi kutoka Umoja wa Mataifa katika wiki za mwisho za mwezi Machi. Tarehe 23 Machi, 1955 Nyerere alijiuzulu ualimu. Ilikuwa adhuhuri Nyerere alipokuja Dar es Salaam kutoka Pugu, akiwa si mwalimu wa shule tena. Inasemekana aliposhuka tu kwenye basi alikwenda moja kwa moja ofisini kwa Abdulwahid katika soko la Kariakoo kumpasha habari rafiki yake. Nyerere alikaa na Abdulwahid katika nyumba yake namba 78 Mtaa wa Stanley. Baadaye kidogo Nyerere alirudi kijijini kwake huko Musoma. John Hatch alipokuja Dar es Salaam kwa mwaliko wa TANU Nyerere alikuwa kwao kijijini. Utaona hapo baadaye kidogo jinsi mgeni huyu Mwingereza alivyomgutusha Schneider Abdillah Plantan kuhusu TANU kuwashirikisha wanawake katika harakati za kudai uhuru.

Hapa ndipo Nyerere alipoifikisha TANU katika uingozi wake wa miezi minane na hali ilianza moto Tanganyika nzima kiasi ya kuwa Nyerere hakuweza tena kuwatumikia mabwana wawili. Hii ndiyo iliyopelekea yeye kuandika barua ya kujiuzulu kazi ya ualimu.

Tafsiri ya barua ya Mwalimu Nyerere kwa Kiswahili
S. Francis College, Pugu, 22 Machi, 1955.

Mwalimu Mkuu, St. Francis College Pugu.

Hayo ambayo Emmanuel ameeleza kuhusu Julius Nyerere yote neno kwa neno yametoka kwenye kitabu cha Abdul Sykes.

Hakika hivyo ndivyo ilivyokuwa.

Barua ya kujiuzulu ilijadiliwa na Kamati ya TANU chini ya Mwenyekiti wake Clement Mohamed Mtamila nyumbani kwake Mtaa wa Kipata na Sikukuu.

Baada ya Nyerere kujiuzulu Nyerere alikwenda kuishi nyumbani kwa Abdul Sykes Mtaa wa Stanley na Sikukuu si mbali na nyumbani kwa Mzee Mtamila.

Kwa bahati mbaya sana katika kitabu cha maisha ya Julius Nyerere waandishi wameandika kuwa Nyerere baada ya kujiuzulu alikwenda kuishi kwa Ally Sykes Mtaa wa Kipata.

Hapa wamekosea.

Mitaa hii imepewa majina ya wazalendo.

Kipata sasa ni Kleist Sykes na Stanley ni Max Mbwana.

1617854204533.png

Kulia ni Mzee Clement Mtamila, Julius Nyerere na Zuberi Mtemvu. Aliyekaa kushoto ni Mama Maria Nyerere.

Hii ni katika moja ya mikutano ya mwanzo ya TANU Mnazi Mmoja

Bwana na Bibi Abdulwahid Sykes.

Hawa ndiyo waliompokea Nyerere mara ya kwanza 1952 alipopelekwa kwao na Joseph Kasella Bantu na mwaka wa 1955 alipojiuzulu kazi walimkaribisha nyumbani kwao.

1617855477085.png

Kulia ni Mshume Kiyate, Julius Nyerere, Max Mbwana na Mwinjuma Mwinyikambi.

Hawa wazee wote mitaa waliyokuwa wakiishi imepewa majina yao na vibao vimebalishwa ila mtaa alioishi Mshume Kiyate. Wahusika sasa karibu miaka 30 wamekataa kubadilisha kibao cha mtaa huo.

1617854756069.png
 
View attachment 1746310

View attachment 1746318

View attachment 1746314
Mataita wa longiii
 
Shukurani mkuu kwa nyongeza hiyo 🙏🙏🙏 hapa nimepata kitu
 
Barua ya kujiuzulu ualimu ya Julius Kambarage Nyerere ilikuwa barua ya kuacha kazi ya ualimu katika shule ya Mtakatifu Francis, Pugu, Dar es Salaam.

Barua ya Nyerere kujiuzuru ualimu.
Mchakato wake na sababu zilizopelekea kujiuzulu
Hotuba aliyotoa Nyerere pale Mnazi Mmoja ambapo aliwaeleza watu kuhusu safari yake kwenda Umoja wa Mataifa ilikuwa ndiyo mwanzo hasa wa historia mpya ya Tanganyika. Kabla ya hapo Waafrika wa Tanganyika hawakupata kuonyesha shauku na matumaini katika mustakabali wao. Katika viwanja vya Mnazi Mmoja Nyerere aliwaeleza halaiki ya watu wenye furaha na waliokuwa wakimsikiliza kwa makini kuwa miongoni mwa mataifa kumi na mbili yanayounda Baraza la Udhamini saba kati yao yalitoa idhini kuwa muda wa utawala wa ndani wa Tanganyika utakapowadia, Waafrika lazima wapewe nchi yao.

Katika hotuba yake Nyerere alitilia mkazo sera ya TANU kuhusu mahusiano mema baina ya Waafrika na watu wa mataifa mengine na aliwaonya wanachama wa TANU ambao walikuwa wameanza kuwabagua watu wa rangi tofauti kuwaambia kuwa hivyo haikuwa sawa. Alisisitiza juu ya umoja miongoni mwa wananachi na hatimaye aliwadhihaki wasikilizaji kwa kuwauliza ikiwa wangesubiri kwa miaka ishirini na tano kuwa huru. Halaiki hiyo ya watu kwa pamoja ilipiga kelele, "hapana". Wananachi kwa pamoja walijibu kwa sauti kubwa wakisema walitaka uhuru kesho au kesho kutwa.

Cheche za TANU na mshtuko kwa Padri Walsh

Julius Nyerere akiwa UNO mwaka 1955.
Nyerere ambaye alikuwa akiogopa kuchukua uongozi wa TANU tangu 1953 alikuwa amefarajika sana na mshikamano huu ulioonyeshwa na wananchi. Sasa ilikuwa dhahiri kwake kwamba rafiki yake Abdulwahid, Ally, Dossa Aziz, John Rupia na uongozi mzima wa TANU pamoja na lile Baraza la Wazee lilikuwa limemsafishia njia kuongoza harakati kwa niaba yao. Lakini Padri Walsh na Wamisionari katika shule ya Mtakatifu Francis, Pugu, walitazama harakati hizi kwa mtazamo mwingine kabisa. Wamishionari hawakuweza tena kumvumilia Nyerere kuwa mmoja wa walimu katika shule yao. Hatima ile ile iliyowasibu wazalendo wengine kabla yake sasa ilimkabili Nyerere. Aliambiwa ama abakie mtumishi mtiifu wa kanisa au ajiuzulu; Kanisa halikuweza kukaa kimya na kumuangalia Nyerere akiwatumikia mabwana wawili.

Nyerere alilipeleka tatizo hili kwa Clement Mtamila, Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya TANU. Mtamila aliitisha mkutano wa kamati kuu nyumbani kwake mtaa wa Kipata na TANU ilijadili tatizo hilo. Miongoni mwa wajumbe wa kamati ile mbali na Rupia na Kambona walikuwa Bibi Titi Mohamed na Bibi Tatu bint Mzee. Kamati Kuu ya TANU ilimshauri Nyerere ajiuzulu. Tafarani hii ilitokea wiki chache tu baada ya kurudi kutoka Umoja wa Mataifa katika wiki za mwisho za mwezi Machi. Tarehe 23 Machi, 1955 Nyerere alijiuzulu ualimu. Ilikuwa adhuhuri Nyerere alipokuja Dar es Salaam kutoka Pugu, akiwa si mwalimu wa shule tena. Inasemekana aliposhuka tu kwenye basi alikwenda moja kwa moja ofisini kwa Abdulwahid katika soko la Kariakoo kumpasha habari rafiki yake. Nyerere alikaa na Abdulwahid katika nyumba yake namba 78 Mtaa wa Stanley. Baadaye kidogo Nyerere alirudi kijijini kwake huko Musoma. John Hatch alipokuja Dar es Salaam kwa mwaliko wa TANU Nyerere alikuwa kwao kijijini. Utaona hapo baadaye kidogo jinsi mgeni huyu Mwingereza alivyomgutusha Schneider Abdillah Plantan kuhusu TANU kuwashirikisha wanawake katika harakati za kudai uhuru.

Hapa ndipo Nyerere alipoifikisha TANU katika uingozi wake wa miezi minane na hali ilianza moto Tanganyika nzima kiasi ya kuwa Nyerere hakuweza tena kuwatumikia mabwana wawili. Hii ndiyo iliyopelekea yeye kuandika barua ya kujiuzulu kazi ya ualimu.

Tafsiri ya barua ya Mwalimu Nyerere kwa Kiswahili
S. Francis College, Pugu, 22 Machi, 1955.

Mwalimu Mkuu, St. Francis College Pugu.

Mpendwa Padri,

Nimelifikiria chaguo ulilonipa, kati ya kazi yangu shuleni na uanachama wangu katika T.A.N.U na nimefikia uamuzi kwamba lazima nijiuzulu katika nafasi yangu shuleni.

Lakini sasa najikuta nimekabiliwa na chaguo kama hilo. Kwa vile TANU inaingiliana na kazi yangu shuleni, suala hilo ni la kibinafsi na hivi karibuni au baadaye nitalazimika kupunguza shughuli zangu katika TANU au kuchagua kati ya TANU na shule. Katika hali hiyo chaguo lingekuwa la kweli; na kama ningegundua kwamba nisingeweza kuyafanya mambo yote hayo mawili kikamilifu ni dhahiri kwamba ningeiacha shule na kwenda kushughulika na TANU. Lakini iwapo kujiuzulu kutoka TANU kutanifanya niendelee na kazi yangu, suala hilo linakuwa ni la uamuzi wa kikanuni. Ni nani nchini Tanganyika yuko huru kujiunga na kuiongoza TANU? Kinadharia ni watu wote wasiokuwa waajiriwa wa serikali. Katika hali halisi nafahamu kwamba waajiriwa wa serikali za mitaa hawako huru, au ni kwamba hawana uhuru kuliko walimu wa mamlaka za kidini. Na kama uhuru wa walimu hao wa kidini utatiliwa mashaka, hali ingekuwa ya mashaka kwani sioni sababu yoyote kwa nini kila mwajiri asitoe masharti kama hayo kwa waajiriwa wake; na uwezekano huo ungekuwa wa kusikitisha. Kwa hiyo, ni lazima nijiuzulu kama njia ya kupinga hali hiyo.

Ninasikitika kwamba shughuli zangu katika TANU ni dhahiri zimeathiri utendaji wangu wa kufundisha; ninasikitika kuhusu matatizo ambayo yatajitokeza kwako na kwa wenzangu kwa muda kutokana na kujiuzulu kwangu; ninasikitika pia kwa matokeo ya kiuchumi ambayo yataikumba familia yangu.

Ningekuwa katika nafasi yako, Padri, ningefanya kama ulivyofanya wewe; tumaini langu pekee ni kwamba utaona inawezekana kwamba ungekuwa katika nafasi niliyo nayo mimi ungechukua hatua kama ambayo nimeichukua.

Nakushukuru wewe na Mapadri wengine kutokana na kushirikiana nami siku zote. Nitazihitaji sala zenu zaidi kuliko ilivyokuwa hapo nyuma. Endelea, Padri, kuniombea.

Mwanao mpendwa katika Kristo,

Julius Nyerere.
Niliisoma tafsiri ya barua hiyo zamani sana miaka ya sabini kwenye kitabu cha Mikiki Mikiki ya Siasa Tanganyika kilichoandikwa na Edward B.M.Balongo. Nilitegemea kuona kopi yake original leo, lakini sikuambulia kitu, ninapelekwa facebook Connectivity kusoma habari za internet connectivity Pakistan.

Kama una image ya barua ile, tafadhali sana shea na sisi tuiweke kwenye kumbukumbu zetu. cc Mohamed Said
 
Kichuguu,
Barua hiyo hapo:

1617933742266.png

Umemtaja Edward Barongo na kitabu chake.

Barongo aliingia TANU siku za mwanzo na lipita pale ofisi ya TANU akawakuta jamaa wanasubiri kufanya mkutano.

Muda wa mkutano ulipowadia yeye akaondoka lakini tayari alikuwa keshaazimia kujiunga na chama.
Kitabu chake hakina tofauti na vitabu vingine vilivyoandikwa kuhusu historia ya TANU.
 
Kichuguu,
Barua hiyo hapo:

View attachment 1747158

Umemtaja Edward Barongo na kitabu chake.

Barongo aliingia TANU siku za mwanzo na lipita pale ofisi ya TANU akawakuta jamaa wanasubiri kufanya mkutano.

Muda wa mkutano ulipowadia yeye akaondoka lakini tayari alikuwa keshaazimia kujiunga na chama.
Kitabu chake hakina tofauti na vitabu vingine vilivyoandikwa kuhusu historia ya TANU.
Asante sana; hii ndiyo nilikuwa nataka kuona.
 
Shukurani mkuu kwa nyongeza hiyo 🙏🙏🙏 hapa nimepata kitu
Emma...
Nakuwekea picha nilipiga miaka kama mitatu iliyopita siku Happy Clement Mtamila aliponitembelea nyumbani.

Happy ni mkubwa kidogo kwangu na alinitangulia St. Joseph's Convent Dar es Salaam.

Miaka mingi tulikuwa hatujaonana.

Kutoka nyumbani kwao hadi kwetu pale Kipata tulitenganishwa na barabara ya Mtaa wa Swahili kiasi cha nyumba kumi utakuwa umefika nyumbani kwetu.

Tukawa tunakumbushana habari za wazee wetu nikamuuliza kuhusu ile hazina ya picha za baba yake na Nyerere zilizokuwa zimetundikwa ukutani nyumbani kwao.

Miaka mingi alikuwa hayupo Tanzania akiishi Ulaya na hakuwa na taarifa zile picha ziko wapi.

Huu ndiyo uhusiano wetu sisi ambao tulizaliwa wakati ule na wazee hawa na tukawajua waasisi wa TANU na wapigania uhuru wa Tanganyika.

Tunaposoma historia hii na tusiwakute wazee wetu wametajwa hili hutushangaza sana.

1617934605274.png
 
Emma...
Nakuwekea picha nilipiga miaka kama mitatu iliyopita siku Happy Clement Mtamila aliponitembelea nyumbani,
Happy ni mkubwa kidogo kwangu na alinitangulia St. Joseph;s Convent Dar es Salaam.

Miaka mingi tulikuwa hatujaonana.

Kutoka nyumbani kwao hadi kwetu pale Kipata tulitenganishwa na barabara ya Mtaa wa Swahili kiasi cha nyumba kumi utakuwa umefika nyumbani kwetu.

Tukawa tunakumbushana habari za wazee wetu nikamuuliza kuhusu ile hazina ya picha za baba yake na Nyerere zilizokuwa zimetundikwa ukutani nyumbani kwao.

Miaka mingi alikuwa hayupo Tanzania akiishi Ulaya na hakuwa na taarifa zile picha ziko wapi.

Huu ndiyo uhusiano wetu sisi ambao tulizaliwa wakati ule na wazee hawa na tukawajua waasisi wa TANU na wapigania uhuru wa Tanganyika.

Tunaposoma historia hii na tusiwakute wazee wetu wametajwa hili hutushangaza sana.

View attachment 1747160
Safi sana. Nafurahi mnatuletea historian za kweli za ukombozi wa nchi yetu
 
Niliisoma tafsiri ya barua hiyo zamani sana miaka ya sabini kwenye kitabu cha Mikiki Mikiki ya Siasa Tanganyika kilichoandikwa na Edward B.M.Balongo. Nilitegemea kuona kopi yake original leo, lakini sikuambulia kitu, ninapelekwa facebook Connectivity kusoma habari za internet connectivity Pakistan.

Kama una image ya barua ile, tafadhali sana shea na sisi tuiweke kwenye kumbukumbu zetu. cc Mohamed Said
Picha ya barua hiyo ninayo.
Ila Shukurani kwa Mohamed Said ameiweka
 
Emma...
Nakuwekea picha nilipiga miaka kama mitatu iliyopita siku Happy Clement Mtamila aliponitembelea nyumbani.

Happy ni mkubwa kidogo kwangu na alinitangulia St. Joseph's Convent Dar es Salaam.

Miaka mingi tulikuwa hatujaonana.

Kutoka nyumbani kwao hadi kwetu pale Kipata tulitenganishwa na barabara ya Mtaa wa Swahili kiasi cha nyumba kumi utakuwa umefika nyumbani kwetu.

Tukawa tunakumbushana habari za wazee wetu nikamuuliza kuhusu ile hazina ya picha za baba yake na Nyerere zilizokuwa zimetundikwa ukutani nyumbani kwao.

Miaka mingi alikuwa hayupo Tanzania akiishi Ulaya na hakuwa na taarifa zile picha ziko wapi.

Huu ndiyo uhusiano wetu sisi ambao tulizaliwa wakati ule na wazee hawa na tukawajua waasisi wa TANU na wapigania uhuru wa Tanganyika.

Tunaposoma historia hii na tusiwakute wazee wetu wametajwa hili hutushangaza sana.

View attachment 1747160
shukurani mkuu 🙏🙏🙏
Kweli ni vyema kukumbuka mambo hayo
 
View attachment 365544
We have to learn this Philosopher who make critical thinking to make choice between White colour job at St. Francis and Politics.

After he made a critical thinking he come up with a conclusion that, he has to resign his colour job in order to have time to work for TANU. As you can I agree with me that his decision helped to make Tanganyika /Tanzania and Africa in General free from colonial rule.

You and I we have to learn from this, because Late Mwl. JK Nyerere thought that at that time Native employees were not free, so to choose to continue to be employee in white color job would never help to solve the problem of lack of freedom and the better things was about the future, his choice become more important for the present and future generations in Tanzania and Africa in General.

This letter will remind you and I and our leaders to make decisions / choice on things which will bring present and future benefits for all.

====

ILIKUWA mwaka 1955 mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliamua kufanya maamuzi magumu ya kuamua kuachana na kazi yake ya ualimu kwenye Shule ya Sekondari Pugu iliyokuwa ikimpa kipato cha kujikimu na kuendesha maisha yake.

Alifanya maamuzi hayo ya kuachana na kazi yake hiyo na kuingia rasmi kwenye shughuli za kisiasa kupitia chama cha Tanganyika African National Union, ambazo kwa wakati huo hazikuwa na malipo zaidi ya kujitolea na wakati mwingine zilipelekea mtu kutiwa hatiani na kubambikiwa kesi.

Barua iliyoandikwa na Mwalimu Nyerere baada ya kutafsiriwa kutoka lugha ya Kiingereza kwenda lugha ya Kiswahili.

S. Francis College,

Pugu,

22 Machi, 1955.

Mwalimu Mkuu,

St. Francis College

Pugu.

Mpendwa Padri,

Nimelifikiria chaguo ulilonipa, kati ya kazi yangu shuleni na uanachama wangu katika T.A.N.U na nimefikia uamuzi kwamba lazima nijiuzulu katika nafasi yangu shuleni.

Lakini sasa najikuta nimekabiliwa na chaguo kama hilo. Kwa vile TANU inaingiliana na kazi yangu shuleni, suala hilo ni la kibinafsi na hivi karibuni au baadaye nitalazimika kupunguza shughuli zangu katika TANU au kuchagua kati ya TANU na shule. Katika hali hiyo chaguo lingekuwa la kweli; na kama ningegundua kwamba nisingeweza kuyafanya mambo yote hayo mawili kikamilifu ni dhahiri kwamba ningeiacha shule na kwenda kushughulika na TANU. Lakini iwapo kujiuzulu kutoka TANU kutanifanya niendelee na kazi yangu, suala hilo linakuwa ni la uamuzi wa kikanuni. Ni nani nchini Tanganyika yuko huru kujiunga na kuiongoza TANU? Kinadharia ni watu wote wasiokuwa waajiriwa wa serikali. Katika hali halisi nafahamu kwamba waajiriwa wa serikali za mitaa hawako huru, au ni kwamba hawana uhuru kuliko walimu wa mamlaka za kidini. Na kama uhuru wa walimu hao wa kidini utatiliwa mashaka, hali ingekuwa ya mashaka kwani sioni sababu yoyote kwa nini kila mwajiri asitoe masharti kama hayo kwa waajiriwa wake; na uwezekano huo ungekuwa wa kusikitisha. Kwa hiyo, ni lazima nijiuzulu kama njia ya kupinga hali hiyo.

Ninasikitika kwamba shughuli zangu katika TANU ni dhahiri zimeathiri utendaji wangu wa kufundisha; ninasikitika kuhusu matatizo ambayo yatajitokeza kwako na kwa wenzangu kwa muda kutokana na kujiuzulu kwangu; ninasikitika pia kwa matokeo ya kiuchumi ambayo yataikumba familia yangu.

Ningekuwa katika nafasi yako, Padri, ningefanya kama ulivyofanya wewe; tumaini langu pekee ni kwamba utaona inawezekana kwamba ungekuwa katika nafasi niliyo nayo mimi ungechukua hatua kama ambayo nimeichukua.

Nakushukuru wewe na Mapadri wengine kutokana na kushirikiana nami siku zote. Nitazihitaji sala zenu zaidi kuliko ilivyokuwa hapo nyuma. Endelea, Padri, kuniombea.

Mwanao mpendwa katika Kristo,

Julius Nyerere.

Baada ya kuandika barua hiyo rasmi Mwalimu Nyerere alijiunga na chama cha TANU.

Mwalimu Nyerere kutokana na uzalendo wake mkubwa kwa taifa hili aliamua kujitoa mhanga na kupoteza malipo yake ya ualimu na kuingia katika mapambano ya kudai uhuru ambako hatma yake Desemba 9, 1961 alifanikisha nchi yetu kuwa huru na tangu wakati huo tupo huru mpaka leo.

72392455.jpg
Mwalimu Nyerere (watatu kutoka kulia) akiwa na viongozi wengine enzi za uhai wake.

View attachment 543636
Uzalendo huu wa Nyerere ni wa kuigwa na mfano kwa viongozi wengine ambao siku zote wanapaswa kuweka kwanza maslahi ya taifa mbele, haijalishi wataumia kiasi gani. Ametufundisha jambo kubwa na muhimu rejea kwenye barua yake aliyoiandika nanukuu “ninasikitika pia kwa matokeo ya kiuchumi ambayo yataikumba familia yangu.” Katufundisha kwamba ukidhamiria kuitumikia nchi yako kwa uadilifu hutaogopa wewe au familia yako kuteseka na njaa, lazima ujitoe bila kujali ni kiasi gani utaumizwa na maamuzi yako, Taifa kwanza.

(picha zote za Mwalimu Nyerere ni zile zilizopigwa enzi za uhai wake wakati akiitumikia nchi yake kwa uadilifu mkubwa)

Imeandaliwa na;

Leonard Msigwa/GPL/MTANDAO.
Figga...
Nimevutiwa sana na maneno hayo hapo chini yaliyohitimisha makala yako kuhusu barua ya kujiuzulu kazi ya ualimu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Baba wa Taifa.

''Baada ya kuandika barua hiyo rasmi Mwalimu Nyerere alijiunga na chama cha TANU.

Mwalimu Nyerere kutokana na uzalendo wake mkubwa kwa taifa hili aliamua kujitoa mhanga na kupoteza malipo yake ya ualimu na kuingia katika mapambano ya kudai uhuru ambako hatma yake Desemba 9, 1961 alifanikisha nchi yetu kuwa huru na tangu wakati huo tupo huru mpaka leo.''

Mwalimu hakujiunga TANU baada ya kuacha kazi.

Mwalimu alitokea TAA akiwa Territorial President nafasi ambayo aliipata baada ya kushinda uchaguzi uliofanyika Arnautoglo Hall tarehe 17 April, 1953 kati yake na Abdulwahid Sykes.

Uchaguzi huu una historia ndefu inayoanza mwaka wa 1952 pale Joseph Kasella Bantu alipompeleka Nyerere nyumbani kwa Abdul Sykes kumtambuisha.

Abdul alikuwa Act. President wa TAA na Secretary.

Ikiwa nitaeleza vipi Nyerere aliweza kuingia katika uongozi wa juu wa TAA mwaka wa 1953 makala hii itakuwa kitabu kizima.

Ninachoweza kusema hapa ni kuwa Nyerere aliingizwa katika uongozi wa TAA baada ya mazungumzo yaliyofanyika nyumbani kwa Hamza Mwapachu, Nansio Ukerewe kati ya Abdul Sykes Hamza Mwapachu na Ali Mwinyi Tambwe, Secretary wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika.

Hamza alimuomba Abdul Sykes amuunge mkono Nyerere na ahakikishe kuwa anapita katika ule uchaguzi wa 1953 na mwaka unaofuatia TANU iundwe na Nyerere aongoze harakati za kudai uhuru.

Hamza alitoa sababu mbili kubwa kwa nini Nyerere achukue uongozi.
Sababu ya kwanza ilikuwa dini ya Nyerere kama Mkristo itawaleta wengi katika chama.

Sababu ya pili Nyerere alikuwa anafaa zaidi kuongoza harakati za uhuru kwa elimu yake kubwa.

Bila ya mkakati huu wa Nansio kwa siasa za mji wa Dar es Salaam ya 1950, nguvu ya fedha na ushawishi wa ukoo wa Sykes, Nyerere asingeweza kusinda uchaguzi ule (African Association iliundwa na Kleist Sykes mwaka wa 1929).

Hii ndiyo hali iliyokuwa inamkabili Nyerere katika uchaguzi ule.

Nyerere alishinda uchaguzi ule akawa Rais wa TAA na Abdul Sykes Makamu wa Rais.

Sasa baada ya kushinda ule uchaguzi kama ilivyokubaliwa Nansio TANU ikaundwa mwaka unaofuatia 1954 na Nyerere akawa Rais wa TANU na John Rupia Makamu wa Rais.

Nyerere hakuacha kazi hivi hivi.

Kulikuwa na mazungumzo ya kina baina yake na viongozi wa TANU katika kamati ya ndani ya TANU iliyokuwa ikiongozwa na Abdul Sykes, John Rupia, Ally Sykes na Dossa Aziz.

Hawa ndiyo waliokuwa wafadhili wakubwa wa TANU na harakati za uhuru wa Tanganyika pale New Street.

Nyerere hakuacha kazi hivi hivi tu hana uhakika wa vipi ataikimu familia yake.

Ndiyo maana Nyerere alipoacha kazi alikwenda kuishi nyumbani kwa Abdul Sykes na mkewe Bi. Mwamvua bint Mrisho.

Nyerere aliishi maisha bora zaidi alipokuwa Rais wa TANU kuliko alipokuwa ndani ya ajira.ya ualimu wa shule.

Bahati mbaya sana historia hii si wengi wanaifahamu na matokeo yake jina linalojitokeza katika kuunda TANU ni la Nyerere peke yake ingawa mikutano ya siri ya kuasisi TANU ilikuwa ikifanyika nyumbani kwa Abdul Sykes Mtaa wa Stanley na Sikukuu na ndiyo Nyerere alikuja kuishi hapo mwaka wa 1955 baada ya kurudi kutoka UNO.

1617971010816.png

Angalia majina ya viongozi waliongia katika uongozi wa TAA na Nyerere 1953: Abdul Sykes, Ally Sykes, Dome Budohi, Dossa Aziz, John Rupia.

1617971753036.png

1617972151996.png

Joseph Kasella Bantu
 
Back
Top Bottom