Elections 2010 Kikwete: Nitachukua fomu wiki ijayo

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,295
33,079
headline_bullet.jpg
Atangaza kikosi cha kumsambazia fomu
headline_bullet.jpg
Ni timu tisa, kila moja ina wanafunzi wanne



Kikwete%2823%29.jpg

Rais Jakaya Kikwete

Wakati joto la Uchaguzi Mkuu likizidi kupanda, Rais Jakaya Kikwete, amesema kwamba anatarajia kuchukua fomu ya kuwania tena kiti hicho kwa awamu ya pili Jumatatu ya Juni 21, mwaka huu.

Akihutubia wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutoka vyuo vya elimu ya juu katika viwanja wa Nyerere Square mjini hapa jana, Kikwete aliwaomba wanachuo hao kumsaidia katika harakati za kutafuta wadhamini.

Alifafanua kwamba vijana hao watamsaidia katika kuzungusha fomu ya kugombea urais anayotarajia kuichukua Jumatatu ya wiki ijayo kwa kumuombea wadhamini.

Alisema kutakuwa na timu tisa na kila timu itajumuisha wanachuo wanne ili kujifunza namna ya kushindana katika uchaguzi.

Aliagiza kila wilaya iwashirikishe wanachuo kwenye shughuli za kampeni ili wajifunze zaidi masuala ya siasa.

Kuhusu maombi ya wanachuo hao kupatiwa ofisi kwa ajili ya kufanya shughuli za chama, mwenyekiti huyo aliahidi kuwasaidia.

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) ambao ni wanachama wa CCM walimchangia Rais Kikwete Sh. milioni 1.2 kwa ajili ya kuchukua fomu na kuchangia chama.

Katika hafla hiyo ambayo wanachama wapya 9,200 kutoka vyuo mbalimali walikabidhiwa kadi za CCM, ilihudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, mawaziri na wabunge kadhaa wa chama hicho.

Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge unatarajia kufanyika Oktoba 31, mwaka huu.

Ratiba ya mchakato wa kupata wagombea wa CCM katika uchaguzi mkuu wa Oktoba inaonyesha kwamba uchukuaji wa fomu kwa wagombea urais wa Jamhuri ya Muungano na Tanzania Visiwani ni Juni 21.

Julai 16 Kupendekezwa kwa wagombea nafasi za urais.
Julai 17 Kutangazwa kwa wagombea wa urais wa Muungano na rais wa Zanzibar,
Julai 26-28 Kutolewa kwa fomu za wagombea wa nafasi ya ubunge, udiwani na ujumbe wa baraza la wawakilishi. 29 Julai-Agosti 7 Kampeni za wagombea hao ndani ya chama
Agosti 9-10 Matokeo ya kura za maoni.
Agosti 11 Kamati za siasa wilaya kujadili wagombea ubunge na uwakilishi.
Agosti 15 Kamati maalum ya halmashauri kuu kuwajadili wagombea wa ubunge na uwakilishi wa majimbo na viti maalum.
Agosti 16 hadi 17 Sekretarieti ya NEC kujadili wagombea.
Agosti 18 na 19 Kamati kuu kupendekeza majina ya wagombea.


CHANZO:
NIPASHE

Nani AtaMshinda Mzee j.Kikwete?
 
staili uluyokuja nayo nimeipenda....wanafunzi! Lakini mbona UDSM huendi mkuu,unaogopa nini?
 
Back
Top Bottom