Elections 2010 JK ni mtu wa watu anajali hata walemavu

Lucchese DeCavalcante

JF-Expert Member
Jan 10, 2009
5,471
733
jk-makete.jpg

Jk kwa kweli ni mtu wa watu cheki hapo anakaa kwenye vumbi kuongea kwa unyenyekevu na mlemavu ni viongozi wachache sana wenye moyo wa kibinadamu kiasi hiki..
 
Mr. Cheap popularity.

That's not cheap popularity, JK yupo kwenye kampeni kazi mojawapo ni kuwafikia wapiga kura.

Walemavu wanahaki sawa kama watu wengine, hii ni kuafaka kwa JK kusalimiana na mpiga kura wake katika mazingira yaleyale aliyopo huyu dada.

JK endelea kukusanya kura za kishindo
 
Punguza pumba wewe! Tanzania kuna walemavu wangapi ama kwakuwa huyu kavaa kiCCM? Kikwete is sick upstairs. Hatudanganyiki na usanii wa kijinga !
 
JK anafanya dhiaka na kuwalaghai walemavu. Kama anataka kujali walemavu akaombe ushauri kwa Bwana Mengi (IPP). Hii ya JK haitoki moyoni ni kwa ajili ya kutafuta kura baada ya hapo hakuna. Hata hakuwapa nafasi ya Ubunge katika Bunge la 2005-2010 mpaka baada ya vifo vya ma-Albino ndio akawakumbuka kwamba nao wanastahili. Unafiki mtupu!
 
Nadhani kuna njia bora nyingi zaidi ya kuwafikia walemavu, njia iliyo bora zaidi kwa sasa ni yeye kuacha hiyo nafsi ya Urais maana ameshindwa ku-deliver karibu ktk kila angle.
 
Wajinga mpigieni kura JK, Ili tujue idadi kamili ya wapumbavu nchini wako asilimia ngapi kwa kuhesabu kura za ccm.:confused2:

Hizi kauli nyengine..... ukichunguza sana unaweza ukakuta inamgusa hata yule BIMKUBWA wako kule kijijini kwenu
pole weh!
 
that's not cheap popularity, jk yupo kwenye kampeni kazi mojawapo ni kuwafikia wapiga kura.

walemavu wanahaki sawa kama watu wengine, hii ni kuafaka kwa jk kusalimiana na mpiga kura wake katika mazingira yaleyale aliyopo huyu dada.

jk endelea kukusanya kura za kishindo

mbona alishindwa kuwa kwenye
mazingira yaleyale waliyokuwepo wafanyakazi mpaka akazikataa hata kura zao?
 
What we dont know is presidency is not just shaking hands with people of various kinds, but is comprising of coordination of people and resources of the entire society, by using best available alternatives, applying all the strenght society have to overcome society weaknesses, playing very well with the opportunities of that society against outside threats, leading (driving) that society towards the desired achievable sustainable goals.
Mtu wa watu yes! Kaweza kuunganisha watu na rasilimali tulizonazo kututoa katika umasikini na kutufikisha tunapokusudia? Kuwasalimia vilema ni kuonyesha unawajali? Mbona kwa miaka mitano ya serikali yake kashindwa hata kutunga sheria ya kuwalazimisha wamiliki wa vyombo mbalimbali kuweka miundombinu ya kuwasaidia walemavu (mfano majengo)?
Think wisely!!!!!!!
 
unyenyekevu huu angeonyesha Diamond Jubilee wakati anahutubia " wazee wa Dar Es Salaam" wala asingehangaika hivi sasa
 
What we dont know is presidency is not just shaking hands with people of various kinds, but is comprising of coordination of people and resources of the entire society, by using best available alternatives, applying all the strenght society have to overcome society weaknesses, playing very well with the opportunities of that society against outside threats, leading (driving) that society towards the desired achievable sustainable goals.
Mtu wa watu yes! Kaweza kuunganisha watu na rasilimali tulizonazo kututoa katika umasikini na kutufikisha tunapokusudia? Kuwasalimia vilema ni kuonyesha unawajali? Mbona kwa miaka mitano ya serikali yake kashindwa hata kutunga sheria ya kuwalazimisha wamiliki wa vyombo mbalimbali kuweka miundombinu ya kuwasaidia walemavu (mfano majengo)?
Think wisely!!!!!!!

Kabisa muungwana.

Kama kujali walemavu ni kusalimiana nao na kuwapa elfu 5 za sembe na maharagwe, and great part of the common voters buys that then u know how deeply the country is doomed.

Tunahitaji rais ambaye hata kama haonekani hadharani lakini anavuta strings na ku-press zile buttons zinazotakiwa na anajua wapi pa kushika ili impact ionekane mpaka kwa mtu wa chini kabisa..
 
Angekuwa anajali walemavu tangu aingie madarakani na kwa kipindi chote angetenda mambo ya wazi yenye manufaa kwa walemavu ambayo yangeliweza kumjengea umaarufu na kuonekana anajili maslahi ya walemavu kama anavyofanya Mzee Mengi kwa angalau kuwafanyia hafla kila mwaka! Yeye kama rais wa nchi angeliweza hata kuunda wizara maalum mathalan ya Walemavu na Waathirika wa Virusi vya Ukimwi n.k. ili angalau wawe na chombo ambacho kingeshughulikia matatizo yao moja kwa moja badala ya kungojea wakati wa uchaguzi ama wakati wa ziara (chache) alizowahi kufanya mikoani kutaka kutuaminisha kwamba anajali walemavu.

Picha yenyewe inamdhalilisha rais, tayari watu wameichukulia hiyo habari kwamba JK sasa amelemewa kiasi cha kuomba kura kwa kuketi mavumbini! Nasikitika kusema hata huyo mama mlemavu haonyeshi heshima yoyote kwa rais wake maana amemshika rais mguu kwa namna ambayo ni compromising!
 
Fedha nyingi zimetumika kuwavisha magwanda/jezi wanaodhaniwa ni mashabiki wa CCM ambao wengi wao wamebebwa na kuletwa mkutanoni.

Picha ya mgombea wa CHADEMA inaonyesha hakuna ghilba ya kuvisha wananchi 'jezi'. Inadhihirisha pia wamekuja mkutanoni kwa hiari yao bila kubebwa kwa usafiri wa dezo wa lori, daladala, bajaji, wala pilipiki, vinavyojazwa mafuta ya bure!
 
Mhe. JK ni mtu watu anawajali kweli walemavu hivi nyie wana JF MNAOSHANGAA ni wananchi wa nchi gani ? Kama ninyi ni watanzania kwanini mnashangaa mtu kujali walemavu,hamjui kuwa hili ni kundi maalum linalohitaji upendo Mhe JK ANALIJUA HILO NDIO MAANA ANAWAJALI WALEMAVU.

CHAGUA CCM CHAGUA JAKAYA MRISHO KIKWETE 2010
 
Mi naona wengine wameenda kusikiliza mziki.
Picha moja inaonyesha wanachama na chama chao nyingine inaonyesha wananchi wa tanzania.
 
SIMBA NA YANGA ...! lol

but on serious not..! MIKUTANO YA CCM HUWA INAHUDHURIWA SAANA NA WANAWAKE WENGI KULIKO WANAUME..!

WANAIPENDA SURA...hata kama wanachota maji kilometa 5 toka wanapoishi...
Hata kama wanalala watatu kitanda kimoja wakati wa kujifungua
hata kama infant mortality rate ipo juuuuu
hata kama wanafuata kumi mbaaaaaali

wao hawajali ili mradi SURA NI NZURI...!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom