Jk: Ni mt makini, ataachia ngazi kabla ya kuruhusu ya tunisia na misri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jk: Ni mt makini, ataachia ngazi kabla ya kuruhusu ya tunisia na misri

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Muke Ya Muzungu, Jan 31, 2011.

 1. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #1
  Jan 31, 2011
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Kwa wale wanaofuatilia maswala ya kisiasa nchini, nadhani mtakubaliana nami kwamba Rais wetu Mpendwa Dr. JK hawezi kuliacha taifa letu tukufu la Tanzania lipatwe na majanga ya Tunisia na Misri. JK ni mzalendo, kwa hiyo nina uhakika kwamba ataachia ngazi kabla ya taifa kuangamia. Swala la Dowans atalijibu kwa muda wake, kwani sasa hivi damu bado moto na mabaya zaidi aynaweza kujitokeza akiingilia hilo swala. Hii ndio sababu kubwa ya JK kuwa kimya, ila pia tambueni kwamba " kimya Kingi kina Kishindo" siku JK anaamka, Mafisadi yote yatajikuta Segerea
   
 2. n

  niweze JF-Expert Member

  #2
  Jan 31, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tena nachukua issue na hiyo statement hapo juu. JK ni mzalendo? Mbona tuna badilisha maana za meneno sasa? Kama Jk ni Mzalendo angekubali kwa Dowans, Richmond, Mauaji Arusha, Wizi wa Kura, na Maafa mengi ya CCM kwa miaka 50. Kama JK ahusiki juzi tu walikuwa kwenye kikao cha kamati kuu, kitu gani tunataka kusema juu JK kama sio msaliti wa Taifa nini? It's the end now...
   
 3. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #3
  Jan 31, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kweli Fisadi Original hata kifikra mzee. Yaani unasema kiongozi wa ki-Afrika ambaye uongozi kwake ni ajira aachie ngazi kabla watu hatujamkaba koo? Wewe naona unacheza vile.

  Utashangaa watu wapo wa kumdanganya kila dakika huko aliko kwamba aa mzee unajua huna tena haja ya kukimbia aibu yoyote kwani tumeshazungumza hata na yule rafiki yako Mchumi mwenzio Askofu Moses Kulola kakupigia chapuo kweli kweli na sasa mambo shwaaaari; si unajua tena Watanzania kwa kusahau mzee.

  Kwa kweli mzee, ilibidi tu tukawaongezee dozi ya Ze Komedi kwa wiki mara tatu wacheeeke wavunjike mbavu na kuachia kile kitenesi chako cha Dowans kitoke tuu maana paymenti voucha tumeshapeleka kule benki kuu ni kusaini tu!!

  Kupe mpaka kubanduliwa mzima mzima ndio ng'ombe kupata kupumua.
   
 4. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #4
  Jan 31, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Thubutuuuuuuuu!
   
Loading...