JK ni Kanali wa JWTZ ama ni Daktari? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK ni Kanali wa JWTZ ama ni Daktari?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Bill, Oct 24, 2010.

 1. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #1
  Oct 24, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,163
  Likes Received: 1,251
  Trophy Points: 280
  Mwalimu JK Nyerere baada ya kuachana na ualimu aliendelea kuitwa Mwalimu, hata pale alipopata Udaktari, alibaki kuitwa Mwalimu na alisisitiza hivyo.

  Kulikoni Jakaya Kikwete kujitukuza/ kutukuzwa kwa udaktari wa heshima kiasi hicho? Au ndo namna ya wanajeshi wote kujipa ujiko kama Field Marshal/execlency Dr. Idd Amin Dada. Mbona hataki kujipambanua kwa kutumumia ukanali wa jeshi - Kanali Jakaya Mrisho Kikwete na kama anaona hiyo haifai basi ajipandishe cheo kuwa General JK.

  Maanake ni kila siku vyombo vya habari hasa vya Umma ni Dr, Dr, Dr!!!!!!!!! what for, huu udokta wa kupewa kishkaji unatufaa nini waTZ. We need material things..... ala.

  Na ninyi waandishi wa habari hasa wa vyombo vya UMMA(SU) acheni kushabikia vitu kama hivyo wakati mnatafuna kodi zetu. Mpeni heshima huyu rais wetu kwa professional yake ya awali na ambayo kaisotea kweli, yaani Kanali Jakaya Mrisho Kikwete kama ilivyo kwa wenzenu wa Libya Kanali Muamar Gadafi, mbona iko poa tu kuliko kudandia vitu vikubwa ambavyo haviendani na uwezo wako kiutendaji.

  Mbona akina Clinton, Bush na Obama wanatesa tu bila kujipachika udaktari wa heshima? Si wangeweza kujipa udokta hadi 7X70? Haisaidii kitu.

  Anyway ni Mawazo tu, mnaweza kufanya mnavyotaka hata ikiwa kumuita mungu wenu ili mradi mikono yenu na wategemezi wenu inaenda kinywani.
   
Loading...