JK ni genius, Matukio yote ni Upepo tu na yamepita.

kapotolo

JF-Expert Member
Sep 19, 2010
3,727
2,213
Kikwete akisema sasa namuamini, Matukio yafuatayo ingawa yalitikisa Nchi, lakini yalikuwa upepo tu na yamepita.

1. Waligoma waalimu na madaktari, watu wakafa wanafunzi wakakosa masomo, hata bila madai yao kushughulikiwa ukawa upepo tu na ukapita.
2. Akakamatwa Ulimboka, akateswa na kukaribia kutolewa uhai, wanaharakati na watanzania wakaja juu, kova akaendesha movie yake, kumbe nao ulikuwa upepo tu na umepita.
3. Wakauawa watu maeneo mbali mbali na polisi kama Arusha, Morogoro na kule Iringa ambapo mwandishi Daudi Mwangosi (RIP) aliuawa na polisi, watu wakapiga makelele sana, wengine wakatishia kuwashitaki viongozi wakuu wa jeshi la polisi The Hague, he.. nao ukawa upepo, umepita, tumemsahau Mwangosi na maisha yanaendelea.
4. Balali, akiwa shahidi mkuu wa wizi ya babilioni kwenye account ya EPA, akatoweka na kwenda kufariki Marekani katika mazingira ya kutatanisha, ingawa mpaka sasa kuna mtu anatweet akijifanya ni Balali lakini labda alikufa. Utata wa kifo chake ulikuwa gumzo kubwa nchini, lakini gumzo hilo lilikuwa upepo tu nao ukapita.
5. Wabungwe wakaomba rushwa, wakajiingiza kwenye biashara na shirika wanalolisimamia, ikaundwa tume ya kuchunguza, kumbe tume yenyewe ilikuwa ni ya kupitisha upepo, wamesafishwa na upepo umepita.
6.Naamini na mtakuja kuniambia, sakata la mabilioni ya Uswiswi ni upepo tu nao utapita.

Najua yapo mengine lakini haya ni moja ya matukio ambayo mwisho wake ulikuwa kama upepo na ukapita, miti ikasimama, maisha yanaendelea.

Watanzania tumekuwa wepesi wa kuacha na kusahau mambo makubwa haraka na kirahisi, nadhani JK anawajua watanzania ndio maana ana uhakika tukio lolote hata liwe kubwa kiasi gani, litasemwa na mwishowe litasahaulika. Alishasema kelele za mlangoooooooo......!!! Ukitaka kulaaaaa............!!! W/end njema.
 
Nafikiri hukwenda sunday school,kuina wimbo tulikuwa tunafundishwa ambao unaimbwa hv,,'neno litasimama,neno litasimama,mambo yote yatapita lakini neno litasimama neno'
 
Kweli ndugu yangu, hata Mkapa Umr. No comment umesaidia sana. Kama angukua napambana na Magazeti, saa hizi angekua india anatibiwa, nyie bwabwajeni yeye anakula kukua kwa mrija soda kwa umma.
 
pamoja na kwamba yanaonekana yanapita lakini bado ukweli utabakia palepale na hukumu yake imeanza kuonekana na itaonekana zaidi 2015 na mbeleni. Je ccm bado ina mvuto kama uliokuwepo miaka 7 iliyopita? na kadri muda unavyoyoma inazidi kukimbiwa.
 
mi nishamshitukia, huyu mzee lazima kuna kitu anategemea huwa hasemi bure ukishaona anatoa statement kali kama ule mkwara aliompiga Nimrodi M basi ujue kazi kwisha and not otherwise.
 
Angalieni wakuu JF nayo isijekuwa UPEPO nayo ikaenda zake hiyoo kusikojulikana!
 
Alafu cha kusikitisha kuna watu humu pia wanakubali upepo huo. Anapotokea mwanasiasa kuhoji hayo wanasema 'huo wimbo tumeuchoka hana jipya'. Humu JF wapo tele. Kama huamini angalia mada ya kujadili kauli ya katibu wa CHADEMA jana.Kikwete ashawasoma akili.
 
Kikwete akisema sasa namuamini, Matukio yafuatayo ingawa yalitikisa Nchi, lakini yalikuwa upepo tu na yamepita.

4. Balali, akiwa shahidi mkuu wa wizi ya babilioni kwenye account ya EPA, akatoweka na kwenda kufariki Marekani katika mazingira ya kutatanisha, ingawa mpaka sasa kuna mtu anatweet akijifanya ni Balali lakini labda alikufa. Utata wa kifo chake ulikuwa gumzo kubwa nchini, lakini gumzo hilo lilikuwa upepo tu nao ukapita

Naona unaandika mambo usiyoyajua.

Nani alikwambia kwamba Ballali alitoweka kwneye mazingira ya kutatanisha?
 
Hakuna Rais kama jk anajua kudeal na mambo.Angalia 2015 chadomo wanaweza wakapata jimbo moja tu.
 
Naona unaandika mambo usiyoyajua.

Nani alikwambia kwamba Ballali alitoweka kwneye mazingira ya kutatanisha?
Wewe ni kati ya watu mnaojua alipo balali, whether kafa kweli au changa la macho, who knows, may be maundumula.
 
Wewe ungeshaurije nini kifanyike ili yasipite?
Tuamke watanzania, tumelala mno, tuache woga. Tuhoji mambo kwa kumaanisha, tuseme tunayoyamaanisha, wanaharakati na wahabari waache nguvu za soda kufuatilia mambo, mkwara kidogo kimya. Vinginevyo kichancheda nawe ni upepo tu utapita.
 
Nafikiri hukwenda sunday school,kuina wimbo tulikuwa tunafundishwa ambao unaimbwa hv,,'neno litasimama,neno litasimama,mambo yote yatapita lakini neno litasimama neno'
Hivi kweli eee, nadhani JK ndio anatumia huu wimbo!!!
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom