Jk ndani ya Arusha Wilaya ya Longido! Agawa ng'ombe wapatao 25,000/=, Imekaaje?

Huyu ndiyo kiongozi ametoa uhuru wa kuongea kwa kila mtu na yuko karibu na wananchi kwa kila jambo anawapenda sana watanzania wote yuko pamoja nao katika shida na raha,Raisi msikivu ata kambi ya upinzani bungeni wamethibitisha hilo,hongera sana Jakaya M kikwete mungu akubariki sana kwa mazuri yote wachache tu hawajuhi mazuri yako na si kama hawajuhi kweli wanajifanya wanapotosha umma ila watakukumbuka utakapomaliza uongozi wako,CCM daima!

Nafikiri kati ya watumwa wa chama wee ni kati yao!

Wewe wapelekee taarifa hii ya kwmb raia wameamua kupokea chochote mletacho iwe posho ya chakula,iwe ya ng'ombe,iwe ya hata mbuzi wa maziwa na kondoo wao wanaipokea tu kwn wanajua ni kodi zao ya haki wamerudishiwa.

Hila na njama yote ya magamba tunayo mifukoni tayari!
Yao ni ngumu sana kwa Watanzania!
 
Aaah mkuu unaandika mifugo kama hela? Eti 25000/= tafadhali bwana!
 
JK anataka kumdanganya nani? Tunajua anafanya hivyo kuwahadaa wananchi wa Arusha hususan wale wa Arumeru Mashariki ambao wanajiandaa kwa uchaguzi wa mbunge. Siku zote alikuwa wapi?
 
JK anataka kumdanganya nani? Tunajua anafanya hivyo kuwahadaa wananchi wa Arusha hususan wale wa Arumeru Mashariki ambao wanajiandaa kwa uchaguzi wa mbunge. Siku zote alikuwa wapi?

Huyu papa fisadi hila na mbinu zake tunao mfukoni Kamanda wangu!
Mbinu hii anayoifanya kwa wanainchi ni kwamba anajidanganya na chama chake tu.

Huko Longido alikokuwepo jana ni wiliya ya wafugaji tu!
Hata dhubutu kuja Arumeru mashariki kwani vijana wa huko ambao ndiyo nguvu ya taifa hawataki hata kuwaona hawa mapapa wameza kodi ya wanainchi.
Mi nawashangaa sana ktk hali ninayosikia ya kwamba EL ameachiwa kazi pale Arumeru mashariki ya kuhakiki ushindi unapatikana.

Mi nasubiri kwa hamu kubwa nione ushindi huu utapitia wapi,,,,,,,,,,,Ama wanafikiri hapa ni pale Igunga walikochakachua na kuwamwagia watu wa MUNGU tindi kali.
Huku ni kanda nyingine.

Jk na chama chako mwisho wenu waja!
 
huko arusha si ndio kuna uchaguzi wa Arumeru Mashariki?............tafakari. Mnakumbuka chakula cha msaada Igunga wakati wa uchanguzi mdogo?
 
wa ndugu mm ni mwana jf mpya kama maisha ya kibongo yalivyo mapya,kwanza nawasalimu Aslm alykm.
 
Hivi jamani,mbona naona kama nipo ndotoni,yani wahanga wa gongo la mboto hawajakamilishiwa chao yeye kafumba macho kapeleka kindoo cha maji mtoni?Mhh.
 
Nampa Hongera kwa kugawa mifugo kwa hao wafugaji maana umaskini uliongezeka sana katika maeneo yao!!
Heko JK !!!
 
Akirudi aende na gomz akawaplz kisha awapoze,maana kuna waliolipwa mfuko wa cement bila pesa ya fundi,hata'mamake profecer j yalimkuta,nasikia yeye alilipwa tofali tuu,teh teh teh.
 
Rais anajali wananchi siyo kama kina Mbowe wanaokula posho tu.
8E9U4047.jpg
 
Huyu ndiyo kiongozi ametoa uhuru wa kuongea kwa kila mtu na yuko karibu na wananchi kwa kila jambo anawapenda sana watanzania wote yuko pamoja nao katika shida na raha,Raisi msikivu ata kambi ya upinzani bungeni wamethibitisha hilo,hongera sana Jakaya M kikwete mungu akubariki sana kwa mazuri yote wachache tu hawajuhi mazuri yako na si kama hawajuhi kweli wanajifanya wanapotosha umma ila watakukumbuka utakapomaliza uongozi wako,CCM daima!
images
 
Kuna kutoa pole kama mtu binafsi kuna kuwafariji watu waliopatwa na janga kama kiongozi mkuu ,pia kuna kitengo cha maafa kipo ofisi ya waziri mkuu .sasa basi kuna muda wa kumfariji mtu ukisha pita haifai au haileti maana ya pole .pili kuna kitengo cha maafa hakikuona kama ule ukame ni janga hadi wasubiri mkuu awakumbushe .lakini pia kisiasa ni mwanzo wa kufika arumeru ambako hivi karibuni kutakuwa na uchaguzi mdogo .
 
Nimekuta hii habari kwenye Blog ya Issa Michuzi, naomba wadau tuisome na kuitafakari. Hii ina tofauti gani na mabilioni yaliyotolewa mwaka 2006 na Mhe. JK kwa ajili ya kuwezesha mikoa mkiuchumi? Je mabilioni hayo yameleta faida zipi katika ukuaji wa uchumi na bado yapo ama yameishia wapi.

Chanzo: MICHUZI: JK akabidhi kifuta machozi cha ng'ombe longido, azindua mradi wa uwezeshaji mifugo

Kwanza ninaomba nimpongeze Mh. Rais kwa kutimiza moja ya ahadi zake za mwaka 2010, kwa jamii ya wafugaji wa kimasai.

Na kwa kweli nia yake inawezakuwa ni nzuri, but tatizo utekelezaji wake ni wa kisiasa zaidi (na hivi uchaguzi wa arumeru umekaribia!). Mambo ya kibiashara hayataki Siasa, bali yanazingatia utafiti na mahitaji ya soko/mazingira kwa wakati muafaka. Ushahidi wa hili ni hapo ulipohoji juu ya yale mabilioni ya JK.

Hebu jiulize, kama unataka kunipa mkopo bila kujua ujuzi wangu/uzoefu juu ya biashara kwa nini usinipe mafunzo ya ujasiriamali kwanza? Kipi kinapaswa kutangulia, mafunzo au mikopo? (Hilo ni moja). Jingine ... Hili ndio moja ya chanzo cha kuanguka kwa program ile. Na wanasiasa nao walitia mikono mno cha sabtika mikopo ile.
 
Viongozi wa kabila la Kimasai(Laigwenani) wakimpa Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete zana za kijadi za uongozi mkuki na fimbo wakati wa hafla ya kukabidhi ng’ombe iliyofanyika wilayani Longido jumapili.
 
Viongozi wa kabila la Kimasai(Laigwenani) wakimpa Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete zana za kijadi za uongozi mkuki na fimbo wakati wa hafla ya kukabidhi ng’ombe iliyofanyika wilayani Longido jumapili.
Hivi kwani JK anagombea tena 2015?
 
Back
Top Bottom