JK names 11 new High Court judges!!!

Jibu unalo. Inawezekana nia yake siyo kupendelea ila ni kutaka kuleta urari! Ila langu ni moja tu, usilete urari katika masuala ya haki maana kila watu wana priorities zao. Katika sheria wakristu wapo wengi and the ratio inaweza kuwa mwislamu mmoja kwa wakristo kumi (10%) sasa ukitaka kila ukiteua majaji wawemo waislamu kadhaa in almost equal proportion ni tatizo. Same with gender, ratio ni even worse!

Umejuaje kama jibu ninalo? ndio hivi unaweka hisia kwenye thoughts na action za watu wengine. Kama wanaweza asiwaapoint kwa vile watu watasema anaweka proportions za udini na jinsia, basi ingekuwaje kama hao majaji wateule wangekuwa wote wanaume, wote wanawake, au wote wakristo au wote waislamu? hakuna urari bali equal opportunities to the qualified ones. Pongezi zenu majaji haki itendeke.
 
binafsi simpongezi kikwete kwa kuteua hao majaji, yeye anatangaza tu uteuzi lakini kuteuliwa na mchakato mzima huanzia kwa majaji wengine na kupitishwa na jaji kiongozi kama sikosei then JK anapitisha uteuzi. Uteuzi wa mawaziri hufanyika kwa utashi wa Rais tofautina majaji wanavyoteuliwa.
 
Jibu unalo. Inawezekana nia yake siyo kupendelea ila ni kutaka kuleta urari! Ila langu ni moja tu, usilete urari katika masuala ya haki maana kila watu wana priorities zao. Katika sheria wakristu wapo wengi and the ratio inaweza kuwa mwislamu mmoja kwa wakristo kumi (10%) sasa ukitaka kila ukiteua majaji wawemo waislamu kadhaa in almost equal proportion ni tatizo. Same with gender, ratio ni even worse!

Kwanza nchi haina dini kwa mjibu wa katiba tuliyo nayo.Hata kama unaabudu mawe,mjusi,ng'ombe mlima n.k huwezi kuingiliwa uhuru wako kama hujavunja sheria.
Pili majina haya ya viongozi si kigezo kuwa sasa huyu ni mdini kweli kweli na anafuata misingi ya dini husika.Ukiwapima watu ktk kuongoza kwa majina ya kiislam na kikristo huwatendei haki.Huko kwenye uongozi ni utata tu.
Tunachopima ni uadilifu wao ktk uongozi,je dhamana waliyopewa watasaidia hili Taifa maskini lijikwamue kimaendeleo?
Mbona Rais mstaafu na mkewe walikuwa wanaingia kanisani tena viti vya mbele kabisa na hata mama alikuwa mzee wa usharika lakini ktk uongozi wao wameuteteaje ukristo wao kwa kuwa waaminifu na wazalendo kwa nchi hii?
Kuna viongozi wenye majina ya kiislam kama Nazir karamage et al wameuteteaje uislam walivyokuwa ktk uongozi wa nchi hii?Tusichanganye vitu hivi tena kwa kuangalia majina yanayoanza na uislam na ukristo.
 
Mimi nadhani nijiondoe katika kuchangia mada hii maana naona watu wanatumia ushabiki bila kuleta hoja yenye mantiki. Nani hajui kuwa uteuzi wa majaji Tanzania haufuati uadilifu, uwezo au hata experiences? Nitawapa mifano miwili mitatu. Wakati Amir Manento alipoteuliwa kuwa jaji kiongozi (Mkuu wa Majaji wa Mahakama Kuu) alikuwa na miaka mitano tu kazini na alikuwa anachemka kweli kwenye hukumu zake akiwa Songea. Katika kipindi cha uongozi wake hakuwahi kutoa hukumu ya maana kama walizokuwa wakitoa waliomtangulia (Ukiacha Amir Msumi ambaye naye aliweka basi tu). Soma vitabu vya ripti za kesi hakuna hukumu ya maana aliyotoa huyu mtu. Wakati akiteuliwa walikuwepo majaji wenye uzoefu kama Mroso, Msoffe, Rutakangwa, Kimaro etc. Wakaachwa. Kwa kuzingatia uwezo wao, wakateuliwa kuwa majaji wa Mahakama ya Rufani na kumwacha huko chini hadi alipostaafu mwaka huu. Akamfuati Salum Masati ambaye amekaa kwenye ujaji kwa muda wa miaka miwili na ushee hivi. Wapo Majaji ambao ni wazoefu na wenye uwezo mkubwa kumzidi wameachwa. Hii yote ni kwasababu ya udini ili kama Jaji Mkuu ni Mkristo basi Jaji Kiongozi awe Muislamu. Amiri Mruma ameteuliwa mwaka jana kuwa Jaji akiwa na uzoefu mdogo mno.

Ukija kwa Wanawake, hakuna mtu anayeweza kunihakikishia kuwa yule Jaji Mwanaisha au Iman Aboud wanauwezo kuliko mahakimu au Mawakili ambao hawakuteuliwa. Uzoefu na uwezo wao ni very questionable. Lakini hata kwa ujumla wake, uteuzi wa wanawake na kuwaacha mawakili na Mahakimu wazoefu kama vile Shio, Ndunguru, Kadasso, Malaba, Matupa nk. siyo kwa ajili ya uzoefu, ni upendeleo.

Kwa upande wa wanawake
 
sijaridhika na baadhi ya majina. hapa ni kubebana tu wengi wao tunawajua uwezo wao mdogo ndio maana hawajaandika kila mmoja anaoka wapi na alikuwa nani kabla ya uteuzi.
 
Mimi nadhani nijiondoe katika kuchangia mada hii maana naona watu wanatumia ushabiki bila kuleta hoja yenye mantiki. Nani hajui kuwa uteuzi wa majaji Tanzania haufuati uadilifu, uwezo au hata experiences? Nitawapa mifano miwili mitatu. Wakati Amir Manento alipoteuliwa kuwa jaji kiongozi (Mkuu wa Majaji wa Mahakama Kuu) alikuwa na miaka mitano tu kazini na alikuwa anachemka kweli kwenye hukumu zake akiwa Songea. Katika kipindi cha uongozi wake hakuwahi kutoa hukumu ya maana kama walizokuwa wakitoa waliomtangulia (Ukiacha Amir Msumi ambaye naye aliweka basi tu). Soma vitabu vya ripti za kesi hakuna hukumu ya maana aliyotoa huyu mtu. Wakati akiteuliwa walikuwepo majaji wenye uzoefu kama Mroso, Msoffe, Rutakangwa, Kimaro etc. Wakaachwa. Kwa kuzingatia uwezo wao, wakateuliwa kuwa majaji wa Mahakama ya Rufani na kumwacha huko chini hadi alipostaafu mwaka huu. Akamfuati Salum Masati ambaye amekaa kwenye ujaji kwa muda wa miaka miwili na ushee hivi. Wapo Majaji ambao ni wazoefu na wenye uwezo mkubwa kumzidi wameachwa. Hii yote ni kwasababu ya udini ili kama Jaji Mkuu ni Mkristo basi Jaji Kiongozi awe Muislamu. Amiri Mruma ameteuliwa mwaka jana kuwa Jaji akiwa na uzoefu mdogo mno.

Ukija kwa Wanawake, hakuna mtu anayeweza kunihakikishia kuwa yule Jaji Mwanaisha au Iman Aboud wanauwezo kuliko mahakimu au Mawakili ambao hawakuteuliwa. Uzoefu na uwezo wao ni very questionable. Lakini hata kwa ujumla wake, uteuzi wa wanawake na kuwaacha mawakili na Mahakimu wazoefu kama vile Shio, Ndunguru, Kadasso, Malaba, Matupa nk. siyo kwa ajili ya uzoefu, ni upendeleo.

Kwa upande wa wanawake
Jobo, though majority are accusing you but you're talking sense and it seems you knew the judicial system of Tanzania whether we like it or not!

Inatupasa kubadilika na kuhacha kufanya mambo yetu kwa hisia za udini, hasa sehemu nyeti ambazo 'professionalism' inatakiwa uchukue mkondo wake. Lazima tuteue watu kwa elimu na uzoefu kazini, ushabiki au kuoneana haya utatupeleka pabaya!!
 
binafsi simpongezi kikwete kwa kuteua hao majaji, yeye anatangaza tu uteuzi lakini kuteuliwa na mchakato mzima huanzia kwa majaji wengine na kupitishwa na jaji kiongozi kama sikosei then JK anapitisha uteuzi. Uteuzi wa mawaziri hufanyika kwa utashi wa Rais tofautina majaji wanavyoteuliwa.

.......Mama, uliyoyasema hapo juu yana ukweli sana, si kweli kwamba Rais anakurupuka tu na kuteua majaji.......kwanza kunatokea ombi ambalo hutolewa na Jaji Mkuu kwa Rais juu ya uhitaji (need) wa majaji zaidi, kulingana na bajeti Jaji Mkuu akipewa kibali mchakato mzima (ambao ni siri) huanza miongoni mwa kamati za majaji waliopo wakishikishirikiana na watu kama TLS...........kwa kuwa hii ni Tanzania inawezekana kukawepo na pendekezo moja au mawili direct toka kwa Rais......wote waliopendekezwa hufanyiwa vetting na mapendekezo ya mwisho ya kamati maalum (ikiongozwa na Jaji Mkuu) huwasilishwa kwa Rais kwa uteuzi rasmi,

....sijui hizi hisia za mambo ya udini na gender yanatokea wapi.......i mean that is very low kwa heshima ya JF
 
......ikiwa ni katika kulinganisha idadi ya Wkristo na Waislamu! Come on... in the legal profession u cannot equate religious affiliation. Ninaamini kuwa Nyangalika na Mruke wameteuliwa kwa misingi hiyo!

Huo ni ushamba na ufinyu wa mawazo, kila kitu UDINI. Hivi umekosa hoja za maana unakimbilia UDINI. watu kama nyie ndio mnaotufanya hatuendelei. Watu kama WEWE mkipewa madaraka ndiyo mtakilimbilia kuanzisha udini ili iwe NGAO kwako
 
amir mruma hata hajui kuandika judgment mimi naungana na JOBO. kingereza chake utaona aibu. maajabu wamemhamisha mahakama kuu sasa wamempeleka Commercial Division. mimi sio mdini lakini sioni vigezo vya kumteua mtu huyu na mwenzie massati bila kusahau nyangarika kassim bure kabisa
 
Huo ni ushamba na ufinyu wa mawazo, kila kitu UDINI. Hivi umekosa hoja za maana unakimbilia UDINI. watu kama nyie ndio mnaotufanya hatuendelei. Watu kama WEWE mkipewa madaraka ndiyo mtakilimbilia kuanzisha udini ili iwe NGAO kwako

yaelekea huyo kaukosa huo ujaji, chuki binafsi haijengi!
 
.......Mama, uliyoyasema hapo juu yana ukweli sana, si kweli kwamba Rais anakurupuka tu na kuteua majaji.......kwanza kunatokea ombi ambalo hutolewa na Jaji Mkuu kwa Rais juu ya uhitaji (need) wa majaji zaidi, kulingana na bajeti Jaji Mkuu akipewa kibali mchakato mzima (ambao ni siri) huanza miongoni mwa kamati za majaji waliopo wakishikishirikiana na watu kama TLS...........kwa kuwa hii ni Tanzania inawezekana kukawepo na pendekezo moja au mawili direct toka kwa Rais......wote waliopendekezwa hufanyiwa vetting na mapendekezo ya mwisho ya kamati maalum (ikiongozwa na Jaji Mkuu) huwasilishwa kwa Rais kwa uteuzi rasmi,

....sijui hizi hisia za mambo ya udini na gender yanatokea wapi.......i mean that is very low kwa heshima ya JF

Soma sheria ya Majaji ujue wanateuliwaje, usijisemee tu na kupotosha wengine
 
Huo ni ushamba na ufinyu wa mawazo, kila kitu UDINI. Hivi umekosa hoja za maana unakimbilia UDINI. watu kama nyie ndio mnaotufanya hatuendelei. Watu kama WEWE mkipewa madaraka ndiyo mtakilimbilia kuanzisha udini ili iwe NGAO kwako

Umeingia leo na matusi! Ubarikiwe sana. but you do not know what you are talking about!
 
yaelekea huyo kaukosa huo ujaji, chuki binafsi haijengi!

Ujaji wanateuliwa wanasheria na mahakimu, mie siye mmoja wao. Hata kama ningekuwa mwanasheria nisingependa kuwa jaji wakulipwa visenti vichache na kunyimwa uhuru miaka yako yote!
 
Ingekuwa vema kama mtu ambaye ana-data za walioteuliwa kuwa majaji interms of qualification, experience and competence na vetting iliyotumia ili ku-relate na hoja ya uteuzi wa "upendeleo" wa hawa majaji badala ya kuendelea kujaji uteuzi aliofanya JK kwa HISIA HISIA tu. Bila kufanya hivyo kutakuwa na ubishiiiiiiiiiiiiiiiiii bila mwisho.
 
Vipi mkuu, unaweza kutuwekea hiyo sheria hapa ili tujue mchele na pumba ni ipi hapa.

Soma hii sheria ya Tume ya Mahakama pamoja na Katiba kuhusu uteuzi wa majaji.

[media]http://parliament.go.tz/Polis/PAMS/Docs/2-2005.pdf[/media]
 
Back
Top Bottom