Jk na woga wa wagombea kutoka bara

Warue

JF-Expert Member
Aug 9, 2012
423
809
Kwa mara nyingine tena Jk amevunja katiba ya chama kwa kulazimisha maamuzi yasiofuata katiba na demokrasia ndani ya chama. Ikumbukwe kuwa Uozo ndani ya bunge la sasa imetokana na maamuzi ya JK ya kuzuia uhuru wa kugombea nafasi ya spika mwaka 2010 wakati wa uchaguzi wa spika. Sifa ya mgombea mwanamke alileta kwa lengo la kumkwepa Samwel Sita na hivyo tukapata spika mlinda mafisadi na uozo ndani ya serikali.

Safari hii wagombea wa nafasi ya mwenyekiti UVCCM taifa kutoka Bara wamezuiwa kuchukua fomu za kugombea eti nafasi hiyo ni maalum kwa watu wa zanzibar. Ikumbukwe kuwa mwaka 2008 nafasi ya mwenyekiti uvccm taifa ilipelekwa zanzibar kabla ya mshindi wa nafasi hiyo kuvuliwa madaraka baada ya kutofautiana na mtoto wa Rais. Haiingii akilini kama sifa za mgombea inaweza kuangaliwa kwa mahali anakotoka, hii ni kinyume kabisa na katiba ya chama na hata demokrasia ndani ya chama. Kwa mtindo huu, ushindani ni sifuri na hivyo uwezekano wa kumpata mgombea mwenye uwezo no mdogo sana. Wanachama amkeni! chama kinazamishwa kwa maksudi.
 
Wewe sio mwana CCM damu, mbona unaleta mambo yenu ya chumbani hapa sebukeni?!.

Kwa kukusaidia tuu, kitendo cha JK kulazimisha mgombea wa uenyekiti UV- CCM atoke Zanzibar ni cha kuungwa mkono na wana CCM wote wenye mapenzi mema na chama chao, wataunga mkono!

Tena mna bahati amri hiyo ni kwa UV-CCM pekee, ilipaswa itolewe na kwa UWT na Wazazi kwa sababu hizo ndizo nafasi za juu za mwisho Mzanzibari anaweza kushika ndani ya CCM and that is the only way Wazanzibar watatulia kwa sababu kamwe hawawezi tena kupewa uenyekiti!.

Hii pia inamaani Mzanzibari hawezi tena kupewa urais wa muungano!.

Poleni.

Pasco!.
 
Hakuna namna ya kuiokoa CCM kwasasa, ni kusubiri maziko yake rasmi 2015.
 
Lame excuse, nafasi za juu za chama za kufanya maamuzi magumu wanapewa vila.za kwa ajili ya utaifa??

Kwa nini wasipewe nafasi za chini kidogo lakini hapo kwenye cheo cha juu apewe mtu timamu.

CCM inauwawa na vila.za wasojua walitendalo, kwanza hata aliyeshinikiza mzanzibari apewe kajipambanua kiwangi chake cha uerevu.

Ujinga mtupu, hizi siasa zenu kaeni nazo vyumbani mnanitoa povu bure.
 
utampaje mtu kazi kubwa wakati yeye haamini katika kazi???

Anaogopa kuchoka mwili na kutumua akili??

Yaani hadi 2015, sijui itakuwaje.

Afu kama wanasiasa waliyo unafiki tu, ukute kuna ambao hawaafiki lakini akija anayeshinikiza wanatabasamu tu hawasemi lolote.

Agrrrrrr! ! !
 
Kwa mara nyingine tena Jk amevunja katiba ya chama kwa kulazimisha maamuzi yasiofuata katiba na demokrasia ndani ya chama. Ikumbukwe kuwa Uozo ndani ya bunge la sasa imetokana na maamuzi ya JK ya kuzuia uhuru wa kugombea nafasi ya spika mwaka 2010 wakati wa uchaguzi wa spika. Sifa ya mgombea mwanamke alileta kwa lengo la kumkwepa Samwel Sita na hivyo tukapata spika mlinda mafisadi na uozo ndani ya serikali.

Safari hii wagombea wa nafasi ya mwenyekiti UVCCM taifa kutoka Bara wamezuiwa kuchukua fomu za kugombea eti nafasi hiyo ni maalum kwa watu wa zanzibar. Ikumbukwe kuwa mwaka 2008 nafasi ya mwenyekiti uvccm taifa ilipelekwa zanzibar kabla ya mshindi wa nafasi hiyo kuvuliwa madaraka baada ya kutofautiana na mtoto wa Rais. Haiingii akilini kama sifa za mgombea inaweza kuangaliwa kwa mahali anakotoka, hii ni kinyume kabisa na katiba ya chama na hata demokrasia ndani ya chama. Kwa mtindo huu, ushindani ni sifuri na hivyo uwezekano wa kumpata mgombea mwenye uwezo no mdogo sana. Wanachama amkeni! chama kinazamishwa kwa maksudi.
'

Mkuu we ni chama gani? Maana unaonekana unakisaliti chama kwa maneno hayo ya rangi hapo juu! Na Rais wa JMT nimesikia kuwa lazima atoke Zenji je, jambo hili ni kweli?
:lol:
 
Chama ni sisiemu, uliza kambi?
 
Huu utarabu wa kuchagua viongozi kwa kuangalia jinsi, maeneo waliyotoka utaleta madhara makubwa sana. It is unconstitutional na inamuondolea mwananchi wa kawaida haki yake ya msingi ya kuchagua kiongozi anayeona anafaa! Na pia upo uwezekano madhara yake yakawa ni kuibuka kwa ukabila.

Sidhani kama UVCCM will survive kama kweli watachagua kiongozi kwa kuzingatia anatoka wapi!
 
Huyu alitumwa na mafisadi akagombee sasa maji yamemwagika anaanza kuhangaika.sisi jf hatuna mkataba na wezi,ishia huko huko.
 
Kawaeleze ccm wenzako hapa unapoteza muda,sana unajiumbua na kuanika ulimbukeni wako
 
Huu utarabu wa kuchagua viongozi kwa kuangalia jinsi, maeneo waliyotoka utaleta madhara makubwa sana. It is unconstitutional na inamuondolea mwananchi wa kawaida haki yake ya msingi ya kuchagua kiongozi anayeona anafaa! Na pia upo uwezekano madhara yake yakawa ni kuibuka kwa ukabila.

Sidhani kama UVCCM will survive kama kweli watachagua kiongozi kwa kuzingatia anatoka wapi!

we una hasira ya kuukosa uenyekiti acha kutuzingua apa
 
Mmehangaika huko facebook yamewashinda mmeamua kuja jf,hatuna muda kujadili njaa zenu za madaraka hapa,mkamalizane uko uko.
 
Lakini huyu tutusa asijekutulazimishia na wagombea wa nafasi ya rahisi wa JMT atoke visiwani? Huu mwendelezo unatia shaka huu!
 
Mmehangaika huko facebook yamewashinda mmeamua kuja jf,hatuna muda kujadili njaa zenu za madaraka hapa,mkamalizane uko uko.

moha mie sipo fb, ufahamu kwamba kosa lolote ndani ya chama chochote inawagarimu watanzania wote bila kujali chama. CCM ikifanya kosa kubwa kama hili hakuna anayesalimika na wewe ukuwemo. aangalia yanayotokea kwa makinda
 
Si kweli, mi si mgombea wa nafasi yoyote ile Bali nachukia ufisadi wa demokrasia na maamuzi kufanywa na kichwa kimoja.
 
utampaje mtu kazi kubwa wakati yeye haamini katika kazi???

Anaogopa kuchoka mwili na kutumua akili??

Yaani hadi 2015, sijui itakuwaje.

Afu kama wanasiasa waliyo unafiki tu, ukute kuna ambao hawaafiki lakini akija anayeshinikiza wanatabasamu tu hawasemi lolote.

Agrrrrrr! ! !
pole sana,ndo chama chenu kilivyo.
 
Back
Top Bottom