LOWASSA NA ROSTAM NI MADONI wa BONGO MAFIA
Kwa muda mrefu watu mbalimbali haswa wanahabari wanofuatilia duri za kisiasa hapa nchini, wamekua akinukuliwa wakidai kwamba URAIS WA JK NI WA UBIA jambo ambalo mwenyewe alilisikia na akalikana hadharani kwa kudai kwamba U-raisi wake hauna ubia na mtu yeyote.
Waswahili wana usemi usemao kwamba lisemwalo lipo na kama halipo pasi lipo njiani linakuja Madai ya JK kwamba Uraisi wake hauna ubia hayaendani na matendo yake au matendo ya wale wanaodaiwa kwamba ni Wabia wake. Lakini kabla hatujafika hatua ya kutathmini matendo yanayotia mushkeli kukana kwa JK kwamba Uraisi wake hauna Ubia, nadhani kuna haja ya kuangali kwa undani zaidi, madai na vigezo vya wachuguzi wa kisiasa vilivya tumika katika kuwakilisha madai yao, na kuwainisha wabia wenyewe, tukiangalia msingi na malengo ya wabia wenyewe katika huo ubia wao.
Utatu Wakifisadi:
Wachunguzi wanadai kwamba: Hapo mwanzo (1995) JK aliingia ubia wa kutafuta Uraisi na Bw Lowassa ubia ambao hakufika mbali kwa sababu za juhudi binafsi za Mwalimu Nyerere.
Mara tu baada ya chaguzi za 1995 Lowasaa alitupwa nje (hakupata uwaziri wowote) kutokana na kufunuliwa kwa matendo yake machafu na Hayati Mwl Nyerere. Hapo ndipo chimpuko la utatu lilipojitokeza kwani kwa sababu ambazo sasa wengi tunazijua bwana Roatam Azizi alijiunga rasmi katika Ubia wa bwana JK wakutafuta URAISI.
Wachunguzi wanadai kwamba dalili zote zinaonyesha na kwa sasa wanaweza kudai kwamba wabia hawa aliigia katika utatu huo kwa malengo tofaulti; Jk kwania ya kuleta maendeleo ya nchi na watu wake; .Lowassa kwa nia ya kushika nchi, kumfanya awe Mkubwa/ Kijogoo(Alpha Male) na Rostam kwania kula nchi na kujilimbikizia mali.
Kwa kuzingatia tathmini ya wachunguzi hopo juu tunaona wazi kwamba; Ubia huu wa urais ulikuwa unamafungu mawili yanayokigana kidhamira na kiitikadi, kwani; Lengo la kupenda Ukubwa (Alpha Male) la Lowassa linashabihiana sana na lengo la kijilimbikizia mali na kula nchi la Rostam. Hivyo ubia huu ulikuwa una uwiano wa 1:2 JK upande mmoja / Lowassa na Rostam upande mwingine.
Wachunguzi wanatueleza kwamba Jambo la kwanza alilofanvya bw. Rostam mara tu baada ya kujiunga rasmi katika ubia huu 1996 ni kutafuta namna ya kumsafisha Lowassa; kitu ambacho tunaweza kusema alifanikiwa sana kwani pamoja na uchafu wote uliokuwa unafahamika dhidi ya Bw. Lowassa, bw. Rostam aliweza kuwahadaa watanzania mpaka kiasi cha bw Lowassa kuweza kupitishwa kuwa wazir mkuu na bunge letu lililokuwa la ki-muhuri. Kazi hii ilifanywa na Bw. Rostam kwa kuanzisha rasmi gazetii la kila wiki (WIKI HII) kwa lengo moja tu Kumsafisha Lowassa. Gazeti ambalo baada ya kufanikiwa malengo yake (kumrejesha Lowassa serikalini alipata kiti cha uwaziri wa Umasikini,) - lilifungwa na kuzaa magazeti mengine (Cetizen / Mwananchi) ambayo bw. Rostam amekua akiyatumia katika kuficha matendo yake ya Ki-dhalium yanayo hujumu na kudumaza maendeleo ya Taifa letu na wananchi wake. Mpaka pale wabia wengine (safi) wa gazeti hili walipoamua kumfunga Luku, Muonja Asali haonji mara mmoja - Ili kuendeleza udhalimu wake Rostam akamnunua Jenerali pamoja na Habai Cooparation (Jenerali alikubali kufungwa mdomo kwa miaka 2 kuwaachia Mafisadi wale nchi katika mkataba wake wa kuuza Habari cooperation) ama-kweli kila mtu ana bei yake.
Hapo nyuma niliwahi kuandika kuhusu njama zilizokua zikitumiwa na wabia wa JK (Lowassa na Rostam) katika kuhakikisha kwamba udhalimu na ufisadi wanaufanya katika nchi yetu hauwanikwi kwa kuwanunua waandishi wa habari pamoja na kununua vyomba vyao katika mikataba ya kufunga midomo iliwasiweze kuwaanika. Tumeshuhudia namna walivyoweza kumfumba mdomo mmoja wa wana-mapinduzi wetu maarufu, kaka jenerali Ulimwengu kwa kununua kampuni yake ya Habari Cooperation (Watoaji wa Rai na Mtanzania) na kumuingiza katika mkataba uliomfunga mdomo asiwe na jukwaa la kutoa Raia-huru kwa miaka miwili. Ndiyo kwanza miyororo hiyo imefunguliwa na sasa kaka Ulimwengu ameweza kufungua gazeti lake la Raia Mwema wachunguzi wanadai kwamba Wabia hawa hawakuishia papo tu hata Kijana wetu Kipanja aliwekwa na yuko katika payrools ya mafisadi hawa ili asichore vikatuni vya kubeza uongozi wa bora-mimi wa Lowassa
Nchini Italia kuna Kundi maarufu la kijasusi liitwalo MAFIA ambalo lina matawi katika nchi nyingi hadi Marekani. Kundi hili hutumia mbinu mbali mbali za kifisadi katika kutimiza udhalimu wao dhidi ya Raia wema, nitakua sahihi hapo nikiwafananisha - kwa mbinu - wa bia wa JK na kundi la Mafia.
Hivi karibuni kwa kupitia riport ya kamati ya bunge ya Mwakyembe tumedhihirishiwa kwamba wabia hawa wawili wananguvu katika ubia wao wa urais kupita hata Raisi mwenyewe: Kiasi ilifikia hata maamuzi ya Baraza la Mawaziri ambalo mwenyekiti wake ni JK hayakuwa na maana mbele yao kwani waliweza kubadili na kupuuza maamuzi yake mara tu baada ya vikao vya baraza. kiasi cha kuishagaza hata kamati ya bunge kufikia kuuliza :
(i) Je, kulikuwa na kikao kingine cha Baraza la Mawaziri siku hiyo hiyo ya tarehe 10 Februari, 2006 kilichotengua maamuzi yake ya awali ya siku hiyo hiyo?
Kamati vilevile ilikiri kushangazwa na ujasiri wa kiburi ulioonyeshwa na baadhi ya watendaji wakuu wa serikali kiasi cha kupindisha hata maamuzi ya Baraza la Mawaziri mara tatu mfululizo bila wasiwasi wowote na vile vile kusafishwa na TAKURU (sasaTAKUKURU) Wachunguzi wanatuambia kwamba, Watendaji hawa waliokuwa wanatambua kwamba wabia wenye nguvu katika Uraisi wa JK (Lowassa na Rostam) ndilo wanalolitaka, - kampuni (Richmond) ipewe tenda, hivyo lazima litekelezwe, - Kamati imekiri kwamba kwa ushahidi wa kimaandishi, kimazingira na wa mdomo uinaiona nguvu hiyo kuwa ni ya ((kama ukipenda) GodFather Don Lowassa) Waziri Mkuu.
Mwezi November 2002 Aliyekua waziri Mkuu wa Italy Bw Giulio Andreotti alihukumiwa kifungo cha miaka 24 kwenda Jela kutokana na ushiriki wake wa mauwaji ya Kimafa ya mwaka 1979.
Wachunguzi wanatuarifu kwamba siasa za nchi yetu zimeingiliwa sana na vitendo vya kijasusi vya Kimafia kuliko ambavyo tugependa kukiri. Kuna taarifa za kichunguzi zilizokua zikikusanywa tokea 1996 ambazo zinadhihirisha madai haya: Tumeona kisiasa kuanguka kiajabu ajabu kwa baadhi ya viongozi waliwahi kuonekana kwamba wageweza kumrithi Mkapa; Itakumpukwa Bw Ngwilizi alitajwa kuwa mmoja wa viongozi waliokuwa wakifikiria, mara tu baada ya taaarifa hizi ziliaza kujitokeza juhudi za kijasusi za Rostam kupitia katika magazeti kadhaa likiwemo Wiki HII kumchamba na kumpaka matope tukashuhudia wabunge waliopandikizwa wakiimuuliza maswasli ya kebehi huku magazeti yakichagiza kwamba ameshindwa kazi, ajiuzuluI Wachunguzi wanatueleza kwamba juhudi hizi chafu ndizo zilizotumika sana katika kuwapaka matope wagombea wegine wa Uraisi wa 2005 uliomuimbua JK kuwa Raisi. Sasa tunajua nani walikuwa nyuma ya Hoja za kuwadhalilisha wakina Salimu, Malecela na Sumayi
Nadani kuna haja ya kuishukuru na kuipongeza kamati ya Mwakyembe kwa ujasiri mkubwa walioonyesha pale walipothubutu sio tu kuwaita WEZI - bila kufunika maneno - watu kama kina Lowassa, Rostam na wenzao bali kudiriki kuwafananisha na vibaka; huu ni ujasiri kweli kweki. Naomba ni wanukuu:Mheshimiwa Spika, Kamati Teule sasa inaelewa chimbuko la tabia mbaya iliyoenea nchini ya ajali ikitokea watu kukimbilia kusaidia. Lakini si wote wenye dhamira ya kusaidia, kuokoa. Baadhi yao lengo kuu ni kuiba, kupora! Viongozi tunaobuni miradi kutokana na majanga ya kitaifa, hatuna tofauti na watu wanaokimbilia ajali kama waokoaji kumbe wezi...
Wachunguzi wanatutaadharisha kwaamba mabambano dhidi ya majasusi wa Ki-Mafia hanahitaji watu wazalendo na wenye msimamo kweli-kweli, kwani histori inatuonyesha kwamba wapiganaji wengi katika vita kama hivi katika nchi za Marekani, Italia, Urussi na Hata Japani wamepoteza maisha yao na ya familia zao. Kwani watu kama hawa hawana Utu wala aibu katika udhalimu wao wa kuwadhalilisha Raia wema. Ili wao waabudiwe na kujifanya Mungu watu.
Mwalimu Nyerere aliwahi kututaahadharisha kuhusu mafisadi wa Kimafia pale alipotuonya kwamba tusipoangalia Mafisadi watakuja kutuchagulia Raisi. Inasikitisha tukiona kwamba, ukiondoa chaguzi za kumuongea kipindi cha pili Mkapa, chaguzi za kwanza baada ya kifo cha mwalimu maono yake yamekuwa kweli. JK ameingi IKULU kwa karata iliyochezwa na mafisadi na uthibitisho huu ukowazi kwani siyo tu amekuwa hana nguvu ya kuwachukulia hatua kwa madharau ya waziwazi anayofanyimwa na mafisadi hao bali hata kuwakemea ameshindwa, amebaki akiwatetea baada ya kuumbuliwa (mafisadi) na kamati ya Bunge kwamba KILICHOWAPATA NI AJALI YA KISIASA ama-kweli maneno ya wazee hayapiti bure Ukicheza na Mbwa atakufuata Msikitini.
Kuna haja Watanzania kuwa macho na vita vilivyoanza kati Mafisadi hawa na viongozi wetu kama Spika Sita, Mweyekiti Mbowe, Mzee wetu Butiku Nk.
Mafisadi wa Kimafia wana sifa ya kumkumbatia mtu kwa busi, kisha kumchoma kisu mgongo. Tumeshuhudia Rostan akidai kwamba Makampuni yake yanalipa kodi zaidi ya shilling Bilioni 100 kwa mwaka, na kwamba kama Richmond ingekuwa yake asigeshindwa kazi: sasa swali ni: Mkoa wake wa Tabora ndiyo mkoa wenye wananchi masikini sana Tanzania; Sasa kama huu si unafiki ni nini? Muwakilishi tajiri kabisa Nchini anawakilisha watu ambao ni FUKARA wa mwisho nchini, MUNGU mkubwa.
Wiki ijayo tutawaletea habari zaidi za uchunguzi yakinifu, Mbarikiwe sana na MUNGU awalani Mafisadi kwa kutudhulumu haki zetu. AMIN.
Niandikie
Kiganja wa Mkono: kiganja@hotmail.com