JK na viongozi waandamizi wanyang'anywe pasi, TUMUACHIE WAZIRI WA MAMBO YA NJE TU!

kuku dume

JF-Expert Member
Apr 22, 2012
414
62
Wakuu,

Serikali imekuwa ikitupa hadithi sisizo na maana kila bajeti inapofika.

Neno sungura mdogo huwa ni msamiati bungeni kila bajeti inaposomwa.

Kwa kuwa sungura mwenyewe ni wetu ni lazima awe mkubwa hata kwa dawa za 'kichina'.

Misafara ya viongozi wetu kwenda nje huwa haipungui jambo ambalo kwa namna moja au nyingine linafanya sungura kuwa mdogo.

Nahisi ni bora upangilie kidogo ulichonacho kuliko kwenda kuomba usicho na uhakika nacho.

Sijui kama viongozi wa serikali hutumia passport wanazomiliki wao au ni za wananchi.

Kama huwa ni mali zao basi jambo hili litatugharimu milile. Jaribu kukumbuka Balali alivyoligharimu taifa.

Kama wanatumia passport zetu sie watanzania basi ni nafasi kwetu kuwanyang'anya ili kupeleka fedha za safari kwenye matatizo sugu kama mikopo ya wanafunzi elimu ya juu, afya, mishahara nk.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom