JK NA UONGOZI WA ZIMAMOTO : What is he up to? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK NA UONGOZI WA ZIMAMOTO : What is he up to?

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Nyumbu-, Apr 15, 2011.

 1. N

  Nyumbu- JF-Expert Member

  #1
  Apr 15, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 969
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 60
  Wana JF,

  Nimejaribu kufikiria dira ya uongozi wa JK nimeshindwa. Miaka mitano imepita, sijajua alikuwa ana lengo gani hasa ambalo alilivalia njuga kuhakikisha linafanikiwa. Nilichokiana ni kwamba lengo lake kuu ilikuwa ni kukaa kwenye uraisi miaka kumi na hatimaye aweze ku influence mrithi wake atakayemridhia.Nina baadhi ya sababu zinazonifanya niamini hivyo:
  1. JK aliyavumilia makundi makubwa yaliyokigawa chama chake , si kwa sababu yeye ni mvulivu, la . Lengo lake ilikuwa asiyaudhi hayo makundi ili ayatumie kuukwaa tena uraisi kwa kipindi cha pili; kinyume na uvumi uliokuwa unazagaa kwamba he was meant to be a one term president!
  2.Hakuwa na nia ya dhati ya kuwatumikia watanzania na ndiyo maana alikuwa mgumu sana kuchukua maamuzi.Lengo lake kubwa ilikuwa ukubwa; mengine ni by the way. Kwa ujumla , alitumia nguvu kubwa kufika ikulu si kwa sababu ya kulisaidia taifa, bali ilikuwa kutimiza mradi wake wa kuamini kwamba alikuwa chagua la Nyerere na Mwinyi kumrithi Mwinyi, ila upepo ukageuka kwenda kwa Mkapa ( Kwa sabubu za wazi bila shaka)
  3.Napata shida kujua kwamba anajali au hajali mambo yanayo waumiza wananchi. Kwa mfano kulikuwa na malalamiko mengi ya watu kuhusiana na jinsi blog ya Ze Utamu ilivyokuwa inawachafua watu wasio na hatia ikiwemo viongozi mbalimbali wa nchi, lakini hapakuchukuliwa hatua yoyote ya kudhibit vitendo hivyo. Ni pale kashfa hii ilipomgusa yeye moja kwa moja ndipo serikali yake ikaurupuka na kuufunga mtadao huo. Je hapa aliufunga kwa kunusuru watu wake, au alifunga kwa ubinafsi wa kwamba "bwana mkubwa ameguswa"? Kwa maana nyingine ni kwamba blogu hiyo ingeendelea kuwepo hadi leo, kama si mwenye blogu kumgusa Mr. untouchable.
  4.Kumekuwa na tuhuma miaka yote mitano ya uongozi wake kuhusu yeye kulinda marafiki zake ambao wamechafuka sana kwa tuhuma za ufisadi. JK aliwavumilia na kuwatetea kwa nguvu zake zote na hata kuwapigia kampeni kuwa ni watu safi. Akaingilia hadi Takukuru ( refer weakleaks) kuwakingia kifua wasipelekwe mahakamani. Ameendelea kuwavumilia mpaka wakaingia kwenye kamati nyeti kabisa za bunge na wakadhibiti bungu. JK kimya. LAKINI GHAFLA BIN VUU LEO ANASEMA ANAJIVUA GAMBA, KULIKONI? Jibu ni rahisi: Marafiki zake walishaanza kumzidi kete kuelekea uchaguzi wa 2015. Walishafanikiwa kuzitikisa jumaia zote za CCM kuhakikisaha kwamba come 2012, wampige chini asiwe mwenyekiti wa CCM. Ni baada ya kuguswa maslahi yake , ndo leo anasema anajivua gamba. Tena ni mkali kwelili kweli . Vipi? Mbona hivyo? Kwanini leo, na kwanini Lowasa, Chenge na Rostam"? Mbona akina Mkapa , Kigoda na wengineo hawatoswi? Wale akina Mulla kule Mbeya ambao ni kama wanaserikali yao vipi wale? Kwamba akina Wasira ni wasafi? Tena ghafla, eti iundwe timu ya Wazee ili washauri chama, mbona walipigwa madongo walipojaribu kukinyooshea chama vidole na wakaitwa wahuni na rafiki yake mkuu Makamba? Hata JK mwenyewe alisema " Nilijua watasema , lakini nitawajibu" yaani akiwaponda watu wa kongamano la Nyerere. Leo hii wamekuwa na busara?
  Kwanini ghafla waonekane wana busara. Si ni kwa vile amezidiwa nguvu na marafiki zake; hajafanya hivyo kwa sababu ana uchungu na nchi hii, la hasha! Ni project yake ya kuelekea 2015 ili aweke mtu atakaye endeleza usultani wao.
  Siwatetei akina Lowasa, ila siamini kwamba ndo pekee mafisadi ndani ya CCM na serikali kwa ujumla.
  Ukiangalia jinsi watumishi wa umma wa mashirika kama NSSF, TANAPA, NCAA, TANESCO nk walivyojilimbikizia mali, huwezi ukasema CCM leo imejivua gamba. Hakika imevaa kavu zaidi, na mwisho wake utakuwa mbaya kuliko. Kama mwandishi mmoja alivyoandika kwenye Mwanahalisi " CCM ikijivua gamba itavuja kweli" naanza kuamini. Nasubiri reactions za kundi la Lowasa na wenzake, jinsi zitakavyo litikisa taifa hili.
  Siombei...ila ungozi huu wa kukamiana na kuamua kwa maslahi binafsi haufai.
  3.
   
 2. Comrade Mpayukaji

  Comrade Mpayukaji Senior Member

  #2
  Apr 15, 2011
  Joined: Sep 26, 2007
  Messages: 192
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Well said!!!! Watanzania ni maskini wa kutupa lakini CCM imechapa usingizi ni propaganda tu za kijinga na kihuni kuhakikisha wanaendelea kutawala. Tunasema tumechoka na umaskini na CCM lazima tuizike :rip: kuinusuru nchi ambayo imeshapigwa bei kwa wajanja:bored:
   
 3. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #3
  Apr 15, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mkuu,
  Ni maneno mazito sana uliyonena na yamenipenyeza saana, kuna harufu kali ya VISASI kurindima. Yafanyikayo si kwa manufaa ya nchi/taifa...HAYANA MANUFAA KWA VIUMBE WA NCHI HII.
   
 4. N

  Nyumbu- JF-Expert Member

  #4
  Apr 15, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 969
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 60
  Makala

  [​IMG]

  Hata Mwenyekiti Kikwete ni gamba

  [​IMG]
  Msomaji Raia​
  Aprili 13, 2011[​IMG]
  [​IMG]Uamuzi umechelewa, na una walakini
  KAZI ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kujivua gamba yasemekana imekamilika huko Dodoma mwanzoni mwa wiki hii.
  Ndani ya CCM wapo wanaosema imeanza, lakini Mwenyekiti wa chama aliahidi itafanyika, na kwa kuwa kikao kimekwisha, wengi tunaamini imekamilika.
  Ni kawaida kila baada ya vikao vya CCM kufanyika na kufanya maamuzi, viongozi wa CCM huja hadharani na kudai maamuzi ya kihistoria na magumu yamefanyika. Hata haya yaliyofanyika Dodoma, yanasemekana yalikuwa magumu na ya kihistoria. Tutaona mbele ya safari.
  Niliwahi kujadili dhana ya gamba linalohitaji kuvuliwa. Wengi pia wamejadili na mengi yameibuliwa. Nikiwa mwana CCM, naendelea kuamini kuwa pamoja na magamba mengi yanayoikabili CCM yetu, hata CCM yenyewe ni gamba kwa Taifa, linalohitaji kuvuliwa.
  Sekretariati iliyoondoka ilikuwa ni gamba; Kamati Kuu ilikuwa ni gamba, NEC ni gamba na hata Mwenyekiti Kikwete ni gamba. Kwa mantiki ya vikao vya Dodoma, gamba lililovuliwa ni sekretariati na Kamati Kuu.
  Nauita uamuzi huu kuwa ni uamuzi mzuri lakini uliochelewa na matokeo yake, ni uamuzi wenye walakini kwa kuwa umechelewa.
  Kwa mara ya kwanza, Watanzania wameisikia CCM kupitia Naibu Katibu Mkuu mpya, John Chiligati akisema, wana CCM wenye tuhuma za ufisadi wa aina yoyote wanapewa muda waamue wenyewe na kufanya uamuzi ndani ya siku 90.
  Akaongeza ya kuwa maadamu wananchi wana mashaka na uadilifu wa mtu kutokana na tuhuma hizo, inabidi watuhumiwa hao, wawe wa Richmond, Dowans, Kagoda n.k wachukue hatua haraka.
  Hatua hii ni mpya katika siasa za awamu ya nne ya Rais Kikwete kwa sababu, Kikwete mwenyewe amekuwa akidai tuhuma tu hazitoshi kumwondoa mtu kwenye chama wala nafasi ya uongozi. Ameendelea kusisitiza kuwa ushahidi upelekwe mahakamani na kuthibitishwa ndipo chama kiweze kuchukua hatua za kuachana na wahusika.
  Kutokana na msimamo huo wa Kikwete na Chama kwa ujumla, watuhumiwa wa ufisadi wameendelea na nafasi zao kwenye chama kwa muda mrefu. Wametumia nafasi zao si tu kujinufaisha maamuzi wanayoyapitisha katika Chama na serikali, bali pia wamehujumu kwa kasi mwonekano wa chama mbele ya wapiga kura.
  Kwa msimamo huo huo wa "utawala bora" wa kuendelea kuwashikilia watuhumiwa wa ufisadi, CCM chini ya Jakaya Kikwete ikawaombea kura mbele ya wapiga kura na wakashinda kwa kishindo.
  Mafisadi hao wakaingia bungeni na kwa kutumia ubabe na jeuri ya fedha wakatumia bunge na kuligeuza kuwa chombo cha ushabiki wa kisiasa na kusigina maslahi ya Taifa. Chama kwa kushirikiana na bunge wakafanya wapendavyo katika kuamua nani awe nani katika kamati za bunge, uongozi wa bunge na ilifika hata mhimili wa serikali kuanza kuendeshwa kwa nguvu na ushawishi wa mafisadi.
  Sumu ya watuhumiwa hao ikaenea mpaka kwenye jumuia za chama, bodi za vyombo vya fedha, vyombo vya usalama, halmashauri za wilaya, manispaa na miji, hata katika madhehebu ya dini.
  Wakati wote huo, Rais ambaye ni Mwenyekiti wa chama akaendelea na mizaha yake ya kudai anawapa nafasi wajirekebishe, na kuwa ana orodha yao, na mahali pengine akadai tunajipanga kukabiliana nao.
  Haikuingia akilini mwake hata siku moja kuwa ufisadi ni moto wa hatari mpaka pale nafasi yake kama mwenyekiti wa chama ilipoanza kupigwa mnada ndipo akazinduka.
  Uamuzi uliochukuliwa wa kuvunja Kamati Kuu na Sekretariati na kuuunda upya vyombo hivi, umechelewa sana na madhara yake hayawezi kuponyeshwa kwa mabadiliko ya sura.
  Moyo na dhamira ya Mwenyekiti inabidi vibadilike kabisa. Wapo wanaodai sasa amejifunza japo kwa kuchelewa. Mimi ni Tomaso, niliwahi kusema namjua Kikwete na yeye ananijua sana. Shaka yangu ni kubwa kuliko matumaini yangu kwake.
  Nguvu ya ufisadi ndani ya CCM ni kubwa kuliko uwezo wa dola ya Kikwete, na ni kubwa kuliko uwezo wa chama kuisafisha. Ufisadi ndani ya CCM ni mfumo, si hisia wala dhana ya kufikirika. Ndiyo maana mafisadi wanaweza kuondoka kwenye chama hiki, wakaunda chao na kupata wafuasi wengi na kuwa tishio kwa CCM iliyo madarakani!
  Wanaoitwa mafisadi na ufisadi wao, wana wafuasi wengi ndani ya vyombo vya maamuzi ya CCM na kama ingepigwa kura ya siri ndani ya NEC, leo hii, kuchagua kati ya Kikwete na mafisadi, tunaweza kuona maajabu!
  Kilichotokea Dodoma, ni nguvu ya dola kuwaelemea watuhumiwa wa ufisadi tena wasiozidi watano na kulalamimika kutumia muda mrefu kuwabembeleza ili wakubaliane na malalamiko ya wapiga kura juu yao.
  Inavyoonekana, mradi huu wa kuwabembeleza ili wajivue gamba utaendelea na ndiyo maana zimetolewa siku 90. Huu ni udhaifu mkubwa wa kiuongozi na ndiyo maana nauita uamuzi huu kuwa umechelewa sana na hata ulipofanyika, umekuja na walakini ya ajabu.
  CCM kama chama kimepoteza mvuto kwa wanachama wake na wapiga kura kwa ujumla. Wanaokichagua wanafanya hivyo ama kwa kushinikizwa na nguvu isiyoonekana au kwa kuwa vyama vingine haviwapi matumaini ya uhakika.
  CCM imepoteza nguvu ya kushughulikia ufisadi ndani yake. Haina uwezo wa kuwawajibisha watendaji wake wa ndani mpaka ilazimishwe na vyama vya upinzani au manung'uniko ya wapita njia. CCM hii inalazimika kutumia vyombo vyetu nyeti vya usalama na raslimali za Ikulu ili kupambana na ufisadi uliojikita ndani yake.
  Nguvu hii ya dola na matumizi ya wana usalama katika kuzima moto wa mafisadi ndani ya vikao, zingetumika mapema kubaini mbegu za ufisadi katika uchaguzi, isingelazimika kutumia muda mwingi ndani ya vikao kubembelezana ili kuwajibishana.
  Imeelezwa kuwa mmoja wa watuhumiwa aliyekumbwa na maamuzi ya Dodoma anasema ya kuwa maamuzi hayo yamefanyika ili kupoza moto wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), na si kwamba wao watuhumiwa ni wabaya kwa chama chao.
  Kwamba Mwenyekiti wa chama hana ubaya wowote ila kuna tabia ya visasi na kushughulikiana ndani ya CCM, na kuwa tabia hiyo isipokomeshwa itaimaliza CCM.
  Kama huu ndio ujumbe ambao Mwenyekiti wa Chama, Rais Kikwete, anawaambia pembeni majeruhi wa maamuzi ya Dodoma, basi tukubaliane na hoja ya kuwa CCM haina tena ule uwezo wake wa asili wa kusimamia maadili ndani ya chama.
  Maamuzi ya kinidhamu yasiyokuwa na ridhaa ya kweli ya Mwenyekiti wa chama ni hatari kwa chama chenyewe na yanamvunjia heshima Mwenyekiti mwenyewe. Kumbe ndiyo maana CCM imebakia na uwezo wa kuvunja vyombo vya maamuzi ili wakati wa kuviunda wale wasiotakiwa waachwe nje.
  Huu nao ni udhaifu wa kiuongozi usiotakiwa kuvumiliwa; maana kwanza, unalea udhaifu unaokidhoofisha Chama, na pili, unalea dhana ya mtu binafsi kuwa bora kuliko taasisi.
  Haingii akilini kuwa ndani ya vikao ambamo kuna magwiji wa taratibu za kuendesha taasisi na dola, udhaifu huu unaachwa na kukubalika kuwa sehemu ya mfumo wa kuendesha chama.
  Katika masuala ya kusimia maadili, uadilifu na nidhamu ya taasisi, uamuzi uliochelewa ni mbaya kuliko uamuzi mbaya uliowahi kwa wakati.
   
Loading...