JK na unabii wa Ndio Mzee

MawazoMatatu

JF-Expert Member
Sep 6, 2008
505
61
Yapata miaka takribani 10 tokea wimbo wa msanii wa bongoflava Joseph Haule anayefahamika pia kama Prof Jay (Heavy weight MC, Wamitulinga, MC shupavu) uitwao “ndio mzee “ kuingia sokoni , na yapata miaka 5 toka wimbo huo utolewe kabla ya awamu ya nne ya uongozi wa Taifa letu kuanza chini ya Rais Kikwete.

Jambo la kushangaza na kushtua ni kuwa ujumbe uliomo kwenye wimbo huu, unashabihiana sana na ahadi za kiongozi wetu mkuu wa nchi aliye madarakani, japo ulitoka kabla ya yeye kuchukua madaraka ya nchi na hivyo kuufanya ujumbe huu kuonekana kama “unabii” flani..!

Hebu tujaribu kuusikiliza wimbo huu na kujaribu kuoanisha na ahadi za JK alizozitoa kabla na baada ya kuchukua uongozi wa nchi yetu...! Sikiliza kasha tafakari....!

YouTube - Ndio mzee Professor jay ft Juma nature
 
Yapata miaka takribani 10 tokea wimbo wa msanii wa bongoflava Joseph Haule anayefahamika pia kama Prof Jay (Heavy weight MC, Wamitulinga, MC shupavu) uitwao "ndio mzee " kuingia sokoni , na yapata miaka 5 toka wimbo huo utolewe kabla ya awamu ya nne ya uongozi wa Taifa letu kuanza chini ya Rais Kikwete.

Jambo la kushangaza na kushtua ni kuwa ujumbe uliomo kwenye wimbo huu, unashabihiana sana na ahadi za kiongozi wetu mkuu wa nchi aliye madarakani, japo ulitoka kabla ya yeye kuchukua madaraka ya nchi na hivyo kuufanya ujumbe huu kuonekana kama "unabii" flani..!

Hebu tujaribu kuusikiliza wimbo huu na kujaribu kuoanisha na ahadi za JK alizozitoa kabla na baada ya kuchukua uongozi wa nchi yetu...! Sikiliza kasha tafakari....!

YouTube - Ndio mzee Professor jay ft Juma nature

Licha ya kutanggaza mafanikio ikiwemo kuleta amani nchini, na kuongeza kipato cha watanzania lakini Hii ni kweli kabisa sawa na NDIYO MZEE, Japo yeye kahama kidogo kwenye feedback yake.
FUNGUA MACHO YAKO UAMUE- "WAKATI ULIOKUBALIKA NI SASA
 
Siku zote huwa najiuliza hivi Kikwete haoni aibu kweli! Miaka mitano kama raisi na huna hata dira, unaongoza nchi kwa matukio (Crisis Manager). Yaani siuoni mwelekeo wa Kikwete kama kiongozi wa nchi, no vision, no strategies yaani anacheka tu. But this explains exactly kwamba waliomuweka ni wajanja sana. Wanaweka garasha...!!
 
Na kusubiri kutusomea hotuba zilizotungwa na mwana wa msanii mwenzie makamba
 
Prof J: Ntajenga barabara tano tano za juu na chini...
Kikwete: Endeleeni kununua magari msiogope maana serikali ina mpango wa kujenga barabara za juu..!

Prof J: wanafunzi mkafanyie practical mwezini
Kikwete: Nitahakikisha kila mwanafunzi anakuwa na kompyuta

Prof J: Mkulima kila mmoja nitampatia trekta...
Kikwete: kaja na matrekta ya kilimo kwanza..!

kuna mengi sana humu yameimbwa ambayo yanaleta picha halisi ya kiongozi wa aina ya kina Kikwete
 
Mwelekeo huna wewe kwasababu ya uvivu wako, fursa zipo na wenye kutafuta wanaona mafanikio ya serikali ya JK...wewe kama huoni mwelekeo ni kwakuwa mwenyewe huna mwelekeo umekalia kulalamika..nenda kajiunge na Maaskofu na vijiwaraka vya kulalama...
 
Duuh wapi hoja?? Mkuu Mungu wetu mwenye wingi wa rehema ameshakusamehe maana hujui ulitendalo nenda kwa amani ya bwana..!
 
Mwelekeo huna wewe kwasababu ya uvivu wako, fursa zipo na wenye kutafuta wanaona mafanikio ya serikali ya JK...wewe kama huoni mwelekeo ni kwakuwa mwenyewe huna mwelekeo umekalia kulalamika..nenda kajiunge na Maaskofu na vijiwaraka vya kulalama...

Pumba
 
Back
Top Bottom