JK Na Umangimeza; Tafsiri Yangu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK Na Umangimeza; Tafsiri Yangu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by maggid, May 9, 2011.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  May 9, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180

  “ I want to hear you guys out there in the field!” Anasema Rais Jakaya Mrisho Kikwete.  Ndio, usiku huu nimemsikiliza Jakaya Kikwete kupitia runinga ya TBC1. Kikwete ameongea na watendaji wakuu serikalini kule Dodoma. Na walikuwa wengi ukumbini; Mawaziri , Manaibu Mawaziri, Makatibu Wakuu, Manaibu Makatibu Wakuu na wengine.


  Tafsiri yangu; kwanza kabisa, nimeipenda sana hotuba ya Kikwete ingawa TBC1 hawakuweza kuimalizia kutokana na matatizo ya kiufundi. Nitaitafuta niisome kwa ujumla wake.
  Vinginevyo, katika kile nilichokisia nilimwona Rais aliyekuwa critical kweli kweli kwa watendaji wake.


  Naam. Rais ‘ aliwasema’ kweli watendaji wake, kama nitatumia lugha ya sebule zetu. Kikwete niliyemwona, pasi na shaka, alikuwa mkweli kwa nafsi yake. Alitoa duku duku lake. Watendaji wale walionekana kuwa kimya wakati wote. Kuna ambao waliinamisha vichwa. Hotuba ya Kikwete ilikuwa na ukweli mwingi juu ya hali halisi. Kikwete alikuwa anaongelea sehemu ya kero ya wananchi kwa watendaji wao. Mle ukumbini kuna watakaotoka wakinung’unika; “ Bwana Mkubwa katuumbua!” Watajisemea.


  “ Kazi ya Waziri si kusoma mafaili tu” Anasema Kikwete. Kisha anaongeza; Tokeni!” Na hilo ndilo neno lililosikika mara kwa mara kwenye hotuba ile. Kikwete alilisitiza sana umuhimu wa watendaji kutoka na kwenda kwa wananchi.


  “ Ni nani kati yenu kazi yake iko ofisini tu?” Aliuliza Mkuu wa Nchi. Kama ilivyotarajiwa, hakuna aliyenyosha kidole.


  Na naweza kubashiri, kuwa kuna gazeti litakalotoka kesho na kichwa cha habari; ” JK Awaanika Watendaji Wake”. Kikwete anasema; ” Tubadilike jamani”. Lakini, nilichokiona kwenye sura za wengi wa watendaji wale ni ugumu uliopo wa kubadilika. Inahusu ’ Change of Mindset” na bila shaka JK mwenyewe analijua hilo. Swali ni hili; “ How can you change from a fixed mindset to a growth one?” Mbwa mzee hafundishwi kukaa, au? Inawezekana kama mbwa mwenyewe akiwa na utayari wa kijifunza. Ndio inawezekana.


  Watendaji wale baadhi yao wanasumbuliwa na maradhi ya kuendekeza ‘ Ubwana na Umangimeza” . Si ndio, wanapenda sana ‘ Ubosi’. Na ndio maana itawawia ugumu kweli Waheshimiwa hao kukaa chumba kimoja na vijana Maafisa Habari wao. Si vijana wadogo tu, tena wamemaliza vyuo vikuu juzi tu. Eti bosi mzima a-brief kijana Afisa Habari juu ya habari za Wizara kasha kijana huyo azungumze na umma. Urgently needed, change of mindset! Vinginevyo tutabaki pale pale na kauli za; “ Mimi si msemaji wa Wizara!”


  Lakini, tutakosea pia tukidhani kuwa baadhi ya watendaji wale wako busy tu maofisini wakisoma mafaili, maana kuna ukweli mwingine, ni huu; baadhi ya watendaji wetu wako busy sana kufanya mambo yao binafsi, ndani na nje ya ofisi. Si tunajua, kuwa baadhi ya watendaji wetu ni wafanyabiashara na wengine wanaendesha hata viwanda vya uzalishaji.


  Katika utaratibu wa sasa na hasa baada ya kuondokana na kanuni na maadili ya uongozi ya enzi za Mwalimu, ni vigumu ukawa na mawaziri na watendaji wengine wasio na miradi ya biashara, mashamba na hata viwanda ambayo wao wenyewe ndo wasimamiaji. Hivi, Waheshimiwa hawa watapata wapi muda wa kusimamia biashara, mashamba na viwanda vyao kama si kuiba muda wa kuwatumikia wananchi na hata kutumia rasilimali za umma?


  Inahusu swali hili; Ni nani atauzima mshumaa wa Serikali? Na hapa kuna kisa cha kusimulia;
  Naam, miongoni mwa viongozi waliopata kuongoza dola ya Kiislam hususan baada ya Mtume Muhammad (SAW) na baada ya masahaba ni Amir muuminina Khalifa Umar bin Abdulaziz. Wanazuoni wa Kiislam wanatwambia, kuwa utawala wa Khalifa Umar bin Abdulaziz ulijaa uadilifu. Si kwa viongozi tu, hata kwa raia wake.


  Inasemwa, kuwa moja ya mafanikio makubwa ya utawala wa Khalifa Umar bin Abdulaziz ni kukusanya zakka. Katika Uislam, zakka ni ibada ya lazima kwa mwenye nacho kuwapa masikini, yatima, wajane, wasafiri, raia na wengineo wenye kuhitaji.


  Watu walijengewa imani kubwa, kiasi hakuna aliyethubutu kukwepa kutoa zakka. Hata wale waliopokea zakka walikuwa waadilifu, hawakupokea zakka mara mbili kama walishapokea kabla. Wote waliostahili kupata zakka , walipata zakka. Hakika, zakka zilitolewa zikajaa mabohari.


  Siku moja raia mmoja alikwenda kwenye ofisi ya Khalifa Umar bin Abdulaziz. Wakati wa maongezi yao, Khalifa Umar alikuwa akihangaika kuupuliza na kuuzima mshumaa mmoja na kuwasha mwingine. Alikuwa na mishumaa miwili mezani. Kadri mazungumzo yalivyoendelea, Umar aliendelea kufanya hivyo. Alipuliza mshumaa mmoja ukazimika, kisha akawasha mwingine.


  Jambo hilo lilimstaajabisha sana mgeni wa Khalifa Umar bin Abdulaziz. Akauliza; "Je, ni kwa nini unazima mshumaa huu na kuwasha mwingine, kisha huo nao unauzima na kuwasha ule wa kwanza?
  Khalifa Umar bin Abdulaziz akamjibu; "Mshumaa huu ni wa Serikali, wewe unaponiuliza habari za Serikali nauwasha. Lakini naona mara unauliza habari za familia yangu, ndio maana nauzima wa Serikali na nauwasha mshumaa wangu mwingine nilioununua kwa pesa za mfukoni mwangu. Nachelea nisije fanya dhuluma kwa mali ya nchi."


  Ndugu zangu, bila shaka, hicho ni kisa chenye kutupa mafundisho muhimu juu ya dhana nzima ya Maadili katika Utumishi wa Umma. Tafakari.
  Maggid
  Iringa
  Jumatatu Mei 9, 2011
  MJENGWA - Picha, Habari & Matangazo
  0788 111 765
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  May 10, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,261
  Likes Received: 19,389
  Trophy Points: 280
  kwa huu uchambuzi Mjengwa nakupa tano
   
 3. Obe

  Obe JF-Expert Member

  #3
  May 10, 2011
  Joined: Dec 31, 2007
  Messages: 5,957
  Likes Received: 20,288
  Trophy Points: 280
  Ukiangalia katika hotuba yake ni kama hakukuwa na baraza la mawaziri bali kusanyiko la mawaziri, katika kusanyiko kunakuwa hakuna uratibu unaoeleweka na kuheshimiwa. nadhani kwa hotuba hii tutaanza kuona na kupewa taarifa zenye mashiko na sio kila siku kuona mawaziri wanajipambanua kwa kukanusha bila kutoa takwimu za ukweli na hivyo kubaki wajivua hata ile nguo ndogo waliyobaki nayo.

  Wasemaji wa wizara walibaki kuwa watu wa kutumwa chai na sigara tu na si kufanya yale waliyoandikishwa kuyafanya. Angalau kwa jana JMK maneno yake yamemfanya aonekane kama kiongozi mwenye maneno yanayoonesha maamuzi:third:
   
 4. MawazoMatatu

  MawazoMatatu JF-Expert Member

  #4
  May 10, 2011
  Joined: Sep 6, 2008
  Messages: 505
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  "Rais kawasema kama nini..!" ,"naam...ndiooo" ....typical Mjengwa porojos..!
   
 5. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #5
  May 10, 2011
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280


  Ni yale yale kutengeneza news. Hawa mawaziri si kila wiki anakutana nao kwenye vikao vya baraza? kubweka bweka tu mbele ya camera kutafuta ujiko!

  Halafu hiyo hela ya kuzururia iko wapi? maana tumeambiwa wanatembeza bakuli benki kwa benki!
   
 6. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #6
  May 10, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  ni kweli kabisa mkuu hizi vikao vya chai tu.
  huu muda wa matendo sio porojo
  yeye hapo ikulu hajui bei ya sukari sisi huku walalao mambo si mambo si mambo tumekalia upupu
  tena kushabikia haya maneno yake ya kijuha yasiyo na matendo ni kummaliza zaidi. wananchi wameshasoma namba.
  tunasikilizi siku 90 tu hapa
  pamoja na maisha bora
   
 7. m

  mambomengi JF-Expert Member

  #7
  May 10, 2011
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 829
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Nimwendelezo wa viini macho.
   
 8. peri

  peri JF-Expert Member

  #8
  May 10, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,588
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.
  Alichosema jk ndicho wananchi tunacho kitaka, tatizo la serekali yake ni watendaji.
  Tusimponde tu jk hatakama kapatia.
   
 9. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #9
  May 10, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,779
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Peri... Hao watendaji wameteuliwa na nani? Ni sisi wananchi? Najua unajua unafahamu aliyewateua. Sisi tuliombwa ushauri?! Hili ni jambo dogo,kama aliyewateua anaona baadhi yao hawafai,katiba inamruhusu kuwawajibisha. Haya ni mambo madogo ambayo Jk hapaswi lalamika kwa wananchi. Tunataka kumsikia akizungumzia mambo makubwa siyo haya ambayo yako ndani ya uwezo wake!
   
 10. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #10
  May 10, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,921
  Likes Received: 453
  Trophy Points: 180
  nauliza...Hii ilikuwa ni hotuba kali kuliko ile ya wazee siku chache kabla ya WEF kuhusu mgomo wa wafanyakazi??
   
 11. khayanda

  khayanda JF-Expert Member

  #11
  May 10, 2011
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 248
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  :bange::bange:Hakuna mashindano, wala kushindanisha hotuba hapa, Naomba Mjengwa utujuze baada ya makaripio au makemeo haya pepo aliyewang'ang'ania viongozi wetu ametoka???? Hizi mbwembwe ndizo zinazotukera wananchi wengi maana unamuita mtu kumfunda na unamlipa kwa hela aliyobakiza kuiharibu, waTZ tumekwisha:israel::israel::israel::A S-baby: sisi ni kama watoto kubembelezwa kwa nyonyo tu tunyamaze huku tukijua baba anamkalipia house girl wetu wakati wakitoka hapo wanatunywea tena maziwa yetu:A S-baby::A S-baby::A S-baby::hawa ni ma evil::evil::evil::evil: na laana na iwe juu yao na vizazi vyao
   
 12. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #12
  May 11, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,260
  Trophy Points: 280
  Mimi mwenzenu mpaka leo sijajuwa tofauti kati ya hotuba na mazungumzo, labda mnijuze tu wakuu, maana kwa uelewa wangu siku ile JK alikuwa anapiga soga tu na mawaziri wake ili siku iende wagawane posho.
  Mtu unamchaguwa wewe mwenyewe kuwa waziri, halafu wewe huyo huyo unawaambia asiyeweza ajitoe mwenyewe, hiki ni kichekesho, ni mwana ccm gani ajitoe kwenye ulaji! upuuzi huu unaweza kuusikia peke yake hapa Tanzania.
  Halafu wanatumwa akina Mjengwa humu kuja kupima impact yake imepokewaje. kwa kifupi mimi nasubili uchaguzi mkuu ujao, lakini serikali hii ya JK hakuna lolote itakalofanyika. TAKE A NOTE.
   
Loading...