JK na simu ya mkononi

Tujisenti

JF-Expert Member
May 21, 2008
343
11
Hivi mkuu wa nchi kutembea na simu ya mkononi hata kwenye official events huku anajibu au kupiga simu au anapokea ujumbe ni sawa?
 
Sioni ubaya wowote hapo. Kama anaitumia ku keep in touch na wanae na familia yeake kwa ujumla kuna ubaya gani?
 
Hivi mkuu wa nchi kutembea na simu ya mkononi hata kwenye official events huku anajibu au kupiga simu au anapokea ujumbe ni sawa?

Nadhani wana usalama wake watakuwa wamefanya risk assessment na kuona kuwa haina ubaya
 
Kuwa mkuu wa nchi sio kwamba uweumejitenga na dunia ya nje ya duara linalikuzunguka. Pia kumbuka amesema mara kadhaa kuwa watu humuabarisha mambo anuai kupitia sms. aidha provided kuwa there is no misuse of it; it is ok.
 
Alimradi bwana mkubwa hapokei udaku, umbeya na fitina na kuamini as facts za kuwashughulikia na kuwachukia wengine. Ndiyo maana nchi nyingi duniani haziruhusu Mkuu wa nchi kuhangaika na simu kupokea na kutuma message na ku-beep.
 
Hivi mkuu wa nchi kutembea na simu ya mkononi hata kwenye official events huku anajibu au kupiga simu au anapokea ujumbe ni sawa?
Mie sidhani kama kuna ubaya lakini kiutaratibu kuna wapambe/walinzi wake ndio wanatakiwa kuzibeba na kumpelekea mkuu ujumbe au kilichojiri toka kwenye kilongalonga chake na sio yeye kuibeba mfukoni mwake. Na sio kamba yupo kwenye shughuli fulani ya kitaifa kilonga longa chake kikiita apokee halafu awasiliane na mpigaji wa hiyo simu.
 
Hawa wote wanajibebea simu zao wenyewe.
Obama_270x338.jpg

chavez_Vergatorio_1401395c.jpg

xin_470102051423516751114.jpg

img.435273_t.jpg

610x.jpg

Kuhusu kupokea simu kwenye jambo la kitaifa, chini picha ya rais wa Brazil akiongea na simu yake ya mkononi kabla ya briefing na rais wa China.
340x.jpg
 
Last edited:
Hakuna ubaya wowote kwa Jk kuwa na simu yake. Kama Obama anasimu yake masaa 24 na ni rais ambaye anatakiwa ulinzi tosha, itakuwa Huyo Jk wa developing country.
 
Mwenye simu ya Mh. Rais atupatie kuna maswali na pongezi tunataka kumpa
 
inategemeaa na kazi zake......na umuhimu wake...ila mmmm sidhani kama ni sahihi...
 
Mie sidhani kama kuna ubaya lakini kiutaratibu kuna wapambe/walinzi wake ndio wanatakiwa kuzibeba na kumpelekea mkuu ujumbe au kilichojiri toka kwenye kilongalonga chake na sio yeye kuibeba mfukoni mwake. Na sio kamba yupo kwenye shughuli fulani ya kitaifa kilonga longa chake kikiita apokee halafu awasiliane na mpigaji wa hiyo simu.

huo ndio utaratibu ..simu anakaa nayo mpambe ..ukipiga simu anapima umuhimu wa kumpatia kutokana na nafasi na umuhimu wa ujumbe....

hatari ya rais kukaa na simu moja kwa moja ...anaweza kufikishwa taarifa isiyochujwa na kuweza kuadhiri uamuzi ...ndio maana simu ya Obama siku hizi ipo filtered amewapa CIA na FBI...list ya call group ...ambazo namba zimefuatiliwa ...na hao ndio wanaweza kumpigia rais moja kwa moja na kumpata ....ukitumia namba nje ya hizo humpati...

so tukija kwa jk ...watu wa usalama wanaweza ku set simu yake kwa kumuomba awape list ya watu ambao anapenda kuwasiliana nao mara kwa mara ,mfano mke ,watoto,"wake", mawaziri,wasaidizi,wakuu wa usalama na ulinzi...etc...inaweza hata ikawa list ya watu 500....kwa kutumia technology ...simu hizo ndio zinaweza kumpata rais direct....[kumbuka kuwa wakati wowote akitaka anaweza kuwaambia wasaidizi wake waondoe baadhi ya namba au kuongeza ...au wasaidizi wake wanaweza kuondoa baadhi ya watu bila kumtaarifu kama wakihisi ....wanampa taarifa au kumuambia mambo yasiyo na msingi]..utashangaa tu ukipiga humpatu...hii ni technology rahisi hata kwa watu wa kawaida wanaweza kuitumia...
 
of course ni sawa, atawasiliana kivipi bila simu ya mkononi.... kuna mambo mengine ambayo anahitaji kuwa na private conversations kama vile ya kinyumbani....
 
Ninaomba simu ya JK. Nina mambo mengi ya kuongea naye, kwa manufaa ya taifa. Pengine tukiongea kiushikaji atasikia zaidi!!!! Mwenye hiyo namba naomba anitumie kwenye PM, ni serious jamani!!!!
 
hii namba ndo anakuwa anapokea haraka sana, 0754777775. sijui kwa nini yeye bado anatumia vodacom wakati raia tumeanza kugoma!
 
hiyo ni kitu sahihi,c kla kitu kifahamike kwa ma bodgard,maana mengine ni personal
 
Hamjambo ndugu zangu. Mimi nimejiunga na Jamii forum hivi karibuni nataka kupost mada fulani lakini sijaelewa namna ya ku post. Tafadhari naomba nieleweshwe.

Enny
 
Duh ha ha kwahiyo hata hela asibebe? hamchelewi kusema hata salary asipewe, maana hatumuoni viti virefu na kwenye gahawa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom