JK na PM wake wapingana kuhusu Kipengele cha dini kwenye Sensa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK na PM wake wapingana kuhusu Kipengele cha dini kwenye Sensa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Aikaotana, Aug 12, 2012.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. A

  Aikaotana Senior Member

  #1
  Aug 12, 2012
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 199
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huko Mbeya kwa mujibu wa vyombo vya habari JK kasema haya,
  “Nafahamu kuwepo madai ya baadhi ya watu kutakaswali la watu kuwa na dini gani liingizwe. Swali hili halipo na halikuwahikuwepo kwa nia njema kabisa,” alisema na kuongeza: “Hatupangi mipango yetu yamaendeleo kwa misingi ya dini au rangi za watu bali kwa kuzingatia maeneo nashughuli, mambo ambayo hunufaisha watu wa dini zote”.
  Wazirimkuu NAE ''Kipengele cha dinikimeondolewa katika sensa kwakuwa hakina tija kwa maendeleo ya nchi''
  Inaonesha hapa waziri mkuu ana kumbukumbu kuwa kipengelekilikuwepo, kikaondolewa.Bosi wake hajui,
  Ndugu wanajamvi, waislamu hawahesabiwi kwa sensa isiyo nakipengele cha dini, tunajua pia kuwa BAKWATA watahesabiwa. Ni wazi kuwaserikali inaweza kufanya chochote lakini haiwezi kuwalazimisha watu kufanyachochote, haikuwa hivyo tokea mamlaka zilipoanza kuwepo duniani. KWA HILI LA SENSA YA MWAKA HUU TUNASEMA, WAISLAMUHAWATAHESABIWA BAKWATA, WAKRISTO NA WAPAGANI WAMEKUBALI KUHESABIWA

  1. Kwa nini kipengele cha sensa kiliondolewa?
  Inasadikika kuwa sensa ya mwisho kufanyika wakati waukoloni Tanzania ilikuwa na Waislamu asilimia 60, Tukisema kuwa serikaliilikiondoa kipengele hiki kwa sababu maalumu ikiwemo kuwa na nafasi yakuendeleza na kusadikisha takwimu za uongo ili kushamirisha Mfumo Kristo (MK)Tanzania tunakosea?

  1. Kwa nini taasisi mbalimbali za serikali na binafsi zimekua zikitoa takwimu za watu na dini zao?
  Mfano 0fisiya waziri mkuu inadai wakristo ni 45%-waislamu 35%. TBC1, imetangaza wakristoni 52%-waislamu 32%.Bodi ya watalii -Christianity and Islam are the predominantreligions of Tanzania. About 40-45% of the population practice Christianity,about 35-40% practice Islam.,Tovuti kikatoliki (RCNet) waislamu 34%- na wakristo ni 44%
  Na hapa kuna hoja mbili,
  a) kwa nini takwimu zinatofautiana? na b)kwa nini pamoja na kutofautiana zotezinaonesha wakristo ni wengi kuliko waislamu?
  Kwa kawaida jambo la uongo lazima hukwama, takwimuzinatofautiana kwa sababu ni za uongo, Zote zinaonesha wakristo ni wengi kwa sababu za kukidhimatakwa ya MK.
  Mkurugenzi wa TBC alipoulizwa kuhusu takwimu katoa wapi aliishia kuomba radhi, kakosea,swali ni je kakosea nini? Amekuwa akikosea mambo mangapi ya kitaifa kwa ujumlawake kama lilivyo hili? Huu ndio MK
  3.Kwa nini kiwepo kipengele cha kuhesabiwa kwa nyumba zaibada?
  Waislamu wakisema kuwa kuhesabiwa kwa nyumba za ibadapekee kunaweza kutumiwa na wapotoshoshaji wa Umma kupitia MK, kuwa Wkristo niwengi kwani siku hizi kuna utitiri wa madhehebu kikristo na makanisa binafsi hatakama yana waumini wachache achilia mbali uyoga wa makanisa yanojiita ya wokovu?Kwa nini nyumba za ibada na sio na wanaoabudu humo?, Serikali inataka kugawamisala misikitini na mabench kanisani?
  Waislamu wa leo ni tofauti na wa enzi hizo, wanajuawanachokifanya na hili la sensa ni moja na mengine yatakuja,hatuhitajikumtafuta kiongozi wala Sheikn Ponda kwahili, elimu tulishapata , macho yalishafumbuliwa na Tunaelewa athari za mfumoKristo katika jamii

  1. Tulisadikishwa kuwa waislam hawakusoma, kumbe data zinaonesha NECTA inawapunguza
  2. Tukasadikishwa kwamba hawajengi Mashule na Hospitali ila wanajenga misikiti, kumbe wenzetu wanajenga kupitia fedha wanazopewa na serikali hii hii kupitia MoU
  3. Tukasadikishwa kuwa nchi hii haina dini , kumbe serikali yetu ina mfumo Kristo ambao haukuandikwa popote lakini unafanya kazi zake kwa siri na waziwazi
  TUMEKATAA KWENDA KWA MATAKWA YA MK, NARUDIA WAISLAMUHATUHESABIWI.
   
 2. Leembaswagger

  Leembaswagger Senior Member

  #2
  Aug 12, 2012
  Joined: Aug 1, 2012
  Messages: 100
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  True 100%,..tel em
   
 3. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #3
  Aug 12, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  duh ! ! ! !
   
 4. Tabutupu

  Tabutupu JF-Expert Member

  #4
  Aug 12, 2012
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 5,650
  Likes Received: 4,412
  Trophy Points: 280
  Kuna jamaa seroiusly kwa data zake watanzania tupo million 97.
   
 5. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #5
  Aug 12, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Sasa kama akili zimo vichwani kwenu, ondoeni na Mawakala wa sensa ambao wamo kibao kwenye list ya wahesabuji ili tujue mna machungu ya kumeza wembe.
  Msianze mambo ya DC aliyedai kuvuliwa Hijabu, anayemiliki shamba la NOAH huko Kimara, huku akijidai kuwa yeye ni mwanaibada wenu swafi na hatumii noah.
  Lol! ...vichekesho!
   
 6. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #6
  Aug 12, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 801
  Trophy Points: 280
  Tumesikia, msihesabiwe si basi!
   
 7. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #7
  Aug 12, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Hawa ndugu zetu kwa kukomalia mambo madogo madogo hawajambo.
   
 8. H

  Hansen Nasli JF-Expert Member

  #8
  Aug 12, 2012
  Joined: Mar 18, 2012
  Messages: 881
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45
  HAtuhesabiwi waislam hao bakwata wahesabiwe sisi watuache
   
 9. Leembaswagger

  Leembaswagger Senior Member

  #9
  Aug 12, 2012
  Joined: Aug 1, 2012
  Messages: 100
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  waislam ni great thinkers wameona mbali,athari yake ni kubwa sana
   
 10. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #10
  Aug 12, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,129
  Trophy Points: 280
  Hawa jamaa wanaongea wasio ya simamia. Mbona waislamu kibao wako kwenye kuhesabu watu? Na wengine wanalia kukosa hiyo kazi..
   
 11. T

  Thesi JF-Expert Member

  #11
  Aug 12, 2012
  Joined: Aug 8, 2010
  Messages: 998
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Waislamu wako wengi wenye elimu na wameelimika. Walioelimika hawana akili mgando kama ulizozitoa kwenye hoja ya sensa. Walioelimika wapo wengi tu tena ni viongozi wa nchi hii wengi wao kwa sasa kuliko hata wakristo lakini hawana tena mawazo ya kipuuzi kama mlizokuwa nazo wenzao ambao hamna elimu au mmesoma lakini akili zenu zimezibwa na mafuta ya dini hamwezi kuona vitu kwa uhalisia uliokuwa tofauti na dini.

  Wa kwanza anaitwa Jakaya Mrisho Kikwete, ndiye Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wa pili anaitwa Dr. Gharib Bilal, ndiye Makamu wa Rais, wa tatu anaitwa Dr. Mohamed Shein, ndiye Rais wa Zanzibar, wa nne ni jaji mkuu wa nchi hii, wa tano ni makamu wa Rais wa kwanza na wa pili wa Zanzibar. Wengine ni mawaziri kwenye wizara mbalimbali naa hata mkuu wa tume ya sensa naye ni muislamu pia.

  Hebu wewe unayejiita msomi wa kiislamu niambie huo mfumo ukristo unapita wapi wakati viongozi wakuu wa serikali ni waislamu? Manake kwa wakristo kiongozi mkuu serikalini ni waziri mkuu Mizengo Pinda. Ina maana Pinda kawazidi kete hao viongozi walio waislamu wenzenu?

  Siamini kuwa sensa inapaswa kuhesabu watu kwa dini zao kwani hiyo inaweza kufanywa na madhehebu yenyewe. Kila dini iweke kitabu kwenye msikiti au kanisa na kama ina malengo ya kupata watu wake ni kuwaandika majina kisha kujumlisha idadi yao nchi nzima. Kama hili dogo linawashinda mpaka mnatishia kususia sensa mtaweza lipi?
   
 12. t

  tunda Member

  #12
  Aug 12, 2012
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Very interesting... am researching on factors influenced countries like USA, Egypt and UK did not include a question on Religion on their previous two census. However, UK had it but not mandatory. In US the body dealing with USA data like our Bureau of Statistics is not the source of religious data... the law prohibits. Only religious bodies should be the source of religious data... research continues..... MIND you my research is on reasons!
   
 13. m

  markj JF-Expert Member

  #13
  Aug 12, 2012
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 1,756
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  hiyo itakuwa sio sensa! Na hakutokuwa na details sahihi hapo.
   
 14. Kabembe

  Kabembe JF-Expert Member

  #14
  Aug 12, 2012
  Joined: Feb 11, 2009
  Messages: 2,238
  Likes Received: 931
  Trophy Points: 280
  Islam wengi kuliko Wakristo nchini Tanzania,then what next? kuna faida au hasara gani kwa wingi wa waislam na uchache wa Wakristo?hebu tuelimi sheni enyi msioishiwa na malalamiko na lawama juu ya wengine.
   
 15. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #15
  Aug 12, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,287
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Yaani ugomvi wako ni hizo DINI mbili tu hakuna DINI nyingine?, haya km Waislam ndio wengi utafurahi ili iwe nini.
  Katika wanaohesabu Sensa wengi ni hao Waislam na watakuhesabu hata ukilala Msikitini, Rais amesema hakuna kipengele hicho hata na PM
  Goma usigome tutamtafuta mwenye nyumba wako na Balozi watatuambia tu mlilala wangapi na una wake wangapi? maana najua mnachoogopa
   
 16. K

  Kolero JF-Expert Member

  #16
  Aug 12, 2012
  Joined: Apr 11, 2010
  Messages: 493
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kipengele cha dini kishafutwa tangu 1967, na hakimo pia hata Kenya. Hizi dini zote mbili zimeletwa toka nje na hazina uhusiano na Utanzania wetu na hata maendeleo ya nchi yetu hata tukijua kuwa hizi dini zina wanachama wangapi, after all, haya yanaweza kufanywa na dini zenyewe ili kujua idadi yao.

  Siye tusiyekuwa katika dini zenu hizo za vitabu hatuoni mantiki ya kulumbana, la maana dini zote mbili fanyeni wenyewe sensa yenu mtuletee idadi yenu ingawa sijui itatusaidia nini na kwa tija ipi, kama makanisa jengeni, kama misikiti jengeni kadiri mnavyotaka. Imefikia wakaati tuaache ushabiki usio na maana hasa ukizingatia dini zote hizi zimeletwa tu.

  Na japa ndipo naungana na Karl Marx aliyesema "Dini zinapumbaza" na kweli, ukipumbazwa na dini, basi hali itakuwa kama hii malumbano hata katika masuala ambayo kila dini ingeweza kufanya yenyewe kujua idadi ya wanafuata hizo dini ili kupanga mipango yao ya kidini.
   
 17. Rogate

  Rogate JF-Expert Member

  #17
  Aug 12, 2012
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 215
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakati viongozi wetu wanasain mikataba ya gesi na mafuta kwenye bandari ya mtwra sisi tunalumbana. Tumetegwa patamu. Sasahivi meli zinachukua gesi na mafuta huku wakituhadaa kuwa wanafanya uchunguzi. Tuendelee kulumbana.
   
 18. mndwadage

  mndwadage JF-Expert Member

  #18
  Aug 12, 2012
  Joined: Jul 15, 2012
  Messages: 345
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwani waislam mnataka mhesabiwe ili iweje.?
   
 19. Jiwejeusi

  Jiwejeusi JF-Expert Member

  #19
  Aug 12, 2012
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 755
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  From the begining people used God to justify their unjustifyable.
   
 20. Nkwesa Makambo

  Nkwesa Makambo JF-Expert Member

  #20
  Aug 12, 2012
  Joined: Aug 26, 2011
  Messages: 4,765
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  i
  Kwa sababu una akili na unatafakari, but not the advanced chips. wao,bila serikali kuwahesabu hawatashiriki. lakini na wao ni sehemu ya watanzania,tunalo na hatuna jinsi nibudi tuishi nalo.
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...