Jk na mustakabali wa ccm | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jk na mustakabali wa ccm

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mahangu, Nov 11, 2010.

 1. m

  mahangu Senior Member

  #1
  Nov 11, 2010
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 145
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  mwaka 1982 ndio nilijua CCM vizuri maana wakati huo mwalimu nyerere alikuja kijijini kwetu wakati ambao mwambao wa ziwa nyasa kulikuwa na dalili za kuingia njaa. mwaka 1985 nikawa chipukizi wa ccm na wakati huo chama hiki kilikuwa chama cha Wakulima na Wafanyakazi, lakini kadri muda ulivyoenda chama kiliaanza kupoteza hatamu na hata ile miiko yake ikaanza kupotea hasa baada ya kuingia kwa mpango ulioitwa SAP ( Structural Adjustment Programme), nchi ikianza kuwa ya mabapari na wana CCM waliokatazwa kuchanganya siasa na biashara na kurudikia utajiri wakaanza kuchanganya mambo. Mzee makapa alijitahidi kuepusha ndugu zetu watanzania wa asili ya ASIA kuingia katika chama na kugombea na nafasi, kwa bahati mbaya zaidi mwaka 2005 walijitokeza wengi zaidi na kuanza kushika nafasi, na ndipo kundi la wanamtandao lilipopata nguvu ndani ya chama.
  Baada ya kuisha uchaguzi kj akaanza kuwatenga watu makini waliofanya kazi nzuri na mkapa e.g Magufuri, Mwandosya etc akaingiza wanamtandao wenzake e.g Masha, Membe ( aliyemsaliti Hance Kitine kule Canada), Meghji( aliyeshindwa maliasili), Kapuya ( aliyeharibu elimu tanzania), Mungai ( aliyefiuta umiseta tanzania) etc orodha ni ndefu.
  Alishauriwa bwana hao rafiki zako sio wazuri wana maslahi binafsi akapuuza na kujibu urais wangu hauna ubia na mtu.baada ya majibu hayo wazee wote na makereketwa wa chama wanaojua misingi ya chama wakaanza kukao kando kumwachia jahadi asiyetaka ubia, matokeo yake rushwa ikaenea ndani ya chama, makundi kinzani yakazidi kukua n.k, mwaka 2010 chama kikaadhibiwa na wenye nacho ( wakulima na wafanyakazi), hajasikia tu, kapigana vita kumtoa Sitta uspika. Ndugu zangu CCm yumkini si shwari tena, chama kimekwisha kwa kuongozwa na watu watano au sita ( JK, Makamba, Lowasa, Rostam, Chenge). Kitakufa kabla ya 2015. wabunge wa CCM chagueni spika toka vyama vingine, hao walipitishwa ni kwa maslahi ya wachache na wamefanya hivyo makusudi ili waweze kuwaendesha kirahis walijua Sitta ni chuma cha pua.

  CCm ilipotoka kukaribisha watanzania wasio wazalendo ambao wewe mweusi ukienda kwao huwezi pata hata nafasi ya mwenyekiti wa mtaa, lakini huku sisi weusi ni kama mbwa kwa chatu.
  Tubadilike ndugu zangu, CCM hii si ile ya Mwalimu
   
 2. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #2
  Nov 11, 2010
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Sawa mkuu nimekukubali, CCM sasa imekuwa chama cha Mafisadi na kiongozi wao mkuu ni kikwete. Wakati wa kuikomboa nchi hii kutoka kwa hawa manyang'au umefika miaka 5 siyo mbali sana, ila kama kuna uwezekano lolote litokee hata kufa kwa mtu ili mabadiliko yatokee mapema zaidi.
   
Loading...