JK na mgombea ubunge CCM Muhambwe, Kibondo, (Mkoa wa Kigoma) UOZO, AIBU kubwa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK na mgombea ubunge CCM Muhambwe, Kibondo, (Mkoa wa Kigoma) UOZO, AIBU kubwa!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mwanaukweli, Sep 20, 2010.

 1. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #1
  Sep 20, 2010
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 180
  Na Mwandishi wetu
  Raia Mwema
  Septemba 15-21 (Ukurasa wa Tatu)


  Katibu wa CCM wa Mkoa wa Kigoma, Moudline Castico, aliyedaiwa kupigania chama hicho kutomteua mgombea ubunge anayehusishwa na kashfa za mauaji ya albino na ujambazi, amehamishiwa makao makuu ya CCM, mjini Dodoma, Raia Mwema limebaini.

  Taarifa za uhakika zinasema kuwa Castico alipewa barua ya uhamisho saa sita za usiku siku ambayo mgombea urais wa CCM, Jakaya Kikwete alifika Kigoma kwa ajili ya kampeni.

  Katika moja ya matoleo ya gazeti hili, hasa baada ya kuhitimishwa mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM, Dodoma uliopitisha wagombea ubunge na udiwani, liliripoti kupitishwa mgombea ubunge mwenye kashfa ya mauaji ya albino na ujambazi katika Jimbo la Muhambwe, Kibondo (Jamal Tamim)

  Katika habari hiyo, gazeti hili liliripoti habari za ndani kuwa Katibu wa CCM Mkoa wa Kigoma ndiye aliyeongoza hoja za kumpinga mgombea huyo, akirejea mazingira halisi ya Jimbo anakogombea Jamal Tamim.

  Kwa mujibu wa habari hiyo ya ndani ya NEC-CCM, Katibu huyo alilazimika kutoa maelezo kwa nini mgombea husika asipitishwe. Anadaiwa kutoa maelezo hayo wakati wa mikutano wa Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Kibondo na ya Mkoa wa Kigoma.

  Katika mkutano wa mkoa, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Joseph Simbakalia, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, anadaiwa kuwasilisha ripoti iliyochambua madhambi ya mgombea husika.

  Hata hivyo katika mkutano huo wa NEC , mjumbe mmoja kutoka Kigoma anatajwa kumtetea Jamal Tamim (ambaye ana asili ya kiasia) ambaye anaungwa mkono na wafanyabiashara wakubwa mkoani Kigoma (kwa motisha gani????) ambao maadili yao yana utata. Pia mgombea huyo anaungwa mkono na mfanyabiashara na mwanasiasa maarufu mkoani Tabora ambaye ni mjumbe wa NEC [Rostam Aziz (asili ya kiasia na mfanyabiashara pia)].

  Ikiwa imepita miezi takriban miwili sasa, taarifa za hivi karibuni kutoka Kigoma zinabainisha kuwa kile kinachoelezwa kuwa ni 'fitina' za kundi la wafanyabiashara; hasa wenye utata kimaadili, limepambanua kutumia ushawishi wa 'mtandao' kumng'oa katibu huyo Kigoma.

  Baada ya kupewa barua ya uhamisho, Katibu huyo anadaiwa kutengenezewa zengwe jingine kwamba alijaribu kubadilisha majina ya wagombea saba wa udiwani, Jimbo la Kigoma mjini akikwaruzana na mgombea ubunge, Peter Serukamba.

  Habari kutoka ndani ya CCM Kigoma zinadai kuwa Katibu huyo aling'olewa kutokana na kujaribu kusaidia kuleta vurugu kwa kushawishi kamati za maadili na kamati za siasa kuwaengua na kuwapa alama za chini wagombea walioongoza kwenye kura za maoni. Anadaiwa kudhamiria kuwaengua wagombea zaba wa udiwani Manispaa ya Kigoma Ujiji na kuwaweka washindi wa pili na tatu katika kata za watu hao waliokusudiwa kuenguliwa.

  Hata hivyo gazeti hili liliwasiliana na Katibu huyo ambaye alithibitisha kuhamishwa kutoka Kigoma hadi Dodoma lakini akipinga madai mengine dhidi yake.

  "Sio ajabu kuhamishwa, ni masuala ya kazi. Kuhusu kujaribu kupangua madiwani hilo ni suala la vikao si la kwangu .... sio suala la mtu binafsi. Wanaosema hivyo hawajui chama kinaongozwa vipit.

  "Wananisema kwa sababu wanajua mimi ni mwanasiasa na kiongozi bora, ninayesimamia kazi kikamilifu. Simwogopi mtu yeyote wala sifanyi siasa za makundi. Namwogopa Mungu tu. Nimeonyesha uwezo wangu wa kazi Kigoma na kwingine na ndiyo maana nabadilishwa kazi kutokana na utendaji mzuri. Na kwa sababu wananihusisha kwenye mambo yao kwa nia wanazozijua hiyo inazidi kunijenga kiuongozi maana yake kuna mambo ya msingi nayasimamia bila kujali siasa za makundi,

  "Ukiona wanakuandama au kukujadili kila wanapokutana ujue una thamani fulani ya kiuongozi ambayo labda wao hawana," alijibu Katibu huyo wa zamani wa Kigoma katika mazungumzo yake na mwandishi wa gazeti hili.

  Lakini wakati majibu ya kigogo huyo yakiwa hayo, taarifa zaidi kutoka Kigoma zinaeleza kuwa kiongozi huyo alikuwa akimpigania mbunge (Kijiko) aliyemaliza muda wake katika Jimbo la Muhambwe ambalo CCM imemteua Jamal Tamim anayetuhumiwa kwa mauaji ya maalbino na matukio ya ujambazi.

  Inadaiwa kuwa kiongozi huyo aliyehamishwa alikuwa akiungwa mkono na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Joseph Simbakalia na Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, John Mongela, katika kuhakikisha mgombea ubunge mwenye kashfa za mauaji ya maalbino na ujambazi hagombei kwa tiketi ya CCM ili kunusuru ushindi wa chama hicho.

  Lakini wakati mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya na kiongozi huyo aliyehamishwa wakitajwa wakati wa kura za maoni kuhakikisha Jamal Tamim hachaguliwi, Mwenyekiti wa CCM Kigoma, Azim Premji (mfanyabiashara pia mwenye asili ya kiasia) na mjumbe wa NEC-CCM, Muhsin Abdallah Sheni (mfanyabiashara tajiri mwenye asili ya kiasia na maadili yenye mashaka) walitajwa kumtetea Jamal Tamim (mwenye nguvu ya pesa zenye kutiliwa mashaka, mwenye asili ya kiasia pia) kwenye vikao mbalimbali kwa wakati huo.

  Mgombea huyo anayetetewa na Premji pamoja na Muhsin Sheni huku akipingwa na Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya, kwa kuzingatia taarifa za Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya na Mkoa, anadaiwa pia kuwa amewafungulia mashtaka viongozi wa dini na kujikuta katika mgogoro mzito uliovuka mipaka kutoka kwa viongozi wa dini hadi wapiga kura.

  Viongozi hao wamekuwa wakimtetea Jamal (muasia mwenzao, na mwenye pesa kama wao) ndani ya NEC kwa hoja kuw kama angekuwa anahusika na mauaji ya maalbino au matukio ya ujambazi, basi viongozi wa dola akiwemo Mkuu wa Mkoa, Simbakalia wangepaswa kumchukulia hatua lakini hawakufanya hivyo.

  Lakini wakati hayo yakiendelea, taarifa kutoka jimbo anakogombea mtuhumiwa huyo zinabainisha kuwa mgombea husika amewashtaki Padre wa Kanisa Katoliki ambaye ni Paroko wa Parokia ya Mabamba, Padre Adrian Jimenez, pamoja na kiongozi wa kiislam Maalim wa Madrasa ya Mabamba kwa madai ya kumkashifu.

  Tukio hilo la kufunguliwa kwa kesi hizo linatajwa kuibua mgogoro mkubwa kati ya mgombea huyo na viongozi wa dini, ikielezwa kuwa mgogoro huo sasa umevuka mipaka na wananchi wanaunga mkono viongozi wao wa dini.

  Katika hatua nyingine, habari zaidi za uhamisho wa Katibu wa CCM Kigoma, Castico zinabainisha kuwa alipewa barua ya uhamisho kwenda kuripoti makao makuu ya CCM Dodoma saa sita usiku, siku ya mkutano wa kampeni ya mgombea urais wa CCM, Jakaya Kikwete mkoani Kigoma.

  Chanzo chetu cha habari kinaeleza kuwa kabla ya kikao cha NEC-CCM na hasa baada ya kupata taarifa ya mvutano uliokuwapo Kigoma, Jakaya Kikwete, ambaye ni mwenyekiti wa CCM Taifa aliwaita Dar es Salaam viongozi watatu wa CCM Kigoma ambao wanaingia kwenye kikao cha NEC-Taifa ili kuzungumzia mwenendo wa zilizokuwa kura za maoni ndani ya chama chao Kigoma. Viongozi hao waliokutana na Kikwete kwa wakati huo ni pamoja na Mwenyekiti wa CCM Kigoma, Azim Premji, Katibu wa Mkoa, Castico, na Mjumbe wa NEC, Muhsin Abdallah Sheni.

  Raia mwema iliwasiliana na Mwenyekiti wa CCM Kigoma, Azim Premji kuhusu uhamisho wa katibu huyo na masuala mengine anayohusishwa kuyafanya na hatima ya CCM katika Jimbo la Muhambwe ambalo wanadaiwa kumteua mgombea ubunge mwenye elimu ya darasa la saba na mtuhumiwa wa mauaji ya maalbino ambaye alipendekezwa katika kura zaa maoni zilizoendeshwa na serikali kubaini wauaji na wauzaji wa viungo vya albino.

  Katika majibu yake kuhusu uhamisho wa Katibu huyo, Premji alisema huo ni uhamisho wa kawaida na kwamba yeye si mtu wa kwanza kuhamishwa kituo cha kazi.

  "Suala la kumhamisha kiongozi ni la kawaida, pengine imetokea anahitajika zaidi huko alikopelekwa lakini hakuna matatizo hapa." (!!!!!!!????????) Kampeni zinakwenda vizuri."

  Alipoulizwa kuhusu mgombea mtuhumiwa wa mauaji ya maalbino na ujambazi, ambaye pia ameingia katika mgogoro na viongozi wa dini kwamba mazingira yanaweza kikinyima ushindi CCM, alisema hilo ni suala lake binafsi (Jamal) na si la chama. (!!!!!!!!!???????)

  "Mgombea wa Muhambwa kuwa na matatizo na viongozi wa dini ni lake binafsi, chama hakinga mgogoro na tunaamini tutapata kura (my comment: kwa rushwa???) na viongozi wa dini kwa sababu ni watu wazima wanajua. Ni suala lake binafsi, haliwezi kuathiri kampeni" alisema.
   
 2. PayGod

  PayGod JF-Expert Member

  #2
  Sep 20, 2010
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 1,255
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  kupitishwa mgombea ubunge mwenye kashfa ya mauaji ya albino na ujambazi katika Jimbo la Muhambwe, Kibondo (Jamal Tamim)

  Hivi hawa c c m waka akili sawasawa?
   
 3. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #3
  Sep 20, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Ccm yote imejaa majambazi
   
 4. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #4
  Sep 20, 2010
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 180
  Inayothaminiwa ni pesa. Lakini ona walivyoanza taratibu hawa matajiri wa kiasia: Premji, Sheni, Rostam, Dewji nk na wanateteana. Huyo naye anataka kwenda kuwaongezea nguvu
   
 5. J

  Jafar JF-Expert Member

  #5
  Sep 20, 2010
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Dawa ni kuwang'oa madarakani.

  We Katibu wa CCM njoo CHADEMA.
   
 6. Negotiator

  Negotiator JF-Expert Member

  #6
  Sep 20, 2010
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 303
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wauwaji wanapewa nafasi ya kuibuka kidedea kisa tu ni wana ccm
   
 7. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #7
  Sep 20, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Hiyo ndo ccm bana!!

  Ubabaushaji ni jadi!!
   
 8. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #8
  Sep 20, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135

  Unajua kuna watu makini sana CCM wameamua kuligawa jimbo hili kwa CHADEMA, kwa hiyo msiwe na wasiwasi it is a good work by thithiem
   
 9. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #9
  Sep 20, 2010
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 180
  CCM wanaweza kubadili maandiko yawe hivi:

  "Heri wenye pesa chafu, utawala wa ccm ni wao!

  Heri wenye kuiba, maana wataitwaa nchi!!!"
   
 10. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #10
  Sep 20, 2010
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 180
  Wana JF mliopo Kigoma na Kibondo: makala hii mtusaidie kuisambaza kwa watu.

  Jamal anawanunua kwa rushwa, halafu anarudisha kwa namna zake anazojua.

  Tusimruhusu pesa zake chafu zimwingize bungeni, ni hatari sana.
   
 11. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #11
  Sep 20, 2010
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 180
  Ametumia rushwa sana kwa wananchi. Halafu anatoa rushwa huku akiandika majina ya aliowapa pesa, na kuwatisha kuwa akishindwa atarudi kuchukua pesa zake. Ni Sh. 5000 tu anazotoa kwa watu na ni kwa hizo amenunua kura za maoni.

  TAKUKURU pia inaonekana imenunuliwa kwa bei nzuri na huyu JAMAL, na hawamsumbui hata kidogo katika "mambo" yake.
   
 12. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #12
  Sep 20, 2010
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 180
  Kwa nchi za wenzetu hii ingemrudia JK mwenyewe. Sisi ni kama tumezoea hatushtuki sana.
   
 13. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #13
  Sep 20, 2010
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 180
  Kwa nchi za wenzetu hii ingemrudia JK mwenyewe. Sisi ni kama tumezoea hatushtuki sana.
   
 14. M

  Mkandara Verified User

  #14
  Sep 21, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kama hili lina ukweli basi Chadema wamekabidhiwa silaha nyingine na CCM....
   
 15. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #15
  Sep 21, 2010
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 180
  Hili ni kweli mkuu. Mimi ni wa huko, na inatia kichefuchefu jinsi jamaa wa CCM wanavyothamini fedha za huyu ndugu.

  Lakini Chadema wamemuweka Mh. Ntagazwa ambaye alishawaudhi na kuwachosha wananchi. But kuna chance.
   
 16. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #16
  Sep 21, 2010
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 180
  Restuta James, Sharon Sauwa, Jacqueline Massano na Mary Edward wa Gazeti la Nipashe waliripoti kuhusu ubadilishaji wa taarifa kutoka kwa makatibu wa Wilaya kwenye Kamati Kuu ya CCM, ambao ndio uliwasaidia watu kama Jamal kupitishwa. Hapa nanukuu sehemu ya makala hiyo iliyochapishwa Nipashe Jumapili baada ya Kamati Kuu kukaa.

  " zimezuka tuhuma nzito kuwa taarifa za baadhi ya wagombea zilizofikishwa katika vikao vya chama hicho kwa ajili ya kutolewa uamuzi wa nani amepita kwenye kura za maoni zinadaiwa kubadilishwa.

  Taarifa zilizopatikana jana kutoka ndani ya kikao cha Kamati Kuu ya CCM (CC) ambayo ilikuwa ikipitia majina hayo kwa ajili ya kupelekwa kwenye Halmashauri Kuu (NEC) ili kutolewa uamuzi wa mwisho zimedai kuwa baadhi ya wagombea ambao walipita katika kura za maoni wameilalamikia sekretariati ya chama hicho kuwa taarifa zao zimebadilishwa.

  Wajumbe hao wamelalamika kuwa taarifa ambazo walitakiwa kuziwasilisha kwa kutumia `flash' badala ya kuzichapisha, zilibadilishwa kwa lengo la kubadili matokeo ili waondolewe kwenye nafasi zao.

  Viongozi hao ambao hawakupenda majina yao yaandikwe gazetini, walisema sehemu kubwa ya taarifa zilizowasilishwa kwa flash zimebadilishwa.

  Malalamiko ya viongozi hao yamezidi kudai kwamba utaratibu wa kuwasilisha mapendekezo ya mikoa na wilaya yakiwa hayajachapishwa, ni mkakati wa kubadilisha taarifa kwa ajili ya kuwabeba baadhi ya wagombea.

  "Taarifa nyingi zimebadilishwa na ukumbuke kwamba katibu wa wilaya akishawasilisha taarifa hawezi kuipata tena hivyo hata ikibadilishwa hawezi kutoa ufafanuzi popote," alisema kiongozi mmoja wa CCM.

  Taarifa za mkoa wa Kigoma zinaonyesha kwamba mapendekezo ya kamati ya siasa ya halmashauri kuu ya Wilaya ya Kibondo, ilipinga ushindi wa Jamal Tammim lakini taarifa iliyowasilishwa kwenye sekretarieti imeonyesha kupendekeza agombee.

  Taarifa ya kikao cha kamati hiyo cha Agosti 3, 2010 kilichomalizika saa 8:10 usiku, kiliwapendekeza wagombea wawili katika jimbo la Muhambwe ambao ni mbunge aliyemaliza muda wake, Felix Kijiko na Richard Kigaraba ambao wanadaiwa kuenguliwa na sekretarieti baada ya taarifa hiyo kubadilishwa.

  "Pamoja na kwamba Tamim alishinda lakini alitumia rushwa, ana kesi dhidi ya kanisa Katoliki na tuhuma nyingi mbele ya jamii," ilisema sehemu ya taarifa ya kamati hiyo.

  Mchungaji wa Kanisa la Anglican katika Wilaya ya Kibondo, Benjamin Saimon, alisema muungano wa makanisa wilayani humo hayatamuunga mkono Jamal Tamim.


  Taarifa zaidi kutoka Kibondo zinaeleza kwamba wanachama wa CCM wameanza kukusanya kadi zao kwa nia ya kuzirejesha, iwapo uongozi wa juu wa chama utampitisha mgombea huyo.

  Tayari wagombea 10 wamekataa ushindi wa Jamal akiwemo Arcado Ntagazwa ambaye ameshakihama chama hicho, Barakabitse Mbogoyo, Brighton Gwamagobe, Dk. Chrispine Shami, Edgar Mkosamali, Emmanuel Gwegenyeza, Regina Kayabu, Felix Kijiko, Salome Chuma na Thomas Buhahate.
   
 17. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #17
  Sep 21, 2010
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Tatizo la Muhambwe ni kwamba Chadema wamemuweka Mzee Ntagazwa ambaye kwa kweli amechoka kisiasa. Kwa wale waliokaa Kibondo muda mrefu watakubaliana nami kuwa mzee huyu pamoja na kuwakilisha wilaya hiyo kwa muda mrefu, hana rekodi yeyote ya kujivunia hadi awe nafasi ya kumshinda Jamal.
  Wote wawili wanatokea vijiji jirani mpakani na Burundi, wanafahamiana vizuri na ni Jamali huyu huyu ambaye CCM wilayani wamekuwa wakimtegemea wakati wa kampeni au kunapokuwa na ugeni wa kitaifa wilayani.

  Upinzani wangeweza kuchukua jimbo hili kama wagombea wengine makini wangejaribu na siyo Ntagazwa!
   
 18. O

  Ome Member

  #18
  Sep 21, 2010
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 79
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15
  nipo pamoja nawe kakalende, huyo Ntagazwa hafai hata kidogo kushika madaraka, amekosa soko CCM ndio mana kakimbilia CHADEMA. mi naona kungekuwa na sheria mtu akihama chama kwenda kingine sio afike na kugombea awekwe benchi kwanza bse hiyo ni uroho wa madaraka.
   
 19. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #19
  Sep 23, 2010
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 180
  But if we are to go with the lesser Evil: Who will be the ideal choice? Ntagazwa or the Notorious Jamal Tamim?
   
Loading...