JK na 'Mduara' wake

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,825
287,849
Rais Kikwete sasa aendeleza 'mduara'

Na Saed Kubenea
Mwanahalisi

RAIS Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko ya tano ya Baraza la Mawaziri tangu ashike madaraka ya kuongoza nchi, takribani miaka miwili na nusu iliyopita.

Hata hivyo, wachunguzi wa mambo wanasema, “Kikwete bado anashindwa kutumia nafasi anazopata kuimarisha serikali yake. Badala ya kujenga serikali, mabadiliko mengi yanaishia kuibomoa.”

Wanatoa mfano wa rais kuwazungukia watu walewale kana kwamba nchi haina watu wengine wenye uwezo wa kushika nyadhifa za juu serikalini.

Katika mabadiliko ya sasa, rais amemteua Dk. Shukuru Kawambwa kuwa Waziri wa Miundombinu, kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Andrew Chenge, aliyejiuzulu wadhifa huo kutokana na tuhuma za ufisadi katika ununuzi wa rada.

Dk. Kawamba ni mbunge wa Bagamoyo, mkoani Pwani ambaye tayari amekuwa waziri katika wizara tatu na sasa ameingia wizara ya nne katika kipindi cha miaka miwili na nusu.

Wengine walionufaika na kujiuzulu kwa Chenge, ni Celina Kombani. Awali alikuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI). Kombani sasa amekuwa waziri kamili katika wizara hiyo.

Mwingine aliyenufaika na mabadiliko hayo, ni Aggrey Mwanri, ambaye ameingia kwa mara ya kwanza serikalini baada ya kuutema ukatibu wa Idara ya Itikati na Uenezi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ngazi ya taifa.

Inadaiwa Mwanri aliondolewa nafasi yake katika CCM kutokana na kile wengi wanasema alikuwa mtu wa kukubaliana tu na kauli za Katibu Mkuu Yusuf Makamba hadi akaitwa “Mr. Yes Man.”

Katika mabadiliko hayo, Stephen Wassira amehamishwa kutoka Wizara ya Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa (TAMISEMI) kurudi Wizara ya Kilimo na Ushirika.

Wengine waliohusika na mabadiliko haya ni Profesa Peter Msolla anayetoka Kilimo, Chakula na Ushirika na sasa ameingia Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.

Wizara ya TAMISEMI sasa imeshikwa na Celina Kombani ambaye alikuwa naibu waziri wa wizara hiyohiyo.

Naibu mawaziri wawili, Makongoro Mahanga Miundombinu na Ezekiel Chiburunje wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana wamebadilishana wizara.

Mabadiliko ya sasa katika baraza la mawaziri yanachukuliwa na wachunguzi wa masuala ya siasa na utawala kuwa ya kukidhi haja ya muda mfupi tu.

Kwanza, haya ni mabadiliko ya wizara tu lakini sura za watendaji ni zilezile zilizoko serikalini. Inakuwa vigumu kuelewa iwapo hao wanaobadilishwa wanapelekwa kwenye maeneo wanayomudu zaidi au ni suala la kuziba nafasi iliyotokea.

Pili, inakuwa vigumu pia kwa wafuatiliaji wa menejimenti ya siasa kujua iwapo ni lazima kweli kwa waziri mmoja kuzungushwa wizara tatu au nne katika kipindi cha miaka miwili.

Ni kweli kwamba uwaziri ni kazi ya kisiasa, lakini katika mazingira ya Tanzania waziri ana uzito katika kusaidia kupanga na kusimamia utekelezaji katika wizara yake na taifa kwa ujumla.

Hii ina maana kwamba ili waziri aweze kutenda kazi zake hizo na nyingine, sharti awe amekaa katika wizara hiyo kwa muda muwafaka wa kumwezesha kujua taifa linataka nini kupitia wizara yake.

Hebu tuagalie wanaotokana na mabadiliko ya baraza ya wiki iliyopita. Dk. Shukuru Kawambwa alianzia Wizara ya Maendeleo ya Mifugo, akaenda Wizara ya Maji; akateuliwa kuongoza Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia na sasa ametua Wizara ya Miundombinu.

Katika hali ya kawaida huu ni “mchiriku wa kisiasa.” Ni kuzunguka na kuchezea hapohapo kama wafanyavyo wacheza ngoma ya mchiriku maarufu sana pwani ya Bahari ya Hindi.

Kama uteuzi wa waziri unaendana na mteuaji kujua kuwa yule anayemteua ana uelewa wa kuongoza wizara husika, basi mzunguko kama huu aliofanya Dk. Kawambwa unaweza kuonekana kuwa aina fulani ya utalii.

Vinginevyo, hii inaweza kuwa njia ya kuwapa baadhi ya mawaziri “fursa ya kujifunza” nini kinafanyika wapi katika wizara mbalimbali. Lakini, na kwa vyovyote vile, siyo kutenda kazi kama walivyotarajiwa.

Kwa waziri aliyeshika wizara nne katika kipindi cha miaka miwili, bila shaka hajui vya kutosha ni kitu gani kinahitajika katika kila wizara alimokwenda.

Mfano mwingine ni ule wa Stephen Wassira. Huyu naye tayari amezunguka wizara nne na kurudi mara ya pili katika wizara hiyohiyo ya kilimo.

Kwanza alikuwa Wizara ya Maji, akaenda Kilimo na Ushirika na baadaye TAMISEMI kabla ya kurejea Kilimo na Ushirika.

Kuna taarifa kwamba chini ya uongozi wa Wassira katika wizara ya kilimo na ushirika, tatizo la kukopa wakulima katika zao la korosho lilikuwa limeanza kukabiliwa kwa juhudi binafsi za waziri.

Vilevile kuna madai kuwa Wassira alikuwa anajiandaa kumaliza tatizo la wakulima wa pamba la kukopwa mazao yao na wafanyabiashara. Kabla hajamaliza kazi hiyo na kujenga misingi endelevu, akakwapuliwa na kupelekwa TAMISEMI.

Huko nako hakudumu. Mabadiliko ya juzi yamemrudisha katika wizara ya Kilimo. Wapo wanaotania kwa kusema Wassira “ameondoka hata kabla hajamfahamu katibu muhtasi wake.”

Mwingine ambaye amezunguka kama pia ni Profesa Msolla. Uteuzi wa sasa unafuatia kushika nafasi za waziri katika Wizara ya Sayansi, Elimu ya Juu na Teknolojia, na Wizara ya Kilimo na Chakula kabla ya kurejea wizaya yake ya awali iliyobadilishwa jina.

Kwa mpango huu wa Rais Kikwete, wa kufanya mabadiliko kwa kuzungukia watu walewale, mtu mmoja anaweza akashika nafasi ya uwaziri katika wizara hata 10 katika kipindi kifupi.

Kama inavyosemwa kwamba Wassira ameondoka kabla ya kufahamu karani wake, vivyo hivyo ndivyo mawaziri wanavyoondoka bila kujua kazi za wizara ambazo wanakuwa wamekabidhiwa. Hii ni kasoro kubwa.

Kuna mawazo kwamba mawaziri wamehamishwa au kuondolewa bila kuwapo sababu za msingi. Wapo waliohamishwa hata kabla ya kuandaa utekelezaji wa mipango ya serikali ndani ya wizara zao.

Wapo wanaosema hatua hiyo ya Kikwete, ya kuhamisha mawaziri katika muda mfupi wa kuteuliwa kwao, inalenga kutimiza kauli yake kwamba “uwaziri hausomewi.”

Lakini wengine wanasema rais anatumia staili hiyo ili kuwatisha mawaziri wake. Anataka wawe waoga kutokana na kutokuwa na uhakika wa kujenga “vibanda” ndani ya serikali yake.

Hii ni staili iliyotumiwa zaidi na aliyekuwa rais wa Urusi, Boris Yetsin. Lakini utaratibu huu unamfanya mhusika kutumia muda wake mwingi kujishughulisha zaidi na kutafuta mali kwa kuwa hajui lini atatupwa nje.

Matokeo ya mtindo huu ni kwamba nchi huingia katika matumizi yasiyo ya lazima na ufungwaji wa mikataba isiyokuwa na manufaa kwa taifa, alimradi wahusika wamechota chao mapema.

Utaratibu kama huu ulishamiri Zanzibar wakati wa utawala wa Alhaji Aboud Jumbe Mwinyi. Katika kipindi hicho, waziri wa serikali alikuwa anaondolewa katika nafasi yake kwa tangazo la redioni.

Hali hiyo ilisababisha ufanisi wa serikali kutoweka. Viongozi waliokabidhiwa dhamana wakageuka wakwapuaji wa mali ya umma.

Kutokana na hali hiyo, tayari baadhi ya wachunguzi wanaona kwamba hatua ya Kikwete ya kumuibua huyu na kumtupa yule, inalenga “kutokomeza wenzake kisiasa.”

Kwa mfano, Gaudence Kayombo, ambaye aliingia katika serikali baada ya kifo cha Juma Akukweti kwa kuteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mipango na Uwezeshaji, ametupwa katika mabadiliko yaliyofuata. Akukweti alikuwa Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Bunge.

Rais Kikwete amewahi kuwa na bahati. Alidumu kwenye nafasi yake ya Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa miaka 10 mfululizo bila kuondolewa. Hiyo ilikuwa wakati wa utawala wa Rais Benjamin Mkapa.

Lakini kama uteuzi wa mawaziri unazingatia mambo mawili makuu ambayo rais anayafahamu fika, kuna haja ya Rais Kikwete kuwa na msimamo wa muda mrefu.

Kwa mujibu wa karibu taratibu zote za kiitifaki duniani, kwanza uteuzi hufanywa kutokana na nguvu ya kisiasa aliyonayo mteuliwa katika eneo lake au nchi nzima.

Hii ni kwa rais kutafuta nguvu na msaada kupitia kwa waziri wake. Jambo hili humsaidia rais kukubalika kwa wapigakura.

Lakini pili, ni kuwa na mteule mwenye uwezo wa ubunifu na utendaji kazi. Moja ya kazi ya waziri ni ubunifu wa kutekeleza mipango ya serikali.

Rais Kikwete hawezi kwenda nje ya wigo huu; na yeye anafahamu fika misingi hii. Je, anaitumia?
 
Kikwete ameishiwa na inabidi aresign tu. Kila nafasi aliyopewa ya kujirekebisha ameshindwa kuitumia.
 
Kikwete sasa aendeleza 'mduara'

Na Saed Kubenea
Mwanahalisi

RAIS Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko ya tano ya Baraza la Mawaziri tangu ashike madaraka ya kuongoza nchi, takribani miaka miwili na nusu iliyopita.

3. Saed Kubenea – Stan Katabalo impostor, only without the education, the sophistication, the principles and steely determination for which Katabalo is remembered for A little Kingmaker in the making, if only he would be aware that he needs to stop being a pawn in the great political game. He gets direct congratulatory calls from Sumaye, Magufuli, Butiku, Warioba and others whenever his paper comes out. He is welcome at Salim A. Salim house. This is such an awesome achievement for a person who is half-schooled and who has never read any major literary work of non-fiction (and who might not get this joke). That our politicians would embrace Kubenea, who still milks the "acid incident", speaks of the level of their desperation to smear each other (in the name of "saving the country").

https://www.jamiiforums.com/showthread.php?t=13378
NUFF SAID
 
Mbona umebadilika ghafla kiasi hicho? Billy gates naye hakwenda shule, lakini alikuwa tajiri wa kwanza duniani mpaka miezi michache ameanguka na kuwa tajiri wa pili mkubwa duniani.

We have seen an average C minus student who failed in everything he has done in his adulthood, elected as the president of the most powerful nation in the World.

Hakuna lolote baya au lenye kasoro aliloandika kubenea. Mabadiliko ya baraza la mawaziri mara tano katika kipindi cha miezi 28 si jambo jema hata kidogo. Mabadiliko ya kila mara yanaonyesha kuna upungufu mkubwa katika utendaji ndani ya serikali unaosababisha mabadiliko takriban kwa wastani wa kila miezi 5.6.
 
Nadhani mabadiliko haya yalibidi yafanyike, lakini naomba tufahamu kuwa Rais humteua mtu si eeti ana uwezo wa utendaji bali kwa vigezo vifuatavyo:
Je anatoka wapi ktk ramani ya Tanzania(mgawanyo sawa wa uwaziri ndani ya baraza) na hii hufanyika ili kunusuru upotevu wa kura kule majimboni na pia kuzuia mgawanyiko ndani ya chama.
 
Nadhani mabadiliko haya yalibidi yafanyike, lakini naomba tufahamu kuwa Rais humteua mtu si eeti ana uwezo wa utendaji bali kwa vigezo vifuatavyo:
Je anatoka wapi ktk ramani ya Tanzania(mgawanyo sawa wa uwaziri ndani ya baraza) na hii hufanyika ili kunusuru upotevu wa kura kule majimboni na pia kuzuia mgawanyiko ndani ya chama.


Hivi unaamini kweli hakuna mgawanyiko ndani ya CCM? Je, mtandao uliopo ndani ya CCM ulisababishwa na kundi la kutoka eneo fulani la Tanzania kukosa uwaziri ndani ya sirikali? Umeshawahi kusikia viongozi wenye nafasi za juu ndani ya chama na sirikali wakitamka hadharani kwamba kuna mgawanyiko ndani ya CCM?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom