JK na maadili ya viongozi

Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,802
613
JK ameona madhara ya viongozi wa kitaifa kufanya biashara na sasa anawashukia kama mwewe.

Habari zaidi saa 2.00 usiku.

Hata hivyo tukumbushane hoja nyingine ya Zitto ilivyozimwa na Ofisi ya Bunge, baada ya kuwasilisha haya hapa chini, alipigwa chenga:

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

PRIVATE MEMBER'S BILL

DAR ES SALAAM

14TH MARCH 2007


ARRANGEMENT OF SECTIONS

Sections Title

PART I

PRELIMINARY PROVISIONS

1. Short title
2. Application
3. Interpretation
4. Objective

PART II

THE ETHICS SECTRETARIAT AND THE ETHICS COMMISSIONER

5. Merging Act No. 13 of 1995 and Act No. 1 of 2005
6. The Ethics Secretariat
7. The Ethics Commissioner



A BILL
For

An Act to merge the Prevention and Combating of Corruption Act, 2007 with the Public Leadership Code of Ethics Act, 1995


NOTICE

The following Bill to be submitted to the National Assembly is presented by a private member.



PART I

PRELIMINARY PROVISIONS

Short title 1. This Act may be cited as the Prevention and Combating of Corruption (Public Leadership Code of Ethics) Act of 2007

Application 2. This Act shall apply to Tanzania Mainland

Interpretation 3. "Commissioner" given the same meaning as provided under the Public Leadership Code of Ethics Act, 1995

"Public Leader" given the same meaning as provided under the Public Leadership Code of Ethics Act, 1995

The Objective 4. The objective of this Act is to provide for the effectiveness of the Public Leaders Code of Ethics Act, 1995, through merging the same with the Prevention and Combating of Corruption Act, 2007, and for the leadership code of ethics to be managed under the department of Good Governance, that is, the Prevention of Corruption Bureau.


PART II
THE ETHICS SECRETARIAT AND THE ETHICS COMMISSIONER


Merging Act 5. The Leadership Code of Ethics Act, 1995 is hereby merged with the Prevention and Combating of Corruption Act, 2007
No. 13 of 1995
and Act No.
1 of 2005

The
Ethics Secretariat 6. The Ethics Secretariat shall be a department within the department of Good Governance, that is, the Prevention of Corruption Bureau under the President' Office.

The
Ethics Commissioner 7. The Ethics Commissioner's Office established under the Ethics Secretariat shall be an office under the department of Good Governance in the President's Office.

Public Leaders at the
District level 8. There shall be established the District Ethics Commissioner's office in the office of the Prevention of Corruption Bureau in every District, whereby Public Leaders, at the District level shall make declaration of their assets and of their interest thereto.


Dar es Salaam

14th March 2007 ZITTTO KABWE (MP)
 
Kuna tetesi kuwa Dr. Idris hatimaye kajiuzulu.. je kuna ukweli wowote.. simu zanguu leo haziingii Dar.. anybody...
 
Halisi, Shukrani!

Tuna isubiri kwa hamu hii taarifa ya habari. Mimi nadhani kama wengi walivo ongelea hapa kuhusu hizi conflict of interest na madhara ya Azimio la Zanzibar, imefika wakati murua hili swala lishughulikiwe ipasavyo, lasivyo hizi scandal kubwa na ufisadi kama utendekavyo Bongo ,will never end... yaani uko hadharani mno.... frauds na scandals will always be there katika nchi yoyote... ila katika Tanzania yetu, ufisadi ni kama umehalalishwa vile..

Kuna mtu mmoja ambaye, swala hili kila linapoongelewa mimi namkumbuka.... naye ni Spika wetu wa Bunge. Yaani nimeona ame facilitate sana kudolola kwa katiba na chachu ambayo inaweza kupatikana kutoka kwa Wabunge wetu ( offcourse majority ni CCM). Huyu speaker angelikuwa mwenye lengo kubwa la kuleta mabadiliko kikatiba, kisheria na hivyo maendeleo ya nchi yetu, inabidi tumkazanie maana anazima sana hoja zinazolenga kuleta maendeleo nchini mwetu, na anafanya hivyo kwa sababu tu zimetolewa na wapinzani.... this is annoying me badly, Bila the likes of Zitto na Dr. Slaa, haya mambo ya BoT na Buzwagi tusingeyaona wala kuyasikia wengi wetu.... and what did the speaker do?... he indeed from his heart played their claims,speculations down.. and now we know what's up at least to some extent about numerous scandals kutokana na harakati na umwanamapinduzi wa wachache uliotaka kuzimwa na wabunge wengi wafata mikumbo na itikadi badala ya maendeleo ya nchi yatu.


SteveD.
 
SteveD,

Lakini pia tuangalie tutazuia vipi viongozi hao hao kuendelea kufanya biashara kupitia wake zao au ndugu zao?

Kama sheria mpya inakuja basi iweke pia makali kwenye tume za maadili na kuhakikisha zina meno na uwezo wa kufanya uchunguzi, vinginevyo hawa jamaa, wataondoa majina yao na kuweka ya ndugu huku ukweli wao wenyewe ndio watakuwa wanafanya biashara.

Kama mkuu Halisi kasema, basi kuna jambo kubwa linakuja leo jioni.
 
SteveD,

Lakini pia tuangalie tutazuia vipi viongozi hao hao kuendelea kufanya biashara kupitia wake zao au ndugu zao?

Kama sheria mpya inakuja basi iweke pia makali kwenye tume za maadili na kuhakikisha zina meno na uwezo wa kufanya uchunguzi, vinginevyo hawa jamaa, wataondoa majina yao na kuweka ya ndugu huku ukweli wao wenyewe ndio watakuwa wanafanya biashara.

Mtanzania,
Kitu kikubwa ni kuwa sheria zetu hazitekelezeki ipasavyo. Nina imani kubwa hilo swala lipo tayari kwenye sheria zetu za kibiashara na kwenye miongozo ya Takururu na sheria za mahakama zetu. Ila ufatiliaji wake ndiyo unaweza kuwa wa kero na wakutia shaka nchini mwetu.

Kawaida ninavyojua, na hili ni katika nchi nchi nyingi, wafanyabiashara wengi wakifanya ma deal yao na kuonekana wata fahamika, wanafanya juu chini na kubadili jina la biashara zao. Kwa huko Ulaya hili swala linafanyika sana kwa wafanyabiashara walioko kwenye entertainment, kwa kubadilisha majina ya clubs... sheria za kufanya hivyo zipo zinawaruhu ila kama kawaida, watu ni wajanja, wanatumia ruhusa hiyo kufanya mengineyo.

Mimi siyo mtaalam wa sheria za kibiashara, lakini nina imani kuwa, kama mtu ana rithisha mali kwa ndugu au mtu kwa nia mbaya ya kukwepa kukamatwa, mtu atakaye rithi hiyo mali naye ni mtuhumiwa vile vile.... ni sawa na kununua kitu cha wizi au magendo bila receipt.... kitu kina kuwa confiscated bila kurudishiwa gharama zako. Sheria za kusimamia swala hili nina imani zipo Tanzania yetu, ila usimamizi wake ndiyo haupo. Auditing za kampuni yoyote ile ikifanyika na mali zake za kurithishwa na zile zake toka awali kama zipo ni rahisi kuijua.... kama ni biashara na iko registered BRELA basi ni lazima itaje capital na funding zote za pembeni....

Kwa hiyo basi, kama wao ni kuondoa majina yao huku wakiendelea kufanya majidubwasha yao ki-proxy, nadhani sheria kama ilivo kawaida yetu ishindwe tu kutekeleza, maana vipengele vya kupinga hilo tayari vipo. Sioni kama sheria ya kurithishwa mali kibiashara ina weza kubadilishwa na kuwekewa ka-clause kamoja kwa ajili ya viongozi tuu... hilo litakuwa vigumu, maana huwezi kutabili kama mtu anaweza kuwa kiongozi au kama ataacha kuwa kiongozi, hii inaweza kusababisha mgongano wa ndani kisheria. Ila nina imani kuna room for improvement as always with sheria zetu including hizi za biashara. Ngoja niwaachie wataalam wa hili.

SteveD.
 
The Objective 4. The objective of this Act is to provide for the effectiveness of the Public Leaders Code of Ethics Act, 1995, through merging the same with the Prevention and Combating of Corruption Act, 2007, and for the leadership code of ethics to be managed under the department of Good Governance, that is, the Prevention of Corruption Bureau.

Ni hatua mabayo mimi bado sijaamini..kama ni kweli. Kinachotakiwa ni kitu ambacho kitareplece Maadili ya uogoi yaliyo FISADISWHA la AZIMIO LA ZAMNZIBER. bASICALY NI KITU KITAKACHOJIBU HOJA KAMA HII:

Mzee Msekwa hebu tuongee kidogo
dk. gideon shoo​

SUALA la Azimio la Arusha kuwa hai au mfu limekuwa likijadiliwa kwa muda sasa. Mjadala huo haukuibuka tu bila sababu yoyote ile ya msingi. Ni wazi kwamba kulikuwapo na kichocheo cha mwibuko huo.

Na ni hicho hicho kichocheo ndicho ambacho hadi leo bado kinaufanya mjadala huo ufoke na kutulia kama ilivyo volcano ya Oldoinyo le Ngai.

Mjadala kuhusu uhai au umauti wa Azimio la Arusha ni matokeo ya uamuzi wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyokutana Zanzibar mwaka 1992 kunyofoa moja ya sehemu kuu za Azimio hilo inayohusu Miiko ya Uongozi kwa sababu ambazo hadi sasa hakuna mshiriki yeyote yule aliyefikia mahali pa kutoa sababu za hatua hiyo zikaingia akilini.

Jambo moja ambalo limejidhihirisha ni kwamba, hakuna aliye tayari kujitokeza hadharani na kutoa sababu za msingi za hatua hiyo ya Halmshauri Kuu ya Taifa. Kumekuwapo na ama ukimya kabisa kutoka kwa baadhi ya wajumbe na hata viongozi wa ngazi za juu za Chama au sababu zimekuwa za ubabaishaji ambazo hazijitoshelezi hata kidogo.

Pengine ni katika kuendeleza utamaduni ule ule wa kutokuwa tayari kusema ni kitu gani hasa kiliwasukuma wajumbe wa Halmashauri Kuu kukimbilia kile kipengele bila hata kutaka kushauriana na wanachama, ndiyo sababu Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Pius Msekwa naye amejikuta katika wakati mgumu na kutoa majibu ambayo yanalazimisha kupatiwa majibu na kurushiwa maswali mengine ya kutaka ufafanuzi.

Mzee Msekwa si tu kwamba aliwahi kukiongoza chama mzazi wa CCM yaani chama cha TANU (Tanganyika African National Union), bali ni msomi mzuri wa sayansi ya siasa ambaye ameandika vitabu na kuwasilisha mada lukuki kuhusu masuala ya chama, chama kushika hatamu na nafasi ya chama katika utawala n.k.

Katika muda mfupi wa chini ya siku tatu, Mzee Msekwa amesikika na kunukuliwa akijaribu kujenga hoja kwamba Azimio la Arusha halijauawa (gazeti la Mzalendo la Novemba 18, 2007 uk.1).

“Kilichotokea Zanzibar si kuua Azimio la Arusha bali ilikuwa ni kufanya marekebisho madogo katika azimio hilo….

Mzee Msekwa anaendelea kutoa ufafanuzi kuhusu hayo marekebisho madogo kwamba ni “kuondoa kifungu kimoja cha Azimio hilo na kukihamishia mahali pengine kwenye Sheria ya Maadili ya Viongozi…”

Sasa wakati mwingine pamoja na kujiepusha kuingia katika kuumbuana, unaweza kujikuta ukilazimika kupiga yowe la ukunga kama uliyeshambuliwa na chui. Mzee Msekwa ananilazimisha kupiga yowe la ukunga.

Bila shaka hapana ubishi kwamba Azimio la Arusha ni waraka wa Dira ya Taifa ulioainisha sera na ambao kamwe haujawahi kuwa sheria kama zilivyo sheria za nchi.

Aidha, itakumbukwa kwamba yaliyoainishwa kwenye buku hilo ni makubaliano ya msingi ya wana-TANU kuhusu nini kinachotakiwa kufanyika na kutokufanyika katika jitihada za ujenzi wa ujamaa.

Ujenzi wa ujamaa unahitaji wananchi, na hao wananchi wanahitaji viongozi. Viongozi nao ni lazima waongozwe na dira na sera ambayo wanaikubali. Ni lazima kiongozi awatumikie wananchi na ili afanye hivyo ni lazima kuondoa aina yoyote ile ya mazingira yanayoweza kusababisha mgongano wa maslahi hata kama ni wa kudhaniwa tu.

Maadili ya uongozi katika Azimio la Arusha yaliwekwa makusudi kabisa kuhakikisha kwamba kiongozi anapochukua nafasi ajue kwamba hiyo ni dhamana na akubali kutumikia na kamwe asitumie nafasi ile kwa ajili ya manufaa binafsi.

Miiko ya uongozi ilisema wazi kwamba kiongozi wa Chama asiwe na hisa katika kampuni yoyote, asiwe mkurugenzi katika kampuni yoyote ile ya binafsi, asiwe na mishahara miwili au zaidi na pia asiwe na nyumba ya kupangisha.

Mzee Msekwa anadai kwamba miiko hiyo haikufutwa moja kwa moja. Lakini anakiri kwamba iliondolewa katika Azimio la Arusha na eti kuihamishia kwenye sheria mpya iliyotungwa maalumu kwa ajili hiyo – inayoitwa Sheria ya Maadili ya Viongozi.

Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa ulifanyika mwaka 1992 na wakati huo sheria ilikuwa jikoni na wala haikuwa imekaribia kuwasilishwa bungeni. Hiyo Mzee Msekwa anaikumbuka na anakumbuka kwamba hata muswada huo ulipopelekwa Bungeni mwaka 1994 ulikuwa na matundu na udhaifu mkubwa, ambao hadi leo madhara yake ni jinamizi letu la maisha.

Sasa ni sheria gani hiyo ambayo iliwafanya wajumbe wa Halmashauri Kuu kufikia uamuzi wa kunyofoa kipengele hicho cha maadili ya viongozi? Au kuna sheria nyingine ambayo hatuijui?

Hata kama kwa minajili ya kuendeleza mjadala huu tutakubali kwamba sheria ilikuwapo (ingawa tunajua kwamba haikuwapo) kwa nini ni kipengele hicho tu kilichoonekana kuwa ni kero katika Azimio la Arusha na hivyo kikastahili kunyofolewa haraka haraka?

Mantiki ya uendeshaji wa masuala ya chama na hasa katika nyaraka zake za msingi na muhimu kama lilivyokuwa Azimio la Arusha kwa CCM, inadai kwamba marekebisho yoyote yale ya msingi yanapofanyika katika dira na sera ni lazima yafanywe machapisho mapya ya waraka husika na kusambazwa kwa wanachama ili waweze kujielimisha kuhusu mwelekeo mpya wa chama chao.

Hilo halikufanyika hadi leo. Sasa tueleweje kwamba maamuzi ya Zanzibar yalifanyika bila kuwapo kwa uchukuaji wa kumbukumbu wa aina yoyote ile?

Mzee Msekwa anakubalika ndani na nje ya chama chake. Ni wazi kwamba kwa kuingia katika uongozi wa juu wa Chama wanachama na wasio wanachama wanatarajia na wanatumaini kupata msukumo mpya wa kuhuisha chama na kusaidia katika kuisukuma Serikali itekeleze ipasavyo Ilani ya Chama.

Kitendo cha Mzee Msekwa kutaka kutufanya tuamini kwamba hatua ya kunyofoa miiko ya viongozi kutoka katika Azimio la Arusha “ilichukuliwa kwa sababu maalumu ya kuwezesha viongozi wanaovunja miiko hiyo, waweze kushitakiwa mahakamani kwa kuvunja sheria ya nchi…” si tu kwamba hakina mantiki yoyote, ile bali ni cha ubabaishaji na pengine ingelikuwa vyema akajinyamazia tu kama alikuwa akiona taabu sana kutamka hadharani kwamba kilichofanyika Zanzibar ni kulisaliti Azimio la Arusha na kutoa mwanya kwa baadhi ya viongozi kuhalalisha fedha na mali ambazo tayari walikuwa wamejilimbikizia katika nyadhifa zao.

Kwamba katika kipindi cha chini ya mwaka mmoja tulishuhudia baadhi ya watu ambao tulikuwa tumefanywa tuamini kwamba walikuwa ni watumishi wa umma wasiokuwa na mali za kutangaza wakichomoza mali kama uyoga.

Mzee Msekwa anatambua wazi kwamba miiko ya viongozi haina maana kwamba kiongozi awe masikini, la hasha. Kinachozungumziwa ni kwamba kiongozi aonyeshe uhalali wa kile alichokuwa nacho na kamwe asije kuitumia nafasi yake ya uongozi kwa ajili ya kujinufaisha.

Kwamba kwa kuondoa miiko ile badala ya kuifanyia marekebisho yaendane na wakati, CCM ilitoa mwanya kwa kila aina ya ufisadi katika uongozi ndani ya Chama na Serikali kwa kukifutilia mbali kipengele hicho na kujifanya kwamba kimehamishwa, inasikitisha sana.

Lakini pengine jambo baya zaidi ni kwamba Mzee Msekwa ametoa maelezo hayo mbele ya wanafunzi wa vyuo 13 vya elimu ya juu na walimu wao walio wanachama wa CCM. Nisingependa kuamini kwamba si wanafunzi wala walimu wao walioona udhaifu wa maelezo ya Mzee Msekwa ambayo alianza kuyatoa katika kipindi cha kila wiki cha Mzee mwenzake Simbeye cha ‘This Week in Perspective’ kilichorushwa na Televisheni ya Taifa (TvT) mwishoni mwa wiki.

Jambo moja ambalo linatatiza wengi ni kwamba ni kwa nini Halmashauri Kuu ilikimbilia kunyofoa hiyo miiko badala ya kufanya marekebisho yanayoendana na zama hizo?

Hivi Mzee Msekwa na wengine wanaotaka kuhalalisha kitendo hicho cha Zanzibar hawaoni kwamba kiongozi wa umma kuwa na hisa katika kampuni kunaweza kwa kiasi kikubwa kukazua mgongano wa maslahi katika utumishi wake?

Kwa nini kabla ya kujitumbukiza katika mtego huo hatari haukufanyika utafiti wa kina wa jinsi wenzetu wanavyoendesha mambo, hasa katika zile nchi ambazo zimepiga hatua katika demokrasia ya vyama na serikali ili kujua ni njia zipi zinazotumika katika kuweka mipaka ya maslahi ya umma na maslahi binafsi katika uongozi?

Katika kujaribu kukwepa uhalali wa maswali yanayoibuliwa na uamuzi wa Zanzibar, akina Mzee Msekwa wanakimbilia kusema kwamba si haramu kiongozi kuwa tajiri. Nami pia nakubali kabisa kwamba si haramu kiongozi kuwa tajiri na pengine ni jambo jema akiwa tajiri.

Lakini niseme kwamba ni haramu kabisa kwa kiongozi kutumia nafasi yake ya uongozi kujitajirisha, hata kama ni kuhalalisha utajiri ambao aliupata kwingine na si kwenye uongozi.

Ni lazima kuwa na mfumo ambao utamzuia kiongozi aliye tajiri kutumia nafasi yake ya uongozi kuimarisha utajiri wake. Kuwa tajiri si kosa hata kidogo. Na chama kizuri ni kile ambacho ndani yake kuna matajiri na masikini, ili mradi wote itikadi yao inashabihiana na malengo yao ni yale yale, kama ni kujenga ubepari basi wote wanajenga ubepari kwa sababu ndiyo dira ya chama chao.

Kama wanajenga ujamaa, basi na wajenge ujamaa, kwani ndiyo itikadi ya chama chao, dira na sera zinaelekeza huko.

Azimio la Arusha ni waraka wa sera. Ndani yake kuna dira ya chama ambayo inaelezwa kwa msingi wa itikadi iliyojumuishwa na siasa ya ujamaa na kujitegemea. Kiongozi wa chama hicho anatakiwa kuwa mstari wa mbele, si tu katika uelewa wa sera bali katika kutekeleza yaliyomo ndani ya waraka huo.

Utekelezaji wa yaliyomo ndani ya Azimio la Arusha ni sera ambayo inapewa nguvu na sheria mbalimbali. Sasa kama kuna mabadiliko ya sera ni lazima sheria nazo zitabadilika.

Kwa mantiki hiyo basi, Mzee Msekwa kudai kwamba kipengele husika kilinyofolewa ili kuwezesha viongozi kushitakiwa ni utani wa hali ya juu.

Sheria inatungwa ili kufanikisha utekelezaji wa sera, sasa haiyumkiniki ung’oe kifungu katika sera eti kwa ajili ya kutoa nafasi ya kuigeuza kuwa sheria, eti ili ifanye kazi. Hiyo si kweli. Ukishang’oa kipengele katika waraka wa sera ndilo hitimisho la sera hiyo na kamwe haiwezi kutungiwa sheria.

Ndio sababu baada ya Zanzibar ilitokea kila aina ya vurugu katika duru za uongozi na kila mmoja na waliomhusu aligeuka kuwa bingwa wa biashara, uwekezaji, ujasiriamali na kadhalika. Ili mradi kulikuwapo mbio katika kuzika miiko yote ile ya uongozi iliyokuwa katika Azimio la Arusha.

Ruksa iligeuka kuwa ruksa kwa kila mmoja kutoka juu kabisa hadi chini kabisa. Na hiyo ruksa haikutumiwa kwa uadilifu na baadhi ya watu waliokuwa katika uongozi na wale waliokuwa pembeni nao udenda ukaanza kuwavuja na haishangazi kwamba baada ya hapo nafasi za uongozi zikageuka dili.

Katika kuhitimisha hoja yangu, ni vyema swali la nini kilichofanyika Zanzibar likajibiwa kwa uwazi zaidi na pengine si vibaya kutamka bayana kwamba kuna hitilafu iliyotokea na pengine kiwewe cha mageuzi kilitukumba na hivyo kufanya uamuzi ambao umegeuka kuwa jinamizi letu la kudumu na jinsi ya kumrudisha jini ndani ya chupa imekuwa vigumu mno.

Hapana ubishi kwamba vurugu yote ya sasa ya kutoaminiana, vurugu katika uchaguzi, uhahaji wa kutafuta nafasi za uongozi tunaoushuhudia hivi sasa na madhambi yote ambayo tunayapigia kelele katika uchaguzi chimbuko lake la kwanza ni uamuzi wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kunyofoa hicho kipengele muhimu katika Azimio la Arusha na halafu kujifanya kwamba hakuna lolote baya lililofanyika.

Hatutaki kusema ukweli kwamba kwa kuondoa miiko ya viongozi na bila kuiweka miiko mingine ndani ya waraka muhimu wa chama kama Azimio la Arusha, tulifungulia milango kila aina ya watu ndani ya uongozi wa chama na hatimaye Serikali.

Matokeo yake hata Mzee Msekwa anayajua. Pengine anachokifanya Mzee wetu Msekwa ni kujiandaa kutafuta jibu mwafaka litakalokidhi na kukata kiu ya wadadisi wa mambo; kwamba Azimio la Arusha li wapi?
© Habari Corporation Ltd
All rights reserved

Huchapishwa na Habari Corporation Ltd. P.O. Box 4793, Shekilango Road, Sinza Kijiweni, Dar es Salaam
raihcl@yahoo.com
22.11.2007

Kama kweli hiyo sheria itakuwa inajibu hoja hii ya MAADILI YA UONGOZI...ni ajabu..lets wait and see! Maana ni almost kurudisha Azimio la Arusha. Maana Azimo la Arusha it was the doc ya MIIKO YA UONGOZI jumlisha na CONCEPT NZIMA YA KUJITEGEMEA KIUCHUMI

Mkumbuke Baadaya ya kungofoa MIIKO YA UOGOZI ndio uozo wa kina ulipoanza kujiteza.Ndipo UFISADI ULIKUWA UMEJIFICHA ulianza kujitokeza hadharani

Wengi wanaamini ndio Kigezo alichotumia BENJAMIN MKAPA kujiamnisha na kufanya upuzi aliofunaya IKULU.

Ni kweli kabisa lazima kuleta sheria effective ya kuzuia Hilo.
 
Hivi hawa wamewahi kusikia kitu kinachoitwa Azimio la Arusha ambapo ndani yake kuna "Miiko ya Uongozi"?
 
Wabunge, mawaziri Tanzania kuchagua uongozi au biashara
Na Mwandishi Wetu


RAIS Jakaya Kikwete amewataka wafanyabiashara ambao ni wabunge na mawaziri kujiandaa kuchagua kimoja kati ya biashara au uongozi serikalini

Akizungumza jana katika utaratibu wake wa kila mwezi jana, Rais Kikwete aliwataka kuchagua jambo moja kati ya uongozi au biashara ili wasiendelee kuondokana na mwingiliano wa kimaslahi.

"Viongozi wetu wachague kufanya jambo moja kwa wakati mmoja ama biashara au ubunge na Uwaziri. Kwa ajili hiyo ni makusudio yangu kuanzisha mchakato wa kufanya marekebisho ya Sheria ya Maadili ya Uongozi ili tuingize utaratibu huo," alisema kuongeza.

"Ni jambo lenye maslahi kwa nchi yetu na litasaidia sana kujenga heshima ya viongozi wa umma mbele ya macho ya wananchi. Nafurahi kwamba suala hili tumelizungumza katika kikao maalum cha Kamati Kuu ya CCM tulichofanya Dodoma juzi Januari 29 na tumeelewana."

Alisema upo ushahidi wa kutosha wa kuwapo migongano ya maslahi kwa baadhi ya viongozi hao wa kisiasa suala linalosababisha wananchi kukosa imani na serikali.

Akitoa mfano wa mataifa yaliyoendelea alisema kuwa mataifa hayo yanao utaratibu unaomtaka mtu mwenye shughuli za kibiashara anapokuwa Mbunge au Waziri kuacha kujishughulisha na biashara zake na kwamba unakuwepo utaratibu rasmi unaotambuliwa kisheria wa wadhamini wanaoendesha hizo shughuli bila ya yeye kujihusisha nazo.

Akizungumzia suala la uhamiaji haramu nchini alitoa siku sitini za kwa wahamiaji haramu kujisalimisha. Baada ya hapo hatua zipasazo za kisheria zitachukuliwa kwa wale ambao watakuwa hawa kufanya hivyo.

Alisema kuwa ameamua kuchukua hatua hiyo baada ya kushuhudia mambo yasiyokubalika yakitendeka wakati akiwa kwenye ziara ya siku kumi Mkoani Kagera ambapo alikuta ukiukwaji wa sheria na taratibu za uhamiaji na uingizaji mifugo nchini.

Alisema kwa muda mrefu sasa, raia wa nchi jirani zinazopakana na Mkoa wa Kagera wamekuwa wakiingia na kuishi nchini kwa vibali vya viongozi na watendaji wa vijiji na kata. Baadhi ya watu hao pia wamekuwa wakiingiza mifugo kwa vibali vya viongozi hao hao.


Suala hilo alisema halikubaliki kwani kwa mujibu wa sheria na taratibu za uhamiaji zinatoa mamlaka hayo kwa Maafisa Uhamiaji tu na si vinginevyo na kuwa viongozi na watendaji wa vijiji na kata hawana mamlaka hayo.

Hivyo alisema, vibali vyote walivyotoa viongozi hao si halali na havitambuliki na akapiga marufuku kwa kiongozi au mtendaji wa ngazi yoyote ile nchini kutoa kibali cha mgeni kuingia au kuishi nchini kama siyo Afisa wa Uhamiaji.

"Nilipokuwa Mkoani Kagera niliwaagiza Mkuu wa Mkoa na wakuu wa wilaya kufuatilia utoaji wa vibali unaofanywa na viongozi na watendaji wa vijiji na kata katika maeneo yao.

Nimewataka wawachukulie hatua zipasazo za kinidhamu watumishi hao wa umma pamoja na kuwabana wahamiaji haramu kufuata sheria za uhamiaji za nchi yetu au warudi makwao. Napenda kusema kuwa maagizo hayo ni kwa wakuu wote wa mikoa na wilaya nchini," alisema.

Sambamba na hilo pia ameiagiza Wizara ya Maendeleo ya Mifugo kutoa mwongozo wa jinsi ya usafirishaji mifugo kwa kuwa uvushaji unaoendelea sasa unaweza kusababisha hatari kubwa ya magonjwa ya milipuko kwa mifugo.

Pia alizungumzia la upandaji wa bei ya mafuta duniani akataka wananchi kuwawaangalifu na hasa wabanifu katika matumizi ya mafuta na kuepuka matumizi yasiyo ya lazima.

Alitaka juhudi za kuzalisha nishati mbadala kutokana na mimea hususan miwa, mawese na mbono-kaburi (jatropha) ziongezwe ili kama zikifanikiwa zisaidie kupunguza mzigo wa mafuta yanayoagizwa kutoka nje.

"Nafurahi kwamba juhudi zetu zina muelekeo mzuri na katika miaka michache ijayo tutaanza kunufaika na matunda yake. Pamoja na hayo tunaendelea na juhudi za utafutaji wa mafuta na gesi asilia hapa nchini,"alisema.

Kuhusu Uchunguzi wa Akaunti ya EPA alisema Serikali imedhamiria kulifuatilia suala hilo mpaka mwisho wake ambao utakuwa na maslahi kwa taifa.

Akawashukuru Watanzania kwa kuunga mkono hatua alizochukua na anazoendelea kuchukua kuhusu suala la Benki Kuu. Hata hivyo, alieleza kusikitishwa na taarifa anazozipata kuhusu kuwepo uvumi mwingi unaoenezwa na baadhi yetu kuhusu suala hilo.

Hivyo akakemea wale wote wanaoeneza uvumi na uongo kuacha kufanya hivyo na akawasihi wananchi wawe watulivu na wavumilivu.

"Nawaomba Watanzania wenzangu tuwe na subira. Naamini kazi hii itakamilika ndani ya kipindi cha miezi sita tuliyowapa. Napenda kurudia ombi la Serikali kwa wananchi wenye taarifa zitakazosaidia katika uchunguzi na hatua katika suala hili waisaidie kamati yetu hiyo," alisema.

Akizungumzia ziara ya Rais George W. Bush wa Marekani katikati ya mwezi Februari, 2008 aliwataka wananchi wampokee kwa mujibu wa desturi na ukarimu wa Kitanzania kwani ujio wake unakuja na neema nyingi tofauti na uvumi unaoenezwa kuwa anakuja kuanzisha Makao Makuu ya Kamandi ya Jeshi la Marekani katika Bara la Afrika.

Alisema wakati wa ziara yake hapa nchini, Serikali ya Marekani inatarajia kutiliana sahihi msaada mkubwa wa maendeleo unaoelekezwa katika kuboresha miundo mbinu ya barabara, umeme na maji.

Kwa upande wa hali ya kisiasa na kiusalama ya nchi jirani ya Kenya alisikitishwa na jitihada zanazofanywa na jumuiya mbalimbali za kimatiafa kutozaa matunda hivyo kusababisha hali kuwa mbaya nchini humo kiusalama.

Alisema serikali inaiunga mkono Kamati ya Kofi Annan (Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja wa Mataifa), Rais Mstaafu wa Tanzania, Benjamin Mkapa na mke wa wa Rais mstaafu wa Afrika Kusini, Graca Machel.
 
Nimemsikiliza, ameliongelea na anasisitiza kuwa ataanzisha mchakato wa jinsi ya kutengeneza sheria ya kulifanya litkelezeke. When? How soon? bado ni kitendawili!
 
Nimemsikiliza, ameliongelea na anasisitiza kuwa ataanzisha mchakato wa jinsi ya kutengeneza sheria ya kulifanya litkelezeke. When? How soon? bado ni kitendawili!

Hope he will make sure it is done soon, as it is long due... kama CC ya CCM imepitisha hope it won't take long.
 
Kasheshe;

Nashukuru kwa kunitia moyo! Ninapokea kwa niaba ya watanzania wenzangu ambao wanaliaa na kupoteza imani na uongozi unafanya bishara za Kifisadi kwenye kila ngazi ya uongozi na kuwasahau WATU waliowaweka kwenye uongozi.

Hata wamachinga wanao kula msoto mkali kila siku wakipigwa jua kali, wakinyeshea na mvua, kupigwa upepo na mavumbi bila kusahau usumbufu wa dola yenyewe, hata wao wangehitaji wapate UONGOZI WA JUU SEREKALINI ili uwape nafasi isiyo na usumbufu wafanye bishara zao kiulani!

Kwani ukiwa kiongozi wa chama au serekali..nani atakufuatafuata? nani atakudai kodi, nani atkuzuia kufanya dili chafu chafu...? N awewe ni bwana mkubwa? Naam kweli ukiwa kiogozi unaweza kujifanyia bishara...utakavyo. Muulize Benjamin Wiliam Mkapa mambo yalivyomnyokea. Muulize akuonyeshe alivyoweza kufanya "Buznesi" safi na kukwepa Udhia anoupata mmachinga anayetembeza DVD 2 mji mzima bila kupta hata mnnuzi wa kumfaya ajipatie hata Mmlo wa siku moja.

Amakweli, uongozi ni "dili"

Usiwaone wanagombania uogozi kwa mamilioni ya hela. Wanajua kufanya Biashara kimachinga hufiki mbali. Wengi wa hao viongozi tunaowaona hapo..They have nothing do to With "THE PEOPLE" UOGOZI USIOJALI "WATU" Uongozi unaojali "KUJITAFUTIA KIJIWE CHA BISHAARA" ni viongozi gani? Ni Msingi mkubwa wa ufisadi.

Wa Tanzania Ni wakati wa kuamka.

Hiyo sheria itengenezwe na itumike mara moja!
 
Hotuba yenyewe ni kama ifuatavyo:

HOTUBA YA MHE. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, KWA WANANCHI, 31 JANUARI, 2008

Ndugu Wananchi;

Ninayo furaha kwa mara nyingine tena kuzungumza nanyi kupitia utaratibu huu mzuri wa mawasiliano baina ya Rais na wananchi wa nchi yetu.
Jambo la kwanza ninalopenda kulizungumzia linahusu uzingatiaji wa sheria na taratibu za uhamiaji na kuishi nchini.
Ndugu Wananchi;
Tarehe 23 mwezi huu, nilimaliza ziara ya siku kumi Mkoani Kagera. Jambo moja nililoliona kwenye ziara hiyo ambalo sikufurahishwa nalo, ni ukiukwaji wa sheria na taratibu za uhamiaji na uingizaji mifugo nchini.
Kwa muda sasa, raia wa nchi jirani zinazopakana na Mkoa wa Kagera wamekuwa wakiingia na kuishi nchini mwetu kwa vibali vya viongozi na watendaji wa vijiji na kata. Baadhi ya watu hao pia wamekuwa wakiingiza mifugo kwa vibali vya viongozi hao hao.
Wageni hao wamekuwa wanaingia na kuishi nchini isivyo halali. Sheria na taratibu za uhamiaji zinatoa mamlaka hayo kwa Maafisa Uhamiaji tu na si vinginevyo. Viongozi na watendaji wa vijiji na kata hawana mamlaka hayo. Hivyo basi, vibali vyote walivyotoa viongozi hao si halali na havitambuliki. Napenda kurudia kauli yangu niliyoitoa Mkoani Kagera kwamba ni marufuku kwa kiongozi au mtendaji wa ngazi yoyote ile nchini kutoa kibali cha mgeni kuingia au kuishi nchini kama siyo Afisa wa Uhamiaji.

Ndugu wananchi;
Wageni wanaoishi nchini kwa kutumia vibali ambavyo havikutolewa na Idara ya Uhamiaji wanaishi isivyo halali. Wenzetu hawa wanatakiwa kufanya yafuatayo. Kwanza wajitokeze na kutoa taarifa kwa Maofisa Uhamiaji, Wilayani au katika vituo vya mpakani. Pili, iwapo watachagua kuishi nchini, wafuate taratibu zilizowekwa kuomba kibali cha kuishi nchini. Idara ya Uhamiaji ndiyo itakayoamua. Tunawapa siku sitini za kufanya hivyo. Baada ya hapo, hatua zipasazo za kisheria zitachukuliwa kwa wale ambao watakuwa hawakufanya hivyo.
Nilipokuwa Mkoani Kagera niliwaagiza Mkuu wa Mkoa na Wakuu wa Wilaya kufuatilia utoaji wa vibali unaofanywa na viongozi na watendaji wa vijiji na kata katika maeneo yao. Nimewataka wawachukulie hatua zipasazo za kinidhamu watumishi hao wa umma pamoja na kuwabana wahamiaji haramu kufuata sheria za uhamiaji za nchi yetu au warudi makwao. Napenda kusema kuwa maagizo hayo ni kwa Wakuu wote wa Mikoa na Wilaya nchini kwani inawezekana matatizo haya yanaweza kuwepo katika mikoa mingine.
Najua kwamba kuna Watanzania wenzetu wanaohifadhi wahamiaji haramu kwa kuwa wananufaika kwa kuwafanya vibarua au wafanyakazi wao. Ukweli unabaki pale pale kwamba wanatakiwa waingie na kuishi nchini kwa kufuata taratibu zinazotambulika kisheria. Sheria za nchi, na sio manufaa ya mtu au watu binafsi, ni lazima zizingatiwe.

Ndugu Wananchi;
Jambo lingine baya linalofanyika katika mpaka wetu na nchi jirani Mkoani Kagera ni kuruhusu mifugo kuingia nchini holela. Hiki ni kitendo ambacho kinakiuka taratibu zinazotawala uingizaji wa mifugo kutoka nchi za nje. Pia ni kitendo cha hatari kwani kinaweza kupelekea mifugo yenye maradhi kuingia nchini bila kudhibitiwa na kusababisha maafa makubwa nchini. Kanuni na taratibu zimewekwa kisheria kutawala mifugo kuvuka mipaka na kuepusha hatari za namna hiyo zisitokee.
Jambo linalonishangaza ni kwa nini viongozi wetu hawa hawajifunzi kutoka kwa majirani zetu. Wakati wote tulipofanya zoezi la kurudisha makwao wakimbizi au wahamiaji wasiokuwa halali na mifugo yao wenzetu waliweka sharti la mifugo hiyo hiyo iliyotoka kwao ichanjwe kwanza kabla ya kuvuka mpaka hata kama mifugo hiyo ilitokea nchini kwao na kuja kwetu. Nilidhani hili lingekuwa fundisho kwa viongozi wetu hawa kuwa thabiti kuhakikisha kuwa mifugo kutoka nchi jirani inachanjwa kabla ya kuvuka mpaka kuja Tanzania. Lakini, hawajali kufanya hivyo. Mkuu wa Mkoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi Watendaji wa Wilaya na viongozi na watendaji wa vijiji na kata kuhakikisha kuwa hakuna mifugo inayoingia nchini holela. Lazima sheria na kanuni husika zizingatiwe.
Aidha, nimeelezwa juu ya kufahamika kuwepo vivuko haramu kadhaa mpakani. Nimesema nilipokuwa Kagera na narudia tena leo kwamba, maadamu vivuko hivyo vimejulikana lazima tuvidhibiti. Kadhalika tuanzishe vituo mpakani vya kupokelea mifugo na kila anayeingia na mifugo lazima apitie hapo na kupata idhini husika. Nimetaka viongozi wenzetu hao wasimuonee haya mtu yeyote anayeingiza mifugo nchini kinyume cha sheria na taratibu zilizopo. Kadhalika viongozi na watendaji wanaozembea wachukuliwe hatua kali za kinidhamu mara inapobainika kuwa mifugo imeingia kinyume na taratibu katika maeneo yao.
Kama ilivyo kwa uhamiaji usio halali, tatizo la kuingiza mifugo kinyume na utaratibu linaweza kuwepo mikoa mingine nchini. Hivyo, maagizo haya ni kwa mikoa yote na wilaya zote nchini. Pia yanaihusu Wizara ya Maendeleo ya Mifugo. Lazima Wizara itoe uongozi katika jambo hili muhimu kwa usalama na maendeleo ya mifugo yetu nchini. Napenda kuwakumbusha Watanzania wenzangu kuwa hakuna nchi yoyote duniani inayoruhusu mifugo kuingia holela. Si vizuri Tanzania kuwa ndiyo nchi pekee inayofanya hivyo. Wenzetu na hata hao majirani zetu wanatustaajabu.

Ndugu Wananchi;
Jambo la pili ninalopenda kulizungumzia ni matatizo yanayoukabili uchumi wa dunia hivi sasa. Bado bei ya mafuta iko juu sana na kuathiri uchumi wa nchi zote duniani tajiri na maskini ingawaje nchi maskini zinaathirika zaidi. Hili si jambo geni kwetu. Napenda kurudia kauli zangu za siku za nyuma kwamba, hatuna uwezo mkubwa wa kujikinga na athari za bei za mafuta. Hata hivyo, hatuna budi tuendelee kuwa waangalifu na hasa wabanifu katika matumizi ya mafuta. Tuepuke matumizi yasiyo ya lazima.
Wakati huo huo tunaendelea na juhudi za kuzalisha nishati mbadala kutokana na mimea hususan miwa, mawese na mbono-kaburi (jatropha). Juhudi hizo zikifanikiwa zitatusaidia kupunguza mzigo wa mafuta tunayoyaagiza kutoka nje. Nafurahi kwamba juhudi zetu zina muelekeo mzuri na katika miaka michache ijayo tutaanza kunufaika na matunda yake. Pamoja na hayo tunaendelea na juhudi za utafutaji wa mafuta na gesi asilia hapa nchini. Mpaka sasa leseni 22 za utafutaji mafuta na gesi asilia zimetolewa na kazi inaendelea katika hatua mbalimbali. Tuzidi kumuomba Mwenyezi Mungu atujaalie rehema zake na sisi tujaaliwe kugundua mafuta mengi hapa nchini yatakayotosheleza mahitaji yetu na ziada ya kuuza nje.
Ndugu Wananchi,
Tatizo lingine kubwa linaloukabili uchumi wa dunia sasa linatokana na matatizo yanayoukabili uchumi wa Marekani. Uchumi wa taifa hilo ambao ndiyo mkubwa kuliko wowote duniani umekuwa unapita kwenye misukosuko kwa miezi kadhaa na katika wiki chache zilizopita hali ikawa ngumu zaidi. Kasi ya ukuaji wa uchumi imepungua na thamani ya dola imeshuka. Serikali ya nchi hiyo imeanza kuchukua hatua za kukabiliana na matatizo hayo. Lakini, kwa kuwa uchumi wa Marekani ndiyo uchumi mkubwa kuliko wowote duniani na uchumi wa nchi nyingi duniani una uhusiano nao, matatizo ya uchumi wa nchi hiyo huathiri nchi nyingi. Na sisi Tanzania hivyo hivyo.
Nimeelekeza wachumi wetu wafanye uchambuzi wa kina juu ya athari hizo na kushauri hatua za kuchukua kupunguza makali yake. Moja ya jambo ambalo liko wazi ni lile la kushuka kwa thamani ya dola ya Kimarekani. Sisi tunaweka sehemu kubwa ya akiba yetu ya fedha za kigeni katika dola za Kimarekani. Ni dhahiri kwamba kushuka kwa thamani ya dola za Kimarekani kunatupunguzia uwezo wetu wa kuagiza bidhaa nchi za nje.

Uchunguzi wa Akaunti ya EPA
Ndugu Wananchi;
Jambo la tatu ambalo nimepanga kuliongelea leo ni hili suala la ukaguzi wa Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje na hatua zinazoendelea kuchukuliwa baada ya taarifa ya ukaguzi kutolewa.

Ndugu Watanzania wenzangu;
Kwa mara nyingine tena nawapongeza na kuwashukuru wakaguzi wa Kampuni ya Ernst and Young kwa kazi nzuri waliyoifanya na kutoa taarifa ya kina kuhusu matatizo yahusuyo matumizi ya fedha za Akaunti hiyo. Nawashukuru pia Watanzania wenzangu kwa kuunga mkono hatua tulizochukua na tunazoendelea kuchukua kuhusu suala la Benki Kuu. Hata hivyo, nasikitishwa na taarifa ninazozipata kuhusu kuwepo uvumi mwingi unaoenezwa na baadhi yetu kuhusu suala hili. Baadhi ya uvumi huo umekuwa unapotosha ukweli na kuwachanganya wananchi. Napenda kutumia nafasi hii kuwaomba wanaoeneza uvumi na uongo kuacha kufanya hivyo. Aidha, nawasihi wananchi wawe watulivu na wavumilivu.
Napenda kuwahakikishia kuwa, Serikali inayo dhamira ya dhati ya kulifuatilia suala hili mpaka mwisho wake ujulikane. Mwisho ambao utakuwa na maslahi kwa taifa letu. Pamoja na yote yatakayofanywa, tunataka kuhakikisha kuwa fedha zilizolipwa kinyume cha utaratibu zinarudishwa. Mwanasheria Mkuu wa Serikali na wenzake, yaani Mkuu wa Jeshi la Polisi na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU wameanza kuchukua hatua. Nimewataka watoe taarifa kwa wananchi mara kwa mara kadri inavyowezekana pamoja na haja ya kuwa waangalifu kutokutoa mengi yahusuyo uchunguzi wanaoufanya ili ushahidi usiharibike.
Nawaomba Watanzania wenzangu tuwe na subira. Naamini kazi hii itakamilika ndani ya kipindi cha miezi sita tuliyowapa. Napenda kurudia ombi la Serikali kwa wananchi wenye taarifa zitakazosaidia katika uchunguzi na hatua katika suala hili waisaidie kamati yetu hiyo.


Ujio wa Rais Bush

Ndugu Wananchi;
Natumai mmesoma na kusikia taarifa katika vyombo vya habari kuhusu ziara ya Rais George W. Bush wa Marekani katika nchi yetu kunako katikati ya mwezi Februari, 2008. Tunaendelea kukamilisha ratiba na itakapokuwa tayari tutawapeni taarifa. Hilo ndilo jambo langu la nne leo.
Napenda kutumia nafasi hii kuwaomba Watanzania tumpokee mgeni wetu huyu kwa mujibu wa mazoea na desturi za ukarimu wa Kitanzania. Huu ni ugeni mkubwa na wa heshima kubwa kwa nchi yetu. Rais Gerorge Bush ameipa heshima kubwa nchi yetu kwa kuamua kutumia sehemu kubwa ya ziara yake ya Bara la Afrika hapa kwetu. Ameonyesha upendo mkubwa kwetu nasi tumuonyeshe hivyo hivyo. Nawaomba Watanzania tujitokeze kwa wingi siku hiyo kumpokea mgeni wetu huyo mashuhuri.
Ziara hii ni uthibitisho wa kuimarika kwa mahusiano kati ya Marekani na Tanzania. Mahusiano hayo mazuri yameinufaisha nchi yetu. Marekani sasa ni moja ya nchi zinazoongoza kwa kutoa misaada ya maendeleo kwa Tanzania. Tangu mwaka 2003 kwa mfano, imekuwa inatoa msaada mkubwa ambao umetusaidia sana katika mapambano yetu dhidi ya maradhi ya UKIMWI nchini Tanzania. Kadhalika, Marekani imetusaidia sana katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa malaria nchini.
Ndugu Wananchi,
Wakati wa ziara yake hapa nchini, Serikali ya Marekani inatarajia kutiliana sahihi msaada mkubwa wa maendeleo unaoelekezwa katika kuboresha miundo mbinu ya barabara, umeme na maji. Kwa msaada huo utakaotolewa kupitia Programu ya Mfuko wa Changamoto ya Millenia utatusaidia kutatua baadhi ya matatizo yaliyoonekana sugu katika baadhi ya maeneo hapa nchini.
Pamoja na hayo, ziara ya Rais George Bush nchini mwetu itasaidia kuitangaza nchi yetu na kuinufaisha sana utalii na uwekezaji hasa kwa soko la Marekani na marafiki zake. Tayari katika miaka miwili hii tumeshuhudia ongezeko kubwa la watalii wa Kimarekani kutembelea nchi yetu. Hivi sasa Wamarekani ndiyo wanaoongoza kwa idadi ya watalii wanaotembelea hifadhi za Ngorongoro na Serengeti. Naamini baada ya ziara ya Rais wao watalii wengi zaidi wa Kimarekani watakuja. Hali kadhalika, wawekezaji wengi wa kutoka Amerika watajenga imani ya kuja kuwekeza nchini.
Ndugu Wananchi,
Wapo watu miongoni mwetu na hata nje wanajaribu kueneza uvumi wa uongo na kuihusisha ziara hii na masuala ya Makao Makuu ya Kamandi ya Afrika ya Jeshi la Marekani. Ni uongo na uzushi mtupu. Ziara hii haihusu hayo. Masuala hayo si agenda na wala Marekani haijaiomba Tanzania kuwa mwenyeji wa Kamandi hiyo. Nawasihi Watanzania wenzangu tupunguze hii tabia ya kuzusha na kueneza uongo. Tunajitia hofu wenyewe na wenzetu bila sababu. Haina tija yoyote. Nawaomba tujitokeze kwa wingi kumpokea mgeni wetu huyu. Aondoke nchini salama na arejee kwao akiwa na kumbukumbu nzuri ya nchi yetu na watu wake.

Hali ya Kenya
Ndugu Wananchi;
Jambo la tano ninalotaka kulizungumzia ni hali ya kisiasa na kiusalama ya nchi jirani na rafiki ya Kenya. Kwa kweli inatusikitisha na kutuletea simanzi kubwa. Mioyo yetu inauma kuona na kusikia yanayotokea nchini humo. Jitihada yangu ya kuzungumza na pande zote zinazohasimiana pamoja na zile zilizofanywa na zinazoendelea kufanywa na wenzetu wengine bado hazijazaa matunda. Sisi hatutachoka na wala hatutaacha kuzungumza na pande zinazohusika kuhusu kuacha uhasama, kuacha na mapigano na kutafuta maridhiano kwa njia ya mazungumzo.
Tunaahidi kuendelea kuiunga mkono Kamati ya Mhe. Kofi Annan (Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja wa Mataifa), Rais Mstaafu, Mhe. Benjamin Mkapa na Mama Graca Machel. Viongozi wetu hao wanaifanya kazi hiyo kwa niaba ya Umoja wa Afrika wanastahili msaada wetu na kuungwa mkono nasi. Aidha, tutaendelea kushirikiana na viongozi wenzetu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kusaidia juhudi za upatanishi. Napenda kutumia nafasi kurudia tena yale maombi yangu kwa viongozi wa PNU na ODM na wananchi wote wa Kenya kuyapa mazungumzo nafasi ya kumaliza tofauti zao. Mapanga, marungu na hata bunduki zisipewe nafasi, kamwe hazitasaidia.
Tutenganishe Uongozi na Biashara

Ndugu Wananchi;
Jambo la mwisho ninalotaka kulizungumzia linahusu maadili ya uongozi nchini. Hususan napenda kulizungumzia suala la viongozi wa siasa Mawaziri na Wabunge kuwa pia watu wanaojihusisha na shughuli za biashara moja kwa moja. Upo ushahidi wa kuwepo migongano ya maslahi kwa baadhi. Lakini, pia, hata pale ambapo hakuna dalili za wazi, hisia za kupata manufaa yanayotokana na nafasi zao hutawala. Matokeo ya yote hayo ni watu kupoteza imani na kutilia shaka uadilifu wa viongozi wetu.

Ndugu Wananchi;
Nchi za wenzetu hasa zile za kibepari zinazo taratibu nzuri za kushughulikia hali hizo. Wenzetu wanao utaratibu unaomtaka mtu mwenye shughuli za kibiashara anapokuwa Mbunge au Waziri kuacha kujishughulisha na biashara zake. Unakuwepo utaratibu rasmi unaotambuliwa kisheria wa wadhamini wanaoendesha hizo shughuli bila ya yeye kujihusisha nazo. Anapoacha uongozi wa siasa kama atapenda atachukua tena mali yake na kuendelea na shughuli zake.
Ni makusudio yangu kuwa utaratibu huu tuuanzishe hapa nchini. Viongozi wetu wachague kufanya jambo moja kwa wakati mmoja ama biashara au Ubunge na Uwaziri. Kwa ajili hiyo ni makusudio yangu kuanzisha mchakato wa kufanya marekebisho ya Sheria ya Maadili ya Uongozi ili tuingize utaratibu huo.

Ndugu wananchi;
Ni jambo lenye maslahi kwa nchi yetu na litasaidia sana kujenga heshima ya viongozi wa umma mbele ya macho ya wananchi. Nafurahi kwamba suala hili tumelizungumza katika kikao maalum cha Kamati Kuu ya CCM tulichofanya Dodoma juzi tarehe 29 Januari, 2008 na tumeelewana. Ni matumaini yangu kuwa sote tutaunga mkono.

Mwisho, nawatakia kila la heri kwenye shughuli zenu. Tuendelee kushirikiana kuijenga na kuiendeleza nchi yetu.
Asanteni sana kwa kunisikiliza.
 
Hapo sasa atakuwa ameweka mambo sawa. Siku zote nimekuwa nikisema hoja kuu ni maazimio ya Zanzibar na Arusha...sasa wanafanya biashara hakuna mwiko unaowakataza. Lakini maadam utaanzishwa utaratbu wa kuwabana, basi panaweza kuwa na mabadiliko. Tutaangalia kasi ya wafanyabiashara kukimbilia bungeni...

Sina hakika kama wengi wataweza kuachia shughuli zao kwa kuwa biashara za bongo zinaendeshwa kimafia sana kukwepa kodi na sheria nyingine. wengi wanapenda kuwa mastering wenyewe kuficha mambo haya. Na ndiyo sababu kubwa hawapendi kupanua mitaji kupitia DSE kwa kuwa watawajibika kuwa wawazi zaidi kwa wenye hisa.
 
Hivi hawa wamewahi kusikia kitu kinachoitwa Azimio la Arusha ambapo ndani yake kuna "Miiko ya Uongozi"?

Nimekusoma MMK.

Unafahamu hali iliyoko Tanzania sasa hivi kiuchumi inafafania sana hali iliyokuwepo baada tu ya Tanganyika kupata uhuru kulekea mwaka 1967.

viogozi baada ya kuutwaa uhuru, wengi wao wakaona sasa mambo sihaya? Wakaanza kujikusanyia mali wao binafsi na kuwasahau wananchi waluowaweka madarakani.

Agano la kuupigania uhuru likuwa KILA MWANACHI NA KILA FAMILIA YA TANZANIA IWE HURU NA AWE HURU KIUCHUMI.

KILA MWANANCHI AJITEGEMEE NA RUDIA AJITEGEMEE KIUCHUMI..HILO NDILO AGANO LA KUPIGANIA UHRU WETU!

NI AGANO HEKIMA NA LA KINA!

Lakini bada ya kuupta uhuru baadhi ya viongozi wakawahimiza kujitegemea kiuowongo uwongo..huku wao viongozi wakiwanyonya na KUWATEGEMEA WATU WALIOWAWEKA MADARAKANI..yaani Viogozi wakasaliti Agano la Kujitegemea KIUCHUMI kwa kila Mtanzania.

Ikawa lazima kufanya marekebisho ili kujitegemea ili AGANO LA UHURU lilete maana. Marekebishao kimsingi yalikuwa kuwafanya VIOGOZI MAFISADI wasiweze kabisa kuwategemea WATU waliowaweka madarakani. Kwani watu au tuseme wananchi wanamtegemea nani kujenga uchumu wao? Mwananchi hana wa kumtegemea ila jasho lake binafsi. Hivyo basi hata viongozi wategemee jasho lao na si kuwategemea wananchi wao.

Ndipo ikwawekwa "MIIKO MIKALI YA UONGOZI" Iili kufanikisha AGANO LA UHURU. Agano la kila mananchi ajitegemee kiuchumi!! Na sema Agano lilikuwakila mwananchi wa nchi hii ajitegemee kiuchumi..na sio kwa viogozi tu au tabaka la wachache. AGANO LA UHURU halikusema hivyo. Hata katiba ya nchi inayaweka haya bayana. Ikiwa na maana Kuwa kila mtanzania akijitegemeakiuchumi taifa Litakuwa Huru kiukweli. Litakuwa linajitegema na kuheshimika.

Ni kweli sifikiri viongozi waliopo madarakani sasa wanalijua hili. Au wanlifumbia macho au wanalipuuzia ...itabidi tutafute wote.

MIIKO HIYO YA UONGOZI ikaondolewa bila kuweka mingine pale zanzibar 1992. Hivyo ikiwa na maana kuvunjwa kwa AGANO LA UHURU.

Sheria hiyo kama itapita ..ItaTUFANYA TUREJEE KWNYE AGANO LA UHURU! Kwani Agano la uhuru halikamiliki Bila MIIKO/MAADILI YA UONGOZI!

Mafisadi tulionao wanaona mawazo haya kama Mkuki... Tusubiri tuone sheria ikifanya kazi!!
 
Hapo sasa atakuwa ameweka mambo sawa. Siku zote nimekuwa nikisema hoja kuu ni maazimio ya Zanzibar na Arusha...sasa wanafanya biashara hakuna mwiko unaowakataza. Lakini maadam utaanzishwa utaratbu wa kuwabana, basi panaweza kuwa na mabadiliko. Tutaangalia kasi ya wafanyabiashara kukimbilia bungeni...

Sina hakika kama wengi wataweza kuachia shughuli zao kwa kuwa biashara za bongo zinaendeshwa kimafia sana kukwepa kodi na sheria nyingine. wengi wanapenda kuwa mastering wenyewe kuficha mambo haya. Na ndiyo sababu kubwa hawapendi kupanua mitaji kupitia DSE kwa kuwa watawajibika kuwa wawazi zaidi kwa wenye hisa.

Mbalamwezi;

Nafikiri Kikwete na Viogozi wengine they are learnig faster kwa kinachotokea kwa majirani zetu!

Kujicomit na kuruka hewani kuwa unafanya kitu kama hiki alafu akafanya mzaha, kweli huo sio mzaha wa kuwafanyia wanachi sikuhizi. Itabidi wawe serious vinginevyo nchi inakwenda kubaya. Nafikiri pia sheria itanweza kumcover Benjamin sina hakika..kwani inakuwaje kosa kama ulilifanya kabala sheria haijafanya kazi ..linahesabika? smting of tat nature.. Im not sure! But we hope wataepusha matatizo makubwa kama sheria ikawepo na kuwakweli effective!
 
Kasheshe hivi Azimio la Arusha lilivunjwa na CC hii hii ama na nani ? Maana JK alikuwa ni waziri pia na naamini alishiriki kulivunja haya hakuyaona ?
 
Kufanya mzaha katika hili ni kujipunguzia kwa makusudi credit wakati wa tathmini ya uongozi mwaka wa tatu. Sidhani kama atapenda kuendelea kupunguziiwa units, hasa wakati huu ambapo zogo la madini alilolianzisha bado linamyumbisha
 
Inachekesha sana, yaani mtu kama humjui JK atakuchezea sana, kila siku atakuwaacha mdomo wazi. Haya bwana endeleeni kutega mikono...mkisubiri matunda yadondoke!

Kuna tofauti kubwa sana kati ya kutaka kufanya na kuwa na uwezo wa kufanya

Vilevile kuna tofauti kubwa sana katika siasa kati ya kuwa ofisini na kuwa madarakani..akili ni nywele...
 
Back
Top Bottom