JK na maadili ya viongozi

Why now??? Kuna nini? Sasa akina Dialo na Karamagi waachie ndugu zao hizo biashara? Haieleweki vizuri?

There is a wide gap btn lisemwalo na JK na actual reality! Sasa hawa wote si marafiki na washkaji wake?
 
Mzalendohalisi:

Ninaisubiri hiyo siku! Siku amabayo lilebunge litakwa clearn. Pasiwe na hata mbunge mmoja anayemfanania Raisi wetu mtukufu Mtsaafu BWMkapa.
 
Hotuba Ya Leo Hakuna Jipya..hiii Hotuba Ni ..nitoke Vipi!!!!????..nadhani Mnanpata Hapo...sioni Mtu Wa Kutekeleza Miiko Ya Uongozi Hapo...especially Yeye..atamuambia Nini Rostam Au Karamagi Zaidi Ya Kulalamika Kama Mtoto Wakati Yeye Ndie Rais...wenye Pesa Walishamnunua Tangu 1995.....sijui Price Tag Yake Tu..anayeijua Atuambie..
 
Kwa rais wa nchi masikini kama tz kuongelea uchumi wa dunia ni nonsense,kuyumba uchumi wa US na kuongelewa na JK ni nonsense.Hapa anataka kutuaminisha nini???

Mr president kuongelea wachungaji ngombe ni non sense sasa wakuu wa wilaya ,mikoa wapo huko wanafanya nini???

kusubiri mpaka rais aje atoe maagizo? ama unataka kutuonyesha unawajibika ipasavyo??

Kupoteza mda kuongelea BOT na kuunda tume juu ya tume ni ngojera zilizopitwa na wakati ,hapa isue ilikua fupi sana ni kukamata na kutia ndani wote waliotajwa kwenye hiyo kampuni iliyokagua hizo akounti harafu upelelezi unafanywa na polisi lakini washukiwa wakinyea ndoo.

Mbona nchi hii inasheria za kunyanyasa masikini?? kalimanzira akishukiwa kaiba bata wa juma anakamatwa anapigwa marungu na polisi anatiwa kolokoloni na uchunguzi unaendelea wakati mshukiwa akiwa ndani
mbona hawa wa bot wanapeta na wanaundiwa kamati?? kuna nini ktk sheria zetu??

Na nyie wananchi kwanini pale kibaka mdogo akikwapua kuku pale kariakoo wa sh 500/= anapigwa anachomwa motto .
lakini wezi wanao create vibaka hao wakiingia mikataba ya ku kireate wamatonya na hata wakiimba mambilioni ya fedha bado hata hatuthubutu kuruwarushia jiwe na bado wakija tunawaita waheshimiwa??? something here wrong.

Mr president siku yaja nayo imekaribia ole wao watakaokutwa hai siku hiyo maana watalia na kusaga meno
 
Inachekesha sana, yaani mtu kama humjui JK atakuchezea sana, kila siku atakuwaacha mdomo wazi. Haya bwana endeleeni kutega mikono...mkisubiri matunda yadondoke! Kuna tofauti kubwa sana kati ya kutaka kufanya na kuwa na uwezo wa kufanya Vilevile kuna tofauti kubwa sana katika siasa kati ya kuwa ofisini na kuwa madarakani..akili ni nywele...

Kitila I am afraid i agree with you. Sasa hivi kama kuna kitu kinachoitwa miiko ya uongozi, basi hapa Tanzania hakipo, na anayosema JK ni kuwazuga watu, au naweza kusema anasema ili kutekeleza wajibu anaopaswa kuutekeleza yaani kuzungumza akiwa kama Kiongozi, lakini so far sioni utendaji na utekelezaji wa yale anayosema.
Siamini kama viongozi wetu huwa wanaingia madarakani kwa uchu wa kuiendeleza Tanzania, kwa nia ya kuifanya Tanzania iwe nchi ya watu wenye maisha bora, nchi yenye watu wasiodhalilika kwa kutoishi maisha ya kubabaisha. Ninachoona ni kuwa wengi (sio wote) wanaingia madarakani kwa lengo la kujitajirisha au kutumia nafasi za uongozi kufananikisha mambo yao ya kujitajirisha.
Ninaamini kuwa kama kweli serikali ingekuwa na nia ya kuendeleza nchi, tungeona mabadiliko mengi ambayo ni tangible. Kwenye nchi za wenzetu tukisikia GDP inaongezeka, au uchumi unaendelea vizuri ina maana umaskini unapungua, watu wanakuwa na hopes za kupata ajira na kuwa na maisha mazuri, lakini hapa kwetu ni vice versa.
For sure kutokana na Azimio la Zanzibar, naweza kusema sasa hivi ukiangalia uchumi binafsi wa mawaziri wetu unapaa, EL alivyosema uchumi unapaa, kwa maoni yangu alikuwa anazungumzia uchumi wake binafsi, which is very true, wake na wa mawaziri wengine unapaa haswa.
JKN alisema sasa hivi ukizungumzia Azimio la Arusha (miiko ya uongozi) utakuwa kama mwendawazimu. Mimi binafsi sikubaliani na vipengele vingi vya Azimio la Arusha, kwa sababu vingi ni very utopian, lakini nakubaliana sana na vya miiko ya uongozi. Lakini navyo leo hii havitekelezeki. CCM wamelease chama kwa wafanya biashara, sasa hivi wanataka returns na faida juu, kama ukileta miiko sasa hivi hakuna atakayerudisha investment yake na kupata returns. Ninachokiona sasa hivi ni kuwa tunazungwa tu, na tutaendelea kuzugwa hadi tutakapoamua na kuweza kuchukua hatua, lakini wakati huo watu watakuwa wameneemeka sana, in our expense.
 
kufanya kweli kwa vitendo na kutamka kwa maneno matupu ni mambo mawili tofauti sana. Sijui President atafanya nini kati ya hayo, ila kama kweli atafanya lile la kwanza, basi atakuwa amejizolea heshima kubwa sana kutoka kwangu ambayo huwa siitoi kirahisi kwa wanaisasa. Nitabadilisha mtazamo wangu kwake binafsi na kwa kiasi fulani kwa CCM pia.
 
Nimemsikiliza, ameliongelea na anasisitiza kuwa ataanzisha mchakato wa jinsi ya kutengeneza sheria ya kulifanya litkelezeke. When? How soon? bado ni kitendawili!

Too little too late! Kama kweli ana nia ya kuleta mabadiliko ya kweli katika viongozi wa Tanzania na maadili yao basi aruhusu katiba itungwe upya kabisa sio hivi viraka wanavyoviweka kila kukicha vinavyoulizana mwenzangu umekuja lini!
 
Guyz mimi niliisubiri kwa hamu sana hiyo hotuba na nilifanikiwa kuiwatch. Sijaona chochote kipya. In short there is no substance kwenye hili la maadili ya uongozi, maana alichosema kila mu anaweza kusema na ni kama ambavyo amekuwa akisema. Usaniii tuuu. tuamkeni watz jamani
 
Kuna tofauti kubwa sana kati ya kutaka kufanya na kuwa na uwezo wa kufanya

Mh. Kitila Mkumbo.

Nakubaliana na wewe, lakini at least kwenye cheo kama cha Rais, huwa hafanyi, anaagiza!!!... mpaka pale tayari, sasa ofisi ya Marimo inatakiwa kuja na msimamo baadaye kwamba not feasible au mission has been accomplished!

In fact ingekuwa nchi makini, baada ya rais Kusema tungekuwa tunakula sahani moja na ofisi ya rais utawala bora! na mwanasheria mkuu!!!

Sasa sisi tuna-kaugonjwa kakudhani rais ndiye anayefanya mambo yote!!!

In short tuna matatizo ya kujua who is who!!! mifano iko mingi... unakuta tatizo la halimashauri... linapelekwa serikali kuu,,, tatizo la serikali kuu linapelekwa halimashauri bora kila kitu kimeparanganyika
 
hotuba ni nzuri na inatupa moyo sana ss wananchi kuwa tatizo limeonekana na wamelizungumza na kutuahidi kulifanyia kazi.

tunaomba watekeleze kama walivyolizungumza.

hii ni nchi yetu sote na tuiombee kila la heri na tupongeze pale tunajaribu kujenga misingi ambayo itatusaidia.
 
Inafurahisha kusoma uzobwe wa huyu jamaa.

Kitu kimoja ambacho nitamuunga mkono akikifanya ni kulivunja Bunge, kutengeneza Serikali ya mpito huku akirekebisha Katiba, kisha kuitisha uchaguzi mpya wa Wabunge kukiwa na masharti makali na magumu yanayohusu uadilifu, mali na mapato.

I would rather see us spending money on that process and not waste time and resources in 2010!
 
Wana JF,
Kuna kitu kimenishangaza katika hotuba hii ya Mkuu wa Kaya. Analalamikia watu ambao wengi amewateua yeye (ukiondoa nafasi za kuchaguliwa); then leo anazungumzia kuchanganya biashara na uongozi.
Mheshimiwa anataka tuamini kwamba alilazimishwa kuwateua kina EL, Karamagi, Daillo etc kuunda baraza lake la mawaziri? Kama aliona ni vibaya mtu kufanya biashara ukiwa kiongozi, alipowateua aliamini kwamba wataacha biashara zao?

Hata leo ana uhuru wa kuondokea mawaziri (na viongozi wengine) anaodhani wanachanganya interests(public/personal).
 
Implimentation ya hili jambo naona kama itakuwa ngumu sana. Kwa sababu serikali (Mawaziri) wengi ni wafanyabiashara, na huenda waliingia kwenye siasa ili biashara zao ziende vyema. Pia viongozi wengi wa chama ni Wafanyabiashara, wabunge e.t.c. Kwa kweli huu ni mtihani mzito kwa JK. Wafanya biashara hawa ndo inasemekana wamekuwa wakifadhili chama na hata kampeni za Chama. Baadhi ndo walioshiriki katika kumuweka madarakani.. Acha tuone itakuwaje.
 
Mh. Kitila Mkumbo.

Nakubaliana na wewe, lakini at least kwenye cheo kama cha Rais, huwa hafanyi, anaagiza!!!... mpaka pale tayari, sasa ofisi ya Marimo inatakiwa kuja na msimamo baadaye kwamba not feasible au mission has been accomplished!

In fact ingekuwa nchi makini, baada ya rais Kusema tungekuwa tunakula sahani moja na ofisi ya rais utawala bora! na mwanasheria mkuu!!!

Sasa sisi tuna-kaugonjwa kakudhani rais ndiye anayefanya mambo yote!!!

In short tuna matatizo ya kujua who is who!!! mifano iko mingi... unakuta tatizo la halimashauri... linapelekwa serikali kuu,,, tatizo la serikali kuu linapelekwa halimashauri bora kila kitu kimeparanganyika

Kasheshe,

Kama Raisi angekuwa ni mchapa kazi na kuheshimika kwa wasaidizi wake kama Jakaya na si woga wa kuwa yeye ni Raisi, basi ungeona utekelezaji na ufanisi katika kila ngazi.

Tatizo ni hili; Rais Kikwete ni mbambaishaji na kila mtu analijua hilo ndio maana ulegelege, ugoigoi, uzembe na ufisadi uko kila kona!

If the president is weak, how do you expect his surbodinates to be effective?
 
About ten years ago at JF of that time Nyenzi.com I told somebody that Politics is now the new entrepreneurship!

Watu wakakataa! Look what is happening now. People are looking for cheap ways to accumulate wealth and not putting ther energies to be creative and innovative to build such wealth!
 
Wana JF,
Kuna kitu kimenishangaza katika hotuba hii ya Mkuu wa Kaya. Analalamikia watu ambao wengi amewateua yeye (ukiondoa nafasi za kuchaguliwa); then leo anazungumzia kuchanganya biashara na uongozi.
Mheshimiwa anataka tuamini kwamba alilazimishwa kuwateua kina EL, Karamagi, Daillo etc kuunda baraza lake la mawaziri? Kama aliona ni vibaya mtu kufanya biashara ukiwa kiongozi, alipowateua aliamini kwamba wataacha biashara zao?

Hata leo ana uhuru wa kuondokea mawaziri (na viongozi wengine) anaodhani wanachanganya interests(public/personal).
Roya Roy,

Nakubalina nawe, lakini pia sikubaliani nawe!


a) Ni kweli kwamba Rais ana uamuzi wa kuchagua waziri X... lakini ukumbuke pia hakufahamu ni kwa kiasi gani Waziri wako akiwa/anapokuwa mfanya biashara anaadhiri utendaji wa kazi yake ya umma kwa jamii ya watanzania!
b) Nia ya Rais si kwa Mawaziri tu, na kama ingekuwa hivyo kweli kusingekua na haja ya yeye kuyasemea hayo... lakini upande wa wabunge pia hawawajibiki vizuri. Kwa hiyo kunahitajika muongozo.

c) Nafurahi Rais anayependa kuweka mfumo (system) through legal framework, tofauti na yule ambaye anadhani atafanya tu mwenyewe... tukiacha hili liwe la matakwa ya Rais, basi Rais ajaye anaweza kulirudi kule kule tulipokuwepo.
 
Hivi nyie mnaomponda JK mna ajenda gani? Nchi inakwenda vibaya anarekebisha, badala ya kusubiri matokeo mnaponda tu. Je asipotekeleza hayo anayosema si itakuwa balaa?
 
Kasheshe,

Kama Raisi angekuwa ni mchapa kazi na kuheshimika kwa wasaidizi wake kama Jakaya na si woga wa kuwa yeye ni Raisi, basi ungeona utekelezaji na ufanisi katika kila ngazi.

Tatizo ni hili; Rais Kikwete ni mbambaishaji na kila mtu analijua hilo ndio maana ulegelege, ugoigoi, uzembe na ufisadi uko kila kona!

If the president is weak, how do you expect his surbodinates to be effective?
Rev. Kishoka,

Nakubaliana nawe alafu sikubalini nawe....

Kwa nini!....
a)Binafsi hata niongozwe na kiongozi mbovu vipi nitachapa kazi na nitatimiza wajibu wangu!
b)Jamii ya Tanzania imeparanganyikiwa, kwa sababu haipendi ku-promote system ifanye kazi yake... inaamini mtu mmoja president ndiye afanye kila kitu... huu ni uzembe mkubwa sana kwa Watanzania.

c)Mfumo wa serikali unaruhusu kila mtu afanye upande wake... mkuu wa wilaya, mkuu wa mkoa, police, PCCB, usalama wa Taifa, mahakama... vyombo hivi vikifanya kazi yake vizuri... Rais hana kazi nzito yoyote...
 

By The Citizen Team and Agencies

President Kikwete has hinted at the need for cabinet ministers and members of Parliament to choose between private business and serving the public, in what seemed to be a reverting to the defunct Leadership Code enshrined in the Arusha Declaration.

The head of state made this remark during his end-of-the- month speech on radio and television last evening, raising concern about leaders who have been developing the culture of serving two masters at the same time.

The president said there was credible evidence that people who engaged directly in business and at the same serving as public leaders were prone to conflicts of interest when making decisions, as most decisions they made favoured them and their economic activities.

He said the practice was among major factors bringing about mistrust in public officials, including casting doubt on their leadership ethics and integrity generally.

The president maintained that to enforce the need to separate business from leadership, the Public Leadership Code of Ethics Act of 1995 as reviewed would soon start being implemented.

Public officials would be required to detach themselves from their businesses should they be elected or appointed to serve the people or vice-versa.

He explained that the same system applies in the developed world whereby a person elected to serve as a legislator or appointed to a ministerial post is required to stop engaging in businesses directly until such a leader ceases to serve the people as a public officer.

He said in such countries there is a legal system whereby businesses of public leaders are run by trustees until owners regain direct control after their tenure of office comes to an end.

The scrapped Leadership Code attached to the Arusha Declaration tied public officials to its tenets. The document was considered to be a cornerstone for righteousness among the leaders as it addressed moral and behavioral aspects of public leaders.

But the Arusha Declaration was dissolved in Zanzibar in 1992 giving birth later to the Public Leadership Code of Ethics Act of 1995 which President Kikwete wants reviewed, as it has lacked in enforcement.

In the same speech yesterday the president issued a two-month ultimatum to illegal immigrants living in the country to surrender themselves to the Immigration Department before the law takes its course.

President Kikwete issued the ultimatum following reports that there has been an influx of illegal immigrants entering the country either through illegal entry points or by being given permits by unauthorised officials.

Speaking from the experience he gained when he toured Kagera region last week, President Kikwete said it was unfortunate to learn that some government executives in lower ranks living close to border posts have allowing herders to enter the country without following proper procedures.

Due to this unstable state of affairs at the border posts, the President ordered government officials to institute stern measures against herdsmen crossing into the country or leaders found to be harboring them.

Addressing the issue of investigation on the loss of Sh 133 billion in the External Payment Arrears (EPA) account, President Kikwete said no stone would be left unturned until the money was recovered and those responsible be brought to justice.

He called upon the public to be patient as state organs continue with investigations. I believe this work will be completed in a six month period as I ordered, he affirmed.

The president, however, expressed his concern on misleading reports about the scandal, urging wananchi to disregard them as truth will come out from the investigation team.

But, he could not disclose the reports which he described as misleading rumours. President Kikwete also used the occasion to urge the public to accord cordial welcome to the US President George W. Bush during his state visit mid this month, saying the tour was advantageous to the country.

Meanwhile, experts have asserted that there is dire need for a proper re-examination of the current leadership situation in the country to avert conflicts of interest when entrepreneurs are elected or appointed into public offices.

Prof Marjorie Mbilinyi, a top consultant with the Tanzania Gender Networking Programme told The Citizen yesterday that to solve the problem of conflict of interest Tanzania would have to go back and re-examine the current neo-liberal economic situation that it embarked after the collapse of Ujamma.

You have now an economy that promotes individualism and exports, with total disregard of the effects on the ground.

The multinationals that hold sway utilize and corrupt local companies and individuals including politicians and other influential people to their own advantage,� she asserted.

Dr Haji Semboja of the Economic Research Bureau of the University of Dar es Salaam (UDSM) said leaders should be made to declare their interest before they are appointed to public offices, and if there is an imminent conflict of interest they should refrain from accepting those appointments.

He said a businessman owning or having shares in a commercials bank should not accept becoming a governor of the central bank, for example. It is not bad for businessmen and entrepreneurs to engage in public offices. It is only bad when there is a conflict of interests. And leaders should therefore declare their interest first, he said.

Prof Francis Matambalya of the Faculty of Commerce and Management at the Hill said Tanzania should design some kind of leadership code that would spell out the dos and don�ts for leaders who have business interests.

There is nothing wrong to mix business with politics. In fact entrepreneurs can be very good politicians. Tanzania should learn from those countries that have succeeded in avoiding conflicts of interest. This is not the first country to allow leaders to have some business interests, he further noted.

Prof Matambalya said the problem was that when the Leadership Code of the Arusha Declaration was recanted it was not replaced by another. There is need now to design a new code which might not be as strict as the former.

Prof Mbilinyi said the conflict of interest looms due to a loss of a sense of patriotism and policies that do not promote sustainable economy capable of lifting the lot of the majority poor.

Prof Semboja said leaders should work hard to ensure their business advancements do not retard the advancements of the people they serve.

Leaders who care much for their business interests are more of the results of the kind of the messy we are now in, Prof Mbilinyi intoned, emphasising that unless the current economic direction is not reexamined and reoriented together with the leadership such conflicts of interests would persist.

Prof Matambalya mentioned some countries with good leadership codes where Tanzania can learn from as Austria, Germany, France, and Sweden.

The chairman of the Tanzania Labour Party (TLP), Augustine Mrema expressed surprise over the president's remarks, wondering how he appointed ministers without that knwoledge.

The fact in this country today is that ministers and permanent secretaries are more businessmen than public servants.

They have formed companies which benefit by their influence,� Mr Mrema, a former deputy prime minister, noted. He said the president was not supposed to complain on the matter but to act on the matter soon.

The government has turned to be of businessmen and racketeers. We cautioned this before but our calls went unheeded, Mr Mrema elaborated.

He proposes that when a businessmean is elected or appointed to run the high profile public office, it should be compulsory for them to surrender their business interests to the Administrator General. Reported by Rodgers Luhwago, Damas Kanyabwoya and Bernard James
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom