JK na maadili ya viongozi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK na maadili ya viongozi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Halisi, Jan 31, 2008.

 1. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #1
  Jan 31, 2008
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  JK ameona madhara ya viongozi wa kitaifa kufanya biashara na sasa anawashukia kama mwewe.

  Habari zaidi saa 2.00 usiku.

  Hata hivyo tukumbushane hoja nyingine ya Zitto ilivyozimwa na Ofisi ya Bunge, baada ya kuwasilisha haya hapa chini, alipigwa chenga:

   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Jan 31, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Kuna tetesi kuwa Dr. Idris hatimaye kajiuzulu.. je kuna ukweli wowote.. simu zanguu leo haziingii Dar.. anybody...
   
 3. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #3
  Jan 31, 2008
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Halisi, Shukrani!

  Tuna isubiri kwa hamu hii taarifa ya habari. Mimi nadhani kama wengi walivo ongelea hapa kuhusu hizi conflict of interest na madhara ya Azimio la Zanzibar, imefika wakati murua hili swala lishughulikiwe ipasavyo, lasivyo hizi scandal kubwa na ufisadi kama utendekavyo Bongo ,will never end... yaani uko hadharani mno.... frauds na scandals will always be there katika nchi yoyote... ila katika Tanzania yetu, ufisadi ni kama umehalalishwa vile..

  Kuna mtu mmoja ambaye, swala hili kila linapoongelewa mimi namkumbuka.... naye ni Spika wetu wa Bunge. Yaani nimeona ame facilitate sana kudolola kwa katiba na chachu ambayo inaweza kupatikana kutoka kwa Wabunge wetu ( offcourse majority ni CCM). Huyu speaker angelikuwa mwenye lengo kubwa la kuleta mabadiliko kikatiba, kisheria na hivyo maendeleo ya nchi yetu, inabidi tumkazanie maana anazima sana hoja zinazolenga kuleta maendeleo nchini mwetu, na anafanya hivyo kwa sababu tu zimetolewa na wapinzani.... this is annoying me badly, Bila the likes of Zitto na Dr. Slaa, haya mambo ya BoT na Buzwagi tusingeyaona wala kuyasikia wengi wetu.... and what did the speaker do?... he indeed from his heart played their claims,speculations down.. and now we know what's up at least to some extent about numerous scandals kutokana na harakati na umwanamapinduzi wa wachache uliotaka kuzimwa na wabunge wengi wafata mikumbo na itikadi badala ya maendeleo ya nchi yatu.


  SteveD.
   
 4. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #4
  Jan 31, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  SteveD,

  Lakini pia tuangalie tutazuia vipi viongozi hao hao kuendelea kufanya biashara kupitia wake zao au ndugu zao?

  Kama sheria mpya inakuja basi iweke pia makali kwenye tume za maadili na kuhakikisha zina meno na uwezo wa kufanya uchunguzi, vinginevyo hawa jamaa, wataondoa majina yao na kuweka ya ndugu huku ukweli wao wenyewe ndio watakuwa wanafanya biashara.

  Kama mkuu Halisi kasema, basi kuna jambo kubwa linakuja leo jioni.
   
 5. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #5
  Jan 31, 2008
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Mtanzania,
  Kitu kikubwa ni kuwa sheria zetu hazitekelezeki ipasavyo. Nina imani kubwa hilo swala lipo tayari kwenye sheria zetu za kibiashara na kwenye miongozo ya Takururu na sheria za mahakama zetu. Ila ufatiliaji wake ndiyo unaweza kuwa wa kero na wakutia shaka nchini mwetu.

  Kawaida ninavyojua, na hili ni katika nchi nchi nyingi, wafanyabiashara wengi wakifanya ma deal yao na kuonekana wata fahamika, wanafanya juu chini na kubadili jina la biashara zao. Kwa huko Ulaya hili swala linafanyika sana kwa wafanyabiashara walioko kwenye entertainment, kwa kubadilisha majina ya clubs... sheria za kufanya hivyo zipo zinawaruhu ila kama kawaida, watu ni wajanja, wanatumia ruhusa hiyo kufanya mengineyo.

  Mimi siyo mtaalam wa sheria za kibiashara, lakini nina imani kuwa, kama mtu ana rithisha mali kwa ndugu au mtu kwa nia mbaya ya kukwepa kukamatwa, mtu atakaye rithi hiyo mali naye ni mtuhumiwa vile vile.... ni sawa na kununua kitu cha wizi au magendo bila receipt.... kitu kina kuwa confiscated bila kurudishiwa gharama zako. Sheria za kusimamia swala hili nina imani zipo Tanzania yetu, ila usimamizi wake ndiyo haupo. Auditing za kampuni yoyote ile ikifanyika na mali zake za kurithishwa na zile zake toka awali kama zipo ni rahisi kuijua.... kama ni biashara na iko registered BRELA basi ni lazima itaje capital na funding zote za pembeni....

  Kwa hiyo basi, kama wao ni kuondoa majina yao huku wakiendelea kufanya majidubwasha yao ki-proxy, nadhani sheria kama ilivo kawaida yetu ishindwe tu kutekeleza, maana vipengele vya kupinga hilo tayari vipo. Sioni kama sheria ya kurithishwa mali kibiashara ina weza kubadilishwa na kuwekewa ka-clause kamoja kwa ajili ya viongozi tuu... hilo litakuwa vigumu, maana huwezi kutabili kama mtu anaweza kuwa kiongozi au kama ataacha kuwa kiongozi, hii inaweza kusababisha mgongano wa ndani kisheria. Ila nina imani kuna room for improvement as always with sheria zetu including hizi za biashara. Ngoja niwaachie wataalam wa hili.

  SteveD.
   
 6. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #6
  Jan 31, 2008
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Ni hatua mabayo mimi bado sijaamini..kama ni kweli. Kinachotakiwa ni kitu ambacho kitareplece Maadili ya uogoi yaliyo FISADISWHA la AZIMIO LA ZAMNZIBER. bASICALY NI KITU KITAKACHOJIBU HOJA KAMA HII:

  Kama kweli hiyo sheria itakuwa inajibu hoja hii ya MAADILI YA UONGOZI...ni ajabu..lets wait and see! Maana ni almost kurudisha Azimio la Arusha. Maana Azimo la Arusha it was the doc ya MIIKO YA UONGOZI jumlisha na CONCEPT NZIMA YA KUJITEGEMEA KIUCHUMI

  Mkumbuke Baadaya ya kungofoa MIIKO YA UOGOZI ndio uozo wa kina ulipoanza kujiteza.Ndipo UFISADI ULIKUWA UMEJIFICHA ulianza kujitokeza hadharani

  Wengi wanaamini ndio Kigezo alichotumia BENJAMIN MKAPA kujiamnisha na kufanya upuzi aliofunaya IKULU.

  Ni kweli kabisa lazima kuleta sheria effective ya kuzuia Hilo.
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  Jan 31, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Hivi hawa wamewahi kusikia kitu kinachoitwa Azimio la Arusha ambapo ndani yake kuna "Miiko ya Uongozi"?
   
 8. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #8
  Jan 31, 2008
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Wabunge, mawaziri Tanzania kuchagua uongozi au biashara
  Na Mwandishi Wetu


  RAIS Jakaya Kikwete amewataka wafanyabiashara ambao ni wabunge na mawaziri kujiandaa kuchagua kimoja kati ya biashara au uongozi serikalini


  Akizungumza jana katika utaratibu wake wa kila mwezi jana, Rais Kikwete aliwataka kuchagua jambo moja kati ya uongozi au biashara ili wasiendelee kuondokana na mwingiliano wa kimaslahi.

  "Viongozi wetu wachague kufanya jambo moja kwa wakati mmoja ama biashara au ubunge na Uwaziri. Kwa ajili hiyo ni makusudio yangu kuanzisha mchakato wa kufanya marekebisho ya Sheria ya Maadili ya Uongozi ili tuingize utaratibu huo," alisema kuongeza.


  "Ni jambo lenye maslahi kwa nchi yetu na litasaidia sana kujenga heshima ya viongozi wa umma mbele ya macho ya wananchi. Nafurahi kwamba suala hili tumelizungumza katika kikao maalum cha Kamati Kuu ya CCM tulichofanya Dodoma juzi Januari 29 na tumeelewana."


  Alisema upo ushahidi wa kutosha wa kuwapo migongano ya maslahi kwa baadhi ya viongozi hao wa kisiasa suala linalosababisha wananchi kukosa imani na serikali.


  Akitoa mfano wa mataifa yaliyoendelea alisema kuwa mataifa hayo yanao utaratibu unaomtaka mtu mwenye shughuli za kibiashara anapokuwa Mbunge au Waziri kuacha kujishughulisha na biashara zake na kwamba unakuwepo utaratibu rasmi unaotambuliwa kisheria wa wadhamini wanaoendesha hizo shughuli bila ya yeye kujihusisha nazo.


  Akizungumzia suala la uhamiaji haramu nchini alitoa siku sitini za kwa wahamiaji haramu kujisalimisha. Baada ya hapo hatua zipasazo za kisheria zitachukuliwa kwa wale ambao watakuwa hawa kufanya hivyo.


  Alisema kuwa ameamua kuchukua hatua hiyo baada ya kushuhudia mambo yasiyokubalika yakitendeka wakati akiwa kwenye ziara ya siku kumi Mkoani Kagera ambapo alikuta ukiukwaji wa sheria na taratibu za uhamiaji na uingizaji mifugo nchini.


  Alisema kwa muda mrefu sasa, raia wa nchi jirani zinazopakana na Mkoa wa Kagera wamekuwa wakiingia na kuishi nchini kwa vibali vya viongozi na watendaji wa vijiji na kata. Baadhi ya watu hao pia wamekuwa wakiingiza mifugo kwa vibali vya viongozi hao hao.


  Suala hilo alisema halikubaliki kwani kwa mujibu wa sheria na taratibu za uhamiaji zinatoa mamlaka hayo kwa Maafisa Uhamiaji tu na si vinginevyo na kuwa viongozi na watendaji wa vijiji na kata hawana mamlaka hayo.


  Hivyo alisema, vibali vyote walivyotoa viongozi hao si halali na havitambuliki na akapiga marufuku kwa kiongozi au mtendaji wa ngazi yoyote ile nchini kutoa kibali cha mgeni kuingia au kuishi nchini kama siyo Afisa wa Uhamiaji.


  "Nilipokuwa Mkoani Kagera niliwaagiza Mkuu wa Mkoa na wakuu wa wilaya kufuatilia utoaji wa vibali unaofanywa na viongozi na watendaji wa vijiji na kata katika maeneo yao.


  Nimewataka wawachukulie hatua zipasazo za kinidhamu watumishi hao wa umma pamoja na kuwabana wahamiaji haramu kufuata sheria za uhamiaji za nchi yetu au warudi

  makwao. Napenda kusema kuwa maagizo hayo ni kwa wakuu wote wa mikoa na wilaya nchini," alisema.


  Sambamba na hilo pia ameiagiza Wizara ya Maendeleo ya Mifugo kutoa mwongozo wa jinsi ya usafirishaji mifugo kwa kuwa uvushaji unaoendelea sasa unaweza kusababisha hatari kubwa ya magonjwa ya milipuko kwa mifugo.


  Pia alizungumzia la upandaji wa bei ya mafuta duniani akataka wananchi kuwawaangalifu na hasa wabanifu katika matumizi ya mafuta na kuepuka matumizi yasiyo ya lazima.


  Alitaka juhudi za kuzalisha nishati mbadala kutokana na mimea hususan miwa, mawese na mbono-kaburi (jatropha) ziongezwe ili kama zikifanikiwa zisaidie kupunguza mzigo wa mafuta yanayoagizwa kutoka nje.


  "Nafurahi kwamba juhudi zetu zina muelekeo mzuri na katika miaka michache ijayo tutaanza kunufaika na matunda yake. Pamoja na hayo tunaendelea na juhudi za utafutaji wa mafuta na gesi asilia hapa nchini,"alisema.


  Kuhusu Uchunguzi wa Akaunti ya EPA alisema Serikali imedhamiria kulifuatilia suala hilo mpaka mwisho wake ambao utakuwa na maslahi kwa taifa.


  Akawashukuru Watanzania kwa kuunga mkono hatua alizochukua na anazoendelea kuchukua kuhusu suala la Benki Kuu. Hata hivyo, alieleza kusikitishwa na taarifa anazozipata kuhusu kuwepo uvumi mwingi unaoenezwa na baadhi yetu kuhusu suala hilo.


  Hivyo akakemea wale wote wanaoeneza uvumi na uongo kuacha kufanya hivyo na akawasihi wananchi wawe watulivu na wavumilivu.


  "Nawaomba Watanzania wenzangu tuwe na subira. Naamini kazi hii itakamilika ndani ya kipindi cha miezi sita tuliyowapa. Napenda kurudia ombi la Serikali kwa wananchi wenye taarifa zitakazosaidia katika uchunguzi na hatua katika suala hili waisaidie kamati yetu

  hiyo," alisema.


  Akizungumzia ziara ya Rais George W. Bush wa Marekani katikati ya mwezi Februari, 2008 aliwataka wananchi wampokee kwa mujibu wa desturi na ukarimu wa Kitanzania kwani ujio wake unakuja na neema nyingi tofauti na uvumi unaoenezwa kuwa anakuja kuanzisha Makao Makuu ya Kamandi ya Jeshi la Marekani katika Bara laAfrika.


  Alisema wakati wa ziara yake hapa nchini, Serikali ya Marekani inatarajia kutiliana sahihi msaada mkubwa wa maendeleo unaoelekezwa katika kuboresha miundo mbinu ya barabara, umeme na maji.


  Kwa upande wa hali ya kisiasa na kiusalama ya nchi jirani ya Kenya alisikitishwa na jitihada zanazofanywa na jumuiya mbalimbali za kimatiafa kutozaa matunda hivyo kusababisha hali kuwa mbaya nchini humo kiusalama.


  Alisema serikali inaiunga mkono Kamati ya Kofi Annan (Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja wa Mataifa), Rais Mstaafu wa Tanzania, Benjamin Mkapa na mke wa wa Rais mstaafu wa Afrika Kusini, Graca Machel.
   
 9. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #9
  Jan 31, 2008
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Nimemsikiliza, ameliongelea na anasisitiza kuwa ataanzisha mchakato wa jinsi ya kutengeneza sheria ya kulifanya litkelezeke. When? How soon? bado ni kitendawili!
   
 10. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #10
  Jan 31, 2008
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Hope he will make sure it is done soon, as it is long due... kama CC ya CCM imepitisha hope it won't take long.
   
 11. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #11
  Jan 31, 2008
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Kasheshe;

  Nashukuru kwa kunitia moyo! Ninapokea kwa niaba ya watanzania wenzangu ambao wanaliaa na kupoteza imani na uongozi unafanya bishara za Kifisadi kwenye kila ngazi ya uongozi na kuwasahau WATU waliowaweka kwenye uongozi.

  Hata wamachinga wanao kula msoto mkali kila siku wakipigwa jua kali, wakinyeshea na mvua, kupigwa upepo na mavumbi bila kusahau usumbufu wa dola yenyewe, hata wao wangehitaji wapate UONGOZI WA JUU SEREKALINI ili uwape nafasi isiyo na usumbufu wafanye bishara zao kiulani!

  Kwani ukiwa kiongozi wa chama au serekali..nani atakufuatafuata? nani atakudai kodi, nani atkuzuia kufanya dili chafu chafu...? N awewe ni bwana mkubwa? Naam kweli ukiwa kiogozi unaweza kujifanyia bishara...utakavyo. Muulize Benjamin Wiliam Mkapa mambo yalivyomnyokea. Muulize akuonyeshe alivyoweza kufanya "Buznesi" safi na kukwepa Udhia anoupata mmachinga anayetembeza DVD 2 mji mzima bila kupta hata mnnuzi wa kumfaya ajipatie hata Mmlo wa siku moja.

  Amakweli, uongozi ni "dili"

  Usiwaone wanagombania uogozi kwa mamilioni ya hela. Wanajua kufanya Biashara kimachinga hufiki mbali. Wengi wa hao viongozi tunaowaona hapo..They have nothing do to With "THE PEOPLE" UOGOZI USIOJALI "WATU" Uongozi unaojali "KUJITAFUTIA KIJIWE CHA BISHAARA" ni viongozi gani? Ni Msingi mkubwa wa ufisadi.

  Wa Tanzania Ni wakati wa kuamka.

  Hiyo sheria itengenezwe na itumike mara moja!
   
 12. Nikifufukammekwisha

  Nikifufukammekwisha JF-Expert Member

  #12
  Jan 31, 2008
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 260
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hotuba yenyewe ni kama ifuatavyo:

  HOTUBA YA MHE. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, KWA WANANCHI, 31 JANUARI, 2008

  Ndugu Wananchi;

  Ninayo furaha kwa mara nyingine tena kuzungumza nanyi kupitia utaratibu huu mzuri wa mawasiliano baina ya Rais na wananchi wa nchi yetu.
  Jambo la kwanza ninalopenda kulizungumzia linahusu uzingatiaji wa sheria na taratibu za uhamiaji na kuishi nchini.
  Ndugu Wananchi;
  Tarehe 23 mwezi huu, nilimaliza ziara ya siku kumi Mkoani Kagera. Jambo moja nililoliona kwenye ziara hiyo ambalo sikufurahishwa nalo, ni ukiukwaji wa sheria na taratibu za uhamiaji na uingizaji mifugo nchini.
  Kwa muda sasa, raia wa nchi jirani zinazopakana na Mkoa wa Kagera wamekuwa wakiingia na kuishi nchini mwetu kwa vibali vya viongozi na watendaji wa vijiji na kata. Baadhi ya watu hao pia wamekuwa wakiingiza mifugo kwa vibali vya viongozi hao hao.
  Wageni hao wamekuwa wanaingia na kuishi nchini isivyo halali. Sheria na taratibu za uhamiaji zinatoa mamlaka hayo kwa Maafisa Uhamiaji tu na si vinginevyo. Viongozi na watendaji wa vijiji na kata hawana mamlaka hayo. Hivyo basi, vibali vyote walivyotoa viongozi hao si halali na havitambuliki. Napenda kurudia kauli yangu niliyoitoa Mkoani Kagera kwamba ni marufuku kwa kiongozi au mtendaji wa ngazi yoyote ile nchini kutoa kibali cha mgeni kuingia au kuishi nchini kama siyo Afisa wa Uhamiaji.

  Ndugu wananchi;
  Wageni wanaoishi nchini kwa kutumia vibali ambavyo havikutolewa na Idara ya Uhamiaji wanaishi isivyo halali. Wenzetu hawa wanatakiwa kufanya yafuatayo. Kwanza wajitokeze na kutoa taarifa kwa Maofisa Uhamiaji, Wilayani au katika vituo vya mpakani. Pili, iwapo watachagua kuishi nchini, wafuate taratibu zilizowekwa kuomba kibali cha kuishi nchini. Idara ya Uhamiaji ndiyo itakayoamua. Tunawapa siku sitini za kufanya hivyo. Baada ya hapo, hatua zipasazo za kisheria zitachukuliwa kwa wale ambao watakuwa hawakufanya hivyo.
  Nilipokuwa Mkoani Kagera niliwaagiza Mkuu wa Mkoa na Wakuu wa Wilaya kufuatilia utoaji wa vibali unaofanywa na viongozi na watendaji wa vijiji na kata katika maeneo yao. Nimewataka wawachukulie hatua zipasazo za kinidhamu watumishi hao wa umma pamoja na kuwabana wahamiaji haramu kufuata sheria za uhamiaji za nchi yetu au warudi makwao. Napenda kusema kuwa maagizo hayo ni kwa Wakuu wote wa Mikoa na Wilaya nchini kwani inawezekana matatizo haya yanaweza kuwepo katika mikoa mingine.
  Najua kwamba kuna Watanzania wenzetu wanaohifadhi wahamiaji haramu kwa kuwa wananufaika kwa kuwafanya vibarua au wafanyakazi wao. Ukweli unabaki pale pale kwamba wanatakiwa waingie na kuishi nchini kwa kufuata taratibu zinazotambulika kisheria. Sheria za nchi, na sio manufaa ya mtu au watu binafsi, ni lazima zizingatiwe.

  Ndugu Wananchi;
  Jambo lingine baya linalofanyika katika mpaka wetu na nchi jirani Mkoani Kagera ni kuruhusu mifugo kuingia nchini holela. Hiki ni kitendo ambacho kinakiuka taratibu zinazotawala uingizaji wa mifugo kutoka nchi za nje. Pia ni kitendo cha hatari kwani kinaweza kupelekea mifugo yenye maradhi kuingia nchini bila kudhibitiwa na kusababisha maafa makubwa nchini. Kanuni na taratibu zimewekwa kisheria kutawala mifugo kuvuka mipaka na kuepusha hatari za namna hiyo zisitokee.
  Jambo linalonishangaza ni kwa nini viongozi wetu hawa hawajifunzi kutoka kwa majirani zetu. Wakati wote tulipofanya zoezi la kurudisha makwao wakimbizi au wahamiaji wasiokuwa halali na mifugo yao wenzetu waliweka sharti la mifugo hiyo hiyo iliyotoka kwao ichanjwe kwanza kabla ya kuvuka mpaka hata kama mifugo hiyo ilitokea nchini kwao na kuja kwetu. Nilidhani hili lingekuwa fundisho kwa viongozi wetu hawa kuwa thabiti kuhakikisha kuwa mifugo kutoka nchi jirani inachanjwa kabla ya kuvuka mpaka kuja Tanzania. Lakini, hawajali kufanya hivyo. Mkuu wa Mkoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi Watendaji wa Wilaya na viongozi na watendaji wa vijiji na kata kuhakikisha kuwa hakuna mifugo inayoingia nchini holela. Lazima sheria na kanuni husika zizingatiwe.
  Aidha, nimeelezwa juu ya kufahamika kuwepo vivuko haramu kadhaa mpakani. Nimesema nilipokuwa Kagera na narudia tena leo kwamba, maadamu vivuko hivyo vimejulikana lazima tuvidhibiti. Kadhalika tuanzishe vituo mpakani vya kupokelea mifugo na kila anayeingia na mifugo lazima apitie hapo na kupata idhini husika. Nimetaka viongozi wenzetu hao wasimuonee haya mtu yeyote anayeingiza mifugo nchini kinyume cha sheria na taratibu zilizopo. Kadhalika viongozi na watendaji wanaozembea wachukuliwe hatua kali za kinidhamu mara inapobainika kuwa mifugo imeingia kinyume na taratibu katika maeneo yao.
  Kama ilivyo kwa uhamiaji usio halali, tatizo la kuingiza mifugo kinyume na utaratibu linaweza kuwepo mikoa mingine nchini. Hivyo, maagizo haya ni kwa mikoa yote na wilaya zote nchini. Pia yanaihusu Wizara ya Maendeleo ya Mifugo. Lazima Wizara itoe uongozi katika jambo hili muhimu kwa usalama na maendeleo ya mifugo yetu nchini. Napenda kuwakumbusha Watanzania wenzangu kuwa hakuna nchi yoyote duniani inayoruhusu mifugo kuingia holela. Si vizuri Tanzania kuwa ndiyo nchi pekee inayofanya hivyo. Wenzetu na hata hao majirani zetu wanatustaajabu.

  Ndugu Wananchi;
  Jambo la pili ninalopenda kulizungumzia ni matatizo yanayoukabili uchumi wa dunia hivi sasa. Bado bei ya mafuta iko juu sana na kuathiri uchumi wa nchi zote duniani tajiri na maskini ingawaje nchi maskini zinaathirika zaidi. Hili si jambo geni kwetu. Napenda kurudia kauli zangu za siku za nyuma kwamba, hatuna uwezo mkubwa wa kujikinga na athari za bei za mafuta. Hata hivyo, hatuna budi tuendelee kuwa waangalifu na hasa wabanifu katika matumizi ya mafuta. Tuepuke matumizi yasiyo ya lazima.
  Wakati huo huo tunaendelea na juhudi za kuzalisha nishati mbadala kutokana na mimea hususan miwa, mawese na mbono-kaburi (jatropha). Juhudi hizo zikifanikiwa zitatusaidia kupunguza mzigo wa mafuta tunayoyaagiza kutoka nje. Nafurahi kwamba juhudi zetu zina muelekeo mzuri na katika miaka michache ijayo tutaanza kunufaika na matunda yake. Pamoja na hayo tunaendelea na juhudi za utafutaji wa mafuta na gesi asilia hapa nchini. Mpaka sasa leseni 22 za utafutaji mafuta na gesi asilia zimetolewa na kazi inaendelea katika hatua mbalimbali. Tuzidi kumuomba Mwenyezi Mungu atujaalie rehema zake na sisi tujaaliwe kugundua mafuta mengi hapa nchini yatakayotosheleza mahitaji yetu na ziada ya kuuza nje.
  Ndugu Wananchi,
  Tatizo lingine kubwa linaloukabili uchumi wa dunia sasa linatokana na matatizo yanayoukabili uchumi wa Marekani. Uchumi wa taifa hilo ambao ndiyo mkubwa kuliko wowote duniani umekuwa unapita kwenye misukosuko kwa miezi kadhaa na katika wiki chache zilizopita hali ikawa ngumu zaidi. Kasi ya ukuaji wa uchumi imepungua na thamani ya dola imeshuka. Serikali ya nchi hiyo imeanza kuchukua hatua za kukabiliana na matatizo hayo. Lakini, kwa kuwa uchumi wa Marekani ndiyo uchumi mkubwa kuliko wowote duniani na uchumi wa nchi nyingi duniani una uhusiano nao, matatizo ya uchumi wa nchi hiyo huathiri nchi nyingi. Na sisi Tanzania hivyo hivyo.
  Nimeelekeza wachumi wetu wafanye uchambuzi wa kina juu ya athari hizo na kushauri hatua za kuchukua kupunguza makali yake. Moja ya jambo ambalo liko wazi ni lile la kushuka kwa thamani ya dola ya Kimarekani. Sisi tunaweka sehemu kubwa ya akiba yetu ya fedha za kigeni katika dola za Kimarekani. Ni dhahiri kwamba kushuka kwa thamani ya dola za Kimarekani kunatupunguzia uwezo wetu wa kuagiza bidhaa nchi za nje.

  Uchunguzi wa Akaunti ya EPA
  Ndugu Wananchi;
  Jambo la tatu ambalo nimepanga kuliongelea leo ni hili suala la ukaguzi wa Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje na hatua zinazoendelea kuchukuliwa baada ya taarifa ya ukaguzi kutolewa.

  Ndugu Watanzania wenzangu;
  Kwa mara nyingine tena nawapongeza na kuwashukuru wakaguzi wa Kampuni ya Ernst and Young kwa kazi nzuri waliyoifanya na kutoa taarifa ya kina kuhusu matatizo yahusuyo matumizi ya fedha za Akaunti hiyo. Nawashukuru pia Watanzania wenzangu kwa kuunga mkono hatua tulizochukua na tunazoendelea kuchukua kuhusu suala la Benki Kuu. Hata hivyo, nasikitishwa na taarifa ninazozipata kuhusu kuwepo uvumi mwingi unaoenezwa na baadhi yetu kuhusu suala hili. Baadhi ya uvumi huo umekuwa unapotosha ukweli na kuwachanganya wananchi. Napenda kutumia nafasi hii kuwaomba wanaoeneza uvumi na uongo kuacha kufanya hivyo. Aidha, nawasihi wananchi wawe watulivu na wavumilivu.
  Napenda kuwahakikishia kuwa, Serikali inayo dhamira ya dhati ya kulifuatilia suala hili mpaka mwisho wake ujulikane. Mwisho ambao utakuwa na maslahi kwa taifa letu. Pamoja na yote yatakayofanywa, tunataka kuhakikisha kuwa fedha zilizolipwa kinyume cha utaratibu zinarudishwa. Mwanasheria Mkuu wa Serikali na wenzake, yaani Mkuu wa Jeshi la Polisi na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU wameanza kuchukua hatua. Nimewataka watoe taarifa kwa wananchi mara kwa mara kadri inavyowezekana pamoja na haja ya kuwa waangalifu kutokutoa mengi yahusuyo uchunguzi wanaoufanya ili ushahidi usiharibike.
  Nawaomba Watanzania wenzangu tuwe na subira. Naamini kazi hii itakamilika ndani ya kipindi cha miezi sita tuliyowapa. Napenda kurudia ombi la Serikali kwa wananchi wenye taarifa zitakazosaidia katika uchunguzi na hatua katika suala hili waisaidie kamati yetu hiyo.


  Ujio wa Rais Bush

  Ndugu Wananchi;
  Natumai mmesoma na kusikia taarifa katika vyombo vya habari kuhusu ziara ya Rais George W. Bush wa Marekani katika nchi yetu kunako katikati ya mwezi Februari, 2008. Tunaendelea kukamilisha ratiba na itakapokuwa tayari tutawapeni taarifa. Hilo ndilo jambo langu la nne leo.
  Napenda kutumia nafasi hii kuwaomba Watanzania tumpokee mgeni wetu huyu kwa mujibu wa mazoea na desturi za ukarimu wa Kitanzania. Huu ni ugeni mkubwa na wa heshima kubwa kwa nchi yetu. Rais Gerorge Bush ameipa heshima kubwa nchi yetu kwa kuamua kutumia sehemu kubwa ya ziara yake ya Bara la Afrika hapa kwetu. Ameonyesha upendo mkubwa kwetu nasi tumuonyeshe hivyo hivyo. Nawaomba Watanzania tujitokeze kwa wingi siku hiyo kumpokea mgeni wetu huyo mashuhuri.
  Ziara hii ni uthibitisho wa kuimarika kwa mahusiano kati ya Marekani na Tanzania. Mahusiano hayo mazuri yameinufaisha nchi yetu. Marekani sasa ni moja ya nchi zinazoongoza kwa kutoa misaada ya maendeleo kwa Tanzania. Tangu mwaka 2003 kwa mfano, imekuwa inatoa msaada mkubwa ambao umetusaidia sana katika mapambano yetu dhidi ya maradhi ya UKIMWI nchini Tanzania. Kadhalika, Marekani imetusaidia sana katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa malaria nchini.
  Ndugu Wananchi,
  Wakati wa ziara yake hapa nchini, Serikali ya Marekani inatarajia kutiliana sahihi msaada mkubwa wa maendeleo unaoelekezwa katika kuboresha miundo mbinu ya barabara, umeme na maji. Kwa msaada huo utakaotolewa kupitia Programu ya Mfuko wa Changamoto ya Millenia utatusaidia kutatua baadhi ya matatizo yaliyoonekana sugu katika baadhi ya maeneo hapa nchini.
  Pamoja na hayo, ziara ya Rais George Bush nchini mwetu itasaidia kuitangaza nchi yetu na kuinufaisha sana utalii na uwekezaji hasa kwa soko la Marekani na marafiki zake. Tayari katika miaka miwili hii tumeshuhudia ongezeko kubwa la watalii wa Kimarekani kutembelea nchi yetu. Hivi sasa Wamarekani ndiyo wanaoongoza kwa idadi ya watalii wanaotembelea hifadhi za Ngorongoro na Serengeti. Naamini baada ya ziara ya Rais wao watalii wengi zaidi wa Kimarekani watakuja. Hali kadhalika, wawekezaji wengi wa kutoka Amerika watajenga imani ya kuja kuwekeza nchini.
  Ndugu Wananchi,
  Wapo watu miongoni mwetu na hata nje wanajaribu kueneza uvumi wa uongo na kuihusisha ziara hii na masuala ya Makao Makuu ya Kamandi ya Afrika ya Jeshi la Marekani. Ni uongo na uzushi mtupu. Ziara hii haihusu hayo. Masuala hayo si agenda na wala Marekani haijaiomba Tanzania kuwa mwenyeji wa Kamandi hiyo. Nawasihi Watanzania wenzangu tupunguze hii tabia ya kuzusha na kueneza uongo. Tunajitia hofu wenyewe na wenzetu bila sababu. Haina tija yoyote. Nawaomba tujitokeze kwa wingi kumpokea mgeni wetu huyu. Aondoke nchini salama na arejee kwao akiwa na kumbukumbu nzuri ya nchi yetu na watu wake.

  Hali ya Kenya
  Ndugu Wananchi;
  Jambo la tano ninalotaka kulizungumzia ni hali ya kisiasa na kiusalama ya nchi jirani na rafiki ya Kenya. Kwa kweli inatusikitisha na kutuletea simanzi kubwa. Mioyo yetu inauma kuona na kusikia yanayotokea nchini humo. Jitihada yangu ya kuzungumza na pande zote zinazohasimiana pamoja na zile zilizofanywa na zinazoendelea kufanywa na wenzetu wengine bado hazijazaa matunda. Sisi hatutachoka na wala hatutaacha kuzungumza na pande zinazohusika kuhusu kuacha uhasama, kuacha na mapigano na kutafuta maridhiano kwa njia ya mazungumzo.
  Tunaahidi kuendelea kuiunga mkono Kamati ya Mhe. Kofi Annan (Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja wa Mataifa), Rais Mstaafu, Mhe. Benjamin Mkapa na Mama Graca Machel. Viongozi wetu hao wanaifanya kazi hiyo kwa niaba ya Umoja wa Afrika wanastahili msaada wetu na kuungwa mkono nasi. Aidha, tutaendelea kushirikiana na viongozi wenzetu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kusaidia juhudi za upatanishi. Napenda kutumia nafasi kurudia tena yale maombi yangu kwa viongozi wa PNU na ODM na wananchi wote wa Kenya kuyapa mazungumzo nafasi ya kumaliza tofauti zao. Mapanga, marungu na hata bunduki zisipewe nafasi, kamwe hazitasaidia.
  Tutenganishe Uongozi na Biashara

  Ndugu Wananchi;
  Jambo la mwisho ninalotaka kulizungumzia linahusu maadili ya uongozi nchini. Hususan napenda kulizungumzia suala la viongozi wa siasa Mawaziri na Wabunge kuwa pia watu wanaojihusisha na shughuli za biashara moja kwa moja. Upo ushahidi wa kuwepo migongano ya maslahi kwa baadhi. Lakini, pia, hata pale ambapo hakuna dalili za wazi, hisia za kupata manufaa yanayotokana na nafasi zao hutawala. Matokeo ya yote hayo ni watu kupoteza imani na kutilia shaka uadilifu wa viongozi wetu.

  Ndugu Wananchi;
  Nchi za wenzetu hasa zile za kibepari zinazo taratibu nzuri za kushughulikia hali hizo. Wenzetu wanao utaratibu unaomtaka mtu mwenye shughuli za kibiashara anapokuwa Mbunge au Waziri kuacha kujishughulisha na biashara zake. Unakuwepo utaratibu rasmi unaotambuliwa kisheria wa wadhamini wanaoendesha hizo shughuli bila ya yeye kujihusisha nazo. Anapoacha uongozi wa siasa kama atapenda atachukua tena mali yake na kuendelea na shughuli zake.
  Ni makusudio yangu kuwa utaratibu huu tuuanzishe hapa nchini. Viongozi wetu wachague kufanya jambo moja kwa wakati mmoja ama biashara au Ubunge na Uwaziri. Kwa ajili hiyo ni makusudio yangu kuanzisha mchakato wa kufanya marekebisho ya Sheria ya Maadili ya Uongozi ili tuingize utaratibu huo.

  Ndugu wananchi;
  Ni jambo lenye maslahi kwa nchi yetu na litasaidia sana kujenga heshima ya viongozi wa umma mbele ya macho ya wananchi. Nafurahi kwamba suala hili tumelizungumza katika kikao maalum cha Kamati Kuu ya CCM tulichofanya Dodoma juzi tarehe 29 Januari, 2008 na tumeelewana. Ni matumaini yangu kuwa sote tutaunga mkono.

  Mwisho, nawatakia kila la heri kwenye shughuli zenu. Tuendelee kushirikiana kuijenga na kuiendeleza nchi yetu.
  Asanteni sana kwa kunisikiliza.
   
 13. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #13
  Jan 31, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  asante sana "nikifufuka" na nimemaliza kuiweka kwenye pdf.. kwa wale wanaokusanya documents kama hizi.
   
 14. M

  Mbalamwezi JF-Expert Member

  #14
  Jan 31, 2008
  Joined: Sep 30, 2007
  Messages: 803
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Hapo sasa atakuwa ameweka mambo sawa. Siku zote nimekuwa nikisema hoja kuu ni maazimio ya Zanzibar na Arusha...sasa wanafanya biashara hakuna mwiko unaowakataza. Lakini maadam utaanzishwa utaratbu wa kuwabana, basi panaweza kuwa na mabadiliko. Tutaangalia kasi ya wafanyabiashara kukimbilia bungeni...

  Sina hakika kama wengi wataweza kuachia shughuli zao kwa kuwa biashara za bongo zinaendeshwa kimafia sana kukwepa kodi na sheria nyingine. wengi wanapenda kuwa mastering wenyewe kuficha mambo haya. Na ndiyo sababu kubwa hawapendi kupanua mitaji kupitia DSE kwa kuwa watawajibika kuwa wawazi zaidi kwa wenye hisa.
   
 15. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #15
  Jan 31, 2008
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Nimekusoma MMK.

  Unafahamu hali iliyoko Tanzania sasa hivi kiuchumi inafafania sana hali iliyokuwepo baada tu ya Tanganyika kupata uhuru kulekea mwaka 1967.

  viogozi baada ya kuutwaa uhuru, wengi wao wakaona sasa mambo sihaya? Wakaanza kujikusanyia mali wao binafsi na kuwasahau wananchi waluowaweka madarakani.

  Agano la kuupigania uhuru likuwa KILA MWANACHI NA KILA FAMILIA YA TANZANIA IWE HURU NA AWE HURU KIUCHUMI.

  KILA MWANANCHI AJITEGEMEE NA RUDIA AJITEGEMEE KIUCHUMI..HILO NDILO AGANO LA KUPIGANIA UHRU WETU!

  NI AGANO HEKIMA NA LA KINA!

  Lakini bada ya kuupta uhuru baadhi ya viongozi wakawahimiza kujitegemea kiuowongo uwongo..huku wao viongozi wakiwanyonya na KUWATEGEMEA WATU WALIOWAWEKA MADARAKANI..yaani Viogozi wakasaliti Agano la Kujitegemea KIUCHUMI kwa kila Mtanzania.

  Ikawa lazima kufanya marekebisho ili kujitegemea ili AGANO LA UHURU lilete maana. Marekebishao kimsingi yalikuwa kuwafanya VIOGOZI MAFISADI wasiweze kabisa kuwategemea WATU waliowaweka madarakani. Kwani watu au tuseme wananchi wanamtegemea nani kujenga uchumu wao? Mwananchi hana wa kumtegemea ila jasho lake binafsi. Hivyo basi hata viongozi wategemee jasho lao na si kuwategemea wananchi wao.

  Ndipo ikwawekwa "MIIKO MIKALI YA UONGOZI" Iili kufanikisha AGANO LA UHURU. Agano la kila mananchi ajitegemee kiuchumi!! Na sema Agano lilikuwakila mwananchi wa nchi hii ajitegemee kiuchumi..na sio kwa viogozi tu au tabaka la wachache. AGANO LA UHURU halikusema hivyo. Hata katiba ya nchi inayaweka haya bayana. Ikiwa na maana Kuwa kila mtanzania akijitegemeakiuchumi taifa Litakuwa Huru kiukweli. Litakuwa linajitegema na kuheshimika.

  Ni kweli sifikiri viongozi waliopo madarakani sasa wanalijua hili. Au wanlifumbia macho au wanalipuuzia ...itabidi tutafute wote.

  MIIKO HIYO YA UONGOZI ikaondolewa bila kuweka mingine pale zanzibar 1992. Hivyo ikiwa na maana kuvunjwa kwa AGANO LA UHURU.

  Sheria hiyo kama itapita ..ItaTUFANYA TUREJEE KWNYE AGANO LA UHURU! Kwani Agano la uhuru halikamiliki Bila MIIKO/MAADILI YA UONGOZI!

  Mafisadi tulionao wanaona mawazo haya kama Mkuki... Tusubiri tuone sheria ikifanya kazi!!
   
 16. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #16
  Jan 31, 2008
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Mbalamwezi;

  Nafikiri Kikwete na Viogozi wengine they are learnig faster kwa kinachotokea kwa majirani zetu!

  Kujicomit na kuruka hewani kuwa unafanya kitu kama hiki alafu akafanya mzaha, kweli huo sio mzaha wa kuwafanyia wanachi sikuhizi. Itabidi wawe serious vinginevyo nchi inakwenda kubaya. Nafikiri pia sheria itanweza kumcover Benjamin sina hakika..kwani inakuwaje kosa kama ulilifanya kabala sheria haijafanya kazi ..linahesabika? smting of tat nature.. Im not sure! But we hope wataepusha matatizo makubwa kama sheria ikawepo na kuwakweli effective!
   
 17. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #17
  Jan 31, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Kasheshe hivi Azimio la Arusha lilivunjwa na CC hii hii ama na nani ? Maana JK alikuwa ni waziri pia na naamini alishiriki kulivunja haya hakuyaona ?
   
 18. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #18
  Jan 31, 2008
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Kwenye pdf...Wapi?
   
 19. M

  Mbalamwezi JF-Expert Member

  #19
  Jan 31, 2008
  Joined: Sep 30, 2007
  Messages: 803
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Kufanya mzaha katika hili ni kujipunguzia kwa makusudi credit wakati wa tathmini ya uongozi mwaka wa tatu. Sidhani kama atapenda kuendelea kupunguziiwa units, hasa wakati huu ambapo zogo la madini alilolianzisha bado linamyumbisha
   
 20. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #20
  Jan 31, 2008
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 3,347
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Inachekesha sana, yaani mtu kama humjui JK atakuchezea sana, kila siku atakuwaacha mdomo wazi. Haya bwana endeleeni kutega mikono...mkisubiri matunda yadondoke!

  Kuna tofauti kubwa sana kati ya kutaka kufanya na kuwa na uwezo wa kufanya

  Vilevile kuna tofauti kubwa sana katika siasa kati ya kuwa ofisini na kuwa madarakani..akili ni nywele...
   
Loading...