JK na kibarua kigumu

Negotiator

JF-Expert Member
Aug 9, 2010
303
44
JK na kibarua kigumu


picture-12.jpg

Na M. M. Mwanakijiji - Imechapwa 24 November 2010

Kisima cha Mjadala


Miaka mitano iliyopita, tunaweza kuitafutia udhuru wowote ule kueleza kwa nini baadhi ya mambo hayakufanikiwa. Tunaweza kutafuta sababu ya kwanini baadhi ya mambo yalifanyika na mengine hayakufanyika kama ilivyotarajiwa.
Miaka mitano iliyopita, tunaweza kujaribu hata kumtetea Rais Jakaya Kikwete, kwamba kwanini sehemu ya ilani yake ya uchaguzi haikufanikiwa.
Miaka mitano iliyopita, ingeweza kuamua kabisa nafasi yake katika historia ya taifa letu. Hata hivyo, amepata fursa ya kututumikia kwa miaka mitano mingine.
Hii ndiyo itakayoamua kwa haki nafasi ya Rais Kikwete katika historia ya taifa; ikimalizika itatoa picha kamili ya urais wake.
Lakini kwa sasa picha iliyopo mbele ya wengi, si nzuri hata kidogo kwake.
Historia imeandika mambo matatu. Kwanza, kwa mara ya kwanza wananchi wachache sana walijotokrza kupigakura katika uchaguzi uliomuingiza Kikwete madarakani.
Pili, watu karibu milioni 4 waliomchagua Kikwete mwaka 2005 hawakujitokeza kumchagua tena mwaka huu.
Tatu, kwa mara ya kwanza matokeo ya urais yamesababisha mpasuko wa kisiasa nchini kutokana na hatua ya upinzani kutomtambua rais aliyetangazwa.
Hayo ni machache tu ya yale ambayo tunaweza kuyaangalia na kuyatafakari tunapozungumzia uchaguzi wa mwaka 2010.
Lakini haya yote hayataamua nafasi ya rais Kikwete katika historia, ni imani yangu kwamba yale yanayokuja ndiyo yatakayoamua.
Mtu yeyote anayefikiria historia ya rais Kikwete imeandikwa na imefikia mwisho anatenda kosa. Atahukumiwa na historia ya miaka mitano ijayo kuliko miaka mitano iliyopita.
Kwanza, rais anaweza kuondoka akilichia taifa mfumo mbovu wa uchaguzi. Kwa miaka nenda rudi tumekuwa na mazoea ya kukubali matokeo ya uchaguzi bila kuhoji au kulalamika sana.
Lakini mwaka huu, tumeona mambo mawili makubwa ya kushtua – maelfu ya vijana wamejitokeza “kulinda kura” na pili, matokeo ya uchaguzi wa rais yamegomewa.
Suala la tume ya uchaguzi kuendesha uchaguzi kwa mazoea, haliwezi kuipeleka nchi katika amani, iwapo litaendelea tena katika uchaguzi ujao.
Mfumo wa uchaguzi uliyopo sasa unaweza kuingiza nchi katika kubwa zaidi na kuhatarisha umoja na mshikamano wa taifa.
Kinyume na madai ya wengi, kwamba wanaohatarisha umoja, utulivu na amani ya taifa, siyo CHADEMA wala CCM, siyo Kikwete wala Dk. Slaa, bali ni mfumo huu wa uchaguzi ambao tunaendelea kuulea.
Mtu pekee ambaye naamini ana wito wa kihistoria kuusafisha mfumo huu, ni rais Kikwete. Ameuona kwa macho yake na sidhani angependa rais ajaye amrithishe.
Pili, Kikwete aweza kukiacha chama chake – CCM kikiwa hoi kiungozi. Miaka mitano iliyopita imefichua siri ambayo wengi hatukuijua – hombwe la uongozi ndani ya chama cha rais.
Kwa mara ya kwanza tumeona wabunge wa chama chake wakigawanyika, wakipingana na kutuhumiana hadharani. Tumeona ile “nidhamu ya chama” ikipeperuka kama kware aliyeshituliwa na mwindaji.
Kikwete hawezi kukiacha chama chake katika hali hii, kama kweli anataka kubaki salama na kustaafu kwa amani.
Je, CCM kitaenda kwenye uchaguzi wa mwaka 2015 ikiwa na mgawanyiko na mgongano kama ilivyokuwa miaka mitano iliyopita? Jibu analo Kikwete.
Tunaweza kutabiri kwa uhakika CCM inakoelekea baada ya Kikwete kutangaza baraza lake la mawaziri.
Tatu, Kikwete hawezi kuacha nchi ikiwa na uchumi goigoi. Kwa sasa, uchumi wetu ni tegemezi; hajafikia hata robo ya uwezo wake na hivyo umeshindwa kuinua maisha ya watu wetu wetu.
Nne, Kikwete ataweza kuliacha taifa mikononi mwa mafisadi kama ilivyo sasa, au atabadilika?
Kama tukichukulia jinsi serikali ilivyoshughulikia suala la ufisadi miaka mitano iliyopita kuwa ndivyo itakavyokuwa miaka mitano ijayo, tunaweza kuona kuwa vitendo vya ufisadi vitakuwa vimekoma na watuhumiwa watakuwa wameingia ikulu mwaka 2015.
Kama mwendo wa kushughulikia ufisadi utakuwa ndiyo huu huu basi kazi iliyoko mbele ni ngumu zaidi.
Mfano mzuri, ni jinsi Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) inavyoshughulikia suala kama rada.
Hivi kulikuwa na ulazima gani wa Takukuru kutoa barua ya kumsafisha Andrew Chenge na kuliambia taifa kwamba hata shirika la upelelezi wa makosa makubwa nchini Uingereza (SFO) wamemaliza uchunguzi, na bado mkuu wa Takukuru, Edward Hoseah akabaki ofisini?
Tano, Kikwete ataponya kwa kiasi gani maumivu ya kisiasa? Uchaguzi uliomalizika umeumiza watu wengi na kabla yake mgongano wa kiitikadi na maslahi uliotokea kwenye taifa.
Wapo ambao wako tayari kuishi na maamuzi yao na na wengine wanaogopa maamuzi yao kuwarudia. Maumivu yote yanahitaji kuponywa na bila shaka mwenye ubavu wa kuyasimamia ni rais mwenyewe.
Tayari baadhi ya maumivu rais ameyadokeza na wananchi wanasubiri kuona anayatibu vipi.
Sita, rais anamaliza ngwe yake ya mwisho akiwa na jukumu kubwa la kuangalia makazi ya wananchi wake. Kama kuna kipimo cha mafanikio ya kiuchumi, basi ni wapi watu wanaishi.
Kinyume na wale wanaoamini kuwa tatizo kubwa la maisha ya wananchi ni “umaskini wa kipato” binafsi naamini kuwa tatizo liko kwenye makazi.
Kama kuna ujumbe wowote ambao rais Kikwete anauweza kuubeba kutoka kwa Dk. Slaa, basi ni ajenda yake ya kutaka kusimamia makazi ya wananchi.
Ni lazima tupate sababu ya kutuelezea kwanini bado tuna nyumba za “tembe,” udongo na nyasi. Wengine wamekubali “maisha ya kijijini,” lakini rais analo jukumu kubwa la kusimamia makazi yao.
Saba, rais ameingia katika miaka mitano ya lala salama huku taifa likiwa linaelekea kuwa na mbumbu wengi kutokana na idadi ya wanaojua kusoma na kuandika kushuka mwaka hadi mwaka.
Je, Kikwete atakubali kuliacha taifa likiwa na tatizo la walimu na ubora wa elimu? Naamini hatuwezi kuwa na taifa la kisasa bila ya kuwa na watu walioelimika. Wanaoweza kusoma na kuandika na wenye uwezo wa kujiajiri.
Tunaweza kuwa na vyuo vingi lakini tukiwa na vyuo vingi visivyo bora tunaweza kusema taifa limeendelea? Kimsingi changamoto ni nyingi mno.
Lakini lililokubwa ni kwamba Kikwete ataandikwa vipi na historia.
Rais ameingia katika wingu la shuku, lawama na maumivu, lakini ni yeye pekee anayeweza kuamua anapotoka madarakani miaka mitano ijayo, anataka kutoka katika mwanga gani.
Ni matumaini yangu “hekima” itamfanya aamue nini cha kufanya na kipi cha kutofanya. Akifanya maamuzi kwa ajili ya leo, inaweza kumsadia kwa kesho. Tusubiri tuone. Miaka mitano si mingi, ingawa si haba.
Gazeti toleo na. 216
 
I'm not sure if he never get serous or care that much ,for us to have a notion that he care.

Wako wasemao pengo la ukubwani halioti ,ila always huwa kuna miujiza so lets wish for one cuz if he do some good so do the country be in good shade .
 
Back
Top Bottom