JK na Haki za Binadamu

Mlalahoi

JF-Expert Member
Aug 31, 2006
2,182
883
JK: Watakaothibitika kuua albino kunyongwa

na Esther Mbussi


RAIS Jakaya Kikwete amesema wale wote watakaobainika na hatia ya mauaji ya maalbino nchini watakabiliwa na adhabu ya kifo.

Akizungumza baada ya kupokea maandamano ya kulaani mauaji yanayoendelea dhidi ya jamii ya maalbino, jana katika viwanja vya Karimjee, Rais Kikwete alisema serikali inafuatilia kwa karibu suala hili hasa waganga wa kienyeji wanaotajwa kuwa ndio chanzo cha mauaji hayo.

Alisema hadi sasa watu 47 wanaotuhumiwa kujihusisha na mauaji hayo kutoka mikoa mbalimbali wameshakamatwa na sita kati yao wanatoka Mkoa wa Mara.

Rais Kikwete alisema wengine wawili wanatoka mkoa wa Kagera, Shinyanga mmoja, Mbeya wawili na wengine wanatoka mikoa tofauti.

Alisema serikali inafanya mkakati endelevu wa kupambana na mauaji hayo ingawa kuna ugumu wa kuwapata kutokana na kufanyika kwa usiri mkubwa. Hii yote hutokana na watu kuendekeza imani potofu kwamba albino ni balaa.

“Serikali haitavumilia kuona raia wake wakiuawa kwa imani potofu kama hizo na atakayekamatwa adhabu yake ni kifo pamoja na wanaharakati kupigia kelele kwamba adhabu hiyo ifutwe. Hakuna mabadiliko yoyote adhabu hiyo bado haijabadilika na itatumika dhidi yao hadi hapo itakapofanyiwa marekebisho.

“Mkakati tulioweka ni kuwatambua maalbino wote nchini kwa idadi yao tunawaomba wananchi wasiliachie Jeshi la Polisi pekee, kwani hili ni janga la taifa pamoja na kutoa elimu kwa jamii iondokane na imani potofu na kuwaona albino kuwa sawa na wanajamii wengine,” alisema.

Aidha, Rais Kikwete alimtaka Meya wa Manispaa ya Ilala, kuwapa malbino nafasi ya upendeleo ya kufanyia biashara katika jengo la wafanyabiashara ndogo ndogo ‘Machinga Complex’, ili kujikimu kimaisha.

Awali, akisoma risala kwa niaba ya Chama Cha Maalbino Tanzania, Josephat Torner alisema athari za mauaji hayo ni nyingi zinazosababisha kuporomoka kwa taswira ndani na nje ya nchi kwamba Tanzania ni kisiwa cha amani.

Alisema hali hiyo pia imeleta hofu na mashaka miongoni mwa familia za maalbino ambapo sehemu fulani ya watoto albino wameacha kuhudhuria masomo shuleni kwa kuogopa kuvamiwa na wengine wanalala wakilindwa kama madini ya Tanzanite.

“Siku hizi dharau na kejeli dhidi ya jamii ya maalbino zimevuka mipaka, hata majina ya kawaida ya maalbino siku hizi yamekufa, kila tunapopita tunaitwa ‘dili’, hatujui maana halisi ya neno hili ni ipi kwa wakati huu,” alisema.

Torner alisema siku hizi maalbino wanaogopa kuoa na kuolewa kutokana na tukio lililotokea wilayani Bukombe la msichana Regina aliyekutwa amekufa huku akiwa amenyofolewa baadhi ya viungo siku nne baada ya kuolewa.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, alisema chama chake kinalaani na kupinga mauaji ya albino na kuongeza kuwa ni aibu kwa Watanzania kuendekeza imani za kishirikina katika karne ya 21 ya sayansi na teknolojia.

Alisema hajaridhika na juhudi za serikali, kwani imeshindwa kuyadhibiti mauaji hayo tangu mwanzo hadi yanafikia katika hatua mbaya ambapo maalbino wanauawa kila kukicha.

“Serikali iunde tume ya kufanya uchunguzi kama ambavyo imekuwa ikifanya katika mambo mengine. Kama Vicky Ntetema Mtangazaji wa BBC ameweza kuwahoji waganga wa kienyeji, serikali inashindwa nini, kuwakamata huku imekiri kuwepo kwa mtandao mkubwa katika mauaji haya?” Alihoji.

Aidha, aliitaka jamii, vyama vya siasa na jumuiya za kimataifa kuwawezesha maalbino kufanya kazi kivulini hali itakayowafanya wasikutane na jua ambalo mionzi yake inaharibu ngozi yao na kusababisha kansa.

Sambamba na hayo, alitoa rai kuanzishwa vipindi maalum kwenye vyombo vya habari ili kutoa elimu kwa jamii kuhusu maalbino, kwani vina nafasi kubwa ya kuelimisha.

Huyu JK vipi?Katika hotuba yake Bungeni alidai kwamba moja ya vikwazo vya kuwashughulikia mafisadi wa EPA ni HAKI ZA BINADAMU.Spika akam-criticize kwamba haki za wananchi ni muhimu zaidi kuliko haki za mafisadi.Ok,let's assume JK was right kuhusu haki za binadamu za mafisadi.Iweje leo awe mwepesi kupuuza haki za binadamu za wanaoua albino?

By the way,hii ni cheap political stunt.Kwa mujibu wa sheria,adhabu ya kosa la mauaji ni kifo.Lakini ni muhimu kukumbuka kwamba INATEGEMEA NANI ALIYEUA.Kama ni raia wa daraja la kwanza,eg Kaka Ditto,Kinje,etc then si ajabu aliyeauawa ndio akageuziwa kibao japo hayuko hai.Kama ni raia wa daraja la chini,malalahoi wa kawaida basi hata kama umeaua kuku unaweza kuishia kunyongwa.

Hapa hatuna rais,ni mazingaombwe tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom