MVUMBUZI
JF-Expert Member
- Jan 8, 2011
- 5,182
- 2,304
Akihojiwa na Ali Mutasa wa BBC huko Afrika ya Kusini leo asubuhi, JK amejaribu kueleza kile kinachomfanya asikae kitako nchini kwake kama marais wengine na badala yake kuwa kiguu na njia akipiga hodi nchi za wengine kila kukicha.
Jk amesema anajaribu kutafuta wawekezaji na akajaribu kutoa takwimu zisizoshawishi za wawekezaji wa Afrika kusini(Makaburu) waliowekeza nchini.
Amesema kwa sasa kuna wawekezaji makaburu wapatao 178 nchini na wamewekeza jumla ya Shilingi za kitanzania bilion 600 na kufanikiwa kutoa ajira kwa waTZ 18,000(elfu kumi na nane).
Hawa watu ni asilimia 0.0759% ya work force ya TZ yenye watu million 23.6 na contribution ya mapato yao kwa pato la taifa ni negligible.
Pia namshangaa JK kujidai kutafuta wawekezaji wakati mojawapo ya matatizo makubwa ya uchumi wa nchi hii siyo uwekezaji bali ni serikali kutotoza kodi icluding misamaha mingi ya kodi, na matumizi mabovu na yaliyokidhiri ya fedha za umma. Na hili IMF wanalijua.
Kwa mfano, mwaka 2010 pato la taifa yaani GDP ilikuwa kiasi cha dola bilion 62.22(USD 62.22 Billion).
Wakati huohuo kiwango cha kodi zilizokuwa zinakusanywa zilikuwa chini ya asilimia 15 ya pato la taifa , matumizi ya serikali yakiwa zaidi ya asilimia 25 ya pato la taifa, sehemu kubwa ikiwa ni kulipa mishahara( na mishahara hewa ikiwamo)
Wote tunajua kodi kubwa zinazosamehewa ni za wawekezaji kwa mtindo wa "tax holiday". Kama ni hivyo, ni kwa vipi hawa jamaa ambao hawalipi kodi kwa kiasi kikubwa wanakumbatiwa na JK na kutaka waTZ waamini eti safari zake za nje ni kwa ajili ya kuwatafuta hawa wawekezaji. Hivi tangu lini JK akawa na juhudi na uchungu mkubwa kiasi hicho kwa waTZ na kumfanya asipate usingizi bali lale home ili kuwangaikia waTZ. Mi naona hizi ni geresha na watakao amini hayo ni wale wanaolamba viatu vyake ila kwa sisi watu wazima hatutadanganyika kwa hizi fikra za kifukara za JK juu ya uwekezaji..
Kama yuko serious naomba atueleze jumla ya safari alizofanya na idadi ya wawekezaji aliopata tangu aingie madarakani na figures ya trend ya mchango wa wawekezaji hao ktk uchumi wa taifa.
Maswali haya yanaulizwa kwa sababu hatuoni kama kile serikali inachokisema kuhusu kukua kwa uchumi kina shabihiana na hali halisi ya maisha ya mtanzania wa kawaida kwani hali ya maisha ya mtanzania inaendelea kuwa ngumu kila uchao. Mkuu tutakuelewa kama unayosema taswira yake tutaiona ktk maisha ya mtanzania wa kawaida sio tu kwa kipimo cha kupungua kwa waTZ walioko chini ya msatari wa umaskini bali kuongezeka kwa idadi ya waTZ walio wengi wa kuweza kufanya manunuzi ya mahitaji muhimu.