Mkandara mawazo yako ni mazuri sana, Ukweli umeshajionyesha wazi Kikwete si kiongozi muadilifu hana tofauti na mtawala wa mabavu; hivi sasa watanzania swali la kujiuliza kiongozi huyu yupo kwa kuleta mabadiliko? watanzania wajiandae kufunga mikanda hali ya kiuchumi itaendelea kudidimia siku hadi siku; Kikwete hana jibu la matatizo ya uchumi wa Tanzania kama umefuatilia kwa makini majibu yake kila anachoulizwa jibu ni mainfesto ya chama jee wanaccm wenzangu hii manifesto ya chama mnaijua? Hivi sasa watanzania wanachopaswa bila kujali itikadi zao kuishinikiza serikali kuleta ufanisi, tumekaa kimya sana tukitegemea mungu atuletee ukombozi. Rev. Kishoka ameongelea kuongeza mapato na kubana matumizi, mapato yapo Tanzania, tatizo ni ufisadi wa maksudi unaofanywa na viongozi wetu hilo la kubana matumizi ni ndoto Kikwete is an emperor who turned our country to his personal enterprise. He will do whatever necessary to please his inner circle . Haijawahi kutokea kongozi mwenye ahadi zisizo na ukweli katika historia ya Tanzania kama Kikwete, hii ni balaa kubwa sana, ninachomshauri kama anataka mabadiliko ya kweli baraza lake la mawaziri aweke hata kutoka vyama vya upinzani ili kuleta ufanisi kwa Taifa letu.