Jk na awamu ya pili...

Mkandara mawazo yako ni mazuri sana, Ukweli umeshajionyesha wazi Kikwete si kiongozi muadilifu hana tofauti na mtawala wa mabavu; hivi sasa watanzania swali la kujiuliza kiongozi huyu yupo kwa kuleta mabadiliko? watanzania wajiandae kufunga mikanda hali ya kiuchumi itaendelea kudidimia siku hadi siku; Kikwete hana jibu la matatizo ya uchumi wa Tanzania kama umefuatilia kwa makini majibu yake kila anachoulizwa jibu ni mainfesto ya chama jee wanaccm wenzangu hii manifesto ya chama mnaijua? Hivi sasa watanzania wanachopaswa bila kujali itikadi zao kuishinikiza serikali kuleta ufanisi, tumekaa kimya sana tukitegemea mungu atuletee ukombozi. Rev. Kishoka ameongelea kuongeza mapato na kubana matumizi, mapato yapo Tanzania, tatizo ni ufisadi wa maksudi unaofanywa na viongozi wetu hilo la kubana matumizi ni ndoto Kikwete is an emperor who turned our country to his personal enterprise. He will do whatever necessary to please his inner circle . Haijawahi kutokea kongozi mwenye ahadi zisizo na ukweli katika historia ya Tanzania kama Kikwete, hii ni balaa kubwa sana, ninachomshauri kama anataka mabadiliko ya kweli baraza lake la mawaziri aweke hata kutoka vyama vya upinzani ili kuleta ufanisi kwa Taifa letu.
 
Kwanza kabisa ondoa maneno "visasi" au "Uchadema na UCCM" i am not of that type. I am trying to just be "serious". Wewe unataka tukubali kuwa CCM has done it illigetimate then we should not bother these issues let us join them. Ninachosema CCM did it wrong; then; kwa sababu ile misingi iliyokuwepo ishabomolewa; leo ili uwe kiongozi CCM cha kwanza sifa kubwa lazima uwe corrupt; mwongo nk nk No ethics at all. CCM inajenga society gani?? Swahiba wewe na mimi tumesoma siku zilee! Education was free and it was meant for all, literacy was above 90%. Leo hii Literacy sijui ni below 60% hivi huoni kuwa Taifa lipo hatarini? Kigumu kipi kufanya shule zetu zisomeshe watu?

Swahiba ulishaenda kijijini juzijuzi; au ndiyo umejichimbia huko mida yote? Sasa wewe ukitaka kujua CCM na madhambi yake nenda kijijini; ndiyo utajua dunia ya Afrika ni dhihaka. Not only no health care nor Education; kwanza watu wanaishi kama wanyama, huko kuna mbunge na mkuu wa wilaya. Mkuu wa wilaya akitembelea huko vijijini anapewa gunia la mahindi mbuzi hata kuku. Tanzania ilibidi iwe inapanda juu siyo kushuka chini.

Nikirudi kwenye topic hapo juu ni kuwa Tanzania iliyopo sasa hivi haitabidilika mikonni mwa CCM, kama itabadilika basi ni kwenda chini meaning kuwa it will be worse. It will take at least two years to recoup all resources utilised by Mr. Kikwete during election; that is massive amount of cash money. Sijui wali-print wapi zile pesa. Hiyo inflation itakuwa kubwa sana. In this case system ya CCM ishakuwa hivyo haiwezi kubadilika. Sasa hivi lazima tujenge vyama vyenye nguvu at least hata kama haviwezi kutawala lakini uwezo wa ku-influence decision uwepo. Slaa factor was very very strong na iliwatia kiwewe watawala. That is what we want.

Kushirikiana na CCM ni kucheza muziki wao; ndiyo maana nimesema kuwa; raslimali ya CCM ni matajiri na mafisadi hawawezi kukusikiliza wewe; lakini wanasahahu kuwa vijana ndiyo ingekuwa raslimali kubwa zaidi; na hii ndiyo Chadema inabidi wai-exploit. Sasa hivi CCM si chama cha Wafanyakazi na Wakulima tena.

Halafu ule msemo kuwa CCM ipo vijijini imeimarika, thubutu; wananchi wa vijijini wameangushwa tu na wasimamizi wa uchaguzi, lakini majority wamechagua opposition. That was Slaa factor. Watu bwana wanapenda maadili siyo propoganda. Huku unaiba kule unasema ni chama cha wanachi.

Soma hiii article ambayo imeandikwa na East African ukishamaliza niambie:
The East African: - News |How CCM won an election but felt the earth move under its feet
Nakusikia sana, hivyo ikiwa CCM wameyafanya hayo yoote mabaya na kweli tukikubali kushirikiana nao n sawa na kupeana mkono na shetani. Basi, ktk imani hizi za Ushetani huwapo wakati hata Shetani akayafanya yenye kheri japokuwa kwa njia haramu..Nachokiomba mimi ni kheri tupu pamoja na kwamba naelewa fika itakuwa sii rahisi lakini ndio kusema tukubali kwa mabaya yoote yanayotukabiri...
 
Ndugu yangu Mkandara, fahamu kwamba huyu RAisi wetu aliingia madarakani akijua kuongoza nnchi ni suala la kifari na kujijengea mazingira ya kuwa na jina duniani hivyonbkuingia kwenye historia na kupata umaarufu.

Hivyo alikuwa na nia na dhamira tofauti kabisa na Uraisi, kwan umesahau baraza lake la kwanza la mawazir? Baadae akalivunja.. Hajui cha kufanya uoeo ni mdogo sana. RAisi gani hajui kwa nini nchi ni maskini? Kana kwamba haitoshi hata suala la foleni kwake ni maisha bora..

UShauri wako kwake ni sawa na kumwaga sukari baharini, kama huamini ngija uone baraza lake la mawaziri. Na usishangae jina la spika mpya, na wale wote mawaziri waliopigwa chini tokea kura za maoni kupewa madara.. How? Ukistaajabu ya MUsa utayaona ya firauni.

Sakijoli;

Nimeona nilisemee hili pia!

Baada ya Mika 2 yaani ilipofika 2007 .. Ilibidi nikubaliane na nilichokuwa nakiona kwa Mheshimiwa Rais wangu.

Pale madarakani... alifika kujiwekea rekodi YAKE ... alikuwa anatizama kalenda miaka 10 itakwisha lini ..niwe kwenye watu maarufu ...Rais wa Jamhuri ya muungano... Kudhibisha hili...kama una vedeo ya kutangazwa kwa mshindi wa mwaka huu ..utaona ...alivyotajwa tu ..alichokifanya ...kaangalie..utaona alikuwa anaongeja hiyo kauli tu...kwani rekodi tayari...

Rais hayuko pale kwa ajili ya hata mtanzania mmoja...
Rais hayuko pale hata kwa ajili ya familia yake...
Yuko pale kuukamilisha umaarufu kwa ajili ya nafsi yake..

Atakuwa mwaangalifu sana, asitoe mashihisho kwa wanaokosea...au pale dosari inapotokea...why? asije jiaharibia urais wake ...Naam anajua kuulea na kuutunza...hataki hata kugombana na yeyote..na hivyo ni kucheka muda wote ...ili mradi ..asije akaharibu ... Lulu yake!
Atafanya chochote kile..amalizie awamu ya pili....asije kuwa wa kwanza kuongoza kwa awamu moja...

Yuko pale kuutukuza na kujenga umaarufu wake duniani kote... kwa gharama yeyote..kwa ajili yake yeye binafsi...na hili si jambo la kujivunia hata kidogo!!!
 
mkuu mkandara tatizo kubwa la jk na viongozi wa africa kiujumla ni "they don't listen". ushauri uliotoa ni mzuri sana lakini hata ukifikishwa kunakohusika, they can simply say hiyo haipo kwenye ilani yetu. Lakini enwayz hii isituzuie kuwapa ushauri whenever possible. Mimi msisitizo wangu zaidi kwenye elimu, yaani hapo tunahitaji ikiwezekana hata kutangaza hali ya hatari. The situation is really pathetic.

Tunahitaji kucombine quantity and quality, pia kuwe na incetives kwa walimu mfano bili za maji na umeme walipe nusu. Kuwe say na housing schemes kwa walimu, maabara bora na library za kisasa (audio books zianze pia kutumika).
and also they dont care
 
Maadam uchaguzi umekwisha na rais wetu Mh. Jakaya Mrisho Kikwete ameshakabidhiwa mamlaka ya kuiongoza nchi yetu nadhani huu ni wakati muafaka wa kuzungumzia kero za wananchi -Mnataka JK afanye nini? au. Kifanyike kipi na serikali iliyoingia madarakani ili kuijenga nchi yetu toka hapa tulipo kwani kuendelea kulalalamika haiwezi kusaidia kitu bali kuongezea machungu. Na kwa Unafiki wetu hatuwezi hata kushirikiana na kukubaliana kwa jambo lolote muhimu linalohusu mustakabali wa nchi yetu.. Hivyo ni bora zaidi tugange yajayo maanake imeshakuwa uchawi mtupu.

Inawezekana Mkandara unaakili nyingi sana kupita wananchi wengi wa Tanzania. Uchaguzi gani huo unaoongelea? Wizi wa kura ndiyo unasema uchaguzi. Napata kichefuchefu na threads ''zinazowatongoza'' watanzania wakubali wizi wa kura. Unategemea wezi wa kura walete mabadiliko gani Mkandara?, Sikuelwei kabisa kabisa. Kama ni mabadiliko si angeacha wananchi walete mabadilko ya uongozi kwa kura. Unadai mabadiliko kwa watu wanaopinga mabadiliko kwa wizi wa kura, unashangaza kweli. Kwa taarifa yako kuiba kura za wananchi ni kukataa kuwajibika kwao na huo ni Udikiteta. Ni ajabu kuwa wewe unategemea mabadiliko yaletwe na Madikteta. Mabadiliko yataletwa na wananchi na mchakato wa kuyaleta ndiyo kwanza umeanza. Huyo JK ni rais wa NEC na CCM siyo wananchi.
 
MTWA MKWAWA mfalme wa wahehe baada ya kuona amezidiwa nguvu alikoka moto ,akachukua bunduki, akaupa mgongo moto kisha akajipiga risasi na mwili wake ukadondoea kwenye moto,HII yote ni kwamba alikuwa na lengo kwamba hata akiwa mfu kamwe hakutaka mjerumani aguse walau maiti yake.MIMI KWA KUFUATA ITIKADI YA MTWA WANGU PIA SIKO TIYARI KUSHIRIKIANA NA SELIKAKI HII YA WEZI WALA KUMSHAULI MTU YOYOTE ASHIRIKIANE NA MAFISADI HAWA. KUMBUKA KWA MIAKA 49 SASA HAKUNA MWENYE UCHUNGU KATI YAO NA UMASKINI WETU.NDUGU USIKUBALI KUSHIKANA MKONO NA SHETANI
 
Mkuu Mkandara, kwa kweli umeongea mambo muhimu sana ambayo ni START ya kulisaidia Taifa.

Jk sasa ni wakati wa kufanya kazi, na kila mtu anayechaguliwa kama waziri au nafasi yoyote lazima achaguliwe kwa sababu moja tu nayo ni UTENDAJI KAZI KWA MASLAHI YA WANANCHI.

Kila mtu anayechaguliwa lazima awekewe benchmark ya utendaji ie Waziri wa Fedha, lazima kodi zinazokusanywa ziongezeke kwa kiasi x%, na exmeptions zipunguzwe kwa y%.

Ukiwa waziri wa miundombinu lazima barabara zijengwe kwa kiwango cha mkataba, na kila kitu kiwe transparent. TANROADS ufisadi UISHE ASAP, na tuone barabara zinajengwa.

Kuanzia leo, VALUE FOR MONEY kwenye kila matumizi ya serikali iwe wazi na kila waziri au mtendaji awe responsible.

JK akiweza tu kupush watendaji na kuacha mambo ya mzaa, nadhani malengo yetu ya maendeleo yataanza kuonekana mara moja, maana serikali iliyopita tunaweza kusema karibu 50% ya budget ilikuwa mambo ya kijingajinga kama posho, semina, safari za nje na ndani nk

Tunataka sasa Development budget iwe inakuwa say 20% kila mwaka kuanzia 2011.
 
..Kusema mali ya wizi imeshapatikana, tusahau wizi uliofanyika bali tupange namna ya kutumia mali hiyo ni kijinyima authority ya kuzuia wizi. Vorster wa Afrika ya kusini aliwahi kusema watu weusi ni wasahaulifu sana wakipata chochote kidogo. Kama tuliona tumetukanwa wakati huo, ni kwa nini leo tunataka kujitukana wenyewe leo? Wenzetu wanamaliza mmbo magumu ya aina hii mahakamani, siyo kinyeji. Kushindwa kuonyesha utii kwa sheria kubwa sana ya uchaguzi ni dalili ya wazi kuwa hatutaweza kutii sheria ndogo ndogo nyingi sana za kutoonea wanyoge. Kikwete ana watu wengi sana wa kufadhili kwa kumsaidia wizi wa uchaguzi ambao hatawafanya lolote kipindi kijacho hata wakivunja sheria gani.

Kichuguu:

Nakusikia mkuu. Lakini kuna kitu kimoj ni lazima tujiulize? Je kasoro zilizopo sasa ni za ki-system au ni za mtu mmoja? Kama ni za ki-system basi hata Dr. Slaa, Prof. Lipumba, Sikonge, Rev. Kishoka wakipata nafasi aliyonayo JK wanaweza kurudia yale anayofanya JK na kundi lake. Lakini kama matatizo haya ni ya mtu mmoja au kundi la watu basi tusimame kuwaondoa hao watu.

Huyo Voster aliweka system ambayo ilimfanya mwafrika alidhike na vitu vidogo na baadaye akafanya generalization. Na kilichofanyika ni kuondoa system hile.

Watanzania tunakubali yanayotokea sasa kwa sababu katiba ya sasa imetuweka katika mazingira haya. Nchi haina check and balance. Na Dr. Slaa akifanya rais na akafanya vizuri atafanya hivyo kwa matakwa yake, but that's a deadly proposition.
 
Maadam uchaguzi umekwisha na rais wetu Mh. Jakaya Mrisho Kikwete ameshakabidhiwa mamlaka ya kuiongoza nchi yetu nadhani huu ni wakati muafaka wa kuzungumzia kero za wananchi -Mnataka JK afanye nini? au. Kifanyike kipi na serikali iliyoingia madarakani ili kuijenga nchi yetu toka hapa tulipo kwani kuendelea kulalalamika haiwezi kusaidia kitu bali kuongezea machungu. Na kwa Unafiki wetu hatuwezi hata kushirikiana na kukubaliana kwa jambo lolote muhimu linalohusu mustakabali wa nchi yetu.. Hivyo ni bora zaidi tugange yajayo maanake imeshakuwa uchawi mtupu.

1. Baraza la Mawaziri.
JK anatakiwa kupunguza baraza hilo na kuwa na wizara chache iwezekanavyo na kama yawezekana arudishe upya wizara tulokuwa nazo enzi ya Mwinyi na mamlaka ya kimaendeleo yashikwe zaidi na Hamalshauri husika.

2. Kuondoa viti vya Wakuu wa mikoa na Wilaya ambao kusema kweli kwa muda mrefu wamekuwa mzigo kwa serikali kwa sababu hawa watu hawana makazi zaidi ya kuzunguka nchi nzima. Hivyo hushindwa kuendeleza sehemu moja wakijua kesho watahamishwa tena kwenda sehemu nyingine wakati makazi yao haswa ni mikoa wasiyoiongoza. Ujamaa ilikwisha zikwa na wakuu hawa sehemu hizi sii kwao, why should they care? - Kama wakuu wa mikoa na wilaya wataendelea kuwepo basi iwe ni wakazi wa sehemu hizo na cheo hiki wakishike kwa jumla ya miaka minne ya uchaguzi kumwakilisha rais aliyepo madarakani.

3.Uchumi.
Ili kukuza uchumi wetu ni muhimu kwa Kikwete kufahamukwamba tanzania ni nchi maskini na haiwezi kuondoka ktk umaskini kwa kuomba. Hata siku moja nchi ombaomba haiwezi kuondokana na kilema hicho maadam hiyo mikopo ndiyo imekuwa source of income kwa Taifa. Hivyo ni muhimu sana kwa uojgozi wake kutumia vema mikopo na misaada inayopatikana hasa ktk sekta za Miundombinu ambayo haihitaji usanii wa kuwapa wazalendo uwezo mkubwa ktk ujenzi wa vitu hivi. Ufisadi mkubwa umefanyika na fedha nyingi tumepoteza wakati miundombinu yetu imebakia kuwa hafifu na isiweza kukimu mahitaji yetu.

Nguvu kubwa iongezwe ktk Kilimo kwa mfano n vizuri sana kwa rais wetu kufanya ziara nchi za Pakistan au India ili kupata mbegu asili za mpunga aina ya Pishori (Bismati) na nchi kama Thailand ili kupata mbegu za aina ya Jasmine (mchele wa Mbeya). Jitihada kubwa iongezwe ktk kupata soko la kilimo cha Kahawa kwa kushirikiana na mashirika makubwa duniani ambayo ndiyo wanunuzi na wasambazaji wa kahawa dunia nzima. Kilimo cha asili kama mahindi, mihogo, ndizi, na matunda pia kipewe kipaumbele zaidi kwa kutafuta masoko hata nchi za jirani (Freetrade) kwani Unguja ni moja ya nchi zinazosifika duniani kwa uzalishaji wa matunda lakini sifa hizo zimeishia visiwani hazina soko hata Tanzania Bara na hakuna sababu zaidi ya ukiritimba wa sheria na taratibu kinzani ya utandawazi. Na mwisho, rasilimali watu na maliasili zetu ni lazima zitumike kwa manufaa ya nchi yetu kwani ni aibu kubwa sana kuona Mkenya au Mganda akija nchini na kuchukua ajira za wananchi kwa sababu tu ya lugha ya kigeni.

Sheria ya madini lazima ianze kazi yake kama alivyoahidi, wawekezaji wote ni lazima walipe kodi kwani ndivyo alivyowaahidi wananchi ifikapo mwaka 2010 mashirika yote ya madini yatatakiwa kulipa corporate tax. Na hakuna tena mashirika kuuzwa baada ya miaka mitano ya msamaha, wakishindwa kulipa yachukuliwe (Taifishwa) na accounts zao kuwa freezed.

4. Elimu na Afya
Ni wakati mzuri kwa rais kutazama upya wizara hizi hasa ktk maswala ya wahudumu wake. Walimu na Madaktari wapewe mishahara mizuri zaidi ili kuwawezesha kuishi pasipo kutegemea kazi ya pili..Marufuku kwa mwalimu au Daktari kufanya kazi au kufungua shughuli yoyote inayohusiana na ajira alopewa na serikali. Maadam chama kinaamini kwamba elimu na Afya bure HAIWERZEKANI basi ni bora kupitia upya gharama hizo kwa wanafunzi wa shule za sekondari kufikia kidato cha sita.

Kutokana na upungufu wa walimu ningependekeza sana kila mwalimu mmoja awezeshwe kufundisha zaidi na masomo manne au matano tofauti, hivyo kila shule hailihitaji walimu wengi na tofauti kufundhisha masomo tofauti. Hapa Canada ndivyo wenzetu wanavyofanya utakuta shule ina waalimu wachache lakini wana uwezo mubwa wa kufundisha masomo tofauti..Bila shaka kama walimu watakuwa Graduates wanaolipwa mishahara mizuri,mbinu hii inawezekana kabisa kutumiwa kuliko kuendelea kutumia walimu wa UPE kuzailisha zaidi (quantity) wakati tunaua elimu yenyewe.

5. UFISADI...
Hili ni kubwa kuliko uwezo wa Kikwete mwenyewe lakini bado anaweza kupunguza Ufisadi kwani nina imani kubwa kwamba itahitaji utawala mpya na tofauti kabisa kuweza kuua Ufisadi nchini kwani ndio wanaotawala nguzo zote za kiuchimi na sheria. Hata hivyo, ahadi yake ya kuondoa kofia mbili kwa viongozi wa serikali ni lazima aitekeleze kwani nina mashaka sana kama baraza hili la mawaziri halitakuwa na wafanya biashara. Sidhani kama sheria hii itatumika ktk uchaguzi wa baraza hili la mawaziri maadam Azimio la Zanzibar bado linatumika, hivyo, sidhani kama itatokea kinyume....

Lakini pia zipo sehemu nyeti sana ambazo anatakiwa kuzitazama upya. Uongozi ktk mashirika kama Bandari, TRA pamoja na mashirika mengine ambayo bado yameshikiriwa na serikali kuu, Sheria za Imports taxation, Utaratibu wa kulipisha kodi baada ya mauzo na sii kukadiria, kuboresha njia za mikopo ktk Uwekezaji wa viwanda na biashara ndogo ndogo, kuthibiti matumizi ya Dollar dhidi ya Tsh. Vibali na liseni za biashara, ufanisi ktk ukusanyaji wa ushuru kulazimu kila Mtanzania kuwa na namba ya kulipia Tax hata kama hana kipato. Mbali na kuthibiti tax, hii itasaidia zaidi ktk utoaji wa vitambulisho vya uraia na hata kurahisisha kupata idadi ya wakazi nchini (sensor).

KATIBA... huko wala siwezi kusema zaidi...

Kwa leo wakuu zangu natanguliza hayo machache nadhani wengine mnaweza changia zaidi au hata kunisahihisha pale nilipokosea ama kutokubaliana..Tupo hapa kujifunza.

Mkandara:

Nakumbuka tukiwa Bsctimes forum kipindi cha Mkapa, mjadala mkubwa ulikuwa ni nani atakaye mrithi Mkapa. Nakumbuka Augustino Moshi alikuwa kipenzi wa Mkapa, lakini kwa sasa sijuhi kama anaweza kurudi sifa alizompa.

Nikiwa natumia user name Pillar, nilikuwa napinga sana mfumo wa kisiasa na hasa katiba. Lakini wengi wenu mlikuwa mnaangalia sana mabadiliko ya kiuchumi.

Kwa maoni yangu binafsi katiba ni kitu muhimu. WaMarekani siku zote watatamba kuhusu uchumi, nguvu za kijeshi na teknolojia lakini deep down Marekani imejengwa kwa misingi ya documents mbili: Declaration of Indepence and Constitution.
 
Zakumi,
Eeeeh mkuu wangu Pillar nakusikia sana, Labda nikukumbushe tu kwamba miaka yote hapa toka Bsctimes mimi nilikuwa napenda mageuzi ya kiongozi wa juu kwanza ili kuondoa mfumo mzima wa CCM ambao bado unakumbatia falsafa za KUTAWALA... Kama unakumbuka vizuri nilipendekeza sana Dr.Salim kugombea wakati ule lakini ndo alibwagwa mapema na JK ambaye kaja kuyaendeleza ya Mkapa. Yaliyomtokea huko (dr. Salim) yalipata baraka za Watanzania na haikuwa issue kubwa hata kama sababu kubwa ni kuwa yeye ni mwarabu na kizazi cha Hizbu..hakuna aliyempa support hata kama Katiba hairuhusu racism na Udini, hii ndio Tanzania tunayovuna leo.

Sasa unapozungumzia declaration mkuu wangu lazima ukumbuke pia Azimio la Zanzibar ndilo lilozaa mfaragano woote huu zaidi ya Katiba yenyewe. Ufisadi kama adui yetu wa kwanza ndiye alozaliwa na Azimio hilo na Mkapa asingekuwa Mkapa huyu kama Azimio hilo bado lingeendelea kulinda Miiko na Maadili ya viongozi..
Tatizo kubwa la katiba yetu sio tu vitu vinavyokatazwa ila pia vitu vinavyoruhusiwa kwa sababu maamuzi mengi yanayofikiwa nchini hayafuati katiba hata kidogo isipokuwa katiba hutumika tu pale tunapopenda kwa maslahi ya watawala..Tanzania tumeshapoteza kabisa Utamaduni ktk Maswala ya miiko na Maadili na ndio maana unaona hata hapa JF swala la Udini linatupa taabu sana kuliweka kando.

Kwa hiyo Unapozungumzia kasoro za Ki system ni hizi zinazotokana na Azimio hilo kuwa sheria, kitu ambacho Dr.Slaa kama mwanamapinduzi alikuwa tayari kulivunja na kurudisha haki ya wananchi iliyopotea. Kwa hiyo naweza kusema matatizo yetu yanaweza kabisa kuondolewa na mtu mmoja maadam akifuta Azimio la Zanzibar na kuweka wazi kwamba kila mmoja wetu ataishi kwa mshahara wake na Uhuru wa kuwekeza fedha zake ktk miradi ya mashirika yetu sokoni kama kununua shares ili kukuza soko letu kwani Uchumi wa dunia hii ya puto na ku gamble unategemea sana mali zetu ktk wallstreet...

Nikirudi kwa jamaa zangu ambao wanapinga hata kuwepo kwa mada hii kwa sababu JK na CCM wametudhurumu haki wananchi..Hivi mbona hamsemi tufanye nini zaidi ya kusema JK ajiuzuru hali mkijua wazi hilo haliwezekani? Mnajua fika hatuwezi kuingia msituni wala kufanya vitendo vya aina yeyyote vya kigaidi ili mradi kurudisha haki hiyo. Sasa tukae tuuu tukiomboleza wakati kuna miaka mitano mbele ambayo ni muhimu sana kwa maisha ya Watanzania hasa kina sisi ambao tupo kumi la mwisho!..Badboyz what U gonna do?...
 
Mkandara unanikumbusha kitu kimoja, ndani ya ccm ni majungu na fitina ndiyo yametawala,uchaguzi huu lilizuka zengwe la udini, badala kutangaza sera na kupitia yale ambayo JK aliahidi miaka 5 iliyopita, ccm tulikuwa hatuna cha kuwaeleza watanzania matokeo yake tulianza kupandikiza udini, sishangai sana hii ni kawaida yetu tutafuta kila sababu kutimiza azma yetu, umenikumbusha suala la Dr. Salim alivyopigwa zengwe la uarabu na uhizbu, unafiki huu nashindwa kuuelewa Dr. Salim ameutumikia umma wa Tanzania miaka yake yote tena kwa uadilifu, ni bora mwarabau huyu kuliko mfisadi mkubwa kama Chenge na Lowasa.
 
Back
Top Bottom