Game Theory
JF-Expert Member
- Sep 5, 2006
- 8,546
- 847
HOTUBA YA MHE. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, KWA WANANCHI, 31 JANUARI, 2008
Ndugu Wananchi;
Jambo la pili ninalopenda kulizungumzia ni matatizo yanayoukabili uchumi wa dunia hivi sasa..........Tatizo lingine kubwa linaloukabili uchumi wa dunia sasa linatokana na matatizo yanayoukabili uchumi wa Marekani. Uchumi wa taifa hilo ambao ndiyo mkubwa kuliko wowote duniani umekuwa unapita kwenye misukosuko kwa miezi kadhaa na katika wiki chache zilizopita hali ikawa ngumu zaidi. Kasi ya ukuaji wa uchumi imepungua na thamani ya dola imeshuka. Serikali ya nchi hiyo imeanza kuchukua hatua za kukabiliana na matatizo hayo. Lakini, kwa kuwa uchumi wa Marekani ndiyo uchumi mkubwa kuliko wowote duniani na uchumi wa nchi nyingi duniani una uhusiano nao, matatizo ya uchumi wa nchi hiyo huathiri nchi nyingi. Na sisi Tanzania hivyo hivyo.
Nimeelekeza wachumi wetu wafanye uchambuzi wa kina juu ya athari hizo na kushauri hatua za kuchukua kupunguza makali yake. Moja ya jambo ambalo liko wazi ni lile la kushuka kwa thamani ya dola ya Kimarekani. Sisi tunaweka sehemu kubwa ya akiba yetu ya fedha za kigeni katika dola za Kimarekani. Ni dhahiri kwamba kushuka kwa thamani ya dola za Kimarekani kunatupunguzia uwezo wetu wa kuagiza bidhaa nchi za nje.
Once again mzee wa Pamba aka JK akisaidiwa na maspeech writers wake anataka kulink shida za waTanzania za maji machafu, na huduma mbovu za jamii kwa SUBPRIME MORTAGES MELTDOWN IN THE USA na hiyo RECESSION inayosadikiwa huko.
Maswali kwa JK:
CREDIT CRUNCH YA USA INAHUSIANA VIPI NA WATANZANIA KUKOSA BARA BARA ZA MAANA?
(mfano bara bara ya Kagera haipitiki wiki ya pili sasa)
US RECESSION INAHUSIANA VIPI NA WATANZANIA AMBAO WAMEOPT KUTUMIA BANDARI YA MOMBASA BADALA YA DAR?
Bandari yetu imejaa urasimu kuliko ya Mombasa na hali inafanya kuwa mbaya na TRA ambao serikali yako umetumia mamilioni kuwasomesha lakini hawajui tofauti ya TV na MONITOR YA COMPUTER)
SUBPRIME MORTGAGES INAHUSIANA VIPI NA HAWA WAZEE KUKOSA MAFAO YAO?
(wazee wa Jumuiya hawajalipwa mafao yao mpaka leo)
JK UNAPOSEMA KUWA UMEWAAGIZA WACHUMI WAKO WAFANYE UCHAMBUZI WA KINA WA HIYO RECESSION AMBAYO IPO KAMA VILE HAIPO NA MAMBO YA CREDIT CRUNCHS SIKUELWEI
(Je huyu jamaa atakuelewa unachosema?)
MHESHIMIWA RAIS HUNA HAJA YA KUWAPA MAAGIZO HAO WATU BALI HIYO NI KAZI YAO NA WALITAKIWA WASHA PREDICT GLOBAL ECONOMY ITAKAVYOKUWA IN 2008
KAZI YA RAIS KAZI YAKO SIYO KUDELEGATE HAO WASHAURI WAKO KUHUSU GLOBAL ECONMIC TRENDS
HIYO NI KATIKA JOB DESCRIPTION YAO NA ILITAKIWA HIZO RIPOTI TAYARI WALISHAZIWAKILISHA KWAKO.
THE SAME KAMA GW BUSH NA OF COURSE BERNAKE NA PAULSON KILA KUKICHA WANAASHUSHA HIZO INTEREST RATES
MHESHIMIWA UKITAKA NIANZE KUKUTAKE SERIOUS PUNGUZA BARAZA LA MAWAZIRI TOKA 60 NITAKUONA UNA NIA YA KUTUOKOA KIUCHIMU NA SIYO KUJA NA SPEECH AMBAZO JAMAA ZAKO WANA CUT AND PASTE ARTICLES TOKA GAZETI LA ECONOMIST
(Je huoni hatuna umuhimu wa haya ma VX? Je unajua hayo ma VX 60 yangejenga kilomita ngapi kule Mafia?
(Baraza lako la mawaziri ni 60 NA kila waziri kapewa gari dizaini hii ambalo si chini ya milioni 60 sasa hebu justify hili nalo)