JK msimamizi mzuri wa fedha za umma? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK msimamizi mzuri wa fedha za umma?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Oct 1, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Oct 1, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kwa muda wa miaka minne ya utawala wake Rais Kikwete amepata nafasi ya kuonesha mwelekeo wake juu ya matumizi wa fedha za umma. Je tunaweza kuuelezea utawala wake kuwa ni msimamizi mzuri wa fedha hizo, ni mfujaji, au ni mkarimu asiye na kikomo? Au ndiyo tusubiri hadi atoke madarakani na kuanza kumhoji na kumzonga kama Mkapa?
   
 2. jambo1

  jambo1 JF-Expert Member

  #2
  Oct 1, 2009
  Joined: Jul 5, 2009
  Messages: 242
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hilo halipo MM.....!!!
  Watanzania tumepunguziwa mabilioni ya misaada kwa sababu ya matumizi mabaya ya fedha au fedha zinazotolewa kutowafikia walengwa..,co naweza sema yeyote atakaye mpamba JK katika hili naye atakuwa fisadi au ananufaika na ufisadi..Hili lipo wazi wala haliitaji elimu ya Chuo kikuu kuelewa......!
  Its total NO....!
   
 3. Shishye

  Shishye JF-Expert Member

  #3
  Oct 1, 2009
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 269
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Shida moja ni kwamba vitu vingi viko covered up sasa hivi. Akishamaliza muda wake ndio watu wake watawekwa pembeni waingie wengine kwenye sehemu nyeti. Hapo ndio makororkoro yote huanikwa. Kwasasa tutaweza kuongea tu bila data na kujudge mienendo.

  Navyoona mie, hana uchungu na hela za watoka jasho wa nchi hii. Kila safari yake ya nje amekuwa akijibebea watu kibao pamoja naye. Hawa wote ni gharama. Sijasikia return yoyote iliyotokana na hizi jumbe zake ndefu na nzito. Ningependa kweli kujua siku moja katika hizi safari zake ni mabilioni mangapi yanatokomea.

  Hivi karibuni tumeona magari mapya ya nyumba kuu.... mgari ya nguvu. Utafikiri tuna kiwanda chetu hapa au tunachimba mafuta! Eeither way, zote hizo ni gharama kwa mvuja jasho wa Tanzania. Sio mbaya kutumia, ila umie kwa busara basi ukijua wengine wanajinyima kukuwezesha.
   
 4. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #4
  Oct 1, 2009
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,419
  Likes Received: 3,767
  Trophy Points: 280
  Akishatoka madarakani ndo tutajuwa. Maana hata haya ya Kiwira tuliyajuwa mwishoni mwishoni. Ila kwa kifupi naye mfujaji, maana jinsi anavywashughurikia mafisadi inaonyesha hivyo.
   
 5. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #5
  Oct 1, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Aaah wapi !!! Cabinet kubwa sana, safari nyingi sana, serikali inakopesha wawekezaji i.e TRL, serikali inatumia hela za walipa kodi kunyanyasa raia i.e Loliondo, bila kusahau milioni 400 kwa uchaguzi wa UVCCM. sijui wana miradi gani hawa?
  Angekuwa msimamizi mzuri basi wale wote wanaoharibu kwenye ripoti ya CAG kwa kipindi chote JK alichokaa madarakani wangekuwa jela.
   
  Last edited: Oct 1, 2009
 6. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #6
  Oct 1, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,328
  Likes Received: 1,794
  Trophy Points: 280
  Mi napata mashaka sana na usimamiaji mzuri wa fedha za umma kwasababu ya safari nyingi za viongozi, tume nyingi kuhusu mambo yanayojitokeza hapa na pale na kesi ambazo hazijulikani kama kweli ipo nia ya kuhakikisha haki inatendeka
  .Zaidi ya yote hayo ni kuendelea kubeba mashirika ambayo yanatakiwa yajiendeshe kwa faida kama TRL na ATCL. Hapo sijagusa TICTS ambao wana underprform na bunge lilishatoa ilani kwa serikali kufikiria upya mkataba uliopo.
   
 7. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #7
  Oct 1, 2009
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,583
  Likes Received: 1,943
  Trophy Points: 280
  Usimamiaji wa fedha hizo zinapokuwa tayari allocated kwa matumizi flani unaweza kuwa justified kama "Usimamizi mzuri" Only kama matumizi hayo pia yamekuwa justified kwamba ni matumizi mazuri.Kwa hiyo kabla ya kujiuliza kama fedha hizo zilitumika ilivyotakiwa,kwanza tujiulize kama matumizi hayo yalitakiwa ama yalikuwa ya muhimu.

  Fedha ni mojawapo ya assets za wananchi zinazosimamiwa na serikali kwa niaba yao...Achilia mbali fedha ambazo ni current asset,bado kuna rasilimali za Taifa na sasa bishara ya Real estate USA....Kwa maoni yangu usimamizi wa nchi fedha na rasilimali vikiwemo si wa kuridhisha,uwajibikaji hakuna na hivyo Taifa kukosa mwelekeo.
   
  Last edited: Oct 1, 2009
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Oct 1, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Je basi CAG aanzishe uchunguzi kama wa stendi ya Ubungo wa safari zote za nje za JK na wasaidizi wake na wasaidizi wao? Au rais ana uhuru wote wa kutumia fedha za umma?
   
 9. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #9
  Oct 1, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Hazina imekauka hata alichoacha Mkapa kimeyeyuka!
   
 10. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #10
  Oct 1, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Yeah dah jamaa kwa safari ni balaa hivi Brazil ameenda?
   
 11. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #11
  Oct 1, 2009
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,583
  Likes Received: 1,943
  Trophy Points: 280
  Matumizi ya fedha za umma ni lazima yawe scrutinized,ndio utawala wa kidemokrasia unavyotakiwa uwe,si kama monarchy....Ndiyo mwanzo wa kuwawajibisha viongozi,kama hatushtushwi na matumizi ya kodi zetu wenyewe then kamwe hatuwezi kutoka kwenye umasikini.Hakuna chombo chenye kuhoji na kuhusu matumizi ya serikali,maana kila siku naona ni Pinda tu mwenye kuona hayo,wengine wote wanaona sawa tu,tatizo wananchi hawajafikia kujuwa haki zao za kimsingi na namna ya kuiwajibisha serikali.
   
 12. M

  Mayolela JF-Expert Member

  #12
  Oct 1, 2009
  Joined: Sep 21, 2009
  Messages: 383
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huyo atakuwa fisadi mdogo????????
   
 13. babukijana

  babukijana JF-Expert Member

  #13
  Oct 1, 2009
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 4,817
  Likes Received: 1,164
  Trophy Points: 280
  da kama ulikuwepo brazil ataenda akirudi kutoka marekani,ataenda kwa ajili ya kusalimia wazazi wake na maximo,na kuangalia samba inachezwaje pia ataongea na wabrazil weusi kuwashawishi warudi bongo kwani wengine walichukuliwa zanzibar kipindi cha biashara ya utumwa
   
 14. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #14
  Oct 2, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  naona mh MJJ umejijibu swali mwenyewe. Ngojea ni-elaborate vizuri. Bongo hakuna data za pesa za umma. Siku tunaposikia numba ni wakati wa bajeti tu. Na hapo nina uhakika asilimia 100% ya waTZ hawaelewi kitu. Mtu akianza kuzungumza in terms of millions, billions and trillions, watu tunashindwa kufuata tarakimu tena. Ni mahesabu yaliyo juu yetu katika uwezo wa kuelewa na ku-process. Na kwa jinsi ninavyocheki usomaji wa bajeti wa nchi mbalimbali...nadhani kwa uhakika tunaweza kusema ufuatiliaji ni zero. Basi sasa, nini kifanyike? Moja ni kuweka zile twakimu katika uelewa mzuri. Mfano, wanaposema pesa za ujenzi...iwekwe a comperative figure. Kwa mfano, serikali imetenga billion moja na nusu kwa ujenzi wa barabara. How much is that in reality? Itajenga barabara ngapi? Kwa hiyo lazima watoe a comperative figure - mfano: kujenga lami km 1 = 1 million. Nadhani umenipata. Hivyo basi, wananchi wakishaelewa kuna pesa kiasi gani na ya kufanya mambo gani, ndipo tutaweza kujua kama ni msimamizi mzuri wa fedha za umma. Lakini bila kujua pesa ya umma ni kiasi gani, na inatumikaje, hatutaweza kuja na a firmitive answer.

  Amen! Ningependa kuelekeza hii blame kwa wabunge, maana wao wana nguvu sana, sema hawatambui hilo. Wanaweza kuwajibisha serikali, nk. Kufuatilia matumizi ya pesa kwao ni rahisi maana hakuna ripoti inayoweza kufichwa mbele ya bunge. Sasa wakwetu wamelala tu. Naudhika mimi, we acha!
   
 15. W

  WildCard JF-Expert Member

  #15
  Oct 2, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Ofisi ya CAG ingeratibu tu UKAGUZI. Ukaguzi wenyewe ungefanywa na kampuni binafsi zenye kuaminika. Tunahitaji sheria ya UHASIBU kali kuliko hata ile ya MANUNUZI (PPA). Tuipe meno NBAA yetu. Isibaki kutunga na kusahihisha mitihani tu! Vinginevyo matumizi Serikalini na TAASISI zake ni balaa.
   
 16. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #16
  Oct 2, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Duh ukija na kufanya critical analysis hapa kwa kiasi gani na matumizi haya bila shaka unaweza kusema kuwa ni hali ni mbaya sana hata kama sio yeye ukweli ni kwamba pesa nyingi sana mali za umma zinapelekwa sehemu sio yake na pia matumizi hata tamekuwa makubwa kupita uwezo wake, jaribu kutazama hata deni la Taifa nakisi yake kwa sasa
   
 17. w

  wasp JF-Expert Member

  #17
  Oct 2, 2009
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 206
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwezi Desemba anakwenda Greenland (nchi ambayo hajaitembelea) kwa mwaliko wa Waeskimo kuona jinsi ya kutengeneza barafu inyoyeyuka juu ya mlima Kilimanjaro.
   
 18. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #18
  Oct 2, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Kila mwaka bajeti zinapitishwa lakini mwaka ukiisha hatuulizani kama pesa iliyotengwa imefanya kazi iliyokusudiwa na kama jibu ni hapana je kwa nini? hatuulizani kama kuna pesa ambayo haikufanyiwa kazi na imebaki kwa mwaka huo irudihshwe serikalini.
  Ndio maana kule mjengoni bajeti ya wizara ikipitishwa inakuwa ni chereko na vigelegele kwa sababu wanajua kinachofuata hapo ni ulaji kwa kwenda mbele na hakuna kuulizana mbele ya safari!
  Kaazi kweli kweli!!
   
 19. The Invincible

  The Invincible JF-Expert Member

  #19
  Oct 2, 2009
  Joined: May 6, 2006
  Messages: 4,723
  Likes Received: 1,213
  Trophy Points: 280
  Teh teh teh! Naona week end imeanza.
   
 20. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #20
  Oct 2, 2009
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,471
  Likes Received: 1,420
  Trophy Points: 280
  JK hana usimamizi wowote zaidi ya ufujaji wa fedha za umma
   
Loading...