JK, Msiba Wa Jirani Na Yanayotokea Dodoma- Tafsiri Yangu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK, Msiba Wa Jirani Na Yanayotokea Dodoma- Tafsiri Yangu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by maggid, Apr 23, 2012.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Apr 23, 2012
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ndugu zangu,

  Katika dunia hii mwanadamu huwezi kumchagua jirani yako. Jirani yako ni jirani yako. Msiba wa jirani ni msiba wako pia, unakuhusu.

  Maana, kuna wanaohoji JK kuacha mambo ya nyumbani na kwenda kushiriki maziko ya Bingu wa Mutharika. Silioni kosa katika hilo. Na hata kama JK angeamua kutokwenda mazikoni Blantyre, bado, asingekwepa lawama. Maana, kuna ambao wangemlaumu JK kwa kutozingatia mila na desturi zetu Waafrika; kushiriki kwenye kumzika jirani yako.


  Tukumbuke, kuwa Wamalawi si tu ni jirani zetu, ni ndugu zetu pia. Kuna Wanyasa wengi wa Malawi katika nchi hii waliochanganyika na makabila yetu. Na tunaambiwa, kuwa siku ya mkesha wa Uhuru wa Malawi, Watanzania wengi kando ya Ziwa Nyasa nao walikesha wakishangilia. Uhuru wa Mnyasa ni Uhuru wetu. Msiba wa Mnyasa, ni msiba wetu.


  Mengineyo...

  Nchi yetu inapita sasa kwenye kipindi kigumu sana. Tusishushe chini kiwango cha mjadala. Kubaki kumjadili JK na safari kwenda kutuwakilisha mazikoni ni kushusha kwa makusudi kiwango cha mjadala. Kwa makusudi tutakuwa tumeacha kujadili hoja za msingi ikiwamo hii ya kashfa za ufisadi wa kutupwa uliodhihiri bungeni na unaotutaka tuweke shinikizo kwa wahusika kuachia ngazi na hata kufikishwa kwenye vyombo vya sheria. Maana, anayeliibia taifa ni mhalifu tena zaidi ya mwizi wa kuku. Huyu ni jambazi. Kumwacha aendelee kukalia ofisi ya umma ni sawa na kumsusia mlevi bia, au kumpa fisi kazi ya kulinda bucha.


  Tuliko sasa ni kubaya. Tunakokwenda kutakuwa ni kubaya sana kama hatutachukua hatua sasa. Nimeona asubuhi ya leo kwenye runinga ( Channel Ten) utetezi wa ajabu kutoka kwa Waziri wa Uchukuzi Bw. Omar Nundu.

  Nundu anadai hawezi kujiuzuru kwa kutoa hoja ambazo kimsingi zinamtaka aachie ngazi haraka iwezekanavyo ili abaki na heshima kwa jamii kama bado anayo.


  Anatwambia Watanzania kuwa amekuwa 'akizungukwa' na Naibu wake Athuman Mfutakamba. Ndio, Waziri Nundu anapojitetea kwa Watanzania kwa kusema haelewani na Naibu wake na kuwa kampuni ya Kichina ilimpeleka Naibu wake China, Mauritania na Equatorial Guinea bila kibali chake inatosha kuonyesha kiwango cha juu cha ukosefu wa nidhamu, uwajibikaji na uadilifu katika baraza la mawaziri . Sioni ni kwa namna gani maelezo ya Nundu yanaweza kumlinda mbali ya kuonyesha ulazima wa kuwajibishwa kwake haraka iwezekanavyo.


  Ndio huwezi kuonyesha kuwa ulijua kilichokuwa kikifanyika, ukabaki kimya mpaka unatwambia hii leo, halafu utake ridhaa ya umma ikuamini kuendelea kukupa dhamana ya kushika nafasi hiyo hiyo.


  Na wahenga walisema; kwenye msako wa nyani ngedere hawezi kusalimika.
  Ndio, tutafanya makosa kudhani kuwa ’madudu’ haya yaliyoibuliwa kwenye ripoti ya CAG yanahusu Wizara tano au sita tu. Hii ni fursa pekee kwa Watanzania kupitia wabunge wao kuendesha ’ msako mkubwa’ wa wote wenye kulitafuna taifa letu tunalolipenda.


  Ni wakati pia wa kuhakikisha Katiba Mpya tunayokwenda kuitolea mapendekezo yetu itusaidie kuziba mianya ya wezi wa mali ya umma kuendelea kuliibia taifa bila ya hofu ya kufikishwa mahakamani na hata kutiwa magerezani.


  Ndio, hatuwezi kuenenda kama tunavyoenenda sasa; maana, unapoona Wananchi wanalalamika, Wabunge wanalalamika, Mawaziri wanalalamika, na Rais analalamika, basi, hilo ni taifa la ajabu sana. Taifa la Walalamikaji.

  Na maradhi ya ' kulalamika' ni ya kimfumo. Ni mfumo mbovu tu ndio unaoweza kuzaa Taifa la Walalamikaji. Turekebishe mfumo wetu kwa kupitia Katiba. Inawezekana.


  Maggid Mjengwa,

  Iringa.
  0788 111 765
  Mjengwa Blog::Habari,Picha,Matangazo
   
 2. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #2
  Apr 23, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Kikwete huu ni muhula wake wa mwisho hana cha kupoteza.
   
 3. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #3
  Apr 23, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Nchi hii ni kama haina Rais kabisa.
  Rais anashindwa kufanya maamuzi magumu.
  Rais anakimbia kivuli chake
  Rais amekuwa mwoga kuwaadabisha watu alio wateua.
  Rais hajui kwa nini Tanzania ni maskini huku watendaji wake wakifanya ufisadi wa kufuru.
   
 4. Kalumbesa

  Kalumbesa JF-Expert Member

  #4
  Apr 23, 2012
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,009
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Mfalme wetu ana ****...anaweza hata kwenda kuzima moto unaoanza kuteketeza nyumba ya jirani akaacha kuendelea kuzima ule ulio kolea nyumbani kwake..kweli ana ****..
   
 5. A

  Aine JF-Expert Member

  #5
  Apr 23, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,613
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Binafsi nimesikitika saana kusikia kwamba ameenda kuzika nje ya nchi badala ya kushughulikia suala hili zito la Mawaziri mbaya san ni pale wabunge wanapowasilisha hoja ya PM kujiuzulu, yaani yeye haoni kuwa jambo hilo ni zito sana kiasi cha kumkoseha usingizi kabisa, badala yake anaenda kuzika!!!!!!! si angemtuma mwakilishi tu jamani kwani lazima kila tafrija ahudhurie yeye mwenyewe! kweli Mungu atusaidie nchi yetu isije angamia
   
 6. k

  kilolambwani JF-Expert Member

  #6
  Apr 23, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 395
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mambo mengi mazito ya kitaifa amewahi kuacha hapa nchini, yeye akaenda kutalii huko nje, mfano ni mgomo wa madakatari
   
 7. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #7
  Apr 23, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  kiherehere
   
 8. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #8
  Apr 23, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Huyu Rais inabidi aingie kwenye Guinness book of records kwa kuwa rais wa ajabu duniani ambaye hajawahi na hatapata kutokea!
   
 9. The Stig

  The Stig JF-Expert Member

  #9
  Apr 23, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 881
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 80

  Mahusiano kati ya mataifa ni tofauti na mahusiano kati ya mtu na mtu. Huu mfano wako wa jirani kufiwa hau-apply katika medani za kidiplomasia. Inaruhusiwa kabisa kwa rais kumtuma mwakilishi wake kwenye msiba na nchi iliyofiwa ikampokea kwa uzito ule ule ambao angepewa rais.

  Vile vile, inaruhusiwa kabisa kwa rais kumtuma waziri wa mambo ya nje kumpokea mkuu wa nchi airport kama yuko busy.
   
 10. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #10
  Apr 23, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Asante kwa tafsiri yako!
   
 11. King2

  King2 JF-Expert Member

  #11
  Apr 23, 2012
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 1,289
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Jakaya Kikwete is a disaster
   
 12. Rufiji

  Rufiji JF-Expert Member

  #12
  Apr 23, 2012
  Joined: Jun 18, 2006
  Messages: 1,710
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 160
  Maggid,

  Wazungu wanasema charity begins at home, kwa hiyo wewe unaenda kwenye msiba nyumba ya jirani wakati nyumba yako hiko kwenye matatizo makubwa. Watu wa Pwani tuna priorities za ajabu sana! Tumeona marais mbali mbali waki-cancel safari pale nchi zao zinapokuwa na matatizo au wakitaka kupitsiha miswada mikubwa.
   
 13. mgen

  mgen JF-Expert Member

  #13
  Apr 23, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 15,148
  Likes Received: 1,882
  Trophy Points: 280
  acha wafu wazike wafu wenzao!
   
 14. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #14
  Apr 23, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kwa nini asimtume Rais wa Zanzibar kama Makamu wake hana nafasi au kama waziri wa mambo ya nchi za nje yuko kikaoni Dodoma? Wazanzibar wangefurahi kuona rais wao naye kapata heshima wanazolilia hii ni busara ya kawaida tu ingwa hatambuliki kupata heshima hiyo katika seriakli ya Muungano.
   
Loading...