Jk mjeshi wa shoka

salimkabora

JF-Expert Member
Nov 10, 2012
2,441
651
Kwa hili la katiba mpya Jk amethibitisha ujeshi wake kwa kusimama na matakwa ya wananchi kuliko kukumbatia itikadi za vyama vya siasa ambazo zimelitumbukiza taifa katika majanga mengi ya kutisha ikiwa ni pamoja na ufisadi, uporwaji rasilimali, ukumbatiaji wenye nacho, nk. Hapa Jk amewatoka majambazi yote yaliyokuwa yanamtia ujinga na kumfunga mdomo asisimamie taifa ipasavyo na badala yake kufata mkondo wa magenge yaliyojipanga kivyama ili kupata nguvu ya pamoja za uporaji. Hapa JK ameonyesha rangi yake ya kweli ya ujeshi kusimama na nchi yake mda wote badala ya kusombwa na mkondo wa waangamiza nchi. Nyerere ni baba wa uhuru na jk ni baba wa taifa jipya. Aliyebezwa na kudharauliwa na kutukanwa hatimaye ameibuka kuwa shujaa. Mwana jf hebu tiririka hapa chini kuhusu Jk kuruhusu mivyama ya kisiasa kufa na kuwang'oa meno wanasiasa na kubakia mapengo matupu. N sema hili ni la JK kwa maana alikuwa na mabavu ya kutosha kulikwamisha nyuma ya pazia na kwa kuwa kaliacha kama lilivyo ni wazi mafuta yamejitenga na maji.
 
Pongezi siwezi kumpa JK, pongezi nitampa kwanza Mtikila aliyepambana tangia mwezi wa tano mwaka 1993. Wakati huo alionekana kama mwehu, lakini yote aliyokuwa anayataka yameingizwa kwenye katiba. Kumbe wananchi wa TZ walikuwa wanataka mambo fulani lakini walikuwa waoga kuyasema.
Pongezi za pili ziende kwa CHADEMA ambao kwenye ilani ya uchaguzi suala la katiba mpya lilikuwepo. Mwenyekiti wa CCM ambaye ni raisi hakuwa na wazo la katiba mpya, na hakulitaka kabisa. Ila aliona atengeneze historia kupitia migongo ya mawazo ya watu wengine. Hata hivyo, sawa tu kwa sababu ni suala la mustakabadhi wa nchi yetu
 
nadhani tuvute subra japo dalili ni nzuri, mpaka hapo nampongeza! the only doubt ni mabaraza ya katiba kuchakachuliwa, nadhani subordinates wake they dont know huyu bwama ana malengo gani! wengiwao ni wanafiki!
 
Kamanda usianze kununua nepi kabla mtoto hajazaliwa. Kwa juu juu unaiona safi kumbuka hii ni Katiba ya Muungano. Tafakari macheche yafuatayo:-
1. Zanzibar wanayo Katiba yao Tanganyika je? Mtakapo ipitisha hii inabidi mchakato
mwingine wa Katiba ya Tanganyika
uanze, Je huo utachukua muda gani? Ni nani atakayekuwa Rais kipindi hicho cha
kutafuta maoni ya Watanganyika
kuandika Katiba yao?
2. Mabaraza ya Katiba yamejaa watu wa chama gani?
3. Suala la Mamlaka ya Rais katika kuteua umeyasoma vizuri?
4. Tume Huru ya Katiba itakuwaje huru wakati wajumbe wake ni wateuliwa wa Rais? yaani Majaji wakuu, Wanasheria
wakuu, Mwenyekiti wa Tume ya Maadili.
Kilichotokea hapo ni sawa na kuambiwa tulia unyolewe.............

Tafakari!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Pongezi siwezi kumpa JK, pongezi nitampa kwanza Mtikila aliyepambana tangia mwezi wa tano mwaka 1993. Wakati huo alionekana kama mwehu, lakini yote aliyokuwa anayataka yameingizwa kwenye katiba. Kumbe wananchi wa TZ walikuwa wanataka mambo fulani lakini walikuwa waoga kuyasema.
Pongezi za pili ziende kwa CHADEMA ambao kwenye ilani ya uchaguzi suala la katiba mpya lilikuwepo. Mwenyekiti wa CCM ambaye ni raisi hakuwa na wazo la katiba mpya, na hakulitaka kabisa. Ila aliona atengeneze historia kupitia migongo ya mawazo ya watu wengine. Hata hivyo, sawa tu kwa sababu ni suala la mustakabadhi wa nchi yetu
Ndugu yangu hebu jaribu kunielewa kidogo sisemi apewe hongera kwa kuleta katiba bali nasema pongezi kwa kukitosa chama chake na kuruhusu kife; katika mazingira ya katiba hii sioni jinsi sisiem inavyoweza kuendelea kupumua baada ya nyenzo za kuibebea kutupiliwa mbali.
 
Kwa hili la katiba mpya Jk amethibitisha ujeshi wake kwa kusimama na matakwa ya wananchi kuliko kukumbatia itikadi za vyama vya siasa ambazo zimelitumbukiza taifa katika majanga mengi ya kutisha ikiwa ni pamoja na ufisadi, uporwaji rasilimali, ukumbatiaji wenye nacho, nk. Hapa Jk amewatoka majambazi yote yaliyokuwa yanamtia ujinga na kumfunga mdomo asisimamie taifa ipasavyo na badala yake kufata mkondo wa magenge yaliyojipanga kivyama ili kupata nguvu ya pamoja za uporaji. Hapa JK ameonyesha rangi yake ya kweli ya ujeshi kusimama na nchi yake mda wote badala ya kusombwa na mkondo wa waangamiza nchi. Nyerere ni baba wa uhuru na jk ni baba wa taifa jipya. Aliyebezwa na kudharauliwa na kutukanwa hatimaye ameibuka kuwa shujaa. Mwana jf hebu tiririka hapa chini kuhusu Jk kuruhusu mivyama ya kisiasa kufa na kuwang'oa meno wanasiasa na kubakia mapengo matupu. N sema hili ni la JK kwa maana alikuwa na mabavu ya kutosha kulikwamisha nyuma ya pazia na kwa kuwa kaliacha kama lilivyo ni wazi mafuta yamejitenga na maji.

Hana lolote huyo jk,pongezi naziende kwa CHADEMA waasisi wa mchakato wa katiba mpya, CCM wametumia ilani ya CHADEMA na hii ni dhahiri kuwa CCM hawana jipya hata kwenye ilani yao zaidi ya kubambikiza kesi nk
 
Pongezi siwezi kumpa JK, pongezi nitampa kwanza Mtikila aliyepambana tangia mwezi wa tano mwaka 1993. Wakati huo alionekana kama mwehu, lakini yote aliyokuwa anayataka yameingizwa kwenye katiba. Kumbe wananchi wa TZ walikuwa wanataka mambo fulani lakini walikuwa waoga kuyasema.
Pongezi za pili ziende kwa CHADEMA ambao kwenye ilani ya uchaguzi suala la katiba mpya lilikuwepo. Mwenyekiti wa CCM ambaye ni raisi hakuwa na wazo la katiba mpya, na hakulitaka kabisa. Ila aliona atengeneze historia kupitia migongo ya mawazo ya watu wengine. Hata hivyo, sawa tu kwa sababu ni suala la mustakabadhi wa nchi yetu

naungana na wewe mkuu, CHADEMA ndio kinachoongoza nchi kwa sasa,magamba wanafiki na wababaishaji
 
Vyovyote itakavyokuwa hatuwezi kukwepa kumsifia jk katika hili labda tuwe wachoyo wa shukrani.
 
Pongezi siwezi kumpa JK, pongezi nitampa kwanza Mtikila aliyepambana tangia mwezi wa tano mwaka 1993. Wakati huo alionekana kama mwehu, lakini yote aliyokuwa anayataka yameingizwa kwenye katiba. Kumbe wananchi wa TZ walikuwa wanataka mambo fulani lakini walikuwa waoga kuyasema.Pongezi za pili ziende kwa CHADEMA ambao kwenye ilani ya uchaguzi suala la katiba mpya lilikuwepo. Mwenyekiti wa CCM ambaye ni raisi hakuwa na wazo la katiba mpya, na hakulitaka kabisa. Ila aliona atengeneze historia kupitia migongo ya mawazo ya watu wengine. Hata hivyo, sawa tu kwa sababu ni suala la mustakabadhi wa nchi yetu
Nikweli mzee nakumbuka sana hata jangwani mwaka 1995 mtikila aliliongelea sana mpaka likapandisha watu mori wakuenda kutafuta wabaya wao huko mitaani.
 
Kamanda usianze kununua nepi kabla mtoto hajazaliwa. Kwa juu juu unaiona safi kumbuka hii ni Katiba ya Muungano. Tafakari macheche yafuatayo:-
1. Zanzibar wanayo Katiba yao Tanganyika je? Mtakapo ipitisha hii inabidi mchakato
mwingine wa Katiba ya Tanganyika
uanze, Je huo utachukua muda gani? Ni nani atakayekuwa Rais kipindi hicho cha
kutafuta maoni ya Watanganyika
kuandika Katiba yao?
2. Mabaraza ya Katiba yamejaa watu wa chama gani?
3. Suala la Mamlaka ya Rais katika kuteua umeyasoma vizuri?
4. Tume Huru ya Katiba itakuwaje huru wakati wajumbe wake ni wateuliwa wa Rais? yaani Majaji wakuu, Wanasheria
wakuu, Mwenyekiti wa Tume ya Maadili.
Kilichotokea hapo ni sawa na kuambiwa tulia unyolewe.............

Tafakari!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Kumbuka hawa wateule wa rais wakishateuliwa wanathibitishwa na bunge na rais hawezi kuwaondoa tena bila kibari cha bunge.
 
Hii inaitwa mwaga ugali nimwage mboga, si hawataki kutulia wamwachie nchi atawale sasa na yeye anawachia likatiba wacheze nalo wakiiingia madarakani. ''Mua umeisha utamu''.
 
Hana lolote huyo jk,pongezi naziende kwa CHADEMA waasisi wa mchakato wa katiba mpya, CCM wametumia ilani ya CHADEMA na hii ni dhahiri kuwa CCM hawana jipya hata kwenye ilani yao zaidi ya kubambikiza kesi nk
Hao sisiem ndo chali weshakufa mzee au hujanipata fresh
 
Back
Top Bottom