JK: Miradi mikubwa imenishtua; Ni Miujiza Hivi sasa tunajenga madaraja matatu eti wakati wa JKN moja

Hakukuwa na ulazima wa rais Kikwete kulinganisha utekelezaji wa miradi kipindi chake na wakati wa Mwl Nyerere! It is just not right na inaweza kuzua mijadala isiyo ya lazima.

Mwl Nyerere alijenga viwanda (Tanganyika packers, mwatex, urafiki, machine tools, etc etc), Air Tanzania ilikuwa na ndege, TRL ilikuwa better, elimu bure, huduma za afya bure. Na tukumbuke wakati huo huo Mwl Nyerere alikuwa mshiriki mkubwa wa mapambano ya ukombozi barani Africa. Na yote alifanya kwa vijihela vya korosho na pareto - madini yalikuwa bado ardhini!

Kikwete amefanya yake mazuri, hahitaji kulinganisha kabisa na Mwl Nyerere.
 
Siyo bure kuwa utekelezaji wa miradi mikubwa unafanyika katika miaka hii, hasa awamu hii ya nne.
Sababu nzuri tu zipo na zenye mantiki, nitataja chache tu.
  1. Mabadiliko ya kisaikolojia-alipoingia Rais Mkapa yalitokea mbadiliko makubwa ya kisaikolojia, na kugundua kuwa kuna uwezo mkubwa tu wa kutekeleza miradi mikubwa kwa hela zetu wenyewe.
  2. Kuongezeka uwezo wa kitaalam-kuanzishwa kwa TANROADS kumetatua kwa kiasi kikubwa sana usimamizi wa miradi ya ujenzi ukilinganisha na usimamizi wa miska hiyo kupitia Wizara ya Ujenzi moja kwa moja.
  3. Kuanzishwa kwa Road fund-fedha ya utekelezaji w miradi ya ujenzi imekuwa ni rahisi kwa miaka hii kuliko ilivyokuwa miaka ya awamu ya kwanza au ya pili
  4. Makandarasi wa kichina-pamoja na matatizo yao, wakandarasi hawa wa kichina wametoa changamoto kubwa kupunguza gharama za ujenzi wa miundombinu mingi.Wengi akilini mwao, hasa viongozi,waliwapa umuhimu wa kwanza makandarasi toka Ulaya, makandarasi ambao ni ghali sana pamoja na wasimamizi wao wa miradi.

Sera sahihi za CCM katika fani hii lazima zipongezwe, tupende tusipende.

Ule utegemezi wa mawazo toka World Bank na nchi za Ulaya na Marekani katika utekelezaji wa miradi ya miundo mbinu umepungua sana na ndiyo maana maendeleo yanaonekana.
Hata miaka ya Mwalimu, wakubwa hao(World Bank na nchi za Ulaya/Marekani) walikataa kufadhili TAZARA wakidai mradi huo hauwasaidii watanzania.

Kwa msimamo huo wa kujitegemea katika kufikiri, the sky is the limit!
Acha uongo. Wananchi wamechachamaa katika vita dhidi ya ufisadi + cdm influence in the country ndo msingi wa magamba kufanya kazi. Na bado tutawabana mpaka kieleweke otherwise they are out in 2015
 
Binafsi simchukii kikwete kama mtanzani mwezengu, lakin kama kiongozi wa taifa letu hawezi kutufunga kitambaa cheusi kwa

vijimiradi vichache na kujilinganisha na Mwl JK nyerere.

Kikwete amesoma bure university of Dar es slaam akigharimiwa na pesa ya wakulima wa pamba, chai, buni, karafuu nk, Sasa hivi

pamoja na mikopo lukuki, madini, kilimo nk kuingia pale UDSM ni kazi hasa kwa watoto wa masikini, mbaya zaidi hata hiyo mikopo

itolewayo na serikali ni katika mazingira magumu na kusikitisha. Elimu bora imekuwa ya wachache wenye uwezo tofauti na enzi zile

Hawezi kujinasibu kwa mambo mepesi mepesi bila kujibu hoja za msingi kushindwa kuinua elimu, afya, mfumko wa bei, maslahi

duni kwa wafanyakzi na kumomonyoka kwa
maadili ya viongozi. Haijalishi aliikuta inchi wapi je kuanzia pale alipoikuta amekuwa na

positive gradient kimaendeleo au negative tunapojumlisha the gain and loss for the final summation to complement a judgement

to Mr president?

Kibaya zaidi ametuletea urithi wa ovyo kabisa UDIN (hapa amechafua taswira ya taifa letu na amani na mshikamano wetu

ameuweka rehani, watanzania enzi hizo hatukuchukiana na tulikuwa na dini zetu kama ilivyo leo lakin kwanini kwenye awamu zake?)
 
Siyo bure kuwa utekelezaji wa miradi mikubwa unafanyika katika miaka hii, hasa awamu hii ya nne.
Sababu nzuri tu zipo na zenye mantiki, nitataja chache tu.
  1. Mabadiliko ya kisaikolojia-alipoingia Rais Mkapa yalitokea mbadiliko makubwa ya kisaikolojia, na kugundua kuwa kuna uwezo mkubwa tu wa kutekeleza miradi mikubwa kwa hela zetu wenyewe.
  2. Kuongezeka uwezo wa kitaalam-kuanzishwa kwa TANROADS kumetatua kwa kiasi kikubwa sana usimamizi wa miradi ya ujenzi ukilinganisha na usimamizi wa miska hiyo kupitia Wizara ya Ujenzi moja kwa moja.
  3. Kuanzishwa kwa Road fund-fedha ya utekelezaji w miradi ya ujenzi imekuwa ni rahisi kwa miaka hii kuliko ilivyokuwa miaka ya awamu ya kwanza au ya pili
  4. Makandarasi wa kichina-pamoja na matatizo yao, wakandarasi hawa wa kichina wametoa changamoto kubwa kupunguza gharama za ujenzi wa miundombinu mingi.Wengi akilini mwao, hasa viongozi,waliwapa umuhimu wa kwanza makandarasi toka Ulaya, makandarasi ambao ni ghali sana pamoja na wasimamizi wao wa miradi.

Sera sahihi za CCM katika fani hii lazima zipongezwe, tupende tusipende.

Ule utegemezi wa mawazo toka World Bank na nchi za Ulaya na Marekani katika utekelezaji wa miradi ya miundo mbinu umepungua sana na ndiyo maana maendeleo yanaonekana.
Hata miaka ya Mwalimu, wakubwa hao(World Bank na nchi za Ulaya/Marekani) walikataa kufadhili TAZARA wakidai mradi huo hauwasaidii watanzania.

Kwa msimamo huo wa kujitegemea katika kufikiri, the sky is the limit!

Umeanisha vizuri na itaonekana CCM wanafanya kazi nzuri lakini kutokana na fedha ambazo Tanzania imepata kutoka nje pia uchimbaji wa madini nchini iwapo wangekuwepo watala wengine na sio CCM Tanzania ingekuwa mbali zaidi ya hapo ilipo unachojaribu kuongea ni kumsifia vitu vichache sana walivyofanya CCM huku pesa nyingi wakarudisha nje kwenye account zao binafsi ni sawa na kusifia kupewa baiskeli wakati ulistahili gari.

Kuna mambo CCM wanayataja muda mwingi ambayo hayana tija ya haraka kwa maisha ya watanzania kama kutaja urefu wa barabra za lami, daraja la kigamboni na kuongezeka wanafunzi vyuo vikuu wakati wakimaliza hawana ajira. Mambo ya haraka wanayohitaji watanzania na ni mambo muhimu duniani na CCM wanayakwepa ni pamoja na kuongeza ajira kukidhi mahitaji ya wananchi, kupunguza mfumuko wa bei, kuongeza pato la mtanzania, kuweka huduma bora za afya angalau turudi wakati wa Mwalimu Nyerere, kujenga viwanda, kupunguza rushwa, madaraka kutopena kindugu na kirafiki na pia kufungulia mashitaka viongozi mafisadi mfano Lowassa, Chenge, Mkullo, Ngereja, Karamagi, Yona na wengine tukumbuke ufisadi ndio chanzo kikuu cha umasikini katika afrika. HAYA NDIO MAMBO MUHIMU KWANZA KWA WATANZANIA NA SIO UREFU WA BARABARA ZA LAMI WALA DARAJA LA KIGAMBONI
 
Hakukuwa na ulazima wa rais Kikwete kulinganisha utekelezaji wa miradi kipindi chake na wakati wa Mwl Nyerere! It is just not right na inaweza kuzua mijadala isiyo ya lazima.

Mwl Nyerere alijenga viwanda (Tanganyika packers, mwatex, urafiki, machine tools, etc etc), Air Tanzania ilikuwa na ndege, TRL ilikuwa better, elimu bure, huduma za afya bure. Na tukumbuke wakati huo huo Mwl Nyerere alikuwa mshiriki mkubwa wa mapambano ya ukombozi barani Africa. Na yote alifanya kwa vijihela vya korosho na pareto - madini yalikuwa bado ardhini!

Kikwete amefanya yake mazuri, hahitaji kulinganisha kabisa na Mwl Nyerere.

Well said Nyerere hawezi linganishwa na kikaragosi Kikwete mbali na maendeleo hakuruhusu ndugu zake kujaa NEC wala kuteua wakuu wa wilaya na wabunge viti maalumu kwa rushwa ya ngono
 
kwa hiyo raisi mzima anaishi kwa miujiza,hana uhakuka na anachokifanya anaona wengewenge tu
kazi yake kujilinganisha na marisi wenzake hana jipya angoje tu 2015 (M4C)

:"YOU CAN AVOID REALITY BUT YOU CANNOT AVOID THE CONSEQUENCES OF AVOIDING REALITY"
 
Umeanisha vizuri na itaonekana CCM wanafanya kazi nzuri lakini kutokana na fedha ambazo Tanzania imepata kutoka nje pia uchimbaji wa madini nchini iwapo wangekuwepo watala wengine na sio CCM Tanzania ingekuwa mbali zaidi ya hapo ilipo unachojaribu kuongea ni kumsifia vitu vichache sana walivyofanya CCM huku pesa nyingi wakarudisha nje kwenye account zao binafsi ni sawa na kusifia kupewa baiskeli wakati ulistahili gari.

Kuna mambo CCM wanayataja muda mwingi ambayo hayana tija ya haraka kwa maisha ya watanzania kama kutaja urefu wa barabra za lami, daraja la kigamboni na kuongezeka wanafunzi vyuo vikuu wakati wakimaliza hawana ajira. Mambo ya haraka wanayohitaji watanzania na ni mambo muhimu duniani na CCM wanayakwepa ni pamoja na kuongeza ajira kukidhi mahitaji ya wananchi, kupunguza mfumuko wa bei, kuongeza pato la mtanzania, kuweka huduma bora za afya angalau turudi wakati wa Mwalimu Nyerere, kujenga viwanda, kupunguza rushwa, madaraka kutopena kindugu na kirafiki na pia kufungulia mashitaka viongozi mafisadi mfano Lowassa, Chenge, Mkullo, Ngereja, Karamagi, Yona na wengine tukumbuke ufisadi ndio chanzo kikuu cha umasikini katika afrika. HAYA NDIO MAMBO MUHIMU KWANZA KWA WATANZANIA NA SIO UREFU WA BARABARA ZA LAMI WALA DARAJA LA KIGAMBONI

Mkuu Mwanamutapa,,nchi hii ni nzuri sana kuliko watu wanavyofikiri.
Kuna oppurtunities kibao!

Ukitaka kuingia biashara,mutapata biashara!
Ukitaka kuona maendeleo utayaona tu-juhudi yako kupekua
Ukitaka kuingia biashara ya siasa - ruksa tu, mradi ukubaliane Msajili wa Vyama!
Ukitaka kuwekeza, hakuna matatizo kabisa!

Na ukitaka kulalama daima dumu, napo ni ruksa- katiba inakuruhusu
Ukitaka kuwapekua wezi na mafisadi, tena hapo wapo kwa wingi sana.

Ndio maana huwaoni watu fulani fulani katika siasa, wako busy. Busy kutengeneza noti, na wanaruhusiwa kisheria. Tafuta wahindi kwenye siasa, utampata mmoja au wawili.

Kwa hiyo leo maendeleo si ya miradi mikubwa tu, lakini hata uchumi umechangamka, ila watu wanachangamkia siasa zaidi hivyo kushindwa kuona oppurtunities zilizopo.
 
Back
Top Bottom