JK: Miradi mikubwa imenishtua; Ni Miujiza Hivi sasa tunajenga madaraja matatu eti wakati wa JKN moja

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,869
1,225
[h=2][/h]JUMAMOSI, NOVEMBA 17, 2012 08:33 NA ELIYA MBONEA, KILIMANJARO

RAIS Jakaya Kikwete amesema ameshangazwa na utekelezaji wa miradi mikubwa katika awamu yake kwa muda mfupi, ikiwamo ujenzi wa madaraja makubwa ya Kigamboni, Malagarasi na Kilombero.

Rais aliyasema kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) juzi, alipozungumza na viongozi wa dini mkoani Arusha.

“Kwa kweli hata mimi, wakati mwingine nashangazwa na mambo mengi tuliyoweza kuyatekeleza katika muda mfupi.

“Hivi sasa tunajenga madaraja matatu Kigamboni urefu wa mita 680, daraja la Malagarasi kilomita 2.75 na Kilombero urefu wa mita 510,” alisema Rais Kikwete na kuongeza:

“Imekuwa ni miujiza ya Mwenyezi Mungu…chukulia mfano ujenzi wa madaraja makubwa nchini kwenye Mito ya Mara, Rufiji, Kilombero, Malagarasi na Kigamboni yalikuwa katika mpango wa pili wa miaka mitano tangu mwaka 1969, lakini hayakuweza kutekelezwa,” alisema.

Alisema wakati awamu ya Mwalimu Julius Nyerere, lilijengwa daraja moja tu kati ya hayo matano.

Alisema lilijengwa daraja la Kirumi ambalo liko mto Mara, wakati daraja la pili ni la Mto Rufiji lilijengwa na Rais wa zamani Benjamin Mkapa.

Akizungumzia suala la amani, Rais Kikwete aliwahimiza viongozi wa dini kuendelea kuiombea nchi ili amani na utulivu uliopo uendelee.

“Nawaombeni jambo moja kubwa, tuendelee kuombea amani na utulivu. Amani ikivurugika hakuna atakayekwenda kanisani, msikitini wala shambani. Amani na utulivu ndio kila kitu,” alisema Rais Kikwete.

Viongozi wa dini walioongoza maombi uwanjani hapo ni Askofu wa Kanisa la Anglikani Dayosisi ya Mount Kilimanjaro (DMK), Stanley Hotay, Askofu Dk. Leonard Majura Mwizarubi wa Kanisa la EAGT.

Wengine ni Kaimu Sheikh wa mkoa wa Arusha, Sheikh Abdilrahman Salim, Askofu Paul Akyoo Dayosisi ya Meru (KKKT) na Askofu Eliud Isangya wa Kanisa la International Evangelism Church.

Katika mazungumzo na maombi yao, kwa nyakati tofauti viongozi hao walisema wanatambua fika mafanikio yaliyopatikana chini ya uongozi wa Rais Kikwete, na yameleta ustawi zaidi kwa wananchi wa Tanzania.

 

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,869
1,225
Hivi Rais KIKWETE pamoja na kujaza familia yake CCM-NEC bado anataka kujilinganisha na Mwl. Nyerere kuleta Maendeleo Tanganyika? Maendeleo ya Nyerere yalikuwa BORA zaidi ya Madaraja ALIJENGA UMOJA, AMANI na UPENDO kwa Wananchi Wake... Hakutukuza UDINI; UKABILA wala UFISADI kama Rais Kikwete na Serikali yake NDANI ya CHAMA walivyo na Hamu ya KULA MALI za TAIFA...

Sasa, ni kwanini aliongelea UDINI na UKABILA wakati wa UCHAGUZI wake 2010 BILA hivyo SASA HIVI Angekuwa BAGAMOYO-KISARAWE akiangalia NDEGE za kimataifa ANGANI...

AACHE KUJILINGANISHA na MARAIS WALIOMPITA - AJARIBU kujenga LEGACY YAKE MWENYEWE...
 

Gad ONEYA

JF-Expert Member
Oct 26, 2010
2,636
1,195
Aulizwe wakati wa Nyerere ni migodi mingapi ilikuwa inachimbwa na wageni na mapato ya serikali yalikuwa yanatoka wapi na yalikuwa yanatumikaje kipindi hicho na sasa ndo aanze kufanya comparison!

Wakati wa Nyerere budget support na misaada lukuki kama hii ya neti wa kupambana na malaria ilikuwepo?
 

sabasita

JF-Expert Member
Oct 29, 2009
1,506
1,225
:nimekataa:nimekataa:nimekataa:nimekataa:nimekataa:nimekataa:nimekataa
 

JERUSALEMU

JF-Expert Member
Sep 19, 2012
2,881
2,000
Kwanza fedha za ujenzi wa daraja la malagarasi amezikuta. ulikuwa ni msaada wa KOREA kama shukrani kwa serikali ya BENJAMINI WILLIAM MKAPA kwa kumuunga mkono na hatimaye kumpigia kura UN ili awe katibu mkuu wa UN.mazungumzo ya win win kati ya serikali ya korea na Tanzania yaliongozwa na aliye kuwa waziri wa mipango uchumi wa wakati ule mh Dr Ngasongwa.kwahiyo yeye amezikuta fedha zipo na ramani ikiwa imechorwa na CHUO CHA ARDHI DARes salaam. Kwahiyo yeye miradi mingi kaikuta hakuna mradi alio ubuni yeye 100% labda udini,kambi, na kukandamiza vyama vya siasa kwa kumtumia JOHN TENDWA.
 

aspen

JF-Expert Member
Jul 13, 2011
502
250
Inabidi tuache chuki kwa kipindi chake amejitahidi sana ukweli ndiyo huu hata kama mchungu ifike mahali akijitahidi tuseme ukweli siyo kwamba hajafanya lolote ndiyo maana individuals hatuendelei kwa sababu ya kiroho
 

masopakyindi

JF-Expert Member
Jul 5, 2011
14,713
2,000
Siyo bure kuwa utekelezaji wa miradi mikubwa unafanyika katika miaka hii, hasa awamu hii ya nne.
Sababu nzuri tu zipo na zenye mantiki, nitataja chache tu.
  1. Mabadiliko ya kisaikolojia-alipoingia Rais Mkapa yalitokea mbadiliko makubwa ya kisaikolojia, na kugundua kuwa kuna uwezo mkubwa tu wa kutekeleza miradi mikubwa kwa hela zetu wenyewe.
  2. Kuongezeka uwezo wa kitaalam-kuanzishwa kwa TANROADS kumetatua kwa kiasi kikubwa sana usimamizi wa miradi ya ujenzi ukilinganisha na usimamizi wa miska hiyo kupitia Wizara ya Ujenzi moja kwa moja.
  3. Kuanzishwa kwa Road fund-fedha ya utekelezaji w miradi ya ujenzi imekuwa ni rahisi kwa miaka hii kuliko ilivyokuwa miaka ya awamu ya kwanza au ya pili
  4. Makandarasi wa kichina-pamoja na matatizo yao, wakandarasi hawa wa kichina wametoa changamoto kubwa kupunguza gharama za ujenzi wa miundombinu mingi.Wengi akilini mwao, hasa viongozi,waliwapa umuhimu wa kwanza makandarasi toka Ulaya, makandarasi ambao ni ghali sana pamoja na wasimamizi wao wa miradi.

Sera sahihi za CCM katika fani hii lazima zipongezwe, tupende tusipende.

Ule utegemezi wa mawazo toka World Bank na nchi za Ulaya na Marekani katika utekelezaji wa miradi ya miundo mbinu umepungua sana na ndiyo maana maendeleo yanaonekana.
Hata miaka ya Mwalimu, wakubwa hao(World Bank na nchi za Ulaya/Marekani) walikataa kufadhili TAZARA wakidai mradi huo hauwasaidii watanzania.

Kwa msimamo huo wa kujitegemea katika kufikiri, the sky is the limit!
 

Father of All

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
3,089
1,225
Nahisi kichefu chefu panya kujilinganisha na Simba. Natamani nimrambe mtu vibao ila sina uwezo. Pumba pumba tupu Kikwete kujilinganisha na Nyerere. Hana adabu wala busara na nachelea kusema ni mpuu. anyways tuyaache. Vidaraja vitatu anavimba kichwa je angejenga Chuo Kikuu, kusomesha na kutibia watoto wote wa kitanzania ukiachia mbali kusaidia ukombozi wa nchi za kusini mwa Afrika si angepasuka bure? Shame on him he who sees no reality!
 

Mthuya

JF-Expert Member
Jun 9, 2011
1,415
1,225
Huyu baba anaakili ndogo kweli miradi yenyewe wanapewa Wa China tena ya mkopo
 

khamsa

Senior Member
Jul 17, 2012
155
195
Nahisi kichefu chefu panya kujilinganisha na Simba. Natamani nimrambe mtu vibao ila sina uwezo. Pumba pumba tupu Kikwete kujilinganisha na Nyerere. Hana adabu wala busara na nachelea kusema ni mpuu. anyways tuyaache. Vidaraja vitatu anavimba kichwa je angejenga Chuo Kikuu, kusomesha na kutibia watoto wote wa kitanzania ukiachia mbali kusaidia ukombozi wa nchi za kusini mwa Afrika si angepasuka bure? Shame on him he who sees no reality!
acha chuki zako wewe! Udom kajenga nani?, hombolo kajenga nani?, maboresho ya muhimbili,mwananyamala na amana kafanya nani, nasema kikwete anao udhaifu kama binadam lkn pia yapo mengi amefanya kwa mafanikio kuliko awamu zote.
 

Father of All

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
3,089
1,225
Mwanangu Hamsa tumia akili vizuri. Huwezi kulinganisha hiyo miradi yako miwili na utitiri wa mambo aliyofanya Mchonga hasa kuwasomesha, kuwatibu na kuwalisha bure hao hao akina Kikwete wanaotoza watu pesa kwa ajili ya elimu na huduma nyingine muhimu.
 

Hashpower7113

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
1,261
2,000
acha chuki zako wewe! Udom kajenga nani?, hombolo kajenga nani?, maboresho ya muhimbili,mwananyamala na amana kafanya nani, nasema kikwete anao udhaifu kama binadam lkn pia yapo mengi amefanya kwa mafanikio kuliko awamu zote.
Mbona mbovu linakutoka na wew gamba nn? Wez wa mali zetu? Mtenda mema hajisifi mwenyew asubir tumsifie

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 

babe S

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
3,862
2,000
Aashangaa nini sasa! Wajibu wake! Tena mbona bdo ukipima miaka aliyokaa waliyoyafanya mabaya a mazuri ukilinganisha na rasilimali mbona bdo sanaa!
 

Donn

JF-Expert Member
Jun 5, 2012
2,438
2,000
Deni la taifa limeongezeka maradufu, ugumu wa maisha mara mbili, ufisadi uweshamiri, pato la madini limekuwa kama ugali kwa picha ya samaki. Amani ya nchi imepungua na udini na ukabila kuongezeka. Alafu leo unasimama kujisifia??!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom