JK-Mchumi dhaifu anayeamini Uchumi wa Nchi kuendeshwa kwa Malori bila Reli

spencer

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
3,599
3,220
GreatThinkers,
Nilikuwa Dar wiki iliyopita, siku hizi Dili ni kuwa na Eneo tuu inakuwa yard ya Makontena na ndiyo sababu ya Kina Masaburi pia kujiuzia UDA-ndiyo wanaitaka ile yard ya kurasini wakodishe ili makontena yahifadhiwe pale.

Sikuamini macho yangu yani hadi Tabata kuna Yard za makontena savi ni jambo la kawaida sana kuona Mandel milimania road Malori zaidi ya miambili yamejipanga kila upande wa barabara yakisubiri kupakia mokentena!

Hiyo ni degree feki, au basi ilikuwa ni Gentleman. Hivi kwa nini bandari ya nchi kavu Isaka iwekufa?? Hivi kwa nini hawaonei huruma watu wa Dar wanavyopata tabu na mijasho ktk Dala dala kwa foleni kisa Malori na uchache wa Barabara?

Ni jambo la Aibu sana kwa kiongozi kupenda matanuzi tuuu wakati nchi inadidimia kiuchumi.
Jk ni kiongozi dhaifu anyeamini Fly Over itapunguza foleni-Jibu ni NEVER. Mwaka 2006/2007 wakati ule wa mafuriko ya Elnino, nakumbuka maeneo hayo hayo ya Tabata barabara ya Mandela karibu na Mabibo kuta za hayo magodown zilivunjwa na maji yaliyotokea Morogoro milimani tena mcha mchana na mvua haikuwepo. Nataka kusema nini Ukifika vingunguti bondeni ule mto Msimbazi umejaa nyumba za walalaho Dar, hakika ikitokea mvua kama ile, Maiti nyingi zitapotelea Baharini!!!

Watu wameuziana viwanja kwa misheni town, niliwahi kuwaza hata kuwa na " Msimbazi Valley Authority-MVA" ili idhibiti ujengaji holela.

Kwa nini huyu haumizi kichwa juu ya taifa? Kwa nini Makao Makuu Reli isihamishiwe hata Pugu watu wakapandie kule au basi ajenge miyadi maeneo ya Gongo la mboto, Kinyerezi kwenda Kimara na Mbezi? huko hakujaa auache mji upumue!

Yote hayo ni kujilisha upepo, hajifunzi kwa kina Kagame au Kibaki matanuzi ya ajbu ajbu hayapo. Saivi ana projekt ya kuwajengea mafisadi paradiso Kigamboni city, ndicho anachokifikiria,hana jingine.

Engine ya Locomotive inaweza kubeba tani hadi 400. namaanisha kontena zaidi ya Ishirini zilizo na tani hadi 18 gross weght. hapo ni malori zaidi ya Ishirini umepunguza Dar umeyaelekeza Isaka Dry Port-Shinyanga vijijini.
Bandari ya Dar Es Salaam kwa siku inapakua zaidi ya kontena 500 kwa siku namaanisha ili ufanisi uwe mzuri, zaidi ya malori 500 kwa siku yazunguke town achilia yale 500 yanayoleta mizigo na mengine 500 yawe standby. Hiyo ndiyo akili ya mchumi inayoamini kuwa uchumi umepanda kwa sababu Dar kuna foleni kumbe mfumo mbovu aliouweka ndio unamfanya ashindwe kujua nini tatizo.

Upeo wake labda unaishia hapo, anaamini kuwa kuna maendeleo kwa kujaza malori mjini Dar.
"Wewe bado mdogo, huwezi kuendesha nchi-Subiri" Mwl. Nyerere 1995.

Maneno hayo siyasahau kwani hatimae nimeelewa ya kuwa Mwl. hakumaanisha kuwa udogo ilikuwa ni Umri bali ilikuwa uwezo wa kuendesha uchumi wa nchi
Nawasilisha.
 
Mkuu umenena.mimi ni mdau wa bandari.kabisaaaa.na ni muhusika.kinachonishangaza mimi,kuna proposal ilitolewa kipindi kile cha congestion bandarini.na kukawa na mzozo sana,kuwa.hz bandari kavu yani ICD'S km hyo hapo tabata AMI.ama Trh n.k.ziingie ubia na bandar.yaan TPA ama TICTS.hawa wanapakuwa,clearing wanakuja wanalipia bandarini.mzigo wanakuta ushakuwa allocated ICD flani.lakini sasa ni tofauti.container linatolewa.wanapewa wenye Yard.ICD.wamcharge clearing.tena na gharama zaongezeka.isitoshe kuna michezo inachezwa kwenye charges.ku undercharge pamoja na storage.matokeo yake kushusha mapato ya serikali.kulikuwa na ulazima gani wa hawa watu kulipia huko hali bandar ipo?so tpa na ticts producers.wale icd ni wholesalers as well as retailers kwa kazi hzo?ikiwemo kujipangia the final charges?serikali iamke.isibane tu wafanyakaz kwenye PAYE.WAKATI WAFANYABIASHARA WANAPETA.MY OPINION.SUMATRA+GOVERNMT.RUDISHENI MALIPO BANDARINI.WAKUSANYE MALIPO ILI TAX COLLECTION YOTE IPATIKANE BILA KUCHAKACHULIWA.HZO YARD ZIHIFADHI.WAINGIE MKATABA NA TPA NA TICTS.WAWE WANALIPWA CHARGES ZAO ZA KUIFADH.NA MZIGO YA ICD IPANGIWE MIDA YA KUTOA NA KUINGIZA.KUKWEPA FOLENI ZA BARABARANI.MANA RELI HAMTAK TENGENEZA.KWA MANUFAA YAO YA ICD'S.I LOV TNZN
 
Umenena kaka, jamaa ana digrii feki ya Uchumi cause hata mimi ambae nimeusoma kidigo Chuoni siwezi ku analyse mambo kama anavyofanya yeye.Ukiangalia kwa makini, upandaji wa bei za bidhaa hasa mikoani husababishwa na gharama kubwa ya kuzisafirisha bidhaa hizo hadi kufika huko.Ameua reli ya kati, na ile ya Zambia tushukuru tu kwamba tunashirikiana na wenzetu wa Zambia.Huyo ni mchumi anayeamini katika kutatua matatizo kwa njia za zima moto, ni mchumi ambaye anafanya assumption kwa kutumia variable moja badala ya kutumia number of factors. Aibu sana kaka.
 
Umenena kaka, jamaa ana digrii feki ya Uchumi cause hata mimi ambae nimeusoma kidigo Chuoni siwezi ku analyse mambo kama anavyofanya yeye.Ukiangalia kwa makini, upandaji wa bei za bidhaa hasa mikoani husababishwa na gharama kubwa ya kuzisafirisha bidhaa hizo hadi kufika huko.Ameua reli ya kati, na ile ya Zambia tushukuru tu kwamba tunashirikiana na wenzetu wa Zambia.Huyo ni mchumi anayeamini katika kutatua matatizo kwa njia za zima moto, ni mchumi ambaye anafanya assumption kwa kutumia variable moja badala ya kutumia number of factors. Aibu sana kaka.

he should take some times learn MULTIVARIATE ANALYSIS!! au aende kwa dani yona amfundishe maana yule hobbie yake ni kufanya hesabu!
 
Kaka reli zinakufa wakati ndo nguzo ya usafirishaji kwenye nchi yeyote inayoongozwa na viongozi makini,wamekazania barabara reli imeachwa wakati ilitakiwa kuwe na link kati ya barabara kutoka vijijin na kwenye station za reli..mi najionea Tazara inavyokufa dah we got long way to go with no direction.
 
Jiziwani wake ana mradi wa malori ya kusafirisha mizigo. Siyo kwamba hajui ila ni biashara ya familia
 
Katika Hili JK is Irrelevant,hausiki kabisaaa mumuache amalize kazi yake aliyoipanga toka anaingia magogoni. nayo si nyingine bali kuwa Raisi na sasa Ameshakuwa Rahisi kwa ngwe ya pili
Solution ya ICD na Msongamano wa Malori njiani
SISI Wananchi kukaa kitako na Serikali za mitaa yetu.kupata muafaka kwani ili mtu apate kibali cha kuweka yard uswahilini lazima Mtendaji na Mwenyekiti wa serikali za mtaa wahusike
Jiulize Yafuatayo
Je unamjua mwenyekiti na mtendaji wa serikali ya mtaa wako?
Jiulize lini ulienda kwenye ofisi ya Mtaa wako?
ulishawahi kuomba report ya matukio ktk mtaa wako?
Ktik ofisi ya mtaa wako kuna Notice Board ya kutoa taarifa,je watu wangapi wanaisoma?
Tuelimishane umuhimu wa nguvu ya UMMA katika maamuzi ya serikali ya mtaa wako


Tafakari Chukua Hatua, hatuhitaji Msaada wa Watu wa USA kujua mambo ya mtaani kwako
 
GreatThinkers,
Tafakari ujumbe wangu kumbuka nilionya juu ya mafuriko lini na leo kunatokea nini?

Mimi mtu wa kawaida, nilitaraji mwajiliwa/waziri wa aridhi alijue mapema hili na kulichukulia hatua.

Kwa nini kila kitu mko vugu vugu na wakati mwingine baridi?

Mauriko haya iwe fundisho, nyadhifa mlizonazo kama wewe siyo greatThinker ikatae hiyo position.

Ni hayo tu, leo Dec 23/2011
 
Ukiona hivyo kuna maslahi ya mkuu wa kaya na wenzake magamba kama kawaida
 
Hivi JK anafanyia kazi kweli maoni yetu?
Laiti kama angesoma thread yangu hii mapema yale maafa ya mafuriko dar yangekuwa kidogo sana.
hii ishu ya reli nayo ngoja tuitafutie dawa kama hasikii
 
Back
Top Bottom