JK may become AU President!

Hivi JK akisha kuwa Prezido nini faida kwa mlala hoi mimi ? Mana nikijua faida kwa Nchi hapo nitasema lolote .Kumekuwa na hata Spika wa Bunge la Africa lakini wizi wizi wizi
 
Uenyekiti wa AU na baba yake OAU ni mzunguko wa kisiasa na hauna maana ya merit kwa anayetunukiwa. Hata Iddi Amin aliwahi kuwa mwenyekiti.
 
Ok kumbe sasa sina haja kujiingiza kujadili hili naweka nguvu zangu kwenye wizi wa BoT
 
Kuna mwanamuziki nadhani wa kile kinachoitwa "Kizazi kipya" ambaya ana wimbo usemao "Sifa za Kijinga". Sikumbuki maneno yake ila hilo jina lake limenifanya niamini yawezekana JK apewe Uenyekiti ili Tanzania ipate sifa, naam, Sifa za kijinga!
 
Ya Tanzania tu yanamshinda usanii kila kukicha! Ya Afrika atayaweza!?
 
Au imekuwa ni club ya wapiga bla bla tu; sioni umuhimu wake kama wameshindwa kutatua mgogoro wa Kenya ambao uko wazi kabisa. Wameamua kuufumbia macho na kumruhusu Kibaki aingie kama Rais wa kenya huku wakijua kuwa ndiye chanzo cha matatizo yanayoikumba Kenya leo hii.

Kwa maoni yangu, kwa vile AU ni irerelevant, mtu yeyote hata mwendawazimu anaweza kuingoza kwani iko kama non-existent.
 
Kuna mwanamuziki nadhani wa kile kinachoitwa "Kizazi kipya" ambaya ana wimbo usemao "Sifa za Kijinga". Sikumbuki maneno yake ila hilo jina lake limenifanya niamini yawezekana JK apewe Uenyekiti ili Tanzania ipate sifa, naam, Sifa za kijinga!

Elimisha jamii kwa kuwaeleza ni nini majukumu ya Mwenyekiti wa AU kwani Tanzania ni Mwanachama halali kama wanachma wengine na ina haki sawa.
Kumbukeni kuwa uwakilishi wa Rais ni uwakilishi wa wa Tanzania wote.
'Ya Kaisari mpeni Kaisari...' Msiwe na chuki na mtu hapa tujadilini na mazuri yake pia.
 
JK kupata Uenyekiti wa AU ni ushindi kwa CCM. Atafanyiwa maandamano makubwa nchi nzima kwa ajili ya hilo. Wale wanaojipendekeza wataandaa maandamano, kulazimisha watu wacache shughuli za uzalishaji mali kumshangilia Mfalme wa Kikwere aliye uchi kuonyesha joho jipya!
 
Hoja Mbili:
1. JK akipewa hicho cheo cha umwenyekiti wa AU haitaathiri utendaji wake nchini, maana hicho cheo ni mere ceremonial, mtu mwenye kazi kubwa ni mwenyekiti wa AU Commmission. Hawa marais hakuna lolote.

2. Mpaka sasa African countries zimeweka wazi kwamba suala la Kenya ni internal issue, na kusisitza kwamba taratibu zote za election zipo chini ya sheria za ndani ya nchi husika, kwa maana hiyo AU has nothing to do with Kenya's irregularities in her election, sana sana watamshauri Mh Kibaki kufanya mazungumzo na ODM. Lakini hiyo haitakuwa agenda ndani ya taratibu za AU meetings.
 
No wonder hata Idd Amin alikua mtu wa muhimu huko AU. Sasa nadhani Jk anaweza tu kupewa uenyekiti.Si suala gumu sana
 
Back
Top Bottom