JK kuwa Rais mpango wa Mungu ili kufikia kusudi la Mungu.

Nikukumbushe

JF-Expert Member
Jun 4, 2013
2,602
0
Kuna vitu viwili tunatkiwa kuvitofautisha.
1.Kusudi na
2.Mpango
Nikianza na mpango,hizi ni njia,mbinu ambazo kila mtu/taasisi hupitia ili kufikia kusudi fulani,huwezi kufikia kusudi kama huna mpango.Mipango inaweza kubadilika au kwa manaeno mengine unaweza kusema,ili kufikia kusudi unaweza kupitia njia mbalimbali,au unaweza kuunganisha hizo njia ili kufikia kusudi.
Tunaposema CHADEMA ni mpango Mungu kuingia Ikulu tunakosea,bali tuseme CHADEMA ni kusudi la Mungu.
Kusudi la Mungu huwa halibadiliki,bali mpango hubadilika.Je,ni mipango ipi ambayo CHADEMA Mungu kaipa ili kufikia KUSUDI la kuingia ikulu?
Mosi,ni mpango wa Mungu kumteua Rais Kikwete ili achaguliwe na wananchi kuwa Rasi wa awamu ya nne,kivipi,kwa kutumia udhaifu wa Jk Mungu ametumtumia kama sehemu ya ku-Disclose mabaya na maovu yote yanayofanywa na serikali ya CCM.Udhaifu huu,ni pamoja na kushindwa kuwachukulia sheria mafisadi,wanaobaka,wauza unga nk.Kutokana na udhaifu huo,Mungu kaipa chadema mpango huu kama njia ya kufikia kusudi la kuingia ikulu.
Pili,mbinu zote chafu zinazotumia na ccm kuhakikisha kuwa CHadema inasambaratika zinavuja ili kuupa umma taarifa ya kile ccm inachokifanya ili mwisho wa siku ije ishindwe kwa sanduku la kura.
Hivyo,udhaifu huu wa Jk(Jj.Mnyika) na serikali yake ni mpango wa Mungu ili chama kingine kipate fursa ya kuingia ikulu.Pengine isingekuwa JK kuwa Rais,uwezekano wa kuingia ikulu ungekuwa mdogo kwa maana pengine angekuwepo rais ambaye haya tunayoyashsuhudia kwa Kikwete tusingeweza kuyaona kamwe.
Kwa hyo Jk kuwa rais ni mpango wa Mungu kumtumia ili upinzani upate sehemu ya kuingilia Ikulu au ili kusudi la Mungu kuona ccm inafikia ukomo wake kupitia Jk ili kuruhusu kusudi la Mungu kuona CDM inaingia ikulu.
Nawasilisha
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom