JK kutumia Mkutano wa CCM kulihutubia Taifa

Mtoto wa Mkulima

JF-Expert Member
Apr 12, 2007
681
126
JK kutohutubia Taifa

Habari Zinazoshabihiana
• Njohole atakiwa Uswisi Jumatatu 31.08.2006 [Soma]
• Matumaini ya wafanyakazi leo ni kwa Kikwete, Karume 01.05.2007 [Soma]
• Mwananchi alia na Wabunge kukanyaga 'Bendera ya Taifa' 07.07.2006 [Soma]

RAIS Jakaya Kikwete hatalihutubia Taifa mwisho wa mwezi huu kama utaratibu ulivyo, kwa vile anatarajia kutoa hotuba ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) unaotarajiwa kuanza Jumamosi hii katika ukumbi wa Kizota, Dodoma.

Taarifa iliyotolewa jana na Ikulu, Dar es Salaam, ilisema katika hotuba hiyo ya ufunguzi, Rais anatarajiwa kutumia fursa hiyo kuzungumza na wananchi wote kwa ujumla na kuelezea na kutoa ufafanuzi wa masuala muhimu ya kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Wakati huo huo, Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Yusufu Makamba, anatarajia kuzungumza na waandishi wa habari, jijini Dodoma leo, huku habari zikisema atatumia mkutano huo kujibu mapigo ya wapinzani.

http://www.majira.co.tz/kurasa.php?soma=tanzania&habariNamba=4386
 
Hii ni dharau, na inaonesha ni jinsi gani viongozi wetu wasivyojua kutofautisha majukumu na mamlaka ya chama na yale ya Serikali. Si mara ya kwanza kufanya hivyo, hata last time wakati kukiwa na mkutano wa Halmashauri Kuu kule Dodoma alifanya hivyo ingawa ilikuwa ni kwa style nyingine. Alisema anaongea na Taifa kupitia Mkutano wake na Wakazi/Wazee wa Dodoma, lakini akatumia muda mwingi sana kuongea mambo ya C.C.M.Hamkumbuki kipindi kile alipowaagiza wana C.C.M. kuwanyima kura wanaojinadi kupitia jina lake? Si hiyo ilikuwa wakati analihutubia Taifa? Sasa mambo ya C.C.M. wakati wa kulihutubia Taifa wapi na wapi? Dharau hiyo!!!!! Si wananchi wote ni wanachama wa C.C.M.
 
Back
Top Bottom